CHADEMA Campaign Machinery | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Campaign Machinery

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Jul 22, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF wote, wanaChadema na wasio wanaChadema wapenda maendeleo na wapenda mabadiliko. Nimeanzisha thread hii makusudi kabisa kuweza kupata mawazo yenu juu ya uendeshaji wa kampeni za Chadema zinazotarajia kuanza muda mfupi ujao. Na ni matumaini yangu kuwa chochote tutakacho changia hapa kitawafikia walengwa.

  Kabla ya yote ningependa kutoa mfano mmoja: Kwanini Obama alifanikiwa katika kampeni zake hadi kupata ushindi wakati alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kushinda. Nafikiri kila mtu atajibu ni kwa sababu alikuwa na timu ya kampeni nzuri.

  Timu yake ilikuwa na vitengo vikuu vinane(8):
  1. Inner circle 2. Early advisors 3. Foreign policy 4. Energy policy 5. Economic policy 6. Domestic policy 7. New Media na 8. Former members.

  Ukiacha vitengo vingine kitengo cha Inner circle ambacho ndicho kilikuwa The leading Team(Engine) kilikuwa na members kama 12 na kila member alikuwa amepewa angalau kitengo kimoja kati ya vinane kukipa ushauri na wala si kukiongoza kwa sababu kila kitengo kilikuwa kinajitegemea na kiliwajibika kuripoti kwa Campaign manager David Plouffe.

  Kitengo cha Inner circle kilikuwa na sehemu kuu zifuatazo;
  1. Campaign Managing Office chini ya David Plouffe
  2. Communications chini ya Robert Gibbs
  3. Media strategy-David Exelrod
  4. Operating office
  5. Handled communications, research and policy
  6. Pollster
  7. Deputy Campaign Manager office
  8. National Finance etc.

  Nimejaribu kuonyesha jinsi Timu ya ushindi ya kampeni ya Obama ilivyokuwa. Si nia yangu kuongelea mambo ya Marekani na si lazima Chadema iige vitengo hivyo ambavyo vingine kwa Tanzania vinaweza visiwe vya lazima. Nia yangu hasa ni kuwa;

  Tutoe mawazo kuisaidia Chadema iweze kuwa na kampeni ya ushindi. Ni kitu gani unachoona kitiliwe maanani kwenye kampeni. Strategies/techniques gani unazodhani zinaweza kuisaidia Chadema kabla wakati na baada ya uchaguzi kufanyika.

  Mchango wangu:

  Chadema iigawe nchi katika makundi yafuatayo
  A. Kanda kuu 6 na kila kanda iwe na kampeni meneja wake aliye makini na asiingiliwe na mtu, awe huru kuamua kulingana na hali halisi ya sehemu yake. Kuwe na

  1. Kanda ya Pwani(Dar na Zanzibar) 2. Kanda ya Kaskazini 3. Kanda ya Kati 4. Kanda ya Nyanda za juu 5. Kanda ya Ziwa 6. kanda ya Magharibi(Tabora, Kigoma).

  B. Majimbo korofi/ Majimbo salama

  C. Sehemu za vijijini ambazo hazijawahi kutembelewa na kiongozi yeyote au zimetembelewa mara chache toka tupate uhuru(kuna kura huko).

  Naomba michango yenu, unaweza kukosoa kupinga lakini katika hali ya kujenga na si kubomoa. Tupingane ki mawazo na si kupigana, kwa sababu nyumba tunayojenga ni moja hakuna sababu ya kugombania fito. Tanzania ni yetu sote.

  Go Slaa Go.
   
 2. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza nakupongeza kwa ushauri mzuri ambao naamini unahitaji kufanyiwa kazi zaidi ili kurefine hii idea ya kanda. Lakini kwa ujumla wake ni jambo jema.

  Kitu kimoja ambacho mimi naona kina shida ni kanda kuwa na mamlaka ya makubwa kabisa ya kutokuingiliwa kwa meneja wake. Hapa nashauri kiongozi anayeongoza kanda awajibike kwa kamati kuu ya kampeni ambayo ndiyo itakuwa inaunganisha na kusimamia kampeni kwa nchi nzima.

