Chadema, CCM yametimia


Wamepagawa na udini na ukabila hiyo ndiyo falsafa kubwa wanayoielewa!!

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Kusingekua na Chadema chini ya uongozi wa Mbowe, iliyolea watu machachali bungeni kama Zitto, Slaa, Wangwe n.k. Nafuu iliyopo ya maisha(japo wengine mtasema haipo) isingekuwepo. Tanzania ingekua mbaya kuishi kuliko mnavyofikiria! Mchango wenu chadema ni mkubwa sana kuwafanya hao wavivu, wazembe, walafi, wezi, na wanyonyaji warekebike angalau hiyo 5% (Lowassa, Rostam, Karamagi, Chenge). Ufisadi ni agenda muhimu, msishawishike kuiacha. Sana sana ongeza agenda ya kukilenga CCM katika ahadi zilizotolewa kipindi cha uchaguzi wasije wakageuza ahadi zile kuwa zilikua za watu sio za chama (Amini usiamini wanampango wa kumchafua kikwete kwa kumbebesha uchafu wote kukisafisha chama mwaka 2015)

Bila upinzani, hakuna demokrasia, hakuna maendeleo. Kaza buti Mnyika, Kaza buti Zitto, Kaza buti Slaa, Kaza buti Lema, Kaza buti Heche, Kaza buti wananchi, TUTAFIKA tuendako muda si mrefu!
 
C lazima nkupende ili uishi ila kwavile unakataa ukweli mi naku-DIS
 
Amempita st. nyerere kwa mbali sana ndani ya 6yrs, barabara, elimu, uhuru, uchumi..list can go on..
Maisha bora kwa kila Mtanzania. Bei ya sukari imepanda kutoka shilingi mia sita kwa kilo enzi za Mkapa hadi elfu mbili mia tano. Umeme wa uhakika ametupatia. Shule za kata zinatoa Watanzania wenye elimu ya kiwango cha juu na uchumi unazidi kupanda kwa mafisadi na wawekezaji Kwa hakika Kikwete ni best President of all time
 
Mkuu katika siasa humu JF kuna makala mbili ambazo zingewwza kutusaidia sana kama Mods wangestick hapo juu; moja ni ya MMM inaongelea mambo ya power triangle (kama sijakosea) na nyingine ni ile ya kwako inayodadavua itikadi za vyama toka mrengo wa shoto kuelekea mrengo wa kulia. Watu hatuchambui siasa bali kejeli na matusi sijui ni kukosa hoja au nini?
Kwa upande mwingine CDM isilaumiwe sana kwani hatukumbuki kuwa walikutana na Rais mara mbili na tangia hapo CDM imekuwa kimya. Kwani hatujui kuwa katika majadiliano kuna win win situation? Tunadhani kwamba CDM wao tu ndio waliibuka washindi kwa kupenyeza hoja zao kwenye sheria ya mchakato wa katiba? Nadhani na serikali pia ilipenyeza matakwa yake; acheni vurugu zenu kwa njia ya maandamano! Tangia hapo maandamano kimyaaaaa!
 

Mkuu Kimbunga,
Naona ili bandiko lako umemaliza kila kitu.
 

Source ya habari hii ni TAZAMA la tarehe 21-02-2012. Ushauri kwako ritz, heshimu kazi za watu
utumiapo kazi ya mtu, kumbuka kuweka wazi kwamba kazi hii ni ya nani. Wana jf nadhani wote
hapa jf tunajuwa mmiliki wa gazeti la TAZAMA na uharamia alotufanyia watz, tunajua pia msimamo
magazeti yake dhidi CHADEMA na wote wanaopigana vita dhidi ya ufisadi, hivyo tunapojadili habari hii
lazima tujiulize lengo lake ninini?
 
