Chadema, CCJ, NCCR, TLP, CUF...


D

Donrich

Senior Member
Joined
Aug 27, 2009
Messages
106
Likes
1
Points
33
D

Donrich

Senior Member
Joined Aug 27, 2009
106 1 33
Ni mtizamo wangu kwamba kutokana na viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani kuamua kugombea ubunge,ni wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka idadi ya wabunge wa upinzani bungeni kwenye uchaguzi ujao,ambapo kusema ukweli ni jambo la busara sana na wanastahili pongezi kwa hili.

Wakati huohuo lingekuwa jambo la busara sana kama vyama vya upinzani vikaamua sasa kusimamisha mgombea mmoja wa kiti cha Uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninajua kila chama kina sera na itikadi zake lakini ninachosema hapa ni kuona vyama hivi vikimsapoti mgombea mmoja kwa kumpigia kampeni,jaribu kufikiria kama CHADEMA,NCCR-MAGEUZI,TLP,UDP,CUF,CCJ(ikipata usajili),the list is going on...vikiamua kumsapoti mgombea mmoja kwa dhati kabisa,ninauhakika tutashuhudia ushindani wa kweli kwenye kumpata Raisi na kwa kiasi fulani Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kwenye demokrasia.

Hali hii itawafanya watu wengi wajitokeze kupiga kura either kutaka kufanya madiliko katika uongozi wa juu au kumfanya kiongozi mtetezi kumalizia kipindi kingine cha miaka mitano,Hili litawezekana tu kama viongozi wa vyama hivi wakiamua kwa dhati na kuacha ubinafsi..Sijui wewe unalionaje hili?
 
Y

Yetu Macho

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Messages
223
Likes
5
Points
35
Y

Yetu Macho

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2008
223 5 35
Yani hata TLP ya Mrema unataka ishirikiane na wapinzani wa kweli? Kama tunania njema na upinzania siafiki kuungana na hawa watu. Hatahivyo Mrema kashatangaza kumuunga mkono JK
 
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
6,446
Likes
393
Points
180
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
6,446 393 180
Haikuchukua muda mrefu kuwafahamu vyema viongozi wa kambi ya upinzani.

wapinzani wa kweli ni wachache mno hawazidi hata 20.
 
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2006
Messages
6,614
Likes
883
Points
280
G

Gagnija

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2006
6,614 883 280
Ok, wapinzani wanaweza kushirikiana kwa kuachiana majimbo na kuweka mgombea urais mmoja. Lakini TLP (Mrema) wameweka wazi kuwa watampigia kampeni Kikwete kwenye urais. Huyu Mrema hata akienda bungeni utajisifu kuwa umeongeza namba ya wapinzani?
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
101
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 101 145
Mimi naanza kuamini kwamba majority ya wapinzani ni watu wadhaifu kwenye siasa ambao wasingeweza kushindana ndani ya CCM na kuwa na vyeo vya kitaifa, hivyo dawa ilikuwa kutoka nje ya CCM.

Kwa wale wanaofuatilia vizuri naomba muangalie na kulinganisha profile ya wapinzani na wale wagombea wa viti 20 vya NEC ya CCM... ulinganishe uwezo achilia mbali mambo mengine.

I remain to be corrected.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
31
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 31 0
Ndugu yangu hilo halitawezekana,tyulishaindwa ushirikiano tutaweza kusimimisha mgobea mmoja?aftarol tusimamishe ili iweje?what if huyu mgombea akashinda manaundaje serikali?bythe way vingine ni vyama ndani ya vyama kwa mfano TLP,NCCR vinafadhaliwa na CCM,wewe huoni nyendo za Mrema?
 
Mgeninani

Mgeninani

Senior Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
190
Likes
0
Points
33
Mgeninani

Mgeninani

Senior Member
Joined Jan 3, 2010
190 0 33
Lazima wapinzani waje na manifesto inayouzika kwa wananchi,urais hawawezi kushinda, mkakati uwe kuing'oa CCM kuanzia bungeni, Japo tunambeza Nyerere alishawahi sema hili, kama ni kweli sheria ya pesa za uchaguzi utafatwa sioni ni kwanini wapinzani wasichukue japo 20% ya viti bungeni.
 
Kilasara

Kilasara

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2008
Messages
578
Likes
8
Points
0
Kilasara

Kilasara

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2008
578 8 0
Kama Augustine Lyatonga Mrema alivyokiri hadharani, yeye ni SHUSHUSHU na mamluki wa chama tawala, na amekwisha sema atampigia debe JK.

Inajulikana pia kwamba viongozi wengi wa NCCR Mageuzi ni waajiriwa wa Usalama wa Taifa, ambao, kama Mrema, wanatafsiri ajira yao kwamba ni lazima kumpigia debe Rais aliyeko madarakani hata kama mwenendo wake binafsi au wa chama chake, unakingana na maslahi ya taifa.

Kutokana na ukweli huo, ingawa ni vyema vyama vya siasa kushirikiana, ni lazima upinzani wa dhati ujihami na uachane na vyama mamluki.
 

Forum statistics

Threads 1,237,251
Members 475,501
Posts 29,282,699