CHADEMA "achaneni" na Dr.Slaa (Ushauri)

CHADEMA "achaneni" na Dr.Slaa (Ushauri)

Kweli CHADEMA ni cha Watanzania na Kila Mtu anaruhusiwa kutoa Maoni yake.Tatizo ni Kwamba Maoni yako ni Dhaifu Mno.

Kama ni dhaifu mbona unatokwa na mapovu.Ukiona halikuhusu/halina maana piga chini.Watanzania mbona mnapenda sana "ndio mzee"?Halafu huu ni ushauri,na wala sio lazima.
 
Soma mwanzo hadi mwisho.Na angalia,nimetumia neno "achaneni",maana yake si impige chini.Dr.Slaa tayari anafahamika kwa wananchi,na wala hauhitaji kumnadi sana.Ushauri wangu ni kwamba Chadema iache kumtegemea zaidi Slaa,mtaji wa chama ni wanachama/wananchi.Usipokubaliana,sikulazimishi.

OK, CHADEMA tumekataa Maoni yako.
 
Angalia neno "achaneni" limetumikaje.Tatizo la wanachama wa Chadema huwa hawapendi ukweli.Ukiwaambia ukweli wanatukana.Mimi niwe na ajenda ya siri kwa ajili ya nini?Kutoa ushauri kama huu ni mapenzi tosha kwa chadema.Jaribuni kuelewa.Nasema Chadema "iachane" na Dr.Slaa.Maana yangu si mfukuze,au ipuze mchango wa Dr.Slaa.Maana yangu ni kwamba tayari Dr.Slaa anauzika,anafahamika,haina haja ya chama kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya mtu mmoja.Iwezeke kwa wanachama/wananchi ambao ndio watakaompigia kura Dr.Slaa wakati wa uchaguzi kama atapitishwa na chama chake.

Hivi ushauri unaotoa lazima ukubaliwe? Basi si ushauri ni amri.

Somo la bure.

Jifunze kutumia njia ambayo itahakikisha ulichokikusudia kinafanikiwa. Kama hakitafanikiwa achana nacho. Ndiyo maana nimekushauri upitie kwenye ofisi za Chadema karibu na ulipo ndio utaratibu wa kusikilizwa maoni yako.
 
MAMBO MATANO MUHIMU KWA CHADEMA.

Kwa sasa Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani Tanzania,ambacho kinawanyima usingizi vigogo wa CCM ambao wako kwenye “fungate” la kufurahia uhuru wa Tanzania.Mara nyingi tumezoea,vyama vya upinzani kuilalamikia CCM kwenye mambo kadhaa,lakini sasa kibao kimegeuka.Wenye dola ndio walalamishi,na kutwa kuishambulia Chadema as if CDM ndio Chama Tawala.Kifupi CCM imechoka,imevubaa na imesinyaa.Kuendelea kuwapa kinachoitwa “kura” kama sio “kula” CCM ni kuendelea kuchimba kaburi la mauti.

Kuna msemo wa “Waliopo hatuwataki,na wanaotaka hatuwaamini”.Je,unaamini Chadema wanaweza kuziba pengo la “marehemu mtarajiwa CCM?Kwa jibu lolote utakalotoa,Chadema kama kweli inataka kushika dola kwa masilahi ya Watanzania wanahitaji kujirekebisha,na kuonyesha utofauti wao na “marehemu mtarajiwa,mheshimiwa CCM.

Mezani kwangu hapa nina mambo matano ya kuwashauri CHADEMA.Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

1. Chadema “achaneni na Dr.Slaa,jengeni chama.

Dr.Slaa ni moja kati ya watu muhimu sana katika Chadema na Taifa kwa ujumla.Tangu Dr.Slaa awe mbunge (1995) ameonyesha utendaji makini na kuweka masilahi ya Taifa mbele.Hata alipoteuliwa na Chadema kuwa mgombea Urais 2010 sikushangazwa.Pamoja kwamba alishindwa kwa “goli la mkono” la CCM lakini ni wazi kwamba alionyesha ushindani mkubwa JK.

