Kuna fikra kwamba Kyerwa inahitaji mtu mbadala kuwawakilisha wanainchi wa jimbo hilo linaongozwa na Bw Justuce Katagira CCM,dhana inayotokana na udhaifu wake mwenyewe na chama chake ktk kushughulikia changamoto zinazolikabiri jimbo la Kyerwa.
Kuna watu wengi ambao wamejitokeza ili kuokoa jahazi na kurejesha hadhi ya jimbo wakati likishikiliwa na mh Mutungirehi na wengi wao wakiamini njia sahihi ni kupitia UKAWA jambo ambalo ukilichunguza kwa undani ni sahihi kabisa changamoto kubwa ni jinsi UKAWA itakavyo zichanga karata zake vema ili kufanikisha kiu ya watu wengi wa jimbo la KYERWA hasa kwa kuzingatia KUREJEA KWA MH BENEDICT MUTUNGIREHI katika siasa za jimbo la Kyerwa.
Mwanzoni habari za Bw Mutungirehi kurejea ktk siasa za Jimbo la Kyerwa kuwania ubunge zilianza kama uvumi ila sasa baada ya kuongea naye ni dhahiri kwamba yupo tayari kuingia ktk kinyang'anyiro habari ambazo tayari zimemfikia hasimu wake Bwana Katagira na huku yeye akiwa tayari ameisha anza kushiriki mikutano mbalimbali jimboni,wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa alikuwa mgeni rasimi ktk kufunga kampeni za UKAWA pale Nkwenda stand mkutano uliopata mahudhurion makubwa sana.
Je anafikiria kugombea kupitia chama gani? Hili swali limekuwa likiwasumbua wafuasi wake wengi hasa ukizingatia chama alichopo kwa sasa TLP hakina tena ushawishi na raia wengi hakitofautishi na CCM hasa kutokana na tabia za mkiti wake Bwana Mrema,nilipojaribu kutafuta jibu la swali hilo kutoka kwake haraka alijibu kuwa yeye hana shida na chama chochote cha siasa tofauti na CCM na akaenda mbali zaidi akidai KYERWA ndipo siasa za UKAWA zilipoanzia akimanisha kuwa kipindi kile akigombea jimbo hilo aliungwa mkono na vyama vyote vya upinzani.
Ukimsikiliza Mutungirehi utagundua bado anakabiliwa na tatizo lake la kutofanya maamuzi kwa wakati ,itakumbukwa wakati uongozi wa TLP wilaya ya Karagwe unahamia Chadema mwaka 2000 kama si 2005 ni Mutungirehi peke yake aliyebaki huku makubaliano ya awali ilikuwa ni kwamba naye angeungana na wenzake ghiliba za Mrema kumuachia uenyekiti zikamfanya awageuke wenzie na hiyo ndo sababu kubwa inayomfanya asiwe na uhakika na mstakabali wake iwapo ataamua kujiunga na Chadema maana viongozi wake wa zamani TLP leo wengi wao wakiwa ndo viongozi wa Chadema jimbo akiwemo rafiki yake wa zamani Bwana DEUS RUTAKYAMIRWA.
Kabla Bwana Mutungirehi hajafanya maamuzi ya kuhamia CDM nahitaji bila shaka kupata kauli ya viongozi wakuu wa chama hicho hasa uhakika wa yeye kugombea Ubunge kupitia chama hicho maamuzi ambayo yatategemea mtazamo wa mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho Bwana Wilfred Rwakatare kutokana na ushawishi alionao kwenye chama taifa na mkoa wa Kagera kwa ujumla .Taarifa kutoka kwa watu wa Karibu na Bwana Rwakatare ni kinyume kabisa na matamanio ya Mh Mutungirehi,Bwana Rwakatare anaamini kuna watu wanaostahili kupata nafasi ya ubunge kupitia chadema Kyerwa hasa kutokana na ujenzi mkubwa wa chama walioufanya wakati yeye Mutungirehi akiwa pembeni.
Ukifuatilia mnyukano huo unagundua bado kuna ugumu wa chadema kumhakikishia Mutungirehi kuwa mgombea pekee kupitia chama hicho na matokeo yake ni kuwa kila upande utaingia kivyake maamuzi yatakayokuwa yameunufaisha upande wa CCM maana ni vigumu kwa Benedict Mutungirehi kushinda kiti cha ubunge iwapo UKAWA wataweka mgombea wao lakini vilevile ni vigumu kwa UKAWA kushinda kiti cha ubunge Kyerwa kama Benedicto ataamua kugombea hata kama angepitia JAHAZI ASILIA.
Nyuma ya changamoto hizi changamoto nyingine ni iwapo makundi mengine yanaweza kuichukulia hali hiyo kama fursa mfano ni pale CUF wanapoweza kuchukua hatua za kumchumbia Mutungirehi ili baadae wamshindanishe ndani ya UKAWA na wagombea kutoka chadema na NCCR-Mageuzi jambo ambalo litakuwa pigo kubwa kwa chadema maana uhakika wa kuweka mgombea utakuwa shakani kutokana na ushawishi wa huyu jamaa.Nje ya hapO,mh MREMA anaonekana kama aliyekata tamaa ila ktk mazingira haya ambapo amepewa siku 80 za kufanya uchaguzi anaweza kujaribu kumhonga Mutungirehi moja ya nafasi ya juu ndani ya chama ili aendelee kuwa ndani ya chama na kukipa uhai walau hapo Kyerwa.Hatima ya Zitto na ACT nayo inaweza kubadili siasa hizi kutegemea na maamuzi yatakayofanyika.
BENEDICT MUTUNGIREHI-KULIA
JUSTICE KATAGIRA -KUSHOTO