Chachu ya mawaziri vijana iko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chachu ya mawaziri vijana iko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jul 13, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Kwa tafsiri yangu binafsi kijana ni yule aliye na chini ya umri wa miaka 55.......................hivyo mawaziri vijana wenye kuangukia umri huo ninawagusa kwenye mada hii.................................

  nimepitia kwa ukaribu sana utendaji wa mawaziri vijana ambao mteuzi wao JK aliahidi wangelikuwa chachu ya maendeleo katika serikali yake lakini kwa maoni yangu hii ni njozi pevu hadi sasa........................ni riwaya ya kufikirika na kusadikika tu lakini haina mwelekeo wa kutokea.................

  Nikianza na Waziri mwandamizi Magufuli ambaye amekuwa akidai yeye ni mtekelezaji mzuri wa sheria zilizopo bila ya kujiuliza hizo sheria zimetungwa kumnufaisha nani..........................wanyonge walio wengi au mabwanyenye walio wachache.......................kwa maoni yangu kabla ya kuanza kuzipigia debe sheria zilizopo ni vyema kujiuliza ni nani ambaye ananufaika na sheria tajwa..................tukija bomoabomoa ambayo Magufuli kajizolea punjepunje za umaarufu kwa asilimia zote sheria hizo za mwaka arobaini na saba hazimjali kumboreshea mnyonge maisha bora............sasa ni za nini kwa nini zisifutwe na kutungwa sheria zenye kulinda msilahi ya wanyonge ambao mara nyingi huburuzwa na serikali yetu isiyomjali myonge huyu?

  magufuli amekuwa akitoa ahadi ya kuwa sasa barabara zitamjali mwendesha baiskeli, pikipiki na mwenda kwa miguu lakini haelezei miaka yote aliyokuwa hapo wizara ya ujenzi/ miundo mbinu kwa nini hayo hayakufanyika hayo....................................cheap politician? I think so kwa sababu nimetafuta wakati ambapo Magufuli amemtetea mnyonge sijawahi kuona ila kila apatapo nafasi ya kumkandamiza mnyonge huichangamkia............kwa sababu haitishii masilahi yake binafsi.....he is definitely an opportunist in chief...........hata zile operesheni za choma nyavu mbali ya ukweli kuwa ni uchafuzi wa mazingira.........................pia zililenga kumfukarisha raia wa kawaida wakati wenye viwanda vya kuzitengeneza nyavu hizo na waagiza wa nyavu hizo toka nje wakiachwa bila ya bughudha yoyote ile.....................je huyu ni kiongozi wa kutumainiwa? Jibu langu ni la hasha....................ila kwenye nchi ya vipofu kama hii yetu............ataendelea kujizolea umaarufu siku hata siku.......................maybe we deserve the lack of quality of leadership in this country............

  Nikija Ngeleja............................tangia alipoukwaa uwaziri yeye ni nishati na madini.........elimu yake ni mwanasheria ambaye kamwe hajawahi kukanyaga mahakamani......................ni ile unakusanya vyeti kwa malengo ya kujiuuza kisiasa..............uzoefu wa shughuli za sheria ni sifuri.....................kwenye nishati sifa aliyonayo ni kutongezea makali ya mgawo na ahadi kibao za kumaliza mgawo baada ya 2015.........................kwenye madini amekuwa kinara wa kutetea misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa..............................tunaelewa ya kuwa mgawo wake na swahiba zake waliomteua si haba hapo.......No wonder JK is adamant that ngeleja is the best man for the job so long as he is serving his own personal interests there at the ministry..........tatizo ni kuwa hii ni dhuluma dhidi yetu...........................

  Halafu dada yangu Ghasia...................................zaidi ya kuwatisha watumishi wa umma wasivujishe siri za ufisadi sikumbuki jingine ambao ametufanyia................................................

  Dada yangu Professa TIbaijuka................................alianza kwa nguvu ya soda hapo ardhi............................sasa ameingia mitini akidai anaanda programu ya utekelezaji.................................nilidhani wizara inayo programu tajwa na hahitaji kuwa na yake binafsi..............vinginevyo wizara itapoteza mwelekeo wa kutegemea programu za kila waziri aingiapo pale ardhi................nionavyo ameamua kumtumikia kafiri ili apate mradi wake....................

