Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Juzi tulisikia huko Tabora Bwana fulani akiwaambia Wananchi kwamba Serikali imekosea badala ya kutatua kero ya Maji inanunua ndege! Inaweza kwa haraka haraka kuonekana na hoja miongoni mwa wenye akili nyepesi. Lakini kwa wanaotafakari kiuchumi zaidi wataona tofauti na hoja za Bwana huyo!
Juzi nikaambiwa na Mzee mmoja kwamba Bwana huyo aliwahi kuwa Serikalini wakati Serikali ikinunua ndege ya Serikali, Rada n.k lakini wakati huo hakujua kama kuna shida ya maji. Pia Mzee huyo akanidokeza kwamba Bwana huyo aliwahi kuwa Waziri Mkubwa na Waziri mwenye dhamana ya Maji na Mifugo, lakini wakati huo hakuona kama Tabora wana tatizo la Maji!
Huko huko kuna Bwana mwingine aliwahi kuwa Waziri mkubwa kwa miaka 10 lakini hakuona tatizo la maji huko Tabora na kwingineko mpaka alipokwenda upande uleeee! Yule Mzee akaniambia kwamba kijana wangu, ukiwa upande huu huwezi kuona mpaka uwe upande ulee! Amesema sababu za kuona vizuri ukiwa kule ni unafiki wa kutaka madaraka kwa gharama yoyote ikiwamo unafiki na kuwafanya watu wajinga! Unaigiza maisha yao ambayo hukuwaza hata siku moja kuyaonja lakini lengo likiwa ni kupata uungwaji mkono!
Utasema Serikali haijafanya chochote tangu tupate uhuru wakati unazurura kwenye Barabara zilizojengwa na Serikali na unalipwa mafao na Serikali unayoitukana! JAMANI! JAMANI! Mungu anawaona lakini kwa unafiki wenu!! Nchi haiwezi kutwaliwa kwa unafiki namna hii!! Mungu anawaona lakini!
Mlidandia hoja ya Katiba ya Wananchi kuombea kura na kwa kweli watu waliaminishwa kwamba mtapigania Katiba, lakini baada ya kuzoa viti vya Madiwani na Wabunge Ajenda hiyo ya Katiba haipo tena! Mungu anawaona lakini ooooh!