Mkuu Mkeshaji,
Huu ndio ukweli unajua kila siku unapiga kelele za ufisadi ufisadi, zimewachosha watanzania lazima Chadema kama chama ibuni falsafa mpya kutegemea kuhubiri ufisadi kama kete yake haitakisaidia Chadema huko tuendako.
Huwezi amini hii ndo kete ya kuibeba CDM na kuiozesha CCM hadi hata kizazi hiki kijapopita
 

Mkuu, acha kulia lia jibu hoja JF ni jukwaa huru wala sio mali ya Chadema.
 
Mkuu Mkeshaji,
Huu ndio ukweli unajua kila siku unapiga kelele za ufisadi ufisadi, zimewachosha watanzania lazima Chadema kama chama ibuni falsafa mpya kutegemea kuhubiri ufisadi kama kete yake haitakisaidia Chadema huko tuendako.
Umesema ukweli mtupu ustaadhi, sasa hivi wananchi wanapenda sana kusikia wananchi wenzao wameuawa na polisi kule Songea, Mwakyembe hakulishwa sumu, wakuu wa wilaya kupewa wajibu wa kukusanya maoni ya katiba mpya, hali ya mfumko wa bei umesababishwa na maandamano yasiyoisha ya CHADEMA, kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni matokeo ya mfumo kristo unao wapendelea wanafunzi wa seminari na st., matatizo ya umeme nchini yataendelea kutatuliwa kidharura............................., kidumu chama cha hawa hawa!!!!!!!!!!1 ccm nambari 10.
 
Kwa taarifa yako CHADEMA inaimalika zaidi kuliko uelewa wako wa siasa
 

Akili zilizofulia utaziona tu , una nasaba na tendwa? Moderator futa huyu tunafutie great thinka plz
 
Kimbunga,
Nakuhakikisha mipango ya maandamano bado ipo pale pale. It is just a matter of time and it has nothing to do with mkutano wa Ikulu kuhusu katiba. Just stay tuned!
 
Akili zilizofulia utaziona tu , una nasaba na tendwa? Moderator futa huyu tunafutie great thinka plz

Mods; wapo makini na kazi zao hawawezi kufanya kazi kupokea maelekezo kutoka kwa wahuni.
 
Kimbunga,
Nakuhakikisha mipango ya maandamano bado ipo pale pale. It is just a matter of time and it has nothing to do with mkutano wa Ikulu kuhusu katiba. Just stay tuned!

Jasusi,
Kama unakumbuka baada ya mkutano wa Chadema na Rais Kikwete Ikulu, Dar es salaam.

Katibu Mwenezi wa Chadema John Mnyika, alisema wameamua kuacha maandamo kwa sababu wamegundua sio njia sahihi.
 
Jasusi,
Kama unakumbuka baada ya mkutano wa Chadema na Rais Kikwete Ikulu, Dar es salaam.

Katibu Mwenezi wa Chadema John Mnyika, alisema wameamua kuacha maandamo kwa sababu wamegundua sio njia sahihi.
Labda Mnyika alikuwa quoted out of context. Nijuavyo mimi suala la maandamano bado lipo pale pale. Ni timing tu.
 
uchunguzi wako ni kwa mujibu wa nini? au unasukumwa na unazi wa kupindukia ulionao juu ya CCM?
Mm sijaona huo mwamko watu walionao juu ya CCM!
Huyu jamaa sasa hivi anajipambanua kama mtafiti. I guess source ya utafiti huu ni yeye mwenyewe.
 
ccm igunga= tik
ccm uzin= tik
ccm arumeru= historia haibadiliki !
Tik hizi zimejaa magumashi mengi sana, mara wizi wa kura, mara vifo vya wasimamiz, mara rushwa. Kwa kweli ni aibu kuelezea ushindi huu wa hila mbele ya siasa za kistaharabu. Kimsingi ni ushindi wa kihuni ambao sio kipimo kizuri cha kukubalika kwa chama chenu mbele ya jamii mana mnatumia nguvu kubwa mno kununua mvuto kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…