  Yupo kijana mwana wa Raisi Mstaafu Mwinyi.................pale ulinzi ni picha tu imewekwa kwa ajili ya kumshukuru Mwinyi kwa kufanikisha Project Kikwete awe Raisi...............................mabomu ya Gongo la Mboto na Mbagala..........yaliyotosha kumtupia Hussein Mwinyi virago vyake..............................lakini kwenye nchi isiyo na maadili na kumwogopa mwenyezi Mungu..........................ninasikia tetesi JK ana mkakati wa kumsimika awe Raisi wetu wa 4..........you can talk of political dynasties in TZ..........kisa ndiye anayeaaminika atalinda wezi na wabadhirifu wa mali ya umma........................na hapo siyo suala la udini hata chembe ila ushuhuda wa ufisadi............................ndilo litakalomfikisha kijana huyu huko IKULU ambako hata baba yake pamoja kuwa na kisomo haba aliweza kufika...................thanks to Nyerere's stupidity..................ya kudai hata wazanzibara wanaweza...............now we know better.......................

  Yupo huyu wa maliasili na utalii...........maige............ ambaye alikwenda Ngorongoro juzi na alipokaribishwa kwa mabango ya wenyeji wakitaka abariki upendeleo wa kikabila katika ajira ya tasisi ya umma ambayo unasigina katiba yetu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania .........yeye pamoja na kuwa aliapa kuilinda na kuitetea katiba tajwa..................ili kujipatia umaarufu wa bei chee aliwaunga mkono wakabila wale wa kimasai.................ambao wanataka shirika la umma liwaajiri wao kwa asilima 75.....................................kwa sababu wao ni wamasai tu hakuna kigezo kingine..................kama tukiruhusu ukabila ushamiri hapa nchini tujue tumekwisha kabisa...........................................kila kabila litadai taasisi za umma zilizopo kwenye maneneo yao wajazwe wao na wakuja wafukuziliwe mbali...........

  Yupo huyu Waziri wa Michezo........nchimbi......... ambaye anafikiri kwa kutokea kwenye dansi mara kwa mara kama mgeni rasmi kama alivyopitia JK kuukwaa Uraisi basi na yeye atatumia zana zilezile!!!!!!!!!!!!!! Kwa kifupi hana jipya.......................ila kulinda mlo wake.....................................

  yupo huyu wa kilimo................Mathayo.............ambaye wakati wa uchaguzi 2010 alikuwa kinara kumkashifu Muumba kwa kugeuza nyimbo zake takatifu kumtukuza JK pale Same..............................kwa chama ambacho kimeingia madarakani kwa kauli mbiyu ya kilimo kwanza.....................ningelimtarajia ashike bango la kuona azma hiyo inatekelezwa kwa vitendo badala ya kuwa ni baragumu la kukusanya mtaji wa kura tu..................................hadi leo sijui alichofanya.........................

  Yupo huyu naibu waziri wa biashara...................alikuja na mbio za kuwafukuza wachina ambao wameitika vyema utandawazi kama sisi tulivyoitika kwa ndugu zetu wapo uchina wakifanya huohuo umachinga.................................kijana huyu ambaye amejizolea sifa kwa nukuu zake za wanafilosofia wa ng'ambo.....hana muda na wa hapa nchini......................alifanya jitihada ya kuwajengea mazingira ya kuwafukuza wachina hao ambao ndiyo wavuja jasho wasiotuibia..................................hata sumuni ile.......................................baada ya kukalishwa kikao na Balozi wa uchina....................siku hizi yuko kimya...............................alianza moto na hivi sasa amegundua kuwa hajui afanyalo...........................kwa hiyo yuko kimya.....................anaendelea kujizolea alawansi za safari za ndani ambazo tija yake inaniacha na maswali mengi..............................ingawaje ni safari za ndani..........na ninafuu zaidi ya mteuzi wake ambaye kajijengea umaarufu wa safari za ng'ambo ambazo hazina tija kwa umasikini wetu huu........................

  wengine hata majina yao siyakumbuki lakini binafsi sijui ujana wao taifa hili limenufaika vipi.......................mwenye taarifa za aina yoyote ile ni vyema anifahamishe................................................
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  [h=3] Wabunge wampania Waziri Ngeleja [/h]
  Na Waandishi Wetu, Dodoma

  WAKATI bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kusomwa Ijumaa wiki hii, dalili zimeanza kujitokeza baada ya wabunge wengi kuonesha shauku ya kuchangia
  mjadala huo kutokana na mgawo wa umeme nchini.

  Hali hiyo ilidhihirika jana wakati wa kipindi cha maswali na majibu baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Bi. Jenista Mhagama kumpa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza mbunge wa Mtambile, Bw. Masoud Abdallah Salim, aliyetaka kujua serikali inawaambia nini Watanzania juu ya ufumbuzi wa tatizo la umeme ambalo linaendelea kuathiri maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

  Miongoni mwa wabunge hao ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe ambaye alipopewa fursa ya kuuliza swali la nyongeza, alisema anashindwa kuelewa kwanini serikali haisemi lolote kuhusu tatizo la umeme, na baadaye baadhi ya wabunge walionesha nia ya 'kumkaba koo' waziri huyo wakati wa bajeti yake.

  Bw. kabwe alisema tatizo hilo linatokana na mashine za kampuni ya Pan African kupata kutu.

  Pia, alisema tangu tatizo hilo lilipoanza Mei mwaka huu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepoteza zaidi ya sh bilioni 800 na kuhoji ni kwa nini mpaka sasa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja na naibu wake, Bw. Adam Malima hawajajiuzulu.

  "Suala la umeme ni kizungumkuti, lakini kuna tatizo la serikali kutosema ukweli kwa wananchi. Tatizo ni kutu zilizopo kwenye mashine," alisema.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Adam Malima, alisema tatizo si visima vya kufulia gesi bali ni mashine za Pan African kuwekwa kemikali ambazo zilisababisha mashine hizo kuwa na kutu.

  Alisema walidhani kuwa mashine hizo zingeweza kudumu kwa miaka 12, lakini zimeharibika kutokana na kemikali.

  Akijibu swali la msingi la Bw. Salim, Naibu Waziri huyo, alisema ni kweli kwamba nchi imekumbwa na tatizo la umeme linalotokana na uwekezaji mdogo usiolingana na ukuaji wa mahitaji kwa muda mrefu.

  "Hata hivyo, nchi yetu ina rasilimali nyingi ambazo zote zinaweza kutumika kuzalisha umeme ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa umeme na serikali ina mipango mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi ya kukabiliana na tatizo hilo na katika kipindi cha muda mfupi, serikali inajielekeza kupambana na tatizo hilo kwa kuharakisha upatikanaji wa mitambo iliyokusudiwa kununuliwa ya megawati 100 Dar es Salaam na megawati 60 Nyakato, Mwanza na hatua za kununua pamoja na kuifunga mitambo hiyo zinatarajiwa kukamilika Aprili mwaka kesho," alisema.

  Alisema kuwa hivi sasa upungufu wa umeme unakadiriwa kuwa megawati 260 kwa sababu ya kukua kwa mahitaji ya umeme na kwamba mitambo hiyo itakapofungwa kutakuwa na nakisi ya megawati 100 na nyongeza itakayotokana na ukuaji wa mahitaji yanayokua kila siku.

  Bw. Malima alisema kuwa serikali imelielekeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kusimamia utaratibu wa kukodi mitambo Machi mwaka huu, ili kufidia uhaba wa megawati 260 uliopo sasa, na shirika hilo limekamilisha makubaliano ya kukodi mitambo ya megawati 100 mwishoni mwa Juni, mwaka huu.

  Wakizungumza na Majira nje ya bunge baadhi ya wabunge walisema wakati wa mjadala wa bajeti hiyo, watamtaka waziri huyo kueleza kila kitu kinachokwamisha umeme kupatikana hadi mgawo wa umeme kuendelea kila mwaka bila kupata suluhisho.


