Blasio Kachuchu
Senior Member
- Sep 7, 2016
- 153
- 111
Moja ya Habari iliyotamba kwenye duru la michezo na kwenye mitandao ya kijamii nchini mwishoni mwa wiki ni klabu ya soka ya Simba kumpata Afisa Mtendaji Mkuu mpya mwanamke , Barbara Gonzalez.
Barbara Gonzalez, mbali na wadhifa huu mpya katika klabu hii kongwe ya soka nchini ni mfanyakazi wa kampuni ya bia Tanzania (TBL) akiwa anashikilia nafasi kubwa ya Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano (Legal & Corporate Affairs Director).
Kwa nafasi kama hii kwenye kampuni kubwa ambayo ina hisa za watanzania wenye itikadi na mapenzi kwa vilabu vya timu mbalimbali, kutumikia klabu ya Simba wakati huohuo kuwa Msemaji na Afisa wa ngazi ya juu wa kampuni anayeunganisha kampuni na Serikali,taasisi na wadau mbalimbali, kuna mgongano wa maslahi ambao unaweza kwa kiasi kikubwa kuathiri kampuni.
Natoa wito kwa watendaji wenye nyadhifa za juu kwenye makampuni ya umma na binafsi ambayo yameuza sehemu ya hisa zake kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye ajira za vilabu vya soka maana masuala ya michezo yana mambo mengi, mpaka wakati wengine kuna misukosuko ambayo kiongozi wa klabu akiipata inaweza pia kuhusisha mwajiri wake.
Barbara hongera kwa kujitoa mhanga kuongoza klabu ya soka ila acha kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja,chagua kuwa CEO wa Simba au Mkurugenzi kwenye kampuni ya TBL