Chad: Askari saba wauawa katika shambulizi la Boko Haram

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,484
54,855
Jeshi la Chad limepoteza askari wake saba na wengine kumi na tano kujeruhiwa katika shambulio la kundi la Boko Haram lililotokea katika Jimbo la Ziwa Chad.

Mapigano kati ya jeshi la Chad na wanamgambo wa Kiislamu yamekuwa yamesitishwa kwa wiki tatu katika eneo hilo, baada ya wapiganaji hao kuanzisha mapigano kwa miezi kadhaa sasa.
Kituo cha jeshi cha Bohama karibu na mji wa Kaïga Kindjiria kwenye pwani ya kaskazini mwa Ziwa Tchad kimeshambuliwa usiku wa manane Jumatatu wiki hii. Washambuliaji, ikiwa ni pamoja na wale wa kujitoa muhanga, waliua askari saba wa Chad na kujeruhi wengine kumi na tano.

Waasi wengi wauawa
Washambuliaji sitini na watatu wameuawa kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la Chad ambalo limebaini kwamba operesheni ya kuwatokomeza inaendelea. Mkuu wa majeshi, Jenerali Taher Erda, amekwenda eneo la tukio kwa helikopta mapema Jumatatu hii asubuhi.
Shambulizi hili, ambalo linatokea baada ya wiki tatu za utulivu, limeua idadi ndogo ya askari ikilinganishwa na lile la Dangdala, mji wa Chad, unaopatikana karibu na Niger. Wakati wa shambulio hilo, askari 20 wa Chad waliuawa na vifaa vya kijeshi kuporwa, hali ambayo ilisababisha baadhi ya wakuu wa jeshi kufutwa kazi.
 
Hayo mataifa manne, Nigeria, Niger, Chad na Cameroon yana uzembe sana. Yanashindwaje kuwaangamiza hao magaidi?
 
Ndio mujuwe wazungu ni watu wabaya sana. Vikundi ivi wamevitengeneza wenyewe kwa lengo la kutuibia mali ze2 kama vile mafuta n.k. amkeni enyi manaswara.
 
Mtaupiga vita sana uislamu lakini hamtafanikisha. Na haukutolea mfano kwenye nchi za makafiri ila kwa waislamu tu.
sasa mwamba vp boko wanawapiga chad wakati chad ndo jeshi lililowaokoa waislamu wa Africa ya kati na ikawapa hifadhi,,,

Hawa boko wanataka nn haswa,,?tuanzie hapo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao boko wanafanya kwa maslahi yao mkuu, na pengine kikundi hicho kimetengenezwa na hao hao wazungu makafiri ili kuuchafua tu uislamu na vile vile kuiba raslimali za nchi hizo....ukiangalia nchi kama nigeria ina waislamu wengi kuliko wakristo

Nigeria 75% waislamu
Chadi 53% waislamu

Kwanini wachaguwe nchi za kiislam tu! Hujiulizi!!!

Ebu pitia kidogo hapa

Vita havipendezi lakini utu haukuweza kuondoa vita katika historia nzima. Katika Quran, mapambano ya watoto wawili wa Adam yametajwa. Mmoja hakuwa na hatia na mwingine ni mgomvi. Yule mgomvi akamuua yule ambaye hakuwa na hatia. (Angalia sura al-Maida, 27-31). Jina la yule ambaye hakuwa na hatia ni Habil; na jina la mgomvi ni Qabil.

Qabil alipomuua ndugu yake, damu ya binadamu ilimwagwa kwa mara ya kwanza duniani. Hata hivyo, damu hii ilizidi kadiri wakati ulivyosogea na ikaenea duniani kote. Habil na Qabil ni wawakilishi wa watu wasio na hatia na wagomvi. Madam watu kama Qabil wapo duniani, watu kama Habil watakuwa na haki ya kujilinda.

Hivyo, Uislamu unaruhusu vita kwa kuzingatia masharti kadhaa ili kuzuia udhalimu wa wakandamizaji na kuhakikisha kuwa amani inaenea kote. Mathalani, tuangalie aya ifuatayo:

“Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.” (al-Hajj, 39)

Aya hii inamwambia Mtume na Maswahaba wake ambao ndio walio katika daraja la kwanza katika Uislamu. Walifanyiwa dhuluma na mateso yaliyosababisha kifo kwa baadhi yao katika mji wa Makkah. Baadhi yao walikwenda Abyssinia kwa kufuata ushauri wa Mtume. Baadaye wengine walihamia Madinah. Takriban kila mara walisikia habari kama zifuatazo: “Watu wa Makka wanashambulia; Watu wa Makka wameshambuliwa.” Waislamu waliruhusiwa kupigana walipokuwa katika hali hizo.

Yafuatayo yameelezwa katika aya nyingine zinazohusu vita:

“Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.” (al-Baqara, 190)

Masuala yafuatayo yametajwa katika aya hiyo:

1- “Piganeni na wale wanaokupigeni.” Yaani, msipigane na wale wasiokupigeni. Kwa hakika, Mtume aliwaamuru makamanda wake wasiwaue watoto, wanawake, wazee na waliojitenga kwa kukaa katika mahekalu.

2- Vita lazima viwe “fi sabilillah”, yaani “katika njia ya Allah.’ Huenda wengine wakapigana ili kuvamia nchi mpya na kupata rasilimali za malighafi, n.k. Hata hivyo, Muislamu anaweza kupigana kwa ajili ya njia ya Allah tu. Yaani, anapambana ili kuzuia ukatili, uovu na vurugu duniani.

3- Hairuhusiwi kuvuka mipaka wakati wa vita au baadaye. Uislamu unawaamuru Waislamu kuua kwa namna nzuri wanapolazimika kufanya hivyo. Mathalani, Uislamu unakataza kuua kwa kutesa na kukata masikio, pua, n.k.

Yafuatayo yameelezwa katika aya nyingine:

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako’’ (an-Nisa,75)

Katika aya hii, Waislamu wanashauriwa kupigana kama wanakandamizwa katika mji au kama wanazuiwa kutekeleza imani yao. Mwishoni mwa vita, Waislamu wanakuwa huru dhidi ya uonevu na wanapata uhuru wa dini na dhamiri; watu wa nchi hiyo wanakuwa huru kusilimu ama laa.

Tunaweza kusema yafuatayo katika kuhitimisha:

Kilicho muhimu katika Uislamu ni amani si vita. Hata hivyo, watu wanapokandamizwa au dola inaposhambulia dola nyingine, vita vitakuwepo. Uislamu unaruhusu vita katika hali hizo. Uislamu haukuanzisha vita katika wakati ambao havikuwepo duniani. Wanaouzingatia Uislamu kuwa ni dini ya vita waangalie historia yao wenyewe, wataona kuwa kulikuwa na vita takribani katika kila kipindi cha historia yao. Kwa hiyo, kuwepo kwa hukumu za vita katika Uislamu si upungufu kwa Uislamu bali ni ukamilifu. Katika hukumu zilizotajwa katika aya na hadithi, uhalisia kama vita ambavyo haviepukiki ulibadilishwa na kuwa ustaarabu na utu kutoka ubedui na unyama.
 
nashkuru sana kwa uchambuzi wako makini kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama kweli uislamu ni amani unajua idadi kamili ya vita alivyopigana mtume pamoja na idadi ya vita alivyotuma majeshi yake yakapigane?
Unaweza pia nitajie idadi ya vita alivyopigana Yesu kristo(Nabii Issa kama mnavyomuita)

Maendeleo hayana chama
Jamaa mbna kakuelewesha vyema kabisa kama s.a.w hakuingia tu vitani na wala hakuwahi anzisha vita alipigana kwa sababu maalum ama hukuelewa uliposoma ama hukuona

Vita vilikuepo kwasababu maalum sio kama alikaa tu akakurupuka kama afanyavyo US Namashoga Zake Wakishashiba Tu Wana Amua Tuwaekee Vikwazo VENEZUELA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi nnee zote zinasumbuliwa na kundi moja tu wanashindwa kuliangamiza hilo kundi, magaidi ni kupiga na kumaliza wote hao
 
Kama wangekua wanamalizwa kwamaneno ya kwenye jf wangekua hawapo tena kwa ss

Njia pekee yakuyaangamiza makundi yakigaidi ni Kuanguka Utawala Wa US Pamoja Nakufutwa ISRAEL Katika Uso Wadunia

Im Done.....

Sio rahisi kuwamaliza,,ni wengi sana halaf wafadhili wao ni marekani na israel silaha wanazowapa ni babkubwa. Sasa cjui mtawamalizaje mjomba!
 
Kama wangekua wanamalizwa kwamaneno ya kwenye jf wangekua hawapo tena kwa ss

Njia pekee yakuyaangamiza makundi yakigaidi ni Kuanguka Utawala Wa US Pamoja Nakufutwa ISRAEL Katika Uso Wadunia

Im Done.....

Sent using Jamii Forums mobile app
UNA USHAHIDI GANI KUWA MAKUNDI HAYO YA KIGAIDI YAMEUNDWA NA US NA ISRAELI AU NI CHUKI ZAKO BINAFSI TU DHIDI YA HIZO NCHI MBILI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom