CHADEMA: Akaunti zetu za chama za YouTube na X (Twitter) zimedukuliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

WITO WA KUSHIRIKI KESI YA MH. TUNDU LISSU, JAMII KUFUATILIA MJADALA WA BUNGE LA ULAYA, NA TAARIFA YA UDUKUZI WA AKAUNTI ZA CHAMA.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuwataarifu Watanzania na jamii ya kimataifa juu ya matukio matatu makubwa yenye athari kwa demokrasia na haki za binadamu nchini Tanzania:

1. Wito Kuhudhuria Kesi ya Mh. Tundu Lissu Kesho, Jumanne 06 Mei 2025 saa 2:00 asubuhi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itasikilizwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Tundu Antiphas Lissu. Kesi hii si ya kawaida. Ni sehemu ya mkakati mpana wa kutumia sheria kwa njia ya kisiasa kukandamiza sauti huru na kuwatisha wapinzani wa kweli.

*Tunatoa wito kwa wanachama, wafuasi, wapenda haki na Watanzania wote kufika kwa wingi kuonesha mshikamano na kusimama na ujasiri wa kisiasa dhidi ya uonevu na vitisho.

2. Bunge la Ulaya Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania
Tarehe 07 Mei 2025, Bunge la Ulaya litafanya mjadala maalum kuhusu hali ya demokrasia na haki za binadamu nchini Tanzania, huku kesi ya Mh. Lissu ikiwa miongoni mwa mambo makuu yatakayoangaziwa.
Tarehe 08 Mei 2025, bunge hilo litapiga kura ya maazimio rasmi kuhusu hali ya kisiasa Tanzania.

CHADEMA inawahimiza Watanzania na marafiki wa demokrasia kufuatilia mjadala huo kupitia vyanzo rasmi. Viongozi wa chama, wanachama na wafuasi wanashauriwa kuandaa maeneo maalum ya pamoja kufuatilia mjadala huo kama sehemu ya kujenga hamasa ya kitaifa.

3. Taarifa ya Udukuzi wa Akaunti Rasmi
Kwa masikitiko makubwa, tunaarifu kuwa akaunti zetu za X (zamani Twitter) - ChademaTZ na YouTube - Chadema Media zimeingiliwa na wadukuzi.

Tunaendelea kuchukua hatua za kiusalama na kisheria kurejesha udhibiti. Kwa sasa, taarifa rasmi za CHADEMA zinapatikana kupitia akaunti ya muda ya X: @ChademaTZ2. Tunaomba wafuasi wawe makini na kupuuza taarifa zinazochapishwa kwenye akaunti zilizodukuliwa hadi tutakapotoa taarifa rasmi ya kurejesha udhibiti.

Kwa pamoja, matukio haya yanaonesha namna haki na demokrasia nchini ziko mashakani. CHADEMA itaendelea kusimama imara na wananchi kwa ajili ya Tanzania yenye uhuru wa kweli, haki kwa wote, na siasa safi isiyozalisha hofu wala ukimya.

Imetolewa leo Jumatatu 05 Mei 2025:
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

Pia soma Pre GE2025 - John Heche: John Mrema amekimbia na Akaunti za YouTube na X za Chama, tuligundua kila wiki analipwa Tsh. Milioni 3
 
John Mrema ndo ana access za email zilizofungulia,
Na mrema atawasumbua sana chadema,

Haya ndo madhara ya taasisi kutumia email za binafsi kufungulia account za taasisi
Bwana Mwesiga ndugu yangu wa Ikulu unacheeka, kazi umeiweza sasa


Britanicca
 
Tobii bado yupo haha

GM
 
Kwa nn hizo account zisifungwe na kufunguliwa zingine?
 
CDM kwa hili ni wao wenyewe.Wanatakiwa wabadili mifumo yao ya TEHAMA mara kwa mara au wataalamu.
 
Mrema sasa pesa kedekede beer kwenda mbele huko segerea
 
Majambazi yameshavamia account za chama yanataka kuudanganya umma kwa kupotosha
"Askari wa Samia" kule TCRA anatimiza wajibu wake pasipo na shaka.
Hawa ndio watu wa kuwadhibiti wasiendelee kuleta uharibifu mkubwa kwenye taifa hili.

Ni bora kuwadhibiti wachache kabla ya sisi kwa sisi kiujumla hatujashikana makoo na kumwaga damu zetu kwa upumbavu wa hawa wachache.
 
Lissu kazuungukwa na wanaharakati wapumbavu sana. Na sio wanasiasa. Wanaharakati ambao katengenezewa na Maria ambae ana lengo tofauti na malengo ya chama Cha siasa.
 

Attachments

  • v49gvz.jpg
    195 KB · Views: 19
Je ni G55 ndio waliodukua akaunti za X za Chama?
 
Ndiyo maana ulisapoti kuuwawa kwa mdude.
 
Ndiyo maana ulisapoti kuuwawa kwa mdude.
Wapi.
Wewe una akili timamu?
Kujifanya chizi hakutawasaidia chochote. Mtasakwa tu popote mlipo na mtawajibishwa na waTanzania wenyewe.
 
Wapi.
Wewe una akili timamu?
Kujifanya chizi hakutawasaidia chochote. Mtasakwa tu popote mlipo na mtawajibishwa na waTanzania wenyewe.
Sasa msingemvamia mdude usiku mngeacha watanzania wamajibishe hata Padri kitima msingemvamia pia. Watu wakisema wasakane sababu hata polisi Wana ndugu na wanaishi mitaani ukaanza ooh watanzania tunanjia zetu.
Sasa Wewe ungekua na akili ungetumwa kuuwa na kweli unaenda kuuwa?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…