CHADEMA "achaneni" na Dr.Slaa (Ushauri)

CHADEMA "achaneni" na Dr.Slaa (Ushauri)

mwankuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
334
Reaction score
120
MAMBO MATANO MUHIMU KWA CHADEMA.

Kwa sasa CHADEMA ndicho chama kikuu cha upinzani Tanzania,ambacho kinawanyima usingizi vigogo wa CCM ambao wako kwenye "fungate" la kufurahia uhuru wa Tanzania.Mara nyingi tumezoea,vyama vya upinzani kuilalamikia CCM kwenye mambo kadhaa,lakini sasa kibao kimegeuka.Wenye dola ndio walalamishi,na kutwa kuishambulia CHADEMA as if CHADEMA ndio Chama Tawala.Kifupi CCM imechoka,imevubaa na imesinyaa.Kuendelea kuwapa kinachoitwa "kura" kama sio "kula" CCM ni kuendelea kuchimba kaburi la mauti.

Kuna msemo wa "Waliopo hatuwataki,na wanaotaka hatuwaamini".Je,unaamini CHADEMA wanaweza kuziba pengo la "marehemu mtarajiwa CCM?Kwa jibu lolote utakalotoa,CHADEMA kama kweli inataka kushika dola kwa masilahi ya Watanzania wanahitaji kujirekebisha,na kuonyesha utofauti wao na "marehemu mtarajiwa,mheshimiwa CCM.

Mezani kwangu hapa nina mambo matano ya kuwashauri CHADEMA.Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

1. CHADEMA "achaneni na Dr.Slaa,jengeni chama.

Dr.Slaa ni moja kati ya watu muhimu sana katika CHADEMA na Taifa kwa ujumla.Tangu Dr.Slaa awe mbunge (1995) ameonyesha utendaji makini na kuweka masilahi ya Taifa mbele.Hata alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea Urais 2010 sikushangazwa.Pamoja kwamba alishindwa kwa "goli la mkono" la CCM lakini ni wazi kwamba alionyesha ushindani mkubwa JK.

Inasemekana Dr.Slaa hakutaka kugombea urais na badala yake alitaka kuendelea na ubunge.Ushawishi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ulifanya Dr.Slaa kukubaliana na ombi hilo ila kwa masharti.Kwamba ikitokea kushindwa kwenye urais,basi alipwe mshahara kama wa mbunge.Chama kilikubaliana na masharti hayo,na mambo yanaendelea.

HOJA YANGU: CHADEMA inawekeza zaidi kwa Dr.Slaa kuliko wanachama (wapiga kura)

Umaarufu na nguvu alizonazo Dr.Slaa ndani ya CHADEMA unaweza kukiangamiza chama kuliko kukisaidia.Kwa jinsi nionavyo ni kwamba Dr.Slaa yuko juu ya CHADEMA,kitu ambacho ni hatari sana.Chama kinajaribu kwa kina namna "kumbembeleza" na kusahau wapiga kura.Lazima CHADEMA watafute balance ya chama.Wakati Dr.Slaa analipwa pesa nyingi chini ya makubaliano maalum,ofisi za mikoani,wilayani na vijijini ziko hoi.

Dr.Slaa ni mtu muhimu sana ndani ya CHADEMA na Taifa,lakini hawezi kuwa juu ya Chama.Chama kiwekeze kwa wanachama kwa kutumia rasilimali fedha kidogo walizonazo.

2. Fedha za Ruzuku.

Hoja hii inafanana kiasi na hiyo hapo juu.Hili ni suala muhimu sana likazingatiwa na CHADEMA.Kumekuwepo na madai mengi,kwamba ruzuku inatumiwa vibaya.Sijui ukweli ukoje,ila mimi ningewashauri kuelekeza ruzuku wanazozipata huko matawini.Inawezekana wanafanya hivyo,lakini impact yake haiendani na hali halisi.Ofisi za mkoa na wilayani ziko hoi.

Muda wa kujenga chama ni huu,wasisubiri wakati wa uchaguzi.Kuna watu wengi sana wako tayari kusaidia harakati bila malipo,lakini ni vema chama kikatambua na angalau kuwawezesha vitendea kazi.Support wanayopata CHADEMA (hata ukiangalia chaguzi ndogo zilizopita) ni ndogo sana ukilinganisha na mwamko wa wananchi.

3.DECENTRALIZATION.

CHADEMA wana sera ya majimbo,sasa ingekuwa vema wangeanza kuifanyia kazi ndani ya chama ili iwe mfano.Hapa juzi walichagua viongozi wa kuongoza kanda,Sawa,lakini suala hili linatakiwa la kiutendaji zaidi.Wananchi/wanachama wapewe mamlaka/madaraka ya kujiamulia mambo yao (kwa kufuata katiba).Hili suala la hata jambo dogo kuamuliwa makao makuu sio jema,lina harufu ya udikteta na linazua malalamiko mengi. CHADEMA ijenge chama kwa kuwawezesha wanachama wao kuelewa katiba na miongozo mingine ya chama,ili waendeleze harakati mahala walipo,tofauti na hivi sasa ambapo kila kitu kinahitaji kufanyiwa kazi makao makuu.

4. WABUNGE WA CHADEMA.

Kwa bahati nzuri sana,CHADEMA ina wabunge ambao bongo zao zinafanya kazi.Licha ya kwamba ni wachache bungeni,sauti zao zinasikika zaidi.Sasa ni vema wakatumia nafasi hiyo kuwatetea wananchi.Suala la kususia vikao,sasa waachane nalo.Wapaze sauti na kujenga hoja kistaarabu kila wapatapo nafasi.Hata kama mawazo yao yatapuzwa,lakini wananchi wanajua nani nani anawatetea.Wapunguze jazba licha ya kwamba uongozi wa bunge unaonyesha wazi kupendelea Chama Tawala/Serikali.

Pia ni vema wakayatendea haki majimbo yao.Wahakikishe wanafanya kila linalowezekana kutatua kero za wananchi.Wafanye majimbo yao yawe mfano wa kuigwa ili 2015 iwe rahisi zaidi na kuongeza idadi ya viti vya ubunge.Watambue kwamba wananchi wao ndio maboss wao,wajue kujishusha na kuwa na karibu na wananchi wa kawaida.Ukichaguliwa kuwa mbunge,haina maana kwamba una akili zaidi kuzidi wapiga kura.

5.MIKUTANO YA HADHARA.

Mikutano ya hadhara ni muhimu sana kwa uhai wa chama chochote cha siasa. CHADEMA wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara kila inapowezekana.Kwa mfano Operation Sangara ilifanikiwa sana kwa kuwaamsha watanzania wengi waliolala.

CHADEMA inafanya mikutano ya hadhara katika mazingira magumu sana na ya hatari,kwa sababu CCM wanatumia kila mbinu kukwamisha.Na hivi karibuni tumeshuhudia machafuko (mauaji) katika mikutano ya CHADEMA.Machafuko haya yanasababishwa na polisi ambao wamepewa jukumu jipya (tofauti na tunalolifahamu) la kuiharibia CHADEMA.

Sijajua Plan B ya CHADEMA.Lakini hali hii kiendelea hivi,na kama hakutakuwa na makubaliano (Pinda anasema wapigwe tu),ili kuepusha maafa zaidi kwa wanachama wao,watanzania wenzetu,hebu wajaribu kubadilisha mbinu.Mikutano ya hadhara ambayo haina ulazima wa kuwepo Viongozi wakuu wa chama waachane nayo.

Sasa waanze kampeni ya nyumba kwa nyumba,mtaa kwa mtaa,mtu kwa mtu.Na kazi hii inatakiwa kufanyika na viongozi wa vijiji,kata,wilaya n.k.Kitu cha msingi wawawezeshe.Mikutano mikubwa ifanyike pale panapokuwa na ulazima.
 
Hapa kama nimekuelewa vile, lkn hayo mengine niwaachie wengine
 
Sasa kama una kiri kuwa Dr Slaa ni Mtu Muhimu CHADEMA, sasa Mbona tena unahsauri CHAMA kiachane nae.
Hilarious
 
Wenzako kina TUNTEMEKE and co. walijitahidi sana kupenyeza mawazo mfu kama haya hawakufanikiwa sijui kama wewe utaweza, mbona la ugaidi halijaisha au mmeona halina tija.
 
-Unataka ujue Plan B ya CHADEMAhuku ukiwa umeshajipambanua kuwa Adui?

-Ni jambo la ajabu sana kama atatokea Aduiyako akakushauri juuya aina ya silaha ya kutumia wakati wa mapambano na wewe ukakshawishika na kukubali

Kurukaruka kote kumbe Headache ni Dr.Slaa? Habari mbaya kwako CHADEMA ni Taasisi,U-Dr.Slaa ni taasisi.Wapo Dr.Slaa wengi kwenye kanda n.k.

Ni jambo la ajabu unaleta hoja za upotoshaji humu.Kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita zimeratibiwa na viongozi wa kanda tu.Sijui unataka kusema nini hapo kwenye hoja ya Decentralization. Jenga hoja ndani ya mantiki ndugu yangu utakuja kujifedhehesha hapa siku nyingnine

Ondoa basi hiyo picha uliyoweka ya Nelson Mandela maana hufanani nae kwenye matendo na kifikra kwa post hii tu uliyoandika
 
nimekusoma mkuu, ila ujasema CHADEMA hiachane na Dr slaa kivipi? Na sababu gani hasa?
 
Who are you kuishauri Chadema? Acha ulimbukeni.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Nani anastahili kuishauri CHADEMA? CHADEMA ipo kwa ajili ya nani?
Ninyi ndio mnaharibu chama. CHADEMA ni chama cha Watanzania,hivyo kila mtu anahaki ya kuwasifia na kuwakosoa.Acha mawazo mgando hayo.
 
Sasa kama una kiri kuwa Dr Slaa ni Mtu Muhimu CHADEMA, sasa Mbona tena unahsauri CHAMA kiachane nae.
Hilarious

Soma mwanzo hadi mwisho.Na angalia,nimetumia neno "achaneni",maana yake si impige chini.Dr.Slaa tayari anafahamika kwa wananchi,na wala hauhitaji kumnadi sana.Ushauri wangu ni kwamba Chadema iache kumtegemea zaidi Slaa,mtaji wa chama ni wanachama/wananchi.Usipokubaliana,sikulazimishi.
 
-Unataka ujue Plan B ya CHADEMAhuku ukiwa umeshajipambanua kuwa Adui?

-Ni jambo la ajabu sana kama atatokea Aduiyako akakushauri juuya aina ya silaha ya kutumia wakati wa mapambano na wewe ukakshawishika na kukubali

Ondoa basi hiyo picha uliyoweka ya Nelson Mandela maana hufanani nae kwenye matendo na kifikra kwa post hii tu uliyoandika

Tukubali kutofautiana.Si kala mtu anayekushauri,ushauri ambao hukubaliani nao ni adui yako.Mimi sina matatizo na Chadema.Mimi sio mnafiki,na siogopi kusema kitu ninacho kiona kina ukweli.NAWAPENDA CHADEMA NDIO MAANA NAWASHAURI.Tunataka ukombozi wa nchi yetu,hatutaki kubadilisha sura tu.Chadema lazima ijipange vema ili kuongoza ukombozi tunaoutaka ambao ni mgumu zaidi kuliko enzi za ukoloni.Chadema kubalini kushaurika.Nchi hii ni yetu sote
 
hilo la mwisho nakubaliana a wewe, plab b ya nyumba kwa nyumba itatupelea ikulu! na maCCM watajuta kwann waliamua kuuwa watu for intimidation!
 
mwankuga
...nimejaribu kukuelewa lakini badala ya kukuelewa umezidi kunichanganya kwa maelezo yako yasiyoeleweka...unasema Dr Slaa ni mtu muhimu sana Chadema alfu hapohapo unashauri Chadema iachane na Dr Salaa(mtu muhimu)...hivi unaposema mtu muhimu labda unamaana gani?...
 
Last edited by a moderator:
Nani anastahili kuishauri Chadema?Chadema ipo kwa ajili ya nani?
Ninyi ndio mnaharibu chama.Chadema ni chama cha Watanzania,hivyo kila mtu anahaki ya kuwasifia na kuwakosoa.Acha mawazo mgando hayo.

Kweli CHADEMA ni cha Watanzania na Kila Mtu anaruhusiwa kutoa Maoni yake.Tatizo ni Kwamba Maoni yako ni Dhaifu Mno.
 
Nani anastahili kuishauri Chadema?Chadema ipo kwa ajili ya nani?
Ninyi ndio mnaharibu chama.Chadema ni chama cha Watanzania,hivyo kila mtu anahaki ya kuwasifia na kuwakosoa.Acha mawazo mgando hayo.
Utaratibu ungekwenda ofisi za Chadema ukatoa maoni yako; hata kama si mwana Chadema. Ila kama unavyoambiwa sijui ungejisikiaje kama ungeambiwa/ungeshauliwa uachane na umpendaye kwa sababu anakupenda kiukweli.

Nachukua nafasi kukushauri kupeleka ushauri wako utakapofanyiwa kazi kwa sababu ushauri uliotoa kwa Chadema hauna busara kwa hiyo haukubaliki labda kwa kuongeza posts hapa JF.
 
mwankuga
...nimejaribu kukuelewa lakini badala ya kukuelewa umezidi kunichanganya kwa maelezo yako yasiyoeleweka...unasema Dr Slaa ni mtu muhimu sana Chadema alfu hapohapo unashauri Chadema iachane na Dr Salaa(mtu muhimu)...hivi unaposema mtu muhimu labda unamaana gani?...

Kutoa ushauri kama huu ni mapenzi tosha kwa chadema.Jaribuni kuelewa.Nasema Chadema "iachane" na Dr.Slaa.Maana yangu si mfukuze,au ipuze mchango wa Dr.Slaa.Maana yangu ni kwamba tayari Dr.Slaa anauzika,anafahamika,haina haja ya chama kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya mtu mmoja.Iwezeke kwa wanachama/wananchi ambao ndio watakaompigia kura Dr.Slaa wakati wa uchaguzi kama atapitishwa na chama chake.
 
Utaratibu ungekwenda ofisi za Chadema ukatoa maoni yako; hata kama si mwana Chadema. Ila kama unavyoambiwa sijui ungejisikiaje kama ungeambiwa/ungeshauliwa uachane na umpendaye kwa sababu anakupenda kiukweli.

Nachukua nafasi kukushauri kupeleka ushauri wako utakapofanyiwa kazi kwa sababu ushauri uliotoa kwa Chadema hauna busara kwa hiyo haukubaliki labda kwa kuongeza posts hapa JF.

Angalia neno "achaneni" limetumikaje.Tatizo la wanachama wa Chadema huwa hawapendi ukweli.Ukiwaambia ukweli wanatukana.Mimi niwe na ajenda ya siri kwa ajili ya nini?Kutoa ushauri kama huu ni mapenzi tosha kwa chadema.Jaribuni kuelewa.Nasema Chadema "iachane" na Dr.Slaa.Maana yangu si mfukuze,au ipuze mchango wa Dr.Slaa.Maana yangu ni kwamba tayari Dr.Slaa anauzika,anafahamika,haina haja ya chama kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya mtu mmoja.Iwezeke kwa wanachama/wananchi ambao ndio watakaompigia kura Dr.Slaa wakati wa uchaguzi kama atapitishwa na chama chake.
 
Tukubali kutofautiana.Si kala mtu anayekushauri,ushauri ambao hukubaliani nao ni adui yako.Mimi sina matatizo na Chadema.Mimi sio mnafiki,na siogopi kusema kitu ninacho kiona kina ukweli.NAWAPENDA CHADEMA NDIO MAANA NAWASHAURI.Tunataka ukombozi wa nchi yetu,hatutaki kubadilisha sura tu.Chadema lazima ijipange vema ili kuongoza ukombozi tunaoutaka ambao ni mgumu zaidi kuliko enzi za ukoloni.Chadema kubalini kushaurika.Nchi hii ni yetu sote

ok. naomba nione ushauri wako kwa CCM na jinsi inavyofanya siasa zake hapa nchini. Put a particular emphasis on Mwigulu Nchemba (kama jinsi ulivyomtaja dr. slaa). Come up with a balanced opinion wewe mwenye uchungu na nchi!
 
Back
Top Bottom