  Najua kutakuwa na maswali magumu kama ya kugawanya resources zilizopatikana, hii kamati kuu ya kampeni, kutokana na taarifa zinazopatikana kutoka kwenye kanda ndiyo itakayoratibu maswala yote ya mahitaji muhimu kwa kanda. mfano, Wakati kanda inayohusisha Shinyanga na Mwanza inahitaji usafiri wa aina fulani kufika eneo fulani, kanda inayohusisha Arusha na Moshi usafiri wa aina hiyo hauhitajiki. Sasa hapo ndipo kamati kuu inapochambua na kuamua.

  Respect wakuu.
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwa kupendekezwa hapa jamvini hizi strategies si zitaigwa pia na vyama vingine?
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  naoma wajipange vizuri tu kuweza kufika hasa kule matawini/vijijini, ile style yetu ya HELIKOPTER iendelee kwani itakuwa rahisi kufikia maeneo mengi kwa muda mfupi........sisi wa mitandaoni tupo pamoja nao na sisi wengine tupo kuwasaidia kukampeni na kuhamasisha ikiwa wakiamua kutuita....
  Nchi inachukulika kirahisi tu kama uteuzi wenyewe ndio huu wa DR.SLAA...sioni kama kutakuwa na shida kiasi hicho nasisi wengine tumejipanga vilivyo kuhakikisha hakuina'' UCHAKACHUAJI WA KURA''
  PAMOJA DAIMA KAMA VODACOM VILE....
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mie napendekeza kitu kimoja kuwa:

  Hadi leo, CHADEMA na Dr. Slaa mwenyewe watakuwa wameshasoma au kufanya ka uchunguzi ka haraka haraka ka watu gani hapa JF wamekuwa wakimtaka Slaa kuwa mgomea kwa siku nyingi. Sidhani kama hawa watu walifanya kwa kutania.

  Itakuwa vema watengeneza Mtandao au Chumba maalumu cha kuwaunganisha Watanzania hao wote. Wakifika huko sasa ndiyo haya mawazo yaanze kutolewa. Au watengeneza EMAIL maalumu ambayo watu wataandika na hata namba ya simu ambayo itarekodi mazungumzo yote. Mawazo yao kwa kipindi kama wikimbili yakusanywe na timu iliyochaguliwa ikae na kuyajadili. Kwa CCM wanavyopenda kuiga, sintashangaa wakiiga. Hapa sasa itabidi kucheza chenga za mwili, kufeki na kuweka PLAN A, B, C na D ikibidi.

  Vinginenevyo, nakubaliana sana na wewe Luteni na pia member aliyeandika kuwa TUSIMWAGE MTAMA kwenye kuku wengi.
   
 6. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  TAHADHARI MUHIMU KWA CHADEMA NI KUPIMA RESOURCES ZAO NA KUANGALIA NAMNA WANAVYOWEZA KUZITUMIA RESOURCES ZAO EFFECTIVELY. ZAIDI YA KANDA, NASHAURI WATATHMINI MAENEO AMBAYO WANAWEZA KUWA NA INFLUENCE KUBWA NA KU-DIRECT HUKO LARGE PART YA RESOURCES ZAO ILI ZIWEZE KULETA MAFANIKIO MAZURI.

  VINGINEVYO, WAKITAKA KUSHINDANA NA CCM KWA KUWEKA WAGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YOTE, CAMPAIN ZA RAIS KWENDA KILA PEMBE YA TANZANIA BASI WATAISHIA KUFANYA SHALLOW CAMPAINING NA KUWAPA CCM NAFASI YA KUTAMBA.

  CHA MSINGI NI KUWA NA RESULTS NZURI AMBAZO HATA CCM WAKISHINDA LAKINI ISIWE KWA MARGIN KUBWA NA BILA SHAKA KITU HICHO KITAWAFANYA WANANCHI AMBAO HAWAJAAMUA VIZURI KUBADILISHA MUELEKEO WAO JUU YA VYAMA VINGINE VYA SIASA ZAIDI YA CCM. HATA CCM HAWATAKUWA NA MUDA WA KUJISIFU SANA BALI WATAUMIZA VICHWA VYAO KWANINI WAMESHINDA KWA MARGIN NDONGO NA KUELEWA KUWA KUMBE KUNA WATANZANIA WENGI WASIYORIDHIKA NA UONGOZI WAO NA HIYO INAWEZA KUWAFANYA WACHANGANYIKIWE KWA KUWA HAWAJAZOEA HALI HIYO.

  HAYA NI MAONI YANGU. KWA WENYE MTIZAMO TOFAUTI BASI NAWASIHI WATATHIMIN VYEMA MAONI HAYA KABLA YA KUPINGA.

  PLATO (MMOJAWAPO WA WANAFALSAFA BINGWA WA UGIRIKI) ALIPATA KUSEMA KUWA" Wale Ambao ni Weledi, Mahiri na Waadirifu lakini hawataki kuingia katika siasa, mwishowe hujikuta wakitawaliwa na watu hovyo na wajinga"

  Tunahitaji kushiriki siasa kwa hali na mali ili kuwezezea watu hovyo na wajinga kutotutawala. Wakipata nafasi ya kututawala, bala kuwe na effective check and balance ili wasije tutawala jinsi watakavyo bali wapiga kula wawe na say juu ya namna wanavyotaka watawaliwe.

  Ahsante,
   
 7. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Briliant Idea. YES WE CAN; nchi inachukulika wakuu kama ndio mawazo mazuri haya. Mie nashauri sana wanafunzi wa vyuo vikuu watumike sana hasa kipindi hiki wako likizo;
  Kwanza mipango ya kuanzia Mgombea mmwenza Lipumba aombwe kustep down, ampe Hamad kuwa mwenza wa Slaa; then mambo yapangwe hadi kuwepo na spinning za baraza la mawaziri likiwachukulia watu wasomi na makini; akina zito wafanye kazi kubwa kumuuza Slaa esp this time ambapo bado kampeni kwao hazijaanza; nitarudi tena ngoja nikapate kahawa hapa karibu na kwa bibi; watu safi ndani ya CCM waapewe kabisa assurance ya kupata vyeo ktk baraza la mheshimiwa ambalo litakuwa la kitaifa badala ya kutegemea baraza la chadema tu
   
 8. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu kimoja kimekuwa kinanistua sana nacho ni njisi gani watu tena wengi wao ni wale walioenda shule ambao bila kujua wanaumba kitu ambacho hakipo ila wanalazimisha. Nimeongea na serious kama 10 hivi ambao wote kwa ujumla line yao ya mawazo ni moja na inashangaza. wote wanamkubali Dr slaa lakini wanasema hawezi kushinda. Hawa mapanzi wanaitaji idara yao ambayo kazi yao itakuwa ni kuwaelimisha watu kuwa kama kila mtu akisema anampenda lakini hashindi ajue kuwa yuko kwenye kampeni ya kumwangusha bila kujua
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja...
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nimeupenda mchango wako mkubwa,PAMOJA DAIMA!
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Jamani me narudia tena, watz mlioko home msituangushe, saa ya ukombozi ndo hii manake sidhani kama kwa sasa tunakiongozi anayetufaa kama Slaa, achaneni na kabobo za yeboyebo na kijani kibichi wapeni chadema nafasi hawatafanya kosa!
   
 12. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2010
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwa Tanzania hakuna ambacho hakiwezekani. Nafikiri sasa hivi ni strategic planning, ongeza nguvu za kuelekea vijijini.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante sana Hekima Ufunuo nashukuru tena kwa kunielewa kuhusu Kanda za uchaguzi. Kuhusu madaraka ya Meneja wa kanda nilikuwa na maana ya yeye atakuwa amepewa limits na kitengo kikuu wewe umekiita Kamati kuu ya uchaguzi, limits ambazo ni za uwanja wake wa kijidai, akitaka kuvuka pale lazima apate ridhaa kutoka kwa kampeni meneja mkuu au kamati kuu ya uchaguzi. Kufanya hivi kutamfanya ajiamini na kuifurahia kazi yake ambayo mara nyingi huwa ni za kujitolea zaidi.

  Lengo la kumpa uhuru ni kumfanya aendeshe kampeni ya uhakika kwa vile atakuwa anayajua maeneo husika. Atakuwa anavitambua vijiji na vitongoji say vyenye matatizo ambavyo vinataka attention kubwa. Ataendesha kampeni kwa kufuata ratiba iliyoandaliwa na wanakijiji kuliko kupangiwa ratiba na makao makuu. Mfano mdogo kijiji X kesho kina gulio ambalo watu wengi wanapatikana siku hiyo makao makuu wanaweza wasiwe na habari ya tukio hilo na kumwambia aende kufanya kampeni kijiji Y.

  Lakini hili lengo la kukampeni kikanda ni wazo langu tu na si kuwa ndiyo utakuwa mpango wa Kamati kuu ya uchaguzi, hapa tunajaribu kama tunaweza kusaidia hata idea ndogo tulizonazo. Ninachoamini ni kuwa penye wengi hakiharibiki kitu.
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sikonge

  Nimekupata mkuu, Chadema wanaweza kabisa chini ya Communications Manager wakawa na kitengo cha kufatilia watu mbalimbali potential ikiwemo JF, wasomi, wazoefu, wastaafu, wanafunzi, vyama mbalimbali kikiwemo cha wafanyakazi TUCTA na kuwaomba wakiunge mkono, hii ni strategy nzuri. Chadema wasikae ofisini kusubiri eti makundi haya yatawa support automatically wanatakiwa wayafuate yaliko.

  Mzee nimeipenda campaign technigue yako
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna mwanaJF mmoja amependekeza kauli mbiu ya Chadema iwe; INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO.

  Mimi pia napendekeza kauli mbiu iwe LINDA KURA YAKO IKUPE NEEMA. Ni fupi na nyepesi kueleweka. Ni elimu tosha ya uraia, inatoa ujumbe ulio wazi kwa mpiga kura kuwa kura yake ni mali asipopiga kura na kuilinda hatapata mema aliyokusudia, ni sawa na kauli mbiu ya Jembe ni mali.

  Hata kwenye kampeni ni rahisi kutamkwa na kuitikiwa Linda Kura Yako----itikio----Ikupe Neema.
  Nitaendelea kuishauri Chadema kupitia njia hii.
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Kwa wale wanaodhani CCM haiwezi kushindwa, tuwaambie mbona KANU na UNIP ziliweza kushindwa? Watanzania sio mambumbumbu. Wanajua fika kwamba hali ngumu ya maisha waliyo nayo haitabadilika kama wataendelea kuwachagua watu wale wale. Kama alivyosema Baraka Obama: "You can't do the same thing over and over and expect a different result".

  Kwa sasa, nyongeza yangu kwenye mchakato ni hii:

  (1) Lazima kuwe na uwezo wa kuwafikia watu wengi kwa haraka. Chadema iwe na undugu na radio station kadhaa. Itabidi hotuba za Dr. Slaa zisikike redioni kila siku.

  (2) Simu za mikononi zitumike kwenye kampeni. Kuwe na uwezekano wa kutuma matangazo na ujumbe toka CHADEMA kwenye list kubwa kabisa ya simu za mkononi. Ushirikiano na kampuni za simu za mikononi ujengwe.

  (3) TV advertisements hazitawafikia wengi sana, lakini zina uzito mkubwa. Itabidi kutafuta wataalamu watengeneza commercials chache zitakazoonyesha uozo wa CCM, na kuzirusha wakati muafaka. This will cost money, but it will be money well spent.

  (4) Kuwe na umoja wa waliochoka na ukiritimba wa CCM. TANU na mwanaye CCM wamehodhi madaraka kwa miaka 50 bila kuweza kuleta ahueni kwa Watanzania, na bado wanang'ang'ania. CUF ialikwe kushirikiana na Chadema.
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kama unapinga ufisadi Chagua Chadema,
  kama unaunga mkono ufisadi Chama twawala
   
 18. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kuishinda CCM ni Maji kwa Bilauli...