Inasemekana Dr.Slaa hakutaka kugombea urais na badala yake alitaka kuendelea na ubunge.Ushawishi wa Kamati Kuu ya Chadema ulifanya Dr.Slaa kukubaliana na ombi hilo ila kwa masharti.Kwamba ikitokea kushindwa kwenye urais,basi alipwe mshahara kama wa mbunge.Chama kilikubaliana na masharti hayo,na mambo yanaendelea.

HOJA YANGU: Chadema inawekeza zaidi kwa Dr.Slaa kuliko wanachama (wapiga kura)

Umaarufu na nguvu alizonazo Dr.Slaa ndani ya Chadema unaweza kukiangamiza chama kuliko kukisaidia.Kwa jinsi nionavyo ni kwamba Dr.Slaa yuko juu ya Chadema,kitu ambacho ni hatari sana.Chama kinajaribu kwa kina namna “kumbembeleza” na kusahau wapiga kura.Lazima Chadema watafute balance ya chama.Wakati Dr.Slaa analipwa pesa nyingi chini ya makubaliano maalum,ofisi za mikoani,wilayani na vijijini ziko hoi.

Dr.Slaa ni mtu muhimu sana ndani ya Chadema na Taifa,lakini hawezi kuwa juu ya Chama.Chama kiwekeze kwa wanachama kwa kutumia rasilimali fedha kidogo walizonazo.

2. Fedha za Ruzuku.

Hoja hii inafanana kiasi na hiyo hapo juu.Hili ni suala muhimu sana likazingatiwa na Chadema.Kumekuwepo na madai mengi,kwamba ruzuku inatumiwa vibaya.Sijui ukweli ukoje,ila mimi ningewashauri kuelekeza ruzuku wanazozipata huko matawini.Inawezekana wanafanya hivyo,lakini impact yake haiendani na hali halisi.Ofisi za mkoa na wilayani ziko hoi.

Muda wa kujenga chama ni huu,wasisubiri wakati wa uchaguzi.Kuna watu wengi sana wako tayari kusaidia harakati bila malipo,lakini ni vema chama kikatambua na angalau kuwawezesha vitendea kazi.Support wanayopata chadema (hata ukiangalia chaguzi ndogo zilizopita) ni ndogo sana ukilinganisha na mwamko wa wananchi.

3.DECENTRALIZATION.

Chadema wana sera ya majimbo,sasa ingekuwa vema wangeanza kuifanyia kazi ndani ya chama ili iwe mfano.Hapa juzi walichagua viongozi wa kuongoza kanda,Sawa,lakini suala hili linatakiwa la kiutendaji zaidi.Wananchi/wanachama wapewe mamlaka/madaraka ya kujiamulia mambo yao (kwa kufuata katiba).Hili suala la hata jambo dogo kuamuliwa makao makuu sio jema,lina harufu ya udikteta na linazua malalamiko mengi.Chadema ijenge chama kwa kuwawezesha wanachama wao kuelewa katiba na miongozo mingine ya chama,ili waendeleze harakati mahala walipo,tofauti na hivi sasa ambapo kila kitu kinahitaji kufanyiwa kazi makao makuu.

4. WABUNGE WA CHADEMA.

Kwa bahati nzuri sana,CDM ina wabunge ambao bongo zao zinafanya kazi.Licha ya kwamba ni wachache bungeni,sauti zao zinasikika zaidi.Sasa ni vema wakatumia nafasi hiyo kuwatetea wananchi.Suala la kususia vikao,sasa waachane nalo.Wapaze sauti na kujenga hoja kistaarabu kila wapatapo nafasi.Hata kama mawazo yao yatapuzwa,lakini wananchi wanajua nani nani anawatetea.Wapunguze jazba licha ya kwamba uongozi wa bunge unaonyesha wazi kupendelea Chama Tawala/Serikali.

Pia ni vema wakayatendea haki majimbo yao.Wahakikishe wanafanya kila linalowezekana kutatua kero za wananchi.Wafanye majimbo yao yawe mfano wa kuigwa ili 2015 iwe rahisi zaidi na kuongeza idadi ya viti vya ubunge.Watambue kwamba wananchi wao ndio maboss wao,wajue kujishusha na kuwa na karibu na wananchi wa kawaida.Ukichaguliwa kuwa mbunge,haina maana kwamba una akili zaidi kuzidi wapiga kura.

5.MIKUTANO YA HADHARA.

