CHADEMA Arusha yatoa mkono wa pole kwa jeshi la polisi Arusha

Misri, Tunisia, Libya na Syria mpaka leo wanauwana, so jifunze wewe usipeleke masaburi yako barabarani bila kibali hakika Polisi watayatumbua. Maanadamano sio solution ya kila kitu utaandamana mpaka kiama kikukute huko.
Meza ya majadiliano, OK?
 
Viva CDM chama cha watu makini!!!
Adengenye afanye awezavyo amwamishe kikazi yule mjinga wake OCD zuberi.

Mkuu nadhani hiyo 200,000.00 itakuwa kama damu ya Yesu iliyomwagika msalabani ili kusuluhisha kati ya wanadamu na Mungu wetu, hivyo
nao CDM nadani wanahaja ya kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.
 
Nimeipenda hiyo, Itasaidia kupunguza tofauti zilizojitokeza siku za nyuma hapo ARUSHA. Nawakumbuka hao polisi wetu waliwahi kumwaga damu ya mke wa Dr. Slaa (jembe). Pamaja na kupoteza maisha ya wanachama watatu wa CDM. Welldone CDM lipeni ubaya kwa wema.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilaya ya Arusha kimetoa ubani wa shilingi 200,000 kwa jeshi la polisi mkoani Arusha kwa ajili ya rambirambi ya kifo cha Askari polisi wa kitengo cha upelelezi, Kijanda Mwadu aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayetuhumiwa kuwa jambazi sugu wakati polisi walioongozwa na Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha, Fautine Mafwele walipokuwa katika harakati za kumtia mbaroni eneo la kijiji cha Shangarai wilayani Arumeru.

KKatika tukio hilo, OC-CID pia alijeruhiwa kwa kupigwa risasi begani na kulazwa katika hospitali ya Seliani kwa matibabu.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro aliyeongoza viongozi wa Chadema katika hafla fupi ya kukabidhi ubani huo kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye alisema chama chake kimetoa kiasi hicho kutokana na kuthamini mchango wa askari polisi katika harakati za ulinzi na usalama wa raia na mali zao kama alivyofanya marehemu Kijanda aliyekuwa tayari kukabiliana na wahalifu hadi kwa gharama ya maisha yake.

Kwa upande wake, RPC Andengenye alikishukuru chama hicho kikuu cha upinzani nchini na kuelezea kitendo hicho kama kufungua njia mpya ya ushirikiano kati ya jeshi lake na Chadema na kuonyesha jamii kuwa pande hizo mbili hazina uhasama kama baadhi ya watu wanavyofiri.

Picha ya tukio hilo hapa chini

wU7r6qa08qwgwAAAABJRU5ErkJggg==
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye (katikati) akiwa katika picha ya pomoja na viongozi wa Chadema wilaya ya Arusha mara baada ya kupokea ubani wa shilingi 200,000 zilizochangwa na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Januari 5, mwaka huu katika viwanja vya NMC, Unga Ltd Manispaa ya Arusha kuadhimisha mwaka mmoja wa mauaji yalitokea baada ya jeshi la polisi kuwafuatulia risasi wananchi katika harakati za kuzuia amaandamano hayo ambayo awali yaliruhusiwa kabla ya kupigwa marufuku Saa chache kabla ya kufanyika. Wemgine pichani kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Nagarenaro, Isaya Doita, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, mjumbe wa kamati tendaji wilaya, Sarah Fundikira na mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Arusha, Gloria hio.

e2NjF03Yue57HQdUq3GSYYzEsbOYPm+vleZuGRHBOCWbIhF408Pru0QYeWU0Gnx6sf7e9GpmFi4uuqWujotHrWhY7qNMtqhQxsz5qMxtlcjyRsbr9i6kC1l4prm61B5sm7ayMSnFJeDbmdSdnbIE75hMQggKqgz7iBQhe3jgiICF8coBPWZhizQqZUb87EoktBGNhrBhKVtyh7P8DMYsJmayfYVgAAAAASUVORK5CYII=
RPC Andengenye akipokea kitita cha shilingi 200,000 kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema (Bawacha), wilaya ya Arusha, Gloria Shio ikiwa ni ubani kutoka Chadema kufuatia kifo cha askari polisi, Kijanda Mwadu aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa jambazi sugu katika tukio lililotokea kijiji cha Shangarai wilayani Arumeru. Anayeshuhudia kushoto ni mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro ambaye pia ni diwani wa kata ya Levolosi
 
asante kamanda sasa hicho kichina hapo juu nimeshindwa kusoma nisaidie ulikuwa unaongelea nn:crazy:
 
Rpc Arusha na Chadema.JPG Rpc akipokea kitita.JPG RPC akiagana na chadema.JPG Picha za viongozi wa Chadema wilaya ya Arusha wakiwa pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye walipokwenda ofisini kwa kamanda huyo kutoa mkono wa pole wa Shilingi 200,000 kwa jeshi la polisi kutokana na tukio la mtu anayedaiwa kuwa jambazi sugu kumuuawa kwa kumpiga risasi askari wa kitengo cha upelelezi, Kijanda Mwadu na kujeruhi mkuu wa upelelezi wilaya (OC-CID), Faustine Mafwele wakati walipojaribu kumtia mbaroni katika kijiji cha Shangarai wilayani Arumeru hivi karibuni.

1. RPC Andengenye (mwenye T-shirt nyeupe katikati) akipozi kwenye picha na viongozi wa Chadema kuanzia kushoto ni diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, Mjumbe wa kamati tendaji wilaya, Sarah Fundikira na Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Arusha, Gloria Shio.

2. RPC kulia, akipokea kitita cha 200,000 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bawacha, Gloria Shio. Kulia anayeshuhudia ni Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa Chadema wilaya na diwani wa kata ya Levolosi

3. Kamanda Andengenye akiagana na ujumbe wa Chadema mara baada ya kupokea ubani waliopeleka. Hapa akipeana mkono na mjumbe wa kamati tendaji wilaya ya Arusha, Sarah Fundikira.
 
Ni kweli ubani au ndio njia ya kutaka kupata mteremko?.

Haya mngempa ubani huo Kamanda Zubeir Mombeki wa Arusha town.
 
huyu ant ndo Gloria au Sarah ?weka tujuwe huyu ni nani na yule ni nani?Hawa ndo viongozi wetu wa baadaye bwana ,unajua ni picha za watu wakubwa sana kwetu sisi.
 
Akipokea msaada huo, Andengenye alisema jeshi la Polisi halina uhasama na CDM, which is true. Andengenye hata hivyo asisahau kuwa bado tuna uchungu kwa mauaji ya ndugu zetu aliyoyasimamia. Lazima siku moja, lil haki itendeke, apande kizimbani.
 
They call it social responsbilities....hata kama polisi waliwapiga chadema. Hawana kinyongo..ni wajibu wao
 
Back
Top Bottom