CHADEMA acheni siasa za majitaka, Dk Mary Mwanjelwa hajazomewa

Walimu wakitaka kugoma - chadema
Wanafunzi UDOM wakigoma-chadema
Wanafunzi UDSM wakigoma-chadema
Wanafunzi UDSM wakimzomea Kikwete-chadema
Wassira akizomewa Bunda-chadema
Mwanjelwa akizomewa mwanjelwa-chadema

Kwakweli jina la chadema linavuma kwenye mitaa.
 
Mtoa thread, Mary Mwanjelwa sio Dk for your info. Najua ni ugonjwa wa magamba wa kupenda tittle ya u-Dk.
Hadi anatoka pale PSI mwisho wa 2010, she was doing just Advocacy issues, na yeye si MD na wala hakuwa na PhD and hakuwa anasoma any PhD course, may be atakua ameenda masomo ya PhD ya VODA FASTA, kama za kina magamba.
 
Aaaaaaah! kumbe yule Dr Mwizi wa Mataulo hahahahahaha Magamba bwana ndio pumba zenu hizo
 
Mwakapulule, mwakitalu, mwakambimbi, mwakalundwa, mwakasege, mwakadingi, mwakatobe, mwamalundi, mwananyoko n.k wooote walikuwepo na walizomea. Mimi nimewashangaa sana, kwa nini waliishia kumzomea? Mbona wasimdunde mawe kama walivyovurumishaga majiwe kwenye msafara wa Vasco da Gama kipindi ile ya uchaguzi.

Salamu kwako mwakafunyule. Indungu syako

leka amahelu nungwe, kutunyasya!
 
Jana walikuwa Nzovwe pale Sokoni wakahutubia wanaCCM wasiozidi mia,Sido wakazomewa mwanzo mwisho,hivi kweli wanaweza kupimana upepo na chadema,Mary Mwanjelwa anadhani alivyopata PHD ya utapeli kutoka makanisa ya walokole anaweza akawadanganya wana Mbeya wote wakijua ni mwizi wa mataulo, unajua wameishiwa hata strategy ujenzi wa chama wangeufanya taratibu sio kujidai eti wanafuta Nyayo za Dr Slaa,ajabu kweli
 
Mwakapulule, mwakitalu, mwakambimbi, mwakalundwa, mwakasege, mwakadingi, mwakatobe, mwamalundi, mwananyoko n.k wooote walikuwepo na walizomea. Mimi nimewashangaa sana, kwa nini waliishia kumzomea? Mbona wasimdunde mawe kama walivyovurumishaga majiwe kwenye msafara wa Vasco da Gama kipindi ile ya uchaguzi.

Salamu kwako mwakafunyule. Indungu syako

Mimi nilikuwepo kwenye eneo la mkutano, Mary Mwanjelwa alianza mkutano wake vizuri. Lakini amepata taabu sana kujibu maswali yaliyomnyeshea kama mvua ya mawe. Maswali yenyewe yalikuwa ya kumkataa kuwa yeye si mbunge wa wanaMbeya kwa sababu hakuna mwananchi alieyemchagua, yeye anatetea ccm si wananchi, kama ni mbunge wa wananchi kwa nini anawaacha wananchi wanazama kwenye barabara zenye madibwi ya matope yeye amekuja kwa shangingi? kuhusu swala la katiba wamembana kuwa ccm haina nia njema kwa JK kusaini sheria itakayowafunga watanzania wanapoelimishana ili kuitengeneza iliyo bora. Ni ukweli usiopingika kwamba maswali haya yamempa wakati mgumu na kuishia kusema atayawakilisha kwa wahusika, kitendo kilichopelekea miguno mingi sana na watu wengi kuendelea kuhoji sababu ya yeye kutisha mkutano wa wananchi ambao hana majibu. Tukio la kusikitisha ni kwamba baada ya kuondoka Mary Mwanjelwa, Baunsa wa ccm alishambuliwa na wanachi kama mpira wa kona na kuachwa nusu mfu na kukimbizwa hospitali, sijui kama atapona. Pia kabla ya kuanza Mkutano kizee kimoja cha ccm kilisikika kikitoa tahadhali kwamba Mary amekosea sana kuitisha mkutano eneo la Soko la sido kwa sababu ni eneo hatari sana kwa wanaccm.
 
Mwakapulule, mwakitalu, mwakambimbi, mwakalundwa, mwakasege, mwakadingi, mwakatobe, mwamalundi, mwananyoko n.k wooote walikuwepo na walizomea. Mimi nimewashangaa sana, kwa nini waliishia kumzomea? Mbona wasimdunde mawe kama walivyovurumishaga majiwe kwenye msafara wa Vasco da Gama kipindi ile ya uchaguzi.

Salamu kwako mwakafunyule. Indungu syako

uniongele ingafi!
 
Hii nchi ni ya ajabu sana, pamoja na uwananmke wake na viti maalumu vya uchupi, inawezekanaje mtu aliyeiba tena mataulo hotelini Arusha akathubutu kutaka kuongea na wananchi na mkataka ashangiliwe? anajua nini kuhusu katiba huyu mama? je hajui kwenye katika tumeongelea values za ungozi? kama angeijua angeachia kwanza hiyo nafasi alioyoipata kwa njia za panya na ambayo inaongeze kutunyonya wananchi kwa starehe zao. Very good wana mbeya wapeleke upumbavu wao huko huko walikokuzoea sio mbeya, ndagha mubhombile bhatata, ndagha bha mama mulobwike. Mary mama huna heshima katika jamii, umepata ubunge kwa njia zisizofaa, umechakachua Phd kwa kulipia pale kwa mama Lwakatare, hata PSI ulikokua habari zako tunazotele ukiwatisha wazungu kwamba wewe ni partner wa jamaa, nao wakakuweka tu ili mradi siku zako ziishe, jambo pekee nalo lliheshimi ni jinsi ulivyoweza kujitoa kwenye u secretary, kufoji elimu katika kila level ikiwemo ya kuandikiwa thesis na waganga njaa eti ya chuo cha diplomasia (masters) nasikia kinyaa hawa ndio wabunge wetu katiba unayoipigia debe ifute nafasi hizi zilizojaa harufu ya ufuska na kugeuza bunge letu kuwa ......industry
 
huyu mama aliongea vizuri sana tena anajenga hoja za kimaendeleo bila kujali itikadi za vyama.tatizo la chadema ni chuki binafsi ndo mana unawaona washabiki wengi lakini kwenye uchaguzi wanapigwa.
Si wewe ambaye jana umejionyesha uko Geita Mwanza? unaruka kwa ungo au unaishi kila mahala kwa hisia?
 
Ukiwa mjinga katikati ya wapumbavu kama Mwamakula utakuwa mwerevu,Kwanza huyo mnayemwita DR.Mwanjelwa bali kwangu hana hadhi ya uDr.alihotubia Mwanjelwa alizomewa alipojaribu kumshambulia Sugu kiujanjaujanja,akaondoka kuja Nzovwe ambako kiukweli watu walihudhuria ukilinganisha na mikutano yake ya siku za nyuma na hakuigusa Chadema wala Sugu wake,hata hivyo hakuwa na hoja zozote za msingi kwani alipoanza tu alijitapa kuwa ye ni mcha Mungu atasema kweli tupu na kisha akaanza kuorodhesha misaada mbalimbali aliyoitoa na kila alipoorodhesha akauliza wananchi Je ninawapenda siwapendi?wanaccm walioonekana kuja naye wakamjibu una tupenda!nafanya kazi sifanyi wakajibu unafanya,akaorodhesha moja baada ya nyingine na kisha kutoa tsh.laki mbili kwac NZONDAHAKI SEKONDARI PAPO HAPO.Hivi hizo ndo nondo na hoja za Dr. wenu,hotuba kama zile ni za maana kwa mazezeta wanaodhani kuwa maendeleo yetui yataletwa na vijisenti vya mbunge vil;ivyosal;ia mfukoni mwake baada ya kumaliza dhiki zake,siamini ujinga huo,Kwangu mbunge ni mwakilishi na msimamizi wa rasilimali zangu mwenyewe na kodi zangu ili serikali izitumie kwa TIJA,mbona hasemi nimejenga reli,nimetoa ruzuku ya mbolea,nimetoa ruzuku TANESCO umeme usiongezwe bei ili msiwe ombaomba kwa wabunge, KANUNI YA CCM,WAMASKINISHE UWATAWALE.
 
