demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,250
- 15,116
Wanajamvu huyu mwanadada huwa sijawahi kabisa kumuelewa.
Tangu apate ile nafasi pale Simba SC naona kama amewarudisha sana nyuma wale Jamaa. Hakuna jambo amefanya ambalo mwanasimba anaweza kuona umuhimu wake.
Mwenzake Senzo ana mafanikio ambayo yanaonekana na kuelezeka.
Sasa huyu mwanadada kila atakacho gusa ni lazima kiishie kati.
Alikuja na mkakati wa Kikaragosi Cha Simba SC mwisho wa siku kikaragosi chenyewe hakionekani tangu wadau wadai kuwa kinawatisha watanzania.
Alikuja na mpango wa kuchangisha pesa za uwanja, ikafika hatua wakakusanya mil 60 tu ndani ya miezi 3. Na mkakati huo ukaishia hapo hapo.
Yeye alihusika pakubwa kwenye kuongoza jopo la kumpata kocha mpya. Akakurupuka wakaleta. Didier GOMES Da Rosa. Na sasa kawapoteza mazima na kasepa.
Leo Ameita waandishi wa habari waongozane naye kwenda Bunju ili wachukue tukuo zima ambapo Architect akichukua vipimo. Tena wakiwa wamevaa Reflectors na Helment kabisa.
Sasa unaanza kujiuliza huo ujenzi utaanza kwa kutegemea pesa ya kampeni ya NaniZAIDI? Yaani milioni 101 kweli ndio za kumfanya mtu aanze kutafuta mkandarasi?
Huyu Dada ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwa CEO SENZO wa DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS.
Kama kuna jambo lolote ambalo amefanikiwa ndani ya miama yake 2 akiwa pale naomba mnitaarifu nimekaa pale nasoma Comments zenu!