  Chadema wanatakiwa kufanya yafuatayo...

  1. Waweke powerful powepoint presentation (fupi si chini ya dk 2) ya nini wanafikiri ni matatizo ya nchi yetu, na watoe katika presentation hiyo ni nini wanataka kukifanya ndani ya miaka mitano ambacho ccm wameshindwa kukifanya zaidi ya miaka 40, waache kuwa-criticise CCM na waseme tu ccm imejenga nyumba inayohitajika kuimarishwa na mafundi wengine kwani wao kila walipojenga , nyumba humomonyoka kila kukija masika na inafaa kubadili fundi ili nyumba itengemae wakati wote ije masika kije kiangazi...

  2. Chadema wajue Tanzania ina idadi ya vijiji vingapi, wagawe siku za kampeni na wavifikie robo tatu ya vijiji vyote vya tanzania na suluhisho la matatizo yetu bila kuwa-ctiticise ccm, wawape moyo matumaini watanzania wapiga kura na kusema kwamba tanzania ya neema inawezekana bila ya ccm.

  3. Waweke kitengo maalum ya utafiti na wanasheria ili kuwashitaki ccm haraka iwezekanavyo mara inapothibitika kwamba ccm either wametoa takwimu za uongo, au za kukipaka matope chadema... pia kitengo hiki kifanye utafiti na kuwawekea pingazi wana ccm wagombea ubunge wote wenye mushkeri kisheria au kimasomo.

  4. watafute lugha rahisi kabisa ya kuongea na mpiga kura , itayoeleweka bila utatanisho na cha msingi hapa ni kuhakikisha kwamba wapiga kura wanaelewa ni nini chadema inawaambia, na wanakielewa, wanakitafakari na kukiamini wanachoambiwa , na wanawashia moyo wa matumaini ya kwamba uchaguzi uje haraka ili chadema kichaguliwe...

  5. Waweke slogan fupi watakayo hakikisha kwamba kila mtu , hata mtoto anaijua kwa mfano... MAFISADI WANAPETA, WALALAHOI WANAPETESHWA MAGEREZANI... chagua chadema ikuondolee matatizo yako ya msingi... (Afya, miundombinu, elimi ya bure kwa kira mtu toka chekechea hadi chuo kikuu, umeme usiokatika siku 365 za mwaka na mengine mengi)

  Ni hayo kwa sasa.. nitaongeza mangine baadae
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  That is cool wakuu! Well mimi napendekeza slogan iwe something to do with " KURUDISHA NCHI KWA WANANCHI" ila maneno mafupi na matamu in that respect tusaidiane.

  The other strategy which is very powerful, ni CHADEMA kukampeni on their own words. JK, Makamba na CCM kwa ujumla ni mabingwa wa flip flops and gaffes. Sasa hizi zitengenezewe clips na at least kila wiki kuwe na mpya. Redioni na kwenye TV. I blv humu JF kuna wataalam wa kutengeneza clips.........
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kama wengi mnavyosema Advertisements ni muhimu kuliko kawaida TV radio Magazeti wasanii mbalimbali watumike ni gharama lakini bajeti yao kubwa ijikite huko, kuwe na Live coverage ikiwezekana ianze kwenye mkutano mkuu.

  Kama alivyosema Augustine Moshi wazee wastaafu wasiachwe nyuma ikiwezekana wawe wanatafutiwa vipindi vyao kutoa ushauri wasikike. Pia watu maarufu waalikwe.

  Chadema isiache kutumia helikopta lakini ukubwa wa presidential campaign team upunguzwe ili kupunguza gharama nguvu zielekezwe kwenye kanda za uchaguzi kama nilivyoshauri awali na majimboni. Kwa hiyo presidential team itakuwa inakuta timu ya kanda imewaandalia na kujumuika nayo.

  Nimeipenda slogan ya Nyambala 'Kurudisha nchi kwa wananchi'
   
Loading...