CHADEMA,CCM na Benedict Mutungirehi katika mtihani wa kulipata jimbo la Kyerwa

Mkono

JF-Expert Member
May 7, 2010
568
89
Kuna fikra kwamba Kyerwa inahitaji mtu mbadala kuwawakilisha wanainchi wa jimbo hilo linaongozwa na Bw Justuce Katagira CCM,dhana inayotokana na udhaifu wake mwenyewe na chama chake ktk kushughulikia changamoto zinazolikabiri jimbo la Kyerwa.

Kuna watu wengi ambao wamejitokeza ili kuokoa jahazi na kurejesha hadhi ya jimbo wakati likishikiliwa na mh Mutungirehi na wengi wao wakiamini njia sahihi ni kupitia UKAWA jambo ambalo ukilichunguza kwa undani ni sahihi kabisa changamoto kubwa ni jinsi UKAWA itakavyo zichanga karata zake vema ili kufanikisha kiu ya watu wengi wa jimbo la KYERWA hasa kwa kuzingatia KUREJEA KWA MH BENEDICT MUTUNGIREHI katika siasa za jimbo la Kyerwa.

Mwanzoni habari za Bw Mutungirehi kurejea ktk siasa za Jimbo la Kyerwa kuwania ubunge zilianza kama uvumi ila sasa baada ya kuongea naye ni dhahiri kwamba yupo tayari kuingia ktk kinyang'anyiro habari ambazo tayari zimemfikia hasimu wake Bwana Katagira na huku yeye akiwa tayari ameisha anza kushiriki mikutano mbalimbali jimboni,wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa alikuwa mgeni rasimi ktk kufunga kampeni za UKAWA pale Nkwenda stand mkutano uliopata mahudhurion makubwa sana.

Je anafikiria kugombea kupitia chama gani? Hili swali limekuwa likiwasumbua wafuasi wake wengi hasa ukizingatia chama alichopo kwa sasa TLP hakina tena ushawishi na raia wengi hakitofautishi na CCM hasa kutokana na tabia za mkiti wake Bwana Mrema,nilipojaribu kutafuta jibu la swali hilo kutoka kwake haraka alijibu kuwa yeye hana shida na chama chochote cha siasa tofauti na CCM na akaenda mbali zaidi akidai KYERWA ndipo siasa za UKAWA zilipoanzia akimanisha kuwa kipindi kile akigombea jimbo hilo aliungwa mkono na vyama vyote vya upinzani.

Ukimsikiliza Mutungirehi utagundua bado anakabiliwa na tatizo lake la kutofanya maamuzi kwa wakati ,itakumbukwa wakati uongozi wa TLP wilaya ya Karagwe unahamia Chadema mwaka 2000 kama si 2005 ni Mutungirehi peke yake aliyebaki huku makubaliano ya awali ilikuwa ni kwamba naye angeungana na wenzake ghiliba za Mrema kumuachia uenyekiti zikamfanya awageuke wenzie na hiyo ndo sababu kubwa inayomfanya asiwe na uhakika na mstakabali wake iwapo ataamua kujiunga na Chadema maana viongozi wake wa zamani TLP leo wengi wao wakiwa ndo viongozi wa Chadema jimbo akiwemo rafiki yake wa zamani Bwana DEUS RUTAKYAMIRWA.

Kabla Bwana Mutungirehi hajafanya maamuzi ya kuhamia CDM nahitaji bila shaka kupata kauli ya viongozi wakuu wa chama hicho hasa uhakika wa yeye kugombea Ubunge kupitia chama hicho maamuzi ambayo yatategemea mtazamo wa mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho Bwana Wilfred Rwakatare kutokana na ushawishi alionao kwenye chama taifa na mkoa wa Kagera kwa ujumla .Taarifa kutoka kwa watu wa Karibu na Bwana Rwakatare ni kinyume kabisa na matamanio ya Mh Mutungirehi,Bwana Rwakatare anaamini kuna watu wanaostahili kupata nafasi ya ubunge kupitia chadema Kyerwa hasa kutokana na ujenzi mkubwa wa chama walioufanya wakati yeye Mutungirehi akiwa pembeni.

Ukifuatilia mnyukano huo unagundua bado kuna ugumu wa chadema kumhakikishia Mutungirehi kuwa mgombea pekee kupitia chama hicho na matokeo yake ni kuwa kila upande utaingia kivyake maamuzi yatakayokuwa yameunufaisha upande wa CCM maana ni vigumu kwa Benedict Mutungirehi kushinda kiti cha ubunge iwapo UKAWA wataweka mgombea wao lakini vilevile ni vigumu kwa UKAWA kushinda kiti cha ubunge Kyerwa kama Benedicto ataamua kugombea hata kama angepitia JAHAZI ASILIA.

Nyuma ya changamoto hizi changamoto nyingine ni iwapo makundi mengine yanaweza kuichukulia hali hiyo kama fursa mfano ni pale CUF wanapoweza kuchukua hatua za kumchumbia Mutungirehi ili baadae wamshindanishe ndani ya UKAWA na wagombea kutoka chadema na NCCR-Mageuzi jambo ambalo litakuwa pigo kubwa kwa chadema maana uhakika wa kuweka mgombea utakuwa shakani kutokana na ushawishi wa huyu jamaa.Nje ya hapO,mh MREMA anaonekana kama aliyekata tamaa ila ktk mazingira haya ambapo amepewa siku 80 za kufanya uchaguzi anaweza kujaribu kumhonga Mutungirehi moja ya nafasi ya juu ndani ya chama ili aendelee kuwa ndani ya chama na kukipa uhai walau hapo Kyerwa.Hatima ya Zitto na ACT nayo inaweza kubadili siasa hizi kutegemea na maamuzi yatakayofanyika.

BENEDICT MUTUNGIREHI-KULIA

JUSTICE KATAGIRA -KUSHOTO
 
Attachments

  • KATAGIRA.jpg
    KATAGIRA.jpg
    4 KB · Views: 844
  • Mutungirehi.jpg
    Mutungirehi.jpg
    10.4 KB · Views: 1,312
Mkono, naomba unitumie namba ya huyu dogo ben....namtafuta sana ni room mate wangu A-level pale shule ya wanaume Milambo...
 
Mutungirehi ni traitor. alitusaliti tukiwa Udsm hivyo hafai kuwa mbuge kupitia ukawa. hatufai kwa mapambano ya dhati, aende CCM.
 
Kuna fikra kwamba Kyerwa inahitahiji mtu mbadala kuwawakilisha wanainchi wa jimbo hilo linaongozwa na Bw Justuce Katagira CCM,dhana inayotokana na udhaifu wake mwenyewe na chama chake ktk kushughulikia changamoto zinazolikabiri jimbo la Kyerwa.

Kuna watu wengi ambao wamejitokeza ili kuokoa jahazi na kurejesha hadhi ya jimbo wakati likishikiliwa na mh Mutungirehi na wengi wao wakiamini njia sahihi ni kupitia UKAWA jambo ambalo ukilichunguza kwa undani ni sahihi kabisa changamoto kubwa ni jinsi UKAWA itakavyo zichanga karata zake vema ili kufanikisha kiu ya watu wengi wa jimbo la KYERWA hasa kwa kuzingatia KUREJEA KWA MH BENEDICT MUTUNGIREHI katika siasa za jimbo la Kyerwa.

Mwanzoni habari za Bw Mutungirehi kurejea ktk siasa za Jimbo la Kyerwa kuwania ubunge zilianza kama uvumi ila sasa baada ya kuongea naye ni dhahiri kwamba yupo tayari kuingia ktk kinyang'anyiro habari ambazo tayari zimemfikia hasimu wake Bwana Katagira na huku yeye akiwa tayari ameisha anza kushiriki mikutano mbalimbali jimboni,wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa alikuwa mgeni rasimi ktk kufunga kampeni za UKAWA pale Nkwenda stand mkutano uliopata mahudhurion makubwa sana.

Je anafikiria kugombea kupitia chama gani? Hili swali limekuwa likiwasumbua wafuasi wake wengi hasa ukizingatia chama alichopo kwa sasa TLP hakina tena ushawishi na raia wengi hakitofautishi na CCM hasa kutokana na tabia za mkiti wake Bwana Mrema,nilipojaribu kutafuta jibu la swali hilo kutoka kwake haraka alijibu kuwa yeye hana shida na chama chochote cha siasa tofauti na CCM na akaenda mbali zaidi akidai KYERWA ndipo siasa za UKAWA zilipoanzia akimanisha kuwa kipindi kile akigombea jimbo hilo aliungwa mkono na vyama vyote vya upinzani.

Ukimsikiliza Mutungirehi utagundua bado anakabiliwa na tatizo lake la kutofanya maamuzi kwa wakati ,itakumbukwa wakati uongozi wa TLP wilaya ya Karagwe unahamia Chadema mwaka 2000 kama si 2005 ni Mutungirehi peke yake aliyebaki huku makubaliano ya awali ilikuwa ni kwamba naye angeungana na wenzake ghiliba za Mrema kumuachia uenyekiti zikamfanya awageuke wenzie na hiyo ndo sababu kubwa inayomfanya asiwe na uhakika na mstakabali wake iwapo ataamua kujiunga na Chadema maana viongozi wake wa zamani TLP leo wengi wao wakiwa ndo viongozi wa Chadema jimbo akiwemo rafiki yake wa zamani Bwana DEUS RUTAKYAMIRWA.

Kabla Bwana Mutungirehi hajafanya maamuzi ya kuhamia CDM nahitaji bila shaka kupata kauli ya viongozi wakuu wa chama hicho hasa uhakika wa yeye kugombea Ubunge kupitia chama hicho maamuzi ambayo yatategemea mtazamo wa mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho Bwana Wilfred Rwakatare kutokana na ushawishi alionao kwenye chama taifa na mkoa wa Kagera kwa ujumla .Taarifa kutoka kwa watu wa Karibu na Bwana Rwakatare ni kinyume kabisa na matamanio ya Mh Mutungirehi,Bwana Rwakatare anaamini kuna watu wanaostahili kupata nafasi ya ubunge kupitia chadema Kyerwa hasa kutokana na ujenzi mkubwa wa chama walioufanya wakati yeye Mutungirehi akiwa pembeni.

Ukifuatilia mnyukano huo unagundua bado kuna ugumu wa chadema kumhakikishia Mutungirehi kuwa mgombea pekee kupitia chama hicho na matokeo yake ni kuwa kila upande utaingia kivyake maamuzi yatakayokuwa yameunufaisha upande wa CCM maana ni vigumu kwa Benedict Mutungirehi kushinda kiti cha ubunge iwapo UKAWA wataweka mgombea wao lakini vilevile ni vigumu kwa UKAWA kushinda kiti cha ubunge Kyerwa kama Benedicto ataamua kugombea hata kama angepitia JAHAZI ASILIA.

Nyuma ya changamoto hizi changamoto nyingine ni iwapo makundi mengine yanaweza ikuichukulia hali hiyo kama fursa mfano ni pale CUF wanapoweza kuchukua hatua za kumchumbia Mutungirehi ili baadae wamshindanishe ndani ya UKAWA na wagombea kutoka chadema na NCCR-Mageuzi jambo ambalo litakuwa pigo kubwa kwa chadema maana uhakika wa kuweka mgombea utakuwa shakani kutokana na ushawishi wa huyu jamaa.Nje ya hapO,mh MREMA anaonekana kama aliyekata tamaa ila ktk mazingira haya ambapo amepewa siku 80 za kufanya uchaguzi anaweza kujaribu kumhonga Mutungirehi moja ya nafasi ya juu ndani ya chama ili aendelee kuwa ndani ya chama na kukipa uhai walau hapo Kyerwa.Hatima ya Zitto na ACT nayo inaweza kubadili siasa hizi kutegemea na maamuzi yatakayofanyika.

BENEDICT MUTUNGIREHI-KULIA

JUSTICE KATAGIRA -KUSHOTO

tusubiri tutafakari hili ndio jamvi.
 
Huyo Mutungirehi sio mtanzania, ni mnyarwanda hata hilo jina lake ni la kitutsi
 
Mutungirehi ni traitor. alitusaliti tukiwa Udsm hivyo hafai kuwa mbuge kupitia ukawa. hatufai kwa mapambano ya dhati, aende CCM.
Mkuu huyu jamaa nilimdharau tangu atusaliti mle Nkrumah.

Vyama vinavyounda Ukawa vitafanya kosa ambalo hawatalisahau kama watamkaribisha huyu traitor, Mutungirehi hana tofauti na Zitto ni ma opportunists toka Daruso.
 
Wanyakanyonyo nadhani nyinyi ni ccm damu damu kama humwamini Mutungirehi, Mutungirehi ni jembe najua nyinyi mnao muona kuwa ni msalti mumeongwa na Katagira, Runyogote na Daniel maana Mutungirehi ni tishio kwao na Taifa ili linajua kumu lile jembe. akisimama ukawa jimbo anabeba kwa wepesi sana.
Mutungirehi Peoples Power anaaminika jimbo zima. ccm mnaweweseka kusikia jina lake.
 
UKAWA wakisimamisha huyu traitor hawapati kitu, itakuwa njia nyeupe kwa Ma CCM.
 
Vyovyote iwavyo, wana Kyerwa wanapaswa kumuondoa Katagira kama kweli wanataka maendeleo ya jimbo lao na hasa upande wa masoko ya mazao yao kama kahawa. HUwezi kuwachukua madalali wafanyabiashara kama Katagira wanaojipangia bei za kahawa na kudhibiti wanunuzi wengine kuwa viongozi wako. Wataendelea kuwatumia nyie kama ngazi akishirikiana na swahiba wake Daniel kuwanyonya. Ngoeni hayo magugu ili juwe salama. Ngoeni CCM maana hata diwani kama Runyogote amejigeuza mungu mtu kwa ulevi wa madaraka.
 
