'Cement' na wamachinga, lipi muhimu?


F

FENOVA

Member
Joined
Oct 1, 2016
Messages
51
Likes
106
Points
40
Age
47
F

FENOVA

Member
Joined Oct 1, 2016
51 106 40
Ndugu zangu,

Nimemsikia Mheshimiwa JPM akitoa kauli nzito kuhusu Wamachinga wanaofukuzwa katikati ya miji pia kutoa onyo kwa watendaji wanaowabugudhi Wamachinga hao.

Sina pingamizi na maagizo ya Rais na ninamuunga mkono. Lakini nikiwa kama Mtanzania Mzalendo na ninaipenda Nchi yangu, napenda kuona Nchi yetu inaongozwa kwa Ubora na kwa Kuzingatia Mambo muhimu yenye Faida na Nchi yetu na Wananchi kwa Ujumla wake.

Kwa mtazamo huu na kutoka na hali ya kiuchumi inayo endelea nilitegemea kusikia kauli ya Mh.Rais kuhusu suala la DANGOTE kwani linamgusa kila Mwananchi na Uchumi wa Nchi kwa Ujumla Lakini hadi Leo hii na Baada ya CEMENT kupanda toka elfu 11 hadi elfu 17 sijasikia kauli yoyote toka Serikali Kuu zaidi tu ya Maelezo toka kwa watendaji yasiyo kuwa na mashiko.

Cha kusikitika zaidi Watanzania wengi tunaishii kwa kuongozwa na matukio ya kila siku hasa yasiyo kuwa na Faida yoyote kwa Nchi yetu na ndiyo maana niliposikia Mh.Rais akitoa kauli kali zidi ya zoezi la Wamachinga kutolewa Mjini nilianza kutafakari na kujiuliza kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya 5 na Je wao kama Serikali nini kipaumbele Chao katika utendaji wa kila siku ??? Ndugu wadau wenzangu naomba tujadili hili kwa upana zaidi na kwa uzalendo bila kuingiza munkari wa kisiasa.

Nini muhimu na kinacho changia maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa. Je Kiwanda kama cha DANGOTE au WAMACHINGA mijini. ! Nawasilisha ...
 

Forum statistics

Threads 1,272,951
Members 490,211
Posts 30,465,560