CHADEMA at war

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,235
2,000
Nakikumbuka Kitabu cha" Bush at war" kilichoandikwa na mwandishi wa Marekani, Bob Woodward.
Mara baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Sept 11, Mwandishi Woodward anasimulia jinsi Bush alivyokuwa Kachanganyikiwa mara baada ya mashambulizi yale .
Hasa baada ya hatua za kiusalama zilizolenga kunusuru maisha yake, Bush alikimbizwa haraka kutoka Florida alikokuwa kaenda kwa ziara hadi kwenye kambi kubwa ya kijeshi iliyopo ktk jimbo la Louisiana nchini humo, akiwa kwenye kambi hiyo ya kijeshi, Rais Bush alifichwa kwenye handaki.
"Mr President, America is under attack,you'll have to stay here until the situation calms down "
Kiongozi wa walinzi wa Rais Bush, alimweleza Rais.
Kwa tafsiri isiyo rasmi, Rais Bush alielezwa kuwa, "Bwana Rais, Marekani imevamiwa, itakulazimu ukae hapa hadi hapo hali itakavyotulia ".
Rais Bush alikaa hapo kwa masaa kadhaa, kisha akaondolewa na kurudishwa Washington, kisha baada ya muda mfupi alitoa hotuba fupi kwa taifa akiwa na hasira ,namnukuu kwa ufupi.
"The great nation is attacked,now we want to show the world that we pass this test".
Kwa tafsiri isiyo rasmi Rais Bush alisema.
"Taifa kubwa limepigwa, sasa tunataka kuionyesha Dunia kwamba tunafaulu huu mtihani ".
Mwisho wa kunukuu.
Chadema imepigwa na imepigika hasa, chadema iko vitani, adui kalenga kusambaratisha chama hiki chenye nguvu kubwa kuliko vyote Tanzania kwa sasa.
Adui huwa hachagui staili ya kukupiga, anakupiga kwa staili zote anazojua yeye, lengo lake ni kupata ushindi.
Mapandikizi ya wanausalama ndani ya Chadema ni jambo la kawaida kabisa hasa kwa chama ambacho hakina ndoto ya kuachia madaraka hata Kama kitaangushwa kwenye sanduku la kura.
Vitani hata majenerali wanaoongoza vikosi huwa inatokea wakatekwa au kujisalimisha kwa adui, lakini hiyo huwa haitoi marks za ushindi kwa adui.
ANC ilikuwa na vita kubwa mara 100 ya Chadema, lakini ilishinda hii vita.
Chadema is attaked, now we want show the world that we pass this test.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,458
2,000
Sasa Nani Wa Kuongoza Mapambano Hapo Chadema Mbowe Yuko Jela , Lisu Yuko Mgonjwa Hospitali. Mashinji Amejifungia Chumbani Na Laptop Anabeti Anaogopa Hata Kutoka Nje Asije Kukamatwa Na Polisi. Lowasa Ndio Huyo Kashajiondokea
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,592
2,000
Sasa Nani Wa Kuongoza Mapambano Hapo Chadema Mbowe Yuko Jela , Lisu Yuko Mgonjwa Hospitali. Mashinji Amejifungia Chumbani Na Laptop Anabeti Anaogopa Hata Kutoka Nje Asije Kukamatwa Na Polisi. Lowasa Ndio Huyo Kashajiondokea
ni lini Lowasa aliongoza mapambano chadema? alikuja kwa amani ameondoka kwa amani, CDM wasimkejeli wala kumtukana, wasimame imara na kusonga mbele.
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,399
2,000
Chadema haitakufa sema imekuwa sugu kwa sababu zilizo wazi.
Lakini ili Chadema irudi pale pa Oct 2015 inatakiwa izaliwe upya kabla ya kuungana na vyama kama ACT Wazalendo.
Yapo mambo Chadema ana uwezo na mengine yapo nje ya uwezo wa chama.
Lakini kuna dalili kuwa serikali CCM nayo labda kutokana na shindikizo za ndani ya chama na nje ya chama inatakiwa kufanya siasa za kistaarabu.
Kama siasa za kistaarabu zitaheshimika tena ni wazi Chadema atarudi ulingoni bila woga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom