CHADEMA BILA DR SLAA IMEPWAYA SANA!

CHADEMA BILA DR SLAA IMEPWAYA SANA!

Aloyce mk

Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
76
Reaction score
33
HBR WANAJAMVI!

NAJARIBU KUANGALIA HALI YA KISIASA NCHINI KWA SASA NA NIMEGUNDUA KUWA KUNA TOFAUTI KUBWA WAKATI CHADEMA IKIWA NA DR. SLAA NA YA SASA BILA DR. SLAA. SIJAONA KUIBULIWA KWA HOJA NZITO ZENYE MASHIKO, SIJAONA MIKAKATI ENDELEVU SIJAONA LOLOTE NAONA TU CHAMA KIKIRUDI CHINI CHINI ZAIDI NAWASHAURI CHADEMA KAMPIGIENI MAGOTI DR. SLAA ARUDI AWAPIGE KIKI!
 
Akili za UKAWA wote zinazidiwa na uwezo wa Zitto Kabwe
 
Lile ombi la kukumbukwa wale vijana 46 litawafanya mlale mkiwaza chadema, uchaguzi umeisha impact ya slaa ilitakiwa ionekane wakati wa kampeni lakini alifunikwa vibaya sana Lowasa, na hata ccm lowasa aliwatoa jasho sana ulimwengu maimzima unajua, slaa yeye sasa msaidieni kuirudisha nyumba yake tu kuhusu chadema alisha sahauliwa.
 
Mpaka siku Watanzania wakija kujanjaruka na kumjua msaliti halisi wa harakati za kuiondoa CCM madarakani sijui kama itakuwa leo.Msaliti hasa ni huyu hapa,aliwamaliza kisiasa wale wapinzani wote walioonekana kuwa tishio kwa watawala,akawapachika majina ya usaliti na kisha akawatupia virago. Msaliti huu anasemekana alikuwa ni swahiba mkubwa wa mkulu aliyemaliza muda wake,hawakukutana barabarani.Usitarajie marafiki hawa kusalitiana ktk jambo lolote lile.Wafuatao ndio wanasiasa wapinzani wa kweli ambao harakati zao zilionekana kumtisha huyu msaliti halisi pamoja na jamaa zake wa CCM.Chacha Wangwe,huyu atakumbukwa kwa harakati zake na nia yake thabiti ya kupunguza nguvu za kisiasa za CCM ktk grassroot levels kwa kuiimarisha CHADEMA ktk levels hizo,alipotaka kuigombea uenyekiti wa CHADEMA taifa ili apate jukwaa sahihi la kutekeleza mawazo yake ya kuiimarisha CHADEMA ktk levels zote za uongozi aliitwa majina yote mabaya na mwishowe kumkuta yaliyomkuta.Zitto Kabwe,huyu ni mwanasiasa kijana aliyekuwa na mvuto wa hali ya juu kisiasa na ambaye alionekana mwiba mkali kwa uwepo wa CCM madarakani lkn naye kama ilivyokuwa kwa Wangwe,akajichanganya ktk anga za msaliti kwa kuutaka uenyekiti na msaliti halisi hakupoteza muda,akammalizia hapo hapo kisiasa na the rest is history. Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa upinzani kutwaa viti vingi vya ubunge ili kuwadhibiti CCM na mipango yao ya hovyo huko lkn msaliti halisi akaharibu mipango hiyo ya kutwaa viti vingi vya ubunge akiwadanganya wapinzani kwa watashinda urais chini ya Lowassa hivyo wasiwe na hofu.Sote ni mashahidi namna wagombea ubunge walivyoachwa wahangaike wenyewe bila sapoti kubwa ya viongozi wa Kitaifa wa chama,mbaya zaidi wakasababisha Dr Slaa mtu ambaye alikuwa muhimu sana ktk kuwasaidia wagombea hawa kuuzika kwa wapiga kura wakati wa kampeni kuondoka.Akili,nguvu na rasilimali zote akahamishia kwa mgombea urais,yaliyotupata kila mtu ni shuhuda hapa.Tumerudi pale pale kwenye stori za malalamiko kwamba CCM wanautumia wingi wao vibaya kugandamiza hoja za wapinzani.The guy is genius.
HBR WANAJAMVI!

NAJARIBU KUANGALIA HALI YA KISIASA NCHINI KWA SASA NA NIMEGUNDUA KUWA KUNA TOFAUTI KUBWA WAKATI CHADEMA IKIWA NA DR. SLAA NA YA SASA BILA DR. SLAA. SIJAONA KUIBULIWA KWA HOJA NZITO ZENYE MASHIKO, SIJAONA MIKAKATI ENDELEVU SIJAONA LOLOTE NAONA TU CHAMA KIKIRUDI CHINI CHINI ZAIDI NAWASHAURI CHADEMA KAMPIGIENI MAGOTI DR. SLAA ARUDI AWAPIGE KIKI!
 
Kwa africa sioni faida ya upinzani sababu hata wapinzani wakishinda hawatangazwi
 
chadema wameharibu upinzani toka walipokubali kulamba matapishi ya kusimamisha mgombea ambaye walikuwa wanamtangaza ni fisadi mpaka sasa chama kikubwa kama kile kinashindwa kuteua katibu mkuu
 
HBR WANAJAMVI!

NAJARIBU KUANGALIA HALI YA KISIASA NCHINI KWA SASA NA NIMEGUNDUA KUWA KUNA TOFAUTI KUBWA WAKATI CHADEMA IKIWA NA DR. SLAA NA YA SASA BILA DR. SLAA. SIJAONA KUIBULIWA KWA HOJA NZITO ZENYE MASHIKO, SIJAONA MIKAKATI ENDELEVU SIJAONA LOLOTE NAONA TU CHAMA KIKIRUDI CHINI CHINI ZAIDI NAWASHAURI CHADEMA KAMPIGIENI MAGOTI DR. SLAA ARUDI AWAPIGE KIKI!
Chadema imebaki kuwa ni kitchen party
 
Chadema imebaki kuwa ni kitchen party
Wewe ndiye Dr Mihogo mwenyewe unajipigia upatu nini! Bunge mbona bado hata halijachanganya hoja nzito nzito gani? Hata kamati za bunge haxijakamilika unaongekea hoja nzitonzito? Si ndio kwanza bunge linajipanga kwa kuunda kamati zake na kambi nayo kujipanga kws kuunda baraza lake?
Nyie nyumbu wa ccm kweli hamna akili! Mnajiandikia chochote tu ilimradi uonekane umeandika?
 
HBR WANAJAMVI!

NAJARIBU KUANGALIA HALI YA KISIASA NCHINI KWA SASA NA NIMEGUNDUA KUWA KUNA TOFAUTI KUBWA WAKATI CHADEMA IKIWA NA DR. SLAA NA YA SASA BILA DR. SLAA. SIJAONA KUIBULIWA KWA HOJA NZITO ZENYE MASHIKO, SIJAONA MIKAKATI ENDELEVU SIJAONA LOLOTE NAONA TU CHAMA KIKIRUDI CHINI CHINI ZAIDI NAWASHAURI CHADEMA KAMPIGIENI MAGOTI DR. SLAA ARUDI AWAPIGE KIKI!
Mruhusu mikutano yetu muone kama tumepwaya.
 
Cha kushangaza wana CCM ndio wanamhitaji Mzee Slaa, wakati kipindi kile kabla hajarubuniwa ndio hawa hawa waliokuwa wanasema hafai.
 
Uadilifu wa CHADEMA uliondoka na Dr Slaa, alifanana na matazamio ya masikini wengi. Lakini CHADEMA wapo kwenye nafasi ya kutafuta mgombea urais kijana ambaye ndani ya miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu ujao, anaweza kutembea nchi nzima na kurudishia imani iliyopotea kuhusiana na uadilifu wa upinzani.
 
Hoja yako inapingana na kauli ya mmiliki mpya wa chadema, kubwa 2020 atagombea yeye!
 
Back
Top Bottom