GE2025 Chacha Heche: CHADEMA pekee yake ndiyo mshindani wa CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara, Chacha Heche, amesema kuwa hadi sasa chama pekee cha upinzani chenye uwezo wa kuibana CCM kisiasa na kulazimisha mawazo mapya ni CHADEMA pekee, akisisitiza kuwa hakuna chama kingine cha upinzani chenye ushawishi na nguvu sawa na CHADEMA.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu ya CHADEMA Family jijini Musoma, Heche amesema: “Mshindani anayeweza kusababisha CCM ilale iwaze uchaguzi ni CHADEMA pekee, hakuna chama kingine.”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Heche ameendelea kueleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kulinganisha harakati za sasa na TANU, lakini kwa mtazamo wake, CHADEMA imepitia mapambano makali zaidi kuliko chama chochote cha kisiasa kilichopata kutokea nchini.

Heche amelenga kufafanua kuwa uhuru wa pili unaozungumzwa na CHADEMA ni pamoja na uhuru wa kweli wa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kupitia uchaguzi huru na wa haki.

View attachment 3401311
Ukweli na uwazi
 
yaani leo chadema inajiona kuwa harakati zake zipo juu zaidi ya harakati za TANU?
duuuh! huu ukoo wa heche utatudanganya hadi lini?

#KATAA VIBAKA WA KISIASA
#KATAA MATAPELI WA KISIASA
#OKTOBA TUNATIKI

..kwani uongo?

..Mwalimu Nyerere hana jeraha hata moja kutokana na harakati za kudai uhuru.

..pia hakukaa mahabusu hata siku moja kwa ajili ya kuwadai Waingereza uhuru.

..sasa jiulize viongozi wangapi, na wanachama, wa Cdm wameuwawa, au kujeruhiwa, na serikali ya Ccm.
 
Kwamba Mkoloni Mweupe alikuwa na nafuu?
 
Hapa ndo upumbavu wa chadomo ulipo kwa kuamini kuwa ili kuwa mpambanaji mzuri lazima ujeruhiwe..huu ni ujuha mwingine,
Kwani kipimo cha kuwa mwana chadomo lazima uwekwe remande?
 
Kwamba Mkoloni Mweupe alikuwa na nafuu?

..Ndio! Ndio! Ndio!

..Vyombo vya dola vya Waingereza ktk koloni la Tanganyika vilikuwa na utu na maadili kuliko jeshi letu Polisi.

..Waingereza waliendesha chaguzi mbili kabla ya uhuru wa Tanganyika, na hakuna mgombea hata mmoja wa Tanu aliyeenguliwa, au kuibiwa kura.

..Kwa hiyo mamlaka za uchaguzi za Wakoloni zilikuwa na uadilifu kuliko Tume za uchaguzi zilizoundwa na Ccm.
 
Hapa ndo upumbavu wa chadomo ulipo kwa kuamini kuwa ili kuwa mpambanaji mzuri lazima ujeruhiwe..huu ni ujuha mwingine,
Kwani kipimo cha kuwa mwana chadomo lazima uwekwe remande?

..Ni upumbavu, ujuha, na ukatili, wa Ccm, na vyombo vyake vya dola, kuwauwa, na kuwajeruhi, wanachama wa Chadema.
 
Ni upumbavu na ujuha kuamini kuwa watu wa chadomo kila anayepotea na kufa eti utasikia ameuliwa na polisi..
Chadomo hawana utakatifu wowote..
 
..kila mwanachadema aliyepotea Polisi ndio wanahusika na ndio maana hakuna mhusika yeyote aliyekamatwa. Polisi wangekuwa hawahusiki, basi angalau kungekuwa na matukio ambapo wahusika wamekamatwa.
 
..kwani uongo?

..Mwalimu Nyerere hana jeraha hata moja kutokana na harakati za kudai uhuru.

..pia hakukaa mahabusu hata siku moja kwa ajili ya kuwadai Waingereza uhuru.

