Chadema Arusha wasusia kikao cha Madiwani

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,959
32,344
Wanabodi JF..

Madiwani saba wa Chadema katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha..

Wamesusia kikao cha baraza hilo baada ya kukataliwa kwa hoja ya mmoja wao kuhusu mgogoro wa umeya katika halmashauri hiyo.

Kususa kwa madiwani hao kulitokea baada ya Diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita, kusimama na kuibua hoja kuhusu ufumbuzi wa mgogoro wa umeya.

Wakati diwani huyo akiendelea na hoja yake, Diwani wa Terati kupitia CCM, Julius Sekeyani, alisimama na kupinga hoja hiyo..

Huku akisisitiza kuwa watu wa Jiji la Arusha wamechoshwa na mgogoro huo.

Sekeyani alisema kwa sasa wananchi wa Arusha wanataka maendeleo na si malumbano..

Kauli hiyo iliwafanya madiwani wa Chadema kutokuwa na imani na mwenendo wa baraza kwa kuhisi kuwa wamebaguliwa na kuamua kususa..

SOURCE: MWANANCHI DESEMBA 17. 2011
 
Malipo yao ni 2015.

HATUDANGANYIKI TENA KUWAPA KURA WASANII, WAPENDA MIGOGORO.
 
Wananchi wa Arusha wanaishi kama watoto yatima!
 
mbona mimi nimesikia kwamba kwenye kikao hicho diwani mmoja wa ccm alitoa hoja na kusema wanapinga uteuzi wa rais uliomfanya mbunge aliyepigwa chini(dr wa kike) kupewa ubalozi nchini kenya.
 
vipi wale wa dodoma mahali ambapo maisha yamepanda hadi kusababisha ongezeko la posho.

Mkuu, kule si wapo mchanganyiko wapo CCM, NCCR Mageuzi, Chadema, CUF, TLP, UDP, unaongelea nani kwenye awa niliowataja?
 
Kwa hyo tuache kuona msingi wa tatzo eti kisa maendeleo...ccm mnaongelea maendeleo gani miaka50 ya uhuru ama kuzalisha wana appolo?ama maendeleo ni kupora uongozi kwa nguvu,hayo ndo maendeleo mwataka kusema?ama kisa mnatoneshwa kidonda,fukia kombe mwanaharamu apite?
 
Baada ya kukosa cha kubishana juu ya CDM mmeona muanzishe thread na kuanza kujibizana wenyewe kwa wenyewe, dah creativity ya hali ya juu.
 
Baada ya kukosa cha kubishana juu ya CDM mmeona muanzishe thread na kuanza kujibizana wenyewe kwa wenyewe, dah creativity ya hali ya juu.

Mkuu, hii habari ipo kwenye gazeti la leo Mwananchi 17/12/2011..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom