Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Kitu ambacho kiko wazi ni kuwa CHADEMA ya sasa imekosa dira na hamana kabisa. Wengi tuliionya CHADEMA isithubutu kumchukua Lowassa kwa sababu kwa kufanya hivyo kilikuwa kinapingana na sera yake ya kupinga ufisadi.
Hatukuishia hapo, tukasema kuwa kumleta Lowassa kipindi cha uchaguzi ni kupuuza hazina ya viongozi wa CHADEMA wakiwemo wabunge machachali wa CHADEMA ambao kwa uongozi wa Dr. Slaa walipigana vema vita ya kupinga ufisadi. Walipendwa kiukweli na wananchi, na hata wana CCM waliwapenda sana wapiganaji wa CHADEMA.
Kwa kuwataja wachache ni Mnyika, Mdee, Vincent Nyerere, Mbowe, Tundu Lissu, Msingwa na Wenje. Kipindi hicho wakionekana hao bungeni au majukwaani unahamasika kunatega sikio vizuri.
Dr. Slaa kaondoka na dira ya chama imepotea. Sera endelevu iliyokuwepo ya kurudisha chama kwa wananchi kupitia sera ya ugatuzi imepotea. Mifano michache ni maamuzi ya ngazi ya chini kuamuliwa na viongozi wa juu moja kwa moja, hasa katika uchaguzi wa wagombea ubunge na viti maalum badala ya kuzingatia mchakato wa uchaguzi katika ngazi za chini. Kupotea kwa dira ya CHADEMA kumeenda sambamba na kupotea hamasa kwa wanachama na wananchi mashabiki walio wengi.
Watake wasitake lakini huu ndiyo ukweli wenyewe, CHADEMA imemtupa kiongozi aliyekuwa anaonyesha dira ya chama na kuhakikisha kuwa hamasa ya wananchi na wanachama inabaki juu na kuendelezwa.
Kwa kuonyesha kuwa CHADEMA wamepoteza mwelekeo, wanatengeneza chama ambacho kinazua maswali mengi kuliko majibu. Wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere aliwahi kuulizwa nadhani na mwandishi wa habari kutoka nchi za magharibi kuwa baraza lake la mawaziri limejaa wakatoliki. Kwa kuwa uteuzi wake haukuwa wa upendeleo akashangaa hilo limetoka wapi.
Akaagiza uchunguzi ufanyike kujua ukweli wa jambo hili. Akafikiri kuwa ili kujua ukweli waanze kwa kuwafahamu walioapa kwa biblia na wasioapa kwa biblia. Lakini njia hii isingewatofautisha wakristo wa madhehebu mbalimbali. Hivyo uchunguzi wa kina zaidi ukafanyika. Na akakuta kuwa wakatoliki alikuwa yeye na George Kahama ambaye yeye alikuwa amekwisha endelea zaidi kwa vile alikuwa na mke wa pili isivyotakiwa na imani ya kikristo.
Kioja sasa ni CHADEMA, pamoja na kutuhumiwa kuwa wanatakiwa wa-address taswira ya kusema kwamba chama kile kimejikita zaidi kaskazini, lakini wameleta maswali zaidi. Ukaribu wa Mboe, Lowassa, Sumaye na pia Mbatia ingawa hayupo CHADEMA lakini alikuwa katikati la vuguvugu la kumleta Lowassa kugombea urais, unaleta maswali ya jee hivi Mbowe, Sumaye, Lowassa na Mbatia ni madhehebu gani? Kwa kukosa dira na mwelekeo, CHADEMA hii ya bila Slaa haioni kwamba ni kitu muhimu kujiangalia kama hawakiletei chama taswira na mwelekeo wa dhehebu fulani.
Kwa kawaida mimi si kati ya mashabiki wa siasa za kibaguzi. Lakini kwa kuwa CHADEMA imekosa dira kwa sababu aliyekuwa anaonyesha njia (Dr Slaa) alitupiwa virago na kudhalilishwa, hawa CHADEMA wanaweza kufanya chochote. Wamekosa hisia, dira na wanachama na mashabiki wao nao wamekosa hamasa.