Naona unampigia kampeni Ben kwa mbali.

Kwamba kama UKAWA haitamsimisha Ben basi jimbo litaenda CCM.

Kwamba CUF wanaweza kumtongoza Ben halafu akasimama kwa bendera ya UKAWA.

Makubaliano ya UKAWA ni kwamba chama kilichoshika nafasi ya pili nyuma ya CCM ndiyo kitachopewa jukumu la kumsimamisha mgombea wa UKAWA.

Kama bado kumbukumbu zangu ni nzuri uchaguzi wa 2010 Chama kilichoongoza ni CCM, kikifuatiwa na TLP na halafu CDM.

Hivyo kulingana na huo ushindi chama ambacho kitamsimamisha mgombea wa UKAWA ni CDM kilichoshika nafasi ya 3, kwasababu TLP haiundi UKAWA.

Itakuwa ni kosa kubwa CDM kuwaacha makamanda walioshiriki kukijenga chama for the past five years, halafu wakampatia Ben ambaye alikataa kuwa join makamanda na kubaki na TLP.
 
ila kwa taarifa za chini chini nlizonazo ni kwamba kuna mwalimu wa karagwe secondary anajiandaa kuwania hili jimbo pia.
 
Tatizo la Mutungirehi ni kutojua anachotaka kufanya na kwa wakati gani period!! otherwise he has a sharp political mind kama alivyojibambanua wakati akiwa bungeni; lakini kama anataka kupendelewa katika uteuzi then huyo sio UKAWA material aende huko kwa Magamba; watu wamemenyeka na UKAWA yeye akiwa pembeni leo hii aje apewe upendeleo hiyo haifai!! Hatutaki political thuggery kwenye UKAWA
 
thread yako ni ya kumtetea mtu aaminike kwa viongozi wa cdm, unajaribu kumtongozea mtu, yani wakati wenzake wanatoka tlp yeye alibaki alafu leo anataka akachukue ubunge kupitia cdm, una mpambia sana eti ana kubalika basi kama ni popular apitie huko huko tlp
 
Nilichokifanya hapa ni uchambuzi kwa kuzingatia taaluma yangu ya uandishi wa habari hasa kubalance story! Hayo mengine nawaachie nyie maana siwezi kuzuia tafsiri zenu ktk thread hii.Nimejaribu kuonyesha upande mmoja wa udhaifu wa Mutungirehi,nikaonyesha udhaifu unavyoweza kuathiri upande wa pili.

Mimi sina interest yeyote kwenye hili zaidi ya matamanio yangu kuona jimbo vyovyote iwavyo linaangukia mikononi mwa Chadema mtu muungwana angeliona hilo na kulikiri .
 
Naona unampigia kampeni Ben kwa mbali.

Kwamba kama UKAWA haitamsimisha Ben basi jimbo litaenda CCM.

Kwamba CUF wanaweza kumtongoza Ben halafu akasimama kwa bendera ya UKAWA.

Makubaliano ya UKAWA ni kwamba chama kilichoshika nafasi ya pili nyuma ya CCM ndiyo kitachopewa jukumu la kumsimamisha mgombea wa UKAWA.

Kama bado kumbukumbu zangu ni nzuri uchaguzi wa 2010 Chama kilichoongoza ni CCM, kikifuatiwa na TLP na halafu CDM.

Hivyo kulingana na huo ushindi chama ambacho kitamsimamisha mgombea wa UKAWA ni CDM kilichoshika nafasi ya 3, kwasababu TLP haiundi UKAWA.

Itakuwa ni kosa kubwa CDM kuwaacha makamanda walioshiriki kukijenga chama for the past five years, halafu wakampatia Ben ambaye alikataa kuwa join makamanda na kubaki na TLP.

Binafsi namjua sana Mtungrehi na rafiki yangu, lakini ameshindwa kufanya maamzi mapema na kuna watu wamejenga chama. Kyerwa ni moja ya wilaya ambayo chama kiko imara sana, na kuna muda na raslimali za watu kukijenga chama namna hiyo. Leo huwezi kuwatupa na kumchukua mgombea ambaye hajatoka chama kingine. Binafsi najua kuna kikao atakaa na viongozi wa chama makao makuu na mi pia ntakuwa kwenye kikao hicho labda nisimwage mboga lakini huo ndo msimamo wangu.
 
Back
Top Bottom