Mikutano ya hadhara ni muhimu sana kwa uhai wa chama chochote cha siasa.Chadema wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara kila inapowezekana.Kwa mfano Operation Sangara ilifanikiwa sana kwa kuwaamsha watanzania wengi waliolala.

Chadema inafanya mikutano ya hadhara katika mazingira magumu sana na ya hatari,kwa sababu CCM wanatumia kila mbinu kukwamisha.Na hivi karibuni tumeshuhudia machafuko (mauaji) katika mikutano ya Chadema.Machafuko haya yanasababishwa na polisi ambao wamepewa jukumu jipya (tofauti na tunalolifahamu) la kuiharibia Chadema.

Sijajua Plan B ya Chadema.Lakini hali hii kiendelea hivi,na kama hakutakuwa na makubaliano (Pinda anasema wapigwe tu),ili kuepusha maafa zaidi kwa wanachama wao,watanzania wenzetu,hebu wajaribu kubadilisha mbinu.Mikutano ya hadhara ambayo haina ulazima wa kuwepo Viongozi wakuu wa chama waachane nayo.

Sasa waanze kampeni ya nyumba kwa nyumba,mtaa kwa mtaa,mtu kwa mtu.Na kazi hii inatakiwa kufanyika na viongozi wa vijiji,kata,wilaya n.k.Kitu cha msingi wawawezeshe.Mikutano mikubwa ifanyike pale panapokuwa na ulazima.

Katoe ushauri katika vikao halali vya chama.
 
ok. naomba nione ushauri wako kwa CCM na jinsi inavyofanya siasa zake hapa nchini. Put a particular emphasis on Mwigulu Nchemba (kama jinsi ulivyomtaja dr. slaa). Come up with a balanced opinion wewe mwenye uchungu na nchi!

Siku zote unamshauri unayempenda.Inawezekana hamkubaliani na ushauri wangu.Sawa haina tatizo.Nia yangu ni njema tu.Ila siwezi kuwashauri CCM.Hapa walipofikia,hawashauriki.Kwa mfano,umjadili Mwigulu Nchemba kwa lipi?Kwangu kumjadili Mwigulu Nchemba ni kupoteza muda.Zaidi wapenda busara wakishika dola,Mwigulu ashikiliwe.
 
Hivi ushauri unaotoa lazima ukubaliwe? Basi si ushauri ni amri.

Somo la bure.

Jifunze kutumia njia ambayo itahakikisha ulichokikusudia kinafanikiwa. Kama hakitafanikiwa achana nacho. Ndiyo maana nimekushauri upitie kwenye ofisi za Chadema karibu na ulipo ndio utaratibu wa kusikilizwa maoni yako.

Asante kwa somo lako.
 
Mlihangaika sana na ZZK chama makini kikatulia mmeanza tena ee??

"To know the enemy is half the victory"
 
Tukubali kutofautiana.Si kala mtu anayekushauri,ushauri ambao hukubaliani nao ni adui yako.Mimi sina matatizo na Chadema.Mimi sio mnafiki,na siogopi kusema kitu ninacho kiona kina ukweli.NAWAPENDA CHADEMA NDIO MAANA NAWASHAURI.Tunataka ukombozi wa nchi yetu,hatutaki kubadilisha sura tu.Chadema lazima ijipange vema ili kuongoza ukombozi tunaoutaka ambao ni mgumu zaidi kuliko enzi za ukoloni.Chadema kubalini kushaurika.Nchi hii ni yetu sote

Sijui kwa nia yako njema uliyojipambanua kuwa nayo unaweza kuitumia kumsauri baba yako mambo ya kifamilia sokoni?
 
Chadema wanawekeza kwa wananchi, tatizo lenu wanaCCM mbamuogopa Dr. Slaa mno!

hivi umemwelewa mleta hoja au? mtoa mada usipoteze muda wako kushauri hiki chama tunakipenda sawa ila jf inawadanganya viongoz hawajui hawa wa key-board hata kura hawapigi vijijin ndo kuna kura
 
Dr. Slaa anakunyima usingizi eeh!! Pole sana!! Nakumbuka JK baada ya kutangazwa mshindi 2010 alisema " tulibidi turudi mara mbili tatu katika sehemu nyingine kufanya kampeni upya".

"Cowards die many times before their death" Shakespeare
 
Unaweza kutafsiriwa vibaya kutokana na namna ilivyotumia lugha tatanishi kwenye uandishi, vinginevyo yale mazuri yatazingatiwa na pumba zitaachwa!
 
Sijajua Plan B ya CHADEMA.Lakini hali hii kiendelea hivi,na kama hakutakuwa na makubaliano (Pinda anasema wapigwe tu),ili kuepusha maafa zaidi kwa wanachama wao,watanzania wenzetu,hebu wajaribu kubadilisha mbinu.Mikutano ya hadhara ambayo haina ulazima wa kuwepo Viongozi wakuu wa chama waachane nayo.

Sasa waanze kampeni ya na na viongozi wa vijiji,kata,wilaya n.k.Kitu cha msingi wawawezeshe.Mikutano mikubwa ifanyike pale panapokuwa na ulazima.[/QUOTE]

Ushauri mzuri ila unajichanganya hasa point ya kwanza ambayo imeshindwa kutofautisha charistimatic cum born leader na self-imposed leader. Labda kosa si lako maana vyama vingine na hasa CCM hawana viongozi wenye sifa kama za Slaa. Slaa ni koo chaa uongozi na anaongea lugha ambayo watu wanaelewa na anayaishi yale anayoyasema kwa vitendo. Ndio maana na wewe unakiri amekuwa tishio kwa watawala ambao wanatembea chini ya busati si kwa sababu ya physical power bali intellectual power. Kila muungano wa kiitikadi ungependa kuwa na mtu wa aina kama kiongozi lakini cha kushangaza unashauri kinyume chake.Pili ukishauri basi jitofautishe walau kidogo wasiiona mbali na pua zao. Mshahara halali tena ambao wabunge wanapata na sio marupurupu kama ya wabunge umekuwa ni silaha wanayoitumia CCM kumsema Dr.Slaa ambaye amejitoa kukisaidia chama. Yeye si wakala wa meli wala mfanyabiashara wa meno ya tembo. Muda mwingi ni yeye na chama. Kwanini mshahara umekuwa nong'wa. Ukipungua polisi wataacha kuipiga wana Cdm? Ukipungua mabomu ya machozi na maji ya kuwasha na kesi za kubambika zitaisha? Waziri Mkuu na Wassira watakuwa na hofu ya Mungu. Hivi ndio adui wa demokrasia na sio Dr.Slaa
 
Sijui kwa nia yako njema uliyojipambanua kuwa nayo unaweza kuitumia kumsauri baba yako mambo ya kifamilia sokoni?

Kamanda Ben, mleta uzi msamehe bure may be his is reflecting a problem that we have and is there to stay if we do not remove CCM through ballot box. The problem is fragile education system that has been architected by CCM in a number of ways that need not repeat. Matokeo ni kuwa na watu ambao wanashindwa kujieleza and keep themselves busy beating about a bush. Huwezi kusoma shule za kata tena zisiwe na walimu au zinao wachache lakini wa fasta fasta na ukategemea atajenga hoja ieleweke. Huyu ni wa kusamehe na kwenda naye taratibu maana elimu haina mwisho lakini kwanza ajitambue na kuwa tunaye bado online atajaribu kujiona ni wapi alipokosea. Ukiacha pale ambapo ni controversial kama ambavyo wengine wameanisha elimu vijijini na pembezoni mwa miji ni muhimu katika kukijenga chama. Elimu ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ni muhimu lakini isitoe umuhimu wa public rally. Hii ya nyumba kwa nyumba inaweza kukuoyesha nguvy yako maana utajua unao wanachama wangapi na je wanazo sifa za kupiga kura. Ukishakuwa na list hiyo ni rahis kufanya tathmnini dakika za mwisho kujua wangapi watakuwa tayari kupiga kura maana watakuwa na shahada ambazo ni valid na hazijanunuliwa kwa hila
 
Mtoa mada nadhani nimemuelewa, hata kama alidhani atakuwa ataoa kwa kudhani anaiharibu CHADEMA lakini ukweli ikiwa plan B yaani kuelimisha umma kwa njia ya nyumba kwa nyumba itakuwa ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara, maana wananchi hawatakubali kutishwa kwa lolote kwan watakuwa wameelea vizuri namna ya kujitafutia ukombozi wao wenyewe kuanzia katika familia, mashina na kata zao. Nadhani atakuwa anamaanisha kuwa BIG RESULTS ni muunganiko wa matokeo chanya kwenye mirija mingi....
Mkuu, suala la ruzuku na matumizi yake, milioni 200+, sijui unazionaje, lakini kwa kazi tu za kila siku achana na mshahara wa Dr. Slaa si kitu kabisa. Ni ndogo mno, angalia kazi zinazofanywa ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa magari yaliyoko mitaani kwa shughuli za kichama. Mimi na wewe wenye mapenzi mema tushirikiane kwenye hili, tusaidie kadiri ya uwezo wetu halafu tuhoji pia namna ya matumizi bora ya fedha hizo.
Awe chama chochote kwa huo ushauri mi nadhani anastahili pongezi...Si lazima aupeleke ofisini, popote pale hasa anapodhani utafanikiwa kuufisha ushauri wake kwa haraka zaidi na kupata uchambuzi wa kina inafaa. Hii hoja ya kila kitu kukipeleka kwenye ofisi za chama nadhani ni mifumo isiyo na tija sana hasa katika kipindi hiki chenye muingiliano wa mambo mengi...
 
.

Nakushukuru kwa maelezo yako.Inawezekana kweli tatizo ni elimu yangu.Inawezekana!Hoja ya Dr.Slaa naona haijaeleweka kwa sababu sijaipambanua vilivyo.Nakiri kosa.Lakini sijaona sababu ya wewe "msomi wa enzi za mwalimu" kunishambua,mara nimesoma shule za kata,mara vile.Elimu bila hekima na busara,ni ujinga.Sitaki kufanya kosa la kukushambulia,kama ulivyofanya wewe.Na wala hakuna sababu ya kushindana.
 
Mtoa mada nadhani nimemuelewa, hata kama alidhani atakuwa ataoa kwa kudhani anaiharibu CHADEMA lakini ukweli ikiwa plan B yaani kuelimisha umma kwa njia ya nyumba kwa nyumba itakuwa ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara, maana wananchi hawatakubali kutishwa kwa lolote kwan watakuwa wameelea vizuri namna ya kujitafutia ukombozi wao wenyewe kuanzia katika familia, mashina na kata zao. Nadhani atakuwa anamaanisha kuwa BIG RESULTS ni muunganiko wa matokeo chanya kwenye mirija mingi....
Mkuu, suala la ruzuku na matumizi yake, milioni 200+, sijui unazionaje, lakini kwa kazi tu za kila siku achana na mshahara wa Dr. Slaa si kitu kabisa. Ni ndogo mno, angalia kazi zinazofanywa ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa magari yaliyoko mitaani kwa shughuli za kichama. Mimi na wewe wenye mapenzi mema tushirikiane kwenye hili, tusaidie kadiri ya uwezo wetu halafu tuhoji pia namna ya matumizi bora ya fedha hizo.
Awe chama chochote kwa huo ushauri mi nadhani anastahili pongezi...Si lazima aupeleke ofisini, popote pale hasa anapodhani utafanikiwa kuufisha ushauri wake kwa haraka zaidi na kupata uchambuzi wa kina inafaa. Hii hoja ya kila kitu kukipeleka kwenye ofisi za chama nadhani ni mifumo isiyo na tija sana hasa katika kipindi hiki chenye muingiliano wa mambo mengi...

Nashukuru kwa ushauri wako.Mimi sina chama,ila nawaona Chadema wako kwenye mwelekeo mzuri ukiachana na kasoro ndogondogo ambazo huwa hazikosekani katika maisha ya binadamu.Nimeandika haya kwa moyo mkunjufu,na wala lengo halikuwa kuwabomoa Chadema.Nakiri kwamba Hoja yangu ya kwanza,sikuieleza kwa kina.Tuepuka dhana ya kwamba kila anayeisema Chadema ni adui,mwisho wa siku,adui ataachwa,kwa kuparamia wasio maadui.Pia tukubali kuyasikia hata yale tusiyoyapenda.
 
Back
Top Bottom