Chad: Askari saba wauawa katika shambulizi la Boko Haram

figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,404
Points
2,000
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,404 2,000
Jeshi la Chad limepoteza askari wake saba na wengine kumi na tano kujeruhiwa katika shambulio la kundi la Boko Haram lililotokea katika Jimbo la Ziwa Chad.
Mapigano kati ya jeshi la Chad na wanamgambo wa Kiislamu yamekuwa yamesitishwa kwa wiki tatu katika eneo hilo, baada ya wapiganaji hao kuanzisha mapigano kwa miezi kadhaa sasa.
Kituo cha jeshi cha Bohama karibu na mji wa Kaïga Kindjiria kwenye pwani ya kaskazini mwa Ziwa Tchad kimeshambuliwa usiku wa manane Jumatatu wiki hii. Washambuliaji, ikiwa ni pamoja na wale wa kujitoa muhanga, waliua askari saba wa Chad na kujeruhi wengine kumi na tano.Waasi wengi wauawa
Washambuliaji sitini na watatu wameuawa kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la Chad ambalo limebaini kwamba operesheni ya kuwatokomeza inaendelea. Mkuu wa majeshi, Jenerali Taher Erda, amekwenda eneo la tukio kwa helikopta mapema Jumatatu hii asubuhi.
Shambulizi hili, ambalo linatokea baada ya wiki tatu za utulivu, limeua idadi ndogo ya askari ikilinganishwa na lile la Dangdala, mji wa Chad, unaopatikana karibu na Niger. Wakati wa shambulio hilo, askari 20 wa Chad waliuawa na vifaa vya kijeshi kuporwa, hali ambayo ilisababisha baadhi ya wakuu wa jeshi kufutwa kazi.
 
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2018
Messages
2,701
Points
2,000
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2018
2,701 2,000
Nigeria walituaminisha kuwa boko haram kapoteza nguvu dah

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
3,304
Points
2,000
Age
55
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
3,304 2,000
Hayo mataifa manne, Nigeria, Niger, Chad na Cameroon yana uzembe sana. Yanashindwaje kuwaangamiza hao magaidi?
 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
21,731
Points
2,000
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
21,731 2,000
Usaliti unaanzia kwenye Majeshi ya nchi husika.....
 
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Messages
2,828
Points
2,000
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2016
2,828 2,000
Ndio mujuwe wazungu ni watu wabaya sana. Vikundi ivi wamevitengeneza wenyewe kwa lengo la kutuibia mali ze2 kama vile mafuta n.k. amkeni enyi manaswara.
 
busha

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Messages
683
Points
1,000
busha

busha

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2019
683 1,000
Mtaupiga vita sana uislamu lakini hamtafanikisha. Na haukutolea mfano kwenye nchi za makafiri ila kwa waislamu tu.
sasa mwamba vp boko wanawapiga chad wakati chad ndo jeshi lililowaokoa waislamu wa Africa ya kati na ikawapa hifadhi,,,

Hawa boko wanataka nn haswa,,?tuanzie hapo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Messages
2,828
Points
2,000
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2016
2,828 2,000
sasa mwamba vp boko wanawapiga chad wakati chad ndo jeshi lililowaokoa waislamu wa Africa ya kati na ikawapa hifadhi,,,

Hawa boko wanataka nn haswa,,?tuanzie hapo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao boko wanafanya kwa maslahi yao mkuu, na pengine kikundi hicho kimetengenezwa na hao hao wazungu makafiri ili kuuchafua tu uislamu na vile vile kuiba raslimali za nchi hizo....ukiangalia nchi kama nigeria ina waislamu wengi kuliko wakristo

Nigeria 75% waislamu
Chadi 53% waislamu

Kwanini wachaguwe nchi za kiislam tu! Hujiulizi!!!

Ebu pitia kidogo hapa

Vita havipendezi lakini utu haukuweza kuondoa vita katika historia nzima. Katika Quran, mapambano ya watoto wawili wa Adam yametajwa. Mmoja hakuwa na hatia na mwingine ni mgomvi. Yule mgomvi akamuua yule ambaye hakuwa na hatia. (Angalia sura al-Maida, 27-31). Jina la yule ambaye hakuwa na hatia ni Habil; na jina la mgomvi ni Qabil.

Qabil alipomuua ndugu yake, damu ya binadamu ilimwagwa kwa mara ya kwanza duniani. Hata hivyo, damu hii ilizidi kadiri wakati ulivyosogea na ikaenea duniani kote. Habil na Qabil ni wawakilishi wa watu wasio na hatia na wagomvi. Madam watu kama Qabil wapo duniani, watu kama Habil watakuwa na haki ya kujilinda.

Hivyo, Uislamu unaruhusu vita kwa kuzingatia masharti kadhaa ili kuzuia udhalimu wa wakandamizaji na kuhakikisha kuwa amani inaenea kote. Mathalani, tuangalie aya ifuatayo:

“Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.” (al-Hajj, 39)

Aya hii inamwambia Mtume na Maswahaba wake ambao ndio walio katika daraja la kwanza katika Uislamu. Walifanyiwa dhuluma na mateso yaliyosababisha kifo kwa baadhi yao katika mji wa Makkah. Baadhi yao walikwenda Abyssinia kwa kufuata ushauri wa Mtume. Baadaye wengine walihamia Madinah. Takriban kila mara walisikia habari kama zifuatazo: “Watu wa Makka wanashambulia; Watu wa Makka wameshambuliwa.” Waislamu waliruhusiwa kupigana walipokuwa katika hali hizo.

Yafuatayo yameelezwa katika aya nyingine zinazohusu vita:

“Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.” (al-Baqara, 190)

Masuala yafuatayo yametajwa katika aya hiyo:

1- “Piganeni na wale wanaokupigeni.” Yaani, msipigane na wale wasiokupigeni. Kwa hakika, Mtume aliwaamuru makamanda wake wasiwaue watoto, wanawake, wazee na waliojitenga kwa kukaa katika mahekalu.

2- Vita lazima viwe “fi sabilillah”, yaani “katika njia ya Allah.’ Huenda wengine wakapigana ili kuvamia nchi mpya na kupata rasilimali za malighafi, n.k. Hata hivyo, Muislamu anaweza kupigana kwa ajili ya njia ya Allah tu. Yaani, anapambana ili kuzuia ukatili, uovu na vurugu duniani.

3- Hairuhusiwi kuvuka mipaka wakati wa vita au baadaye. Uislamu unawaamuru Waislamu kuua kwa namna nzuri wanapolazimika kufanya hivyo. Mathalani, Uislamu unakataza kuua kwa kutesa na kukata masikio, pua, n.k.

Yafuatayo yameelezwa katika aya nyingine:

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako’’ (an-Nisa,75)

Katika aya hii, Waislamu wanashauriwa kupigana kama wanakandamizwa katika mji au kama wanazuiwa kutekeleza imani yao. Mwishoni mwa vita, Waislamu wanakuwa huru dhidi ya uonevu na wanapata uhuru wa dini na dhamiri; watu wa nchi hiyo wanakuwa huru kusilimu ama laa.

Tunaweza kusema yafuatayo katika kuhitimisha:

Kilicho muhimu katika Uislamu ni amani si vita. Hata hivyo, watu wanapokandamizwa au dola inaposhambulia dola nyingine, vita vitakuwepo. Uislamu unaruhusu vita katika hali hizo. Uislamu haukuanzisha vita katika wakati ambao havikuwepo duniani. Wanaouzingatia Uislamu kuwa ni dini ya vita waangalie historia yao wenyewe, wataona kuwa kulikuwa na vita takribani katika kila kipindi cha historia yao. Kwa hiyo, kuwepo kwa hukumu za vita katika Uislamu si upungufu kwa Uislamu bali ni ukamilifu. Katika hukumu zilizotajwa katika aya na hadithi, uhalisia kama vita ambavyo haviepukiki ulibadilishwa na kuwa ustaarabu na utu kutoka ubedui na unyama.
 
Mgugu

Mgugu

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Messages
1,551
Points
2,000
Mgugu

Mgugu

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2015
1,551 2,000

Mkuu kama kweli uislamu ni amani unajua idadi kamili ya vita alivyopigana mtume pamoja na idadi ya vita alivyotuma majeshi yake yakapigane?
Unaweza pia nitajie idadi ya vita alivyopigana Yesu kristo(Nabii Issa kama mnavyomuita)

Maendeleo hayana chama
 
Forum statistics

Threads 1,285,012
Members 494,369
Posts 30,847,295
Top