..sasa jiulize viongozi wangapi, na wanachama, wa Cdm wameuwawa, au kujeruhiwa, na serikali ya Ccm.
usimlinganishe Mwalimu J.K Nyerere na Wengine..Yule alikuwa anatumia akili nyingi na jicho la tatu..CHADEMA akili kidogo nguvu nyingi ikiambatana na kulazimisha mambo.
 
..namkubali sana Mwalimu Nyerere.

..lakini ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba vyombo vya dola vya Ccm vimeteka, vimetesa, vime*fira, na kuuwa, kuliko vyombo vya dola vya Wakoloni wa Kiingereza.

..hivi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere angekuwa hai halafu akisikia mambo ya hovyo, kama mauaji, na ufi*raji, yanayofanywa na vyombo vya dola vya Ccm unadhani angefanya nini? Je, angekaa kimya, na kusifia " mama anaupiga mwingi"?

..Mwisho, wakoloni walimfungulia Mwalimu Nyerere kesi moja tu ya uchochezi. Sasa jiulize ni kesi ngapi Ccm wamewafungulia viongozi wa upinzani.

..Cuf, Juma Duni, na wenzake, walifunguliwa kesi ya uhaini. Freeman Mbowe alifungwa, na baadae kufunguliwa kesi ya ugaidi. Tundu Lissu ndiyo huyu ana kesi ya uhaini ya mtu mmoja.

..Sijalinganisha akili, na uanazuoni wa Mwalimu na viongozi wa upinzani. Nimelinganisha mateso, udhalilishaji, na dhuluma, alizopitia Mwalimu, na yaliyowatokea wapinzani. Ukweli utabaki kuwa ukweli.
 
[/QUOTE]kwasasa siasa inafeli pakubwa, si upinzani wala chama tawala kwakuwa wananchi tunapewa upofu hatujui undani wake ndo maana mimi kwasasa naona bora kusiwepo vyama vya siasa nchini basi ikishindikana kibaki chama kimoja tu TANZANIA BILA VYAMA VYA SIASA ITABAKI NGANGARI.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara, Chacha Heche, amesema kuwa hadi sasa chama pekee cha upinzani chenye uwezo wa kuibana CCM kisiasa na kulazimisha mawazo mapya ni CHADEMA pekee, akisisitiza kuwa hakuna chama kingine cha upinzani chenye ushawishi na nguvu sawa na CHADEMA.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu ya CHADEMA Family jijini Musoma, Heche amesema: “Mshindani anayeweza kusababisha CCM ilale iwaze uchaguzi ni CHADEMA pekee, hakuna chama kingine.”

Heche ameendelea kueleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kulinganisha harakati za sasa na TANU, lakini kwa mtazamo wake, CHADEMA imepitia mapambano makali zaidi kuliko chama chochote cha kisiasa kilichopata kutokea nchini.

Heche amelenga kufafanua kuwa uhuru wa pili unaozungumzwa na CHADEMA ni pamoja na uhuru wa kweli wa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kupitia uchaguzi huru na wa haki.
View attachment 3401587
Chanzo: Jambo tv​
To be honest , hii familia imebarikiwa, ndo maana, Mama Heche husema , anawaombea watoto wake tu , na yule anaonekana ni mpole sana , kwake hapendi watoto wake kuwa kwenye siasa ,ila anaamini nature ilishaamua ndo maana anasema kazi yake ni kuwaombea.

Sasa ukiangalia famili ya uzazi wa Heche ,ni watu wa dini tena wasabato, Lissu hivyo hivyo tena , familia ya lissu yupo mchungaji, lema mnamjua vizuri, alimwambia Maghufuli Mungu amemwambia utakufa, akapewa kesi , ndo hivyo .

Itoshe kusema tu ,Mungu yupo kazini kulinda chama cha Chadema kwa Gharama kubwa sana katika ulimwengu wa kiroho usio onekana , so shindana na hili mtapukutika sana ,asema Bwana
 
Back
Top Bottom