Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
kumekuwa na tatizo kubwa la kutopeleka fedha kwa wakati kwenye halmashauri zetu.halmashauri zinatumia muda na pesa nyingi kupanga bajeti lakini fedha za bajeti zimekuwa zikicheleweshwa au kukatawa kabisa.baadaye tunalaumu halmashauri zimeshindwa kutumia fedha lakini ukweli ni kwamba fedha zilzopangwa kwa maendeleo hazifiki kwa wakati na mwisho wa siku halmashauri inatakiwa kuonyesha mchanganuo wa matumizi yake bila kujali imeletewa lini fedha hizo.huu ni unyanyasaji kwa halmashauri zetu,leteni fedha kwa wakati na kama ilivyo kwenye bajeti vinginevyo huu ni uonevu na ukiritimba usiokuwa na maana.