CHADEMA, CCM watwangana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, CCM watwangana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 23, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • POLISI WASUASUA KUKAMATA WALIOHUSIKA

  na Samwel Mwanga, Meatu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  WATU wawili wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, mkoani Shinyanga kutokana na mapigano makali yaliyozuka kati ya vijana wanaosadikiwa kuwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Waliojeruhiwa katika mapigano hayo yaliyozuka juzi majira ya saa 10:30 jioni katika eneo la mnadani mjini Mwanhuzi na kudumu kwa nusu saa, kiasi cha kusimamisha shughuli mbalimbali za biashara zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo, wametambuliwa kuwa ni Jeshi Jumanne na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Masai.
  Kundi kubwa la vijana waliokuwa wamevalia sare za kijani na njaro wakiwa ndani ya gari aina ya Isuzu Tipper lenye namba za usajiri T 792 AHE mali ya Diwani wa Kata ya Mwanhuzi mjini, Eliya Shukiya (CCM) wakiongozwa na kijana aliyetambuliwa kwa jina la Charles Dominick, lilifika katika eneo hilo na kuanza kuwashambulia vijana wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (bodaboda).
  Vijana hao wakiwa wamebeba mapanga, nondo na mawe walianza kuwatwanga vijana waendesha pikipiki za abiria kwa madai kuwa walitaka kwenda kuvuruga mkutano wa hadhara wa CCM ulikokuwa ukiendelea kwa wakati huo katika uwanja wa kituo cha mabasi.
  Mmoja wa vijana aliyeshambuliwa na kujitambulisha kwa jina la Dan John aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakiwa katika kituo chao cha biashara huku wengine wakila nyama choma za mbuzi, waliona gari la mbunge likiwa na vijana likiwasili mahali hapo na ghafla wakaanza kushambuliwa.
  “Tukiwa tunaendelea na shughuli zetu za biashara mara niliona gari la mheshimiwa diwani wetu wa Mwanhuzi likija likiwa limebeba vijana wa CCM waliokuwa wamevalia sare za chama chao …cha kushangaza wakateremka kwa kasi huku wengine wakiwa na mapanga, nondo, sululu na mawe na kuanza kutushambulia,” alisema Dan John.
  Alisema waliamua kuanza kujibu mapigo na ndipo mapigano makubwa yalizuka, kwa zaidi ya nusu saa huku ikidaiwa kuwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya, SP Julius Mjengi, aliyefika eneo hilo muda mfupi tangu kuanza kwa vurugu hizo alilazimika kuita askari polisi zaidi ambao walifika na kuweza kutuliza vurugu hizo.
  Pamoja na polisi kujua chanzo cha vurugu hizo, hawakuweza kuwakamata vijana hao wa CCM ambao walipanda gari lililowaleta na kuondoka katika eneo hilo wakiwa na silaha zao na kurudi kwenye mkutano uliokuwa ukihutubiwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Salum Khamis (Mbuzi), aliyeshindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita na Mbunge wa sasa, Meshack Opulukwa (CHADEMA).
  Hata hivyo, vurugu hizo ziliendelea majira ya saa 1:30 jioni katika eneo la Stendi baada ya kundi hilo la vijana wa CCM kuvamia katika Baa ya Yulitha Stephen, ambaye ni mwanachama wa CHADEMA na kuishambulia kwa mawe na kuharibu mali zilizokuwamo ndani na kupora masanduku mawili ya bia.
  Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kueleza kuwa wanaendelea kuwatafuta watu wote walioanzisha vurugu hizo.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Athumani Diwani, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kutokana na simu yake ya mkononi kupokewa na msaidizi wake mara tatu, ambaye alieleza kuwa kamanda alikuwa katika kikao.
  Hata hivyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwakamata viongozi na wafuasi hao wa CCM waliowashambulia wafuasi wao licha ya kujulikana waziwazi.
  Kwa mujibu wa barua yao ya Desemba, 20, 2011 yenye Kumb. Na. CH/WM/V.II/2011 kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Meatu na kunakilishwa kwa Kamanda wa Mkoa wa Shinyanga na mkuu wa jeshi hilo nchini, CHADEMA walilalamikia jeshi hilo kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa na wafuasi wa CCM.
  “Hii ni mara ya pili kufanyiwa fujo na wafuasi wa CCM. Tukio la kwanza ni la Desemba 4, mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi katika maeneo ya stendi ya Mwanhuzi, walikuja kuvuruga mkutano wetu huku wakitumia gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 426 ATZ mali ya kada wa CCM Juma Mwiburi na tulitoa taarifa katika kituo cha polisi wilayani lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
  Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Chama hicho wilayani humo, Godlisten Kihanda, ilieleza kuwa vitendo vilivyofanywa na wafuasi wa CCM mbele ya OCD inaonyesha wazi jeshi hilo linavyokipendelea chama hicho tawala.
  Akizungumzia barua hiyo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wilayani humo, SP Julius Mjengi, alisema kuwa hajaiona kwani kwa sasa yuko katika semina mjini Tabora, ila alikiri kupata taarifa ya kuwapo kwa barua hiyo ofisini kwake.
  "Mie niko Tabora katika semina ya makamanda ila sijaiona lakini nimepatiwa taarifa kuwa ipo ofisini kwangu… ngoja nikirudi nitaiona ina malalamiko gani kwani sasa hivi siwezi kusema lolote na ukizingatia kuwa mimi ndiye nalalamikiwa ni vizuri niione kwanza kabla sijajieleza chochote,’’ alisema.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,754
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Hao Polisi hawajasoma waraka wa Mwigamba!!
   
 3. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ndo wajibu mpya wa polisi huu.
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko ya kweli hayawezi kuzuiwa kwa nguvu ya dola hata siku moja. Mbaya zaidi hapo kuna uonevu wa dhahiri dhidi ya Chadema.
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  hii habari ilitakiwa iwe na kichwa cha habari kisemacho 'vijana wa ccm wawashambulia vijana wafanyabiashara, yasemekana vijana hao wafanya biashara ni wafuasi wa chadema, nao wajibu mapigo ili kujiokoa'
   
 6. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  polisi ccm,kimsingi hizo ni gharama za ukombozi
   
 7. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hivi hadi leo watu bado wanapigana juu ya vyama?????????hebu tuache kupoteza muda
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu serikali ya ccm wana machungu yaliyotokana na uchaguzi uliopita! na wao ndiyo wachokozi!
  Imagine ni wewe unachokozwa ungeweza kutulia bila kuitetea haki yako mpaka uipate?
  Issue siyo vyama, bali haki!
   
 9. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Tazama,naona mwisho wa poliCCM ukiwa karibu mno!!!
  Watanzania,popote mlipo,mtakaosoma post hii,mjiandae kwa mapambano matakatifu dhidi ya policcm na udhalimu wao!
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tatizo la polisi hasa kada ya ma ocd walio wengi hawajiamini ndo maana huwa wanafikia kuendeshwa hata na viongozi wa ccm ngazi ya wilaya,mkoa na hata kata. inauma sana!
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivi kumbe vijana wenye biashara zao ni CDM? Duh nilikuwa nafikiri labda watakuwa CCM ukizingatia wao ndio wenye nchi sasa naona wao CCM watakuwa wazururaji tu au ndio kusema wana maeneo yao ya biashara? Wapi FF atusaidie juu ya hili?
   
Loading...