Chad yapiga marufuku vazi la Burka

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,756
48,401
130301172112_kabul_burqa_shop_640x360_bbc_nocredit.jpg


Mamlaka ya Chad imepiga marufuku vazi la Burqa kufuatia visa vya walipuaji wa kujitolea muhanga siku ya jumatatu ambavyo vimewaua watu 23.

Waziri mkuu Kalzeube Pahimi Deubet, alitangaza baada ya kuonana na viongozi wa kidini.

Amelaumu kundi la Boko Haram kwa kutekeleza mashambulizi huku kundi hilo likiendelea kuwatumia wanawake kama walipuaji wa kujitolea muhanga kwa kuwa ni rahisi wao kutotambulika.

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Ndjamena tangu milipuko hiyo ambayo iliyalenga makao makuu ya polisi pamoja na chuo cha kutoa mafunzo ya polisi katika mji huo.



Chad yapiga marufuku vazi la Burqa - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom