CHADEMA acheni siasa za majitaka, Dk Mary Mwanjelwa hajazomewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA acheni siasa za majitaka, Dk Mary Mwanjelwa hajazomewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwamakula, Jan 13, 2012.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kumezuka madai kwamba Mbunge wa viti maalum (ccm) mkoa wa Mbeya, Dk.Mary Mwanjelwa amezomewa na wananchi wakati wa ziara yake aliyoifanya Jijini Mbeya leo na kuzungumza na wananchi wa Mwanjelwa na Sido juu ya mchakato wa katiba. Mimi siyo kwamba nina maslahi yeyote kwa Dk. Mwanjelwa lakini jamani tuache uongo Chadema wamezusha uongo huo tu kutokana na siasa zao ambazo nazichukulia kama ni siasa za majitaka.

  Chadema tuache wivu, mbunge huyu siyo kwamba namfagilia lakini ukweli ni kwamba ni mchapakazi mzuri na mkutano wake ulikuwa wa amani na mimi nilikuwepo na wananchi walimshukru sana kwa ahadi aliyotoa ya kwenda kuonana na Mkurugenzi wa Jiji ili tatizo la ubovu wa barabara liweze kupatiwa ufumbuzi. Katika mkutano wake wananchi walimuuliza maswali na yeye aliyajibu kwa umakini mkubwa.

  Mwanadada huyu kiukweli anakubalika sana Mbeya, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni tungekuwa na wabunge watano wanawake kama huyu dada kichwa tungefika mbali anafanyakazi zake kwa vitendo na kwa umakini, anatekeleza ahadi zake kwa vitendo bila bulabula. Sijui ni watu gani wataongea uzushi kuhusu huyu dada huyu.
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kumezuka madai kwamba Mbunge wa viti maalum (ccm) mkoa wa Mbeya, Dk.Mary Mwanjelwa amezomewa na wananchi wakati wa ziara yake aliyoifanya Jijini Mbeya leo na kuzungumza na wananchi wa Mwanjelwa na Sido juu ya mchakato wa katiba. Mimi siyo kwamba nina maslahi yeyote kwa Dk. Mwanjelwa lakini jamani tuache uongo Chadema wamezusha uongo huo tu kutokana na siasa zao ambazo nazichukulia kama ni siasa za majitaka.

  Chadema tuache wivu, mbunge huyu siyo kwamba namfagilia lakini ukweli ni kwamba ni mchapakazi mzuri na mkutano wake ulikuwa wa amani na mimi nilikuwepo na wananchi walimshukru sana kwa ahadi aliyotoa ya kwenda kuonana na Mkurugenzi wa Jiji ili tatizo la ubovu wa barabara liweze kupatiwa ufumbuzi. Katika mkutano wake wananchi walimuuliza maswali na yeye aliyajibu kwa umakini mkubwa.

  Mwanadada huyu kiukweli anakubalika sana Mbeya, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni tungekuwa na wabunge watano wanawake kama huyu dada kichwa tungefika mbali anafanyakazi zake kwa vitendo na kwa umakini, anatekeleza ahadi zake kwa vitendo bila bulabula. Sijui ni watu gani wataongea uzushi kuhusu huyu dada huyu. angalieni blog ya mbeya yetu muone kilichojili ziara ya Dk.mwanjelwa
   
 3. Josephine

  Josephine Verified User

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unatupa taarifa kwa kilichojiri au unataka kujua chadema inasemaje kama taasisi.maana inawezekana kazomewa na wananchi hiyo si chadema.
  Mwisho nampongeza kama mwanamama asonge mbele.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ulikuwepo kwenye mkutano au umekurupuka tok usingizini na kuweka kuandika hii kitu?hivi ilikua ni leo au jana?kweli kazi ipo
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Vp aliwaeleza wanaMbeya juu ya kutuhumiwa kuiba taulo kwenye Hoteli ya Snow Crest huko Mkoani Arusha?
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hiyo habari hiyo umeisoma wapi kuwa huyo mbunge amezomewa au na wewe unaleta majungu hapa?
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huyu mama aliongea vizuri sana tena anajenga hoja za kimaendeleo bila kujali itikadi za vyama.tatizo la chadema ni chuki binafsi ndo mana unawaona washabiki wengi lakini kwenye uchaguzi wanapigwa.
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Na mimi nimepata habari kutoka kwa jamaa yangu aliyeko Mwanjelwa.Kanithibitishia huyu mbunge kazomewa vibaya sana mpaka akatia huruma.
   
 9. M

  MPG JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mwizi wa mataulo nikweli alizomewa na watu wa Mbeya hawaipendi CCM hata kidogo! Mbeya nchi rais Sugu.
   
 10. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu niliwai sikiya huyo mweshimiwa kuiba mapambo kwenye nyumba ya wageni vipi ni cdm walizusha?
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  hakuzomewa na chadema alizomewa na wananchi
   
 12. L

  Luiz JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe mwandika post umekurupuka mimi nilikuwepo sido kuzomewa kazomewa tena wanachama wote wa ccm walionekana kuvalia nguo za kijani pote walipoonekana kupita na nguo za kijani walizomewa na uongo mwingine ni wakusema mery mwanjelwa ni mchapakazi kipi cha maana alichokifanya hapa jiji la mbeya kama sio uongo na unafiki.
   
 13. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  nani katoahilo tamko la kuzomea ndani ya chadema?. je wasira na mkono walizomewa? Mia
   
 14. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ulintungulu m'alafyale, mwamakula, lo!
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  unakanusha yasiyokanushika
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  tukuyu stars

  mwamakula=====mwanjelwa====mwakipogosole=====mwakifulefule=====mwaipondele====mwakasakasaka ====mwampulule=====mwakigogonjela=====mwakikwemakwema=====mwa.......=====mwa===
   
 17. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kangi ntungulu akindilile! Huyo kazomewa kweli. Mwamakula asilete propaganda zake za ccm hapa kama haamini aende maeneo ya sido akaulize.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Acha maji taka wewe mimi nilikuwepo na nilimzomea
   
 19. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  HUyu dada huyu, huyu dada huyu!


  Huyo dada angekuwa na akili asingemtumia mtu kama wewe kukanusha yaliyotokea kama ni kweli yametokea. Unatuambia hapa kuwa KUMEZUKA MADAI, unaweza kutuambia hayo madai yamezuka wapi?

  Tazama ulivyo kilaza hapo kwenye RED unaonesha jinsi ulivyotumwa kiasi unataka kujifanya na wewe ni CDM ila tu umechoshwa na tabia fulani wakati mstari mmoja tu juu yake umeshasahau your true ID na unabadili kauli. CHADEMA WAMEZUSHA UONGO, mara wewe huyo huyo CDM TUACHE WIVU!

  Ujinga wako mwingine ni kuwasingizia wananchi wa Mwanjelwa kuwa wana akili haba kama za kwako. Eti 'wananchi wakamshukuru sana kwa ahadi aliyotoa......ufumbuzi' Unataka kuniambia walimshukuru kwa kupiga magoti na kumsujudia kwa hii AHADI tu?! Ina maana watu wa Mwanjelwa hii ni ahadi yao ya kwanza kuisikia toka kwa viongozi wa CCM? Kwani wakati wa kampeni za urais, kuna kipande cha barabara ambacho hakikuahidiwa na Mh.Dokta kuwa kitageuka lami? Huyo dadaako unayemsifia na Mh.Dokta Safari za Nje ni nani mwenye uwezo hasa wa kuona ahadi za chama chenu zikitimia?

  Mambo ya kujikomba na kuleta hisia peleka MMU
   
 20. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwakapulule, mwakitalu, mwakambimbi, mwakalundwa, mwakasege, mwakadingi, mwakatobe, mwamalundi, mwananyoko n.k wooote walikuwepo na walizomea. Mimi nimewashangaa sana, kwa nini waliishia kumzomea? Mbona wasimdunde mawe kama walivyovurumishaga majiwe kwenye msafara wa Vasco da Gama kipindi ile ya uchaguzi.

  Salamu kwako mwakafunyule. Indungu syako
   
Loading...