Wewe mwandika post umekurupuka mimi nilikuwepo sido kuzomewa kazomewa tena wanachama wote wa ccm walionekana kuvalia nguo za kijani pote walipoonekana kupita na nguo za kijani walizomewa na uongo mwingine ni wakusema mery mwanjelwa ni mchapakazi kipi cha maana alichokifanya hapa jiji la mbeya kama sio uongo na unafiki.

UNATAKA KUJUA ALIYOYAFANYA DK.MWANJELWA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2011 NI HAYA HAPA; HALAFU UFANANISHE NA ALIYOYAFANYA SUGU WAKO;

utekelezaji:
katika shughuli za HUDUMA ZA JAMII:

1. Dec mwaka jana mara tu baada ya kuapishwa, pamoja na wanawake wa jiji la Mbeya kumfanyia tafrija ya kumpongeza pia alikula chakula cha usiku na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuwazawadia vitu mbalimbali.,

2. Ameshakwenda kutembelea soko la mwanjelwa kujionea na kuhoji ucheleweshaji wa soko la kimataifa la Mwanjelwa

3. Ameshatembelea soko la Sido, Uhindini yote yaliyoungua kuwafariji wahanga na kusikiliza kero zao

4. Ameshatembela zaidi ya mara tatu uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe kujua kiini cha ucheleweshaji na kuahidi kufatilia jambo hilo kwa ukaribu kwani kukamilika kwa uwanja huo kutarahisisha maendeleo katika nchi na mikoa jirani.

5.Amekuwa ni chachu katika kuchangia ujenzi wa nyumba za wachungaji, vyombo vya muziki katika makanisa mbalimbali
akiwa kama mgeni rasmi

6. Ameshatembelea vituo vya watoto yatima na kugawa chakula, nguo na mablanketi kituo cha K.K.K.T Iwambi na nuru Orphans Centre vyote vya jijini mbeya.

7.Ameshametoa mbuzi 200 kwa kaya 100 kata ya Nkunga wilayani Rungwe
8.Ameshatoa mbuzi 200 kwa kaya 100 kata ya Kambasegele wilayani Rungwe
9. Ameshatembelea gereza kuu la Ruanda Mbeya, ameshatoa zawadi mbalimbali kwao kama sehemu ya jamii kama vile sabuni, mafuta, jezi n.k. vile vile kuwasikiliza

ELIMU

10. Ameshatoa uniform za shule pamoja na viatu (boots) kwa wanafunzi 50 sekondari ya kata ya Nkunga
11. Ameshatoa unform za shule pamoja na viatu (boots kwa wanafunzi 50 sekondari ya kata yaa Kambasegele
12. Amejenga choo cha shule ya msingi Bagamoyo
13. Ameshatoa vitabu vya kujisomea library boksi 2 katika shule ya sekondari ya kata ya Ndola, Ileje
14. Ameshatoa vitabu vya kujisomea library boksi 2 katika shule ya sekondari ya Wazazi Isansa, Mbozi
15. Ameshatoa vitabu boksi 3 vya kujisomea library katika shule ya sekondari ya Wazazi Meta, Mbeya
16. Ameshatoa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana sekondari ya wazazi Isansa, Mbozi.

UJASIRIAMALI

17. Ameshapita wilaya zote za mkoa huo tayari kuhamasisha wakina mama waanzishe miradi na vikundi vya ujasirialmali
18. Ameshatoa 'semina elekezi' ya siku tatu kwa wah Madiwani wa Viti Maalum wote wa Mkoa wa Mbeya juu ya Uongozi Stadi

AFYA

19. Ameshatoa magodoro 225 katika hospitali za serikali na vituo vya Afya katika wodi za wazazi kwa wilaya za Mbeya Mjini, Mbozi, Ileje na Mbeya Vijijini
20. Ameshatoa na kukabidhi gari la kuhamasisha wananchi vijijini lenye sinema juu ya umuhimu wa kutumia Tiba kwa Kadi=TIKA mpango wa mfuko wa Bima ya Afya, amekabidhi kwa Jiji la Mbeya kwa kuanzia lakini litakuwa ni kwa mkoa mzima.
 
Back
Top Bottom