   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  [h=4] 1 Maoni:
  [/h] [​IMG]
  Anonymous said... atakoma na kuujua uchungu wa cheo
  July 12, 2011 11:27 PM

  [h=4]Post a Comment[/h]
   
 4. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sema chachu ya wafanyabiashara vijana waliomruzuku kikwete na kuchaguliwa kuwa mawaziri hiko wapi?

  jibu iko kwenye makampuni yao ofisi za serikali ni mapango ya biashara simple and clear
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  so it is a selfserving administration................................I agree entirely............
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wabunge wajipanga kumkabili Ngeleja
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 12 July 2011 21:56 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

  Habel Chidawali, Dodoma na Geofrey Nyang'oro, Dar
  KATIKA kile kinachoonyesha kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hauridhishi, baadhi ya wabunge wametahadharisha kuwa bajeti wa Wizara hiyo inayotarajiwa kusomwa kesho kutwa bungeni itakumbana na kingingi na huenda isipitishwe.Jana baadhi ya wabunge waliozungumza na Mwananchi walitahadharisha kuwa lazima bajeti hiyo ije na majibu ya uhakika kwa ajili ya kumkomboa mwananchi katika kupata huduma ya umeme na si kiini macho.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, anatarajia kuwasilisha bajeti yake kesho kutwa ambayo itajadiliwa kwa muda wa siku mbili na kuhitimishwa siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.

  Akizungumza na Mwananchi jana Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde (CCM), alisema bajeti hiyo lazima ije na majibu ya kutosha kwa wananchi, vinginevyo hatakuwa tayari kuipitisha kwa kuwa kufanya hivyo atakuwa akiwasaliti wapiga kura wake.
  Lusinde maarufu kama ‘Kibajaji’, alisema kma majibu ya Serikali itakuja mipango mingi isiyotekelezeka, safari hii haitavumiliwa na atakuwa mtu wa kwanza kuipinga.

  “Mimi kama mbunge ninayetoka chama tawala ni wajibu wangu kuipitisha bajeti ile, lakini siwezi kuipitisha kama haitakuwa na majibu kwa wananchi wa Mtera, kwa kuwa kufanya hivyo nitakuwa nawasaliti wapiga kura wangu ambao wanatoka kwenye chanzo cha umeme, lakini kazi yao ni kulinda tu,’’alisema Lusinde.

  Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi(CCM), alisema kama bajeti ya Nishati haitaleta majibu ya kutosha itazua mjadala mzito kwa kuwa kila mtu anaisubiri bajeti hiyo na kila mtu angependa kuichangia.Zambi alisema kelele za wabunge si tu kwamba wanataka kuonekana na kusikika, bali ni kutokana na Serikali kushindwa kuweka vipaumbele katika maeneo muhimu ikiwemo miradi ya maendeleo ambako kwa sehemu kubwa imekuwwa ikipangiwa fedha kutoka kwa wahisani bila ya kujua kuwa wanaweza kusitisha kutoa misaada.

  “Kwa mfano, wabunge wanataka kujua katika kipindi cha mwaka huu Serikali ilisema kuwa imewekeza fedha nyingi katika miradi ya umeme, kwa hiyo kama kipaumbele kimewekwa huko tunatarajia kuona mambo makubwa, vingine ukumbi wa Bunge hautatosha,’’alisema Zambi.
  Alisema Serikali itahitaji kuwa na majibu ya kutosha na yenye kuondoa mashaka kwa wananchi wanaotegemea kuona mambo mazuri kutoka ndani ya bajeti.
  Mbunge mwingine aliyeitahadharisha Nishati na Madini ni David Kafulila (Kigoma Kusini-NCCR), ambaye alisema hali itakuwa tete siku itakapowasilishwa bajeti ya Wizara hiyo.

  Kafulila alisema Wizara hiyo ni mboni ya jicho la Watanzania kwa hivyo kila mtu anategemea kuona mambo mazuri, vinginevyo ukumbi utakuwa ni mdogo siku ya Ijumaa na Jumatatu.Katika hatua nyingine, Chadema imemwandalia zengwe Waziri Ngeleja anayetarajia kusoma bajeti hiyo baada ya kusambaza waraka unaowataka wabunge wagome kuipitisha.Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa chama hicho kimeomba wabunge wagomee bajeti hiyo mpaka Waziri Ngeleja atakapokuja na mipango mbadala ya kumaliza tatizo la mgawo umeme.

  Kwa mujibu wa habari hizo ambazo baadaye zilithibitishwa na taarifa rasmi iliyoandikwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, kama Waziri Ngeleja hatakuwa na jipya, anapaswa kutangaza kujiuzulu siku hiyo ya bajeti.Kwa mjibu wa taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari, tatizo la mgao wa umeme linaloendelea hivi sasa ni matokeo ya udhaifu wa viongozi hao wa Serikali.

  Alisema hadi sasa Serikali imeendelea kutoa majibu yenye kukatisha tamaa kuhusu namna inavyoshughulikia tatizo la mgawo wa umeme na upungufu wa gesi asilia hapa nchini.“Leo (jana), Julai 12 mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ametoa majibu yenye kuthibitisha kwamba Serikali inaendelea kuachia mgawo huu mkubwa wa umeme na upungufu wa gesi asilia uendelee kwa muda mrefu zaidi,”alisema Manyika katika taarifa hiyo.

  Mbunge huyo wa Ubungo aliitaka Serikali kuwa taayari kujibu hoja zilizomo kwenye bajeti mbadala itakayowasilishwa na kambi ya upinzani bungeni na kutishia kuwa kama haitatoa majibu ya kuridhisha Chadema wataongoza maandamano nchi nzima.

  “Kambi rasmi ya upinzani itawasilisha bajeti mbadala yenye kutoa mwelekeo wa kulinusuru taifa katika sekta ya nishati na madini kwa mwaka wa fedha 2011/12, hivyo tunaitaka Serikali kutoa majibu ya kuridhisha…,” alisema Mnyika.

  Alisema Serikali kwa nyakati tofauti imeonyesha kuwa haina mikakati ya kutatua tatizo hilo huku akidai imekuwa ikitoa kauli za kumkingia kifua Waziri Ngeleja badala ya kuonyesha nia ya kutatua tatizo hilo.Manyika alikumbusha kwamba, Julai 6, 2011 Rais Kikwete alitoa kauli ya kumtetea Waziri Ngeleja kuwa si chanzo cha mgawo wa umeme, bali tatizo kuu ni kupungua mabwawa ya maji katika mitambo ya kuzalisha umeme.Manyika alisema kauli hiyo haikujibu hoja za msingi kuhusu umeme kwa kwa kuwa haikueleza hatua za haraka ambazo Serikali imechukua kuondokana na mgawo na upungufu wa gesi asilia.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  kwa bunge letu lilivyo sasa wala tusitegemee lolote upuuzi mtupu! hiyo party caucus ya ccm haina uzalendo hata chembe
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Ni kweli sera iliyopo ni chukua chako mapema.....................na njia rahisi ya kufanikisha azma hiyo ni kutomkuna mgongo wa mwenzio kwa kukosoa maovu.......................
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  katika khali iliyop[o hata huyu aonekana anafaa.....................

  [​IMG]
  Babu wa Samunge........................
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Hawa ndiyo viongozi wetu...............huhitaji kujua wanachofikiria masaa ishirini na manne......................

  [​IMG]
   
 11. s

  sativa saligogo Senior Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, thanx for your opinion lkn mbona wabunge vijana noa hujawafanyia tathmini? kisha wenye asili ya kiasia je?? Kimsingi nakualiana nawe lkn hata kama ungekua ww ktk nafasi kama hiyo ingeenenda tofauti nao??? kumbuka mfumo uliopo wa serkali ya ccm hata uwe na ngivu za akina musollin/plato nafasi ya kuibuka haipo, nn kilimpata pinda juu ya mashangingi??? nn kilimpata magufuli na bomoabomoa ww shahidi!!!
  Usilaumu ulipoangukia bali ulipojikwaa!!!!!!
  ok now, Who the cap fit in 2015?????
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  +1 #8 Ignace 2011-07-13 10:33 Huyu Ngeleja amejaa siasa tupu, mambo yake mengi anayoongea yanapingana kabisa na masuala ya kiufundi na kitafiti. Mi kwa kifupi yani sina imani naye..!
  Quote

  +1 #7 dude 2011-07-13 10:26 We are tired with the ongoing power problems.Ngeleja you better hang down your boots. We are fed up, tumechoka na story za kisanii kila siku, huna jipya and i believe hivi sasa Rais ana work out kutafuta sabstitute. Umepandikizwa na mafisadi.
  Quote

  0 #6 mabuwe 2011-07-13 09:52 HEY, WAH. ZITTO.KAFULIRA.LISSU.WENJE,MSIGWA.SUSAN.MDEE, FUNGENI MIKANDA HUYO MH WILLIAM AKIONE CHA MOTO TUMCHOKA GIZA.
  Quote

  0 #5 Haika 2011-07-13 09:40 Namshangaa sana huyu waziri na wakurugenzi wote walio chini yake!! kama suala la umeme limewashinda, hata kupanga ratiba ya mgawo na ikafuatwa nayo mmeshindwa!!?? jamani hivi tunaongozwa na viongozi gani wamesoma vyuo gani? MUNGU TUSAIDIEE, MUNGU TUNAKUOMBA UINGILIE KATI MAANA HIINCHI WATU WA CHINI HATUNA HAKI.AMEN
  Quote

  -4 #4 john 2011-07-13 07:43 ni siasa ndio iliyotufikisha hapa tulipo kwa mgawo wa umeme

  watanzania tulikubali wanasiasa waaeke siasa zao kwenye maamuzi ya umeme kwa masilai yao ya madaraka kwa kuchafuana

  chanzo cha matatizo ya umeme ni sitta na makwembe waliotumia swala la umeme kuwachafua wengine kwa masilai yao ya madaraka na kufanya serikali kuwa na ugonjwa ya uoga
  walisema bora nchi iwe gizani kuliko kununua mitambo ya dowans au kununua umeme kutoka dowans na watanzania kushabikia bila kutambua lengo lao ni kuwachafua wengine

  sitta na makwembe tubuni kwa yote mliotufanyia mpaka sasa wengi wanakosa kazi na kipato kwa sababu ya ubnafsi yenu
  Quote

  +4 #3 Rosh 2011-07-13 05:52 Eti 'wabunge wanatishia kutoipitisha budget ya wizara isipotoa majibu ya matatizo ya wananchi'..upumbaf mtupu..Je kuna hata kitu kimoja kibaya ninyi wabunge wote mlichoweza kukizuia cha kumtetea mwananchi maskin wa Tz toka mlipochaguliwa?..kazi yenu imekuwa kula posho, kutoka vitambi na kusinzia bungeni..hamna hata roho ya huruma mnajiongezea posho, magari ya kifahari kwa kazi ya kusign daftari la mahudhurio.!
  Quote

  0 #2 mdau 2011-07-13 02:15 tunakusubiri vijana wetu waje kukukamua utuelezi vizuri umefikia wapi maana umeme hatuna madini ndio hayo yanakwambo mpaka ina semeka madini ya nyuklia yanayotumika IRAN ya kutengenezea umeme yanatokea bongo na utuambie miaka yako yote uliyoka wizara hiyo umepunguza nn ktk shida ya umeme,
  uwekezaji =unahitaji umeme umeme hamna kaka,ccm tuangaline cc walala hoi ipo siku tutakuja kuonana wabaya tumechoka jamani
  Quote

  +4 #1 Rich 2011-07-13 01:56 Mhe Zitto alipendekeza serikali kununua mitambo ya umeme wa Dowans (na IPTL), lakini badala yake imeacha Symbion ya Marekani kununua ili watz waendelee kulipa capacity charges na kununua umeme. Alichotuachia Baba wa taifa Nyerere (kidatu)ndiyo mtambo wa uhakika mpaka leo miaka hamsini ya uhuru.
  Quote  Refresh comments list
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  I like this..............Usilaumu ulipoangukia bali ulipojikwaa!!!!!!..................................tatizo ya hii hoja ni kuwa tunaburuzwa na hoja za kitapeli tapeli hivyo inabidi tuzinduke na kujiuliza hawa vijana wana mwakilisha nani? Mbona hawana chachu zaidi ya kujilimbikizia mali
   
 14. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tunahitaji system ambayo kiongozi wa umma anakuwa accountable kwenye eneo lake, hata kama ni rais wa nchi. vinginevyo utateua mpaka serengeti boys na bado hakuna kitakachotokea. lkn head of state akiwa accountable the rest watakuwa accountable na hapo age zao will not be an issue
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Huo ujana unaouona kwa kuangalia sura na umri ni magamba tu ndugu yangu. Ukiyavua hayo magamba hawa jamaa uliowataja hawana tofauti na Kingunge au Wassira kwa uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo.
   
 16. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngeleja analinda masilahi binafisi ya JK na bosi wake Rostame Aziz. Mwenye namba za simu za Ngeleja amuulize kama alipata mgao kutokana na mauzo ya Dowans kwa Symbion Power.
   
Loading...