Celebrity wa Afrika Akisubiriwa Kwenye Ngazi za Uwanjani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Baba na mama Sama goal wakimsbiri mtoto wao kwenye ngazi za uwanja wa ndege akitokea Nigeria alikoshinda tuzo ya wanasoka wa ndani Afrika

12376181_1497105377262647_8418277203726386907_n.jpg
 
Huku.kufika saa 8 usiku kuna maanisha nini kama sio FITINA? Hakuna ndege za kufika asubuhi au mchana?
 
Saleh Jembe kaandika;

Mfano mzuri ni picha hii inayomuonyesha mzazi wa mwanasoka maarufu zaidi nchini Mbwana Samatta akiwa amekaa kwenye ngazi za uwanja wa ndege kumsubiri mwanaye awasili.

Ally Samatta alikuwa na furaha ya mwanaye kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa wanaocheza Afrika. Aliwasili saa nane usiku, lakini mzee alikuwa pale.

Kila mmoja anajua juhudi binafsi za mzee huyo kumsaidia mwanaye kufikia hapo alipo. Wengi tumemjua baada yam zee huyo na familia yake kupambana tokea mwanzo, mimi ninaamini anastahili heshima kubwa ya mzazi na mlezi bora kabisa.

Hakuna kiongozi wa Fat, TFF, Simba au kwingine aliyewahi kumsaidia wakati akipambana kwa ajili ya Mbwana.

Ameleta heshima kubwa kwa taifa kupitia mwanaye, lakini leo anafikia kwenye ngazi ambazo nadiriki kusema alikaa chini uwanja wa ndege.

Hoja yangu iko hivi, kweli Mzee Samatta hasitahili kutumia sehemu ya VIP ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere?

Nauliza tena, unawajua wangapi waliorejea nchini na kuitumia sehemu hiyo wakiwa hawana kubwa walilotoa kwa ajili ya taifa letu. Kungekuwa na ubaya gani Mzee Samatta angekaa kule wakati akimsubiri mwanaye, halafu wangeungana na watu wengine wakati akitoka nje?

Mara ya mwisho, niliona wakienda kumpokea Kocha Mart Nooij upande wa VIP ambao waliomba ili afikie wakati anawasili. Vipi Baba Samatta na familia yake waonekane hawafai na kwenda kukaa chini?

Hata kama wanatokea Uswahilini kwetu, lakini heshima yao wanastahili kupewa. Viongozi wa TFF wanaonekana hawajali, waliona ni jambo la kawaida tu.
 
Ninawakumbusha, hili ni kati ya mambo zaidi ya mia ninayoonyesha uozo, upuuzi, ubabaishaji na mambo ya hovyo kwenye mpira wetu.
Kama inashindikana uandaaji wa hili la kishujaa la Samatta, nani anasema tunaweza kufanya maandalizi bora ya ukuzaji wa vijana yanayohitaji miaka na uvumilivu wa juu?
TFF hawawezi kulikwepa hili, najua watasema hatukujua lolote, lakini lingekuwa suala linahusisha fedha, wangekuambia sisi ndiyo wasimamizi wa mpira.
Sasa suala la Samatta wakati wa mapokezi yalihusiana na riadha, netiboli au ngumi za kulipwa? Wao walikuwa wapi?
Halafu siku chache, utasikia TFF wameandaa hafla na kumwalika Mzee Samatta na familia yake eti kwa heshima.
Kama hilo limeshindikana, nani anaweza kusema eti kwa viongozi hawa, tunaweza kuwa na ligi bora kabisa yenye ushindani na muonekano bora wakati inahitaji maandalizi ya juu kabisa?
 
nooij tua.JPG

NOOIJ ALIPOKELEWA VIP, HAKUWA AMEIFANYIA LOLOTE TANZANIA NA ALIONDOKA BILA YA KUFANYA LOLOTE. HAPA AKIWA NA VIONGOZI WA TFF WALIOFANYA MIPANGO AFIKIE HUKO.
 
Huyu malinzi ni wa kujiuzuru na kwa hali hii soka letu haliwezi kuimarika huyu abaki kuwa rais tweeter na sio soka maana kama ata mapokezi ya samata yamepangwa na caf sio tff wangepanga tff asingefika usiku wa manane kama mchawi malinzi ata babu tale amekushinda alipanga mapokezi ya diamond vizur
 
Wanawake wa kitanzania sijui huwa mkoje!! Siyo mama Kanumba, mama Diamond mama Hasheem Thabiti!! Khaa yan mwanao akipata jina tu majanga!! Emb ona huyo mama alivyovaa Kiswahili! Limiwani lote hilo na uzee huo ni aibu!!!

Hawa ndo wanaongozana na wanao kwenda club kutengeneza skendo za kwenye magazeti na upashukuna mwingii!! Wanahamia kwa watoto wao na kuwaacha wazee wakisota kwenye vibanda na kwenda kuwa waamuzi wa mambo!! Hovyo kabisa!!

Dah hata kuwaweka pale kwenye ngazi ni huruma tu!! Huyu mama alistaili kuwekwa nje ya eneo la uwanja kabisa!!
 
HII NI AIBU SASA, nimeona mapokezi ya Aubemeyang, kwa kweli tunatia aibu! Kiasi fulani! TFF, wizara ya michezo, HIVI KWELI MPO? Picha hii inaonyesha jinsi mlivyojipanga/ tulivyojipanga kuhusu zoezi zima la kumpokea Samatta! Sitashangaa siku moja Samatta akaja sema maneno yaliyosemwa na Yaya Toure kuhusu Afrika, na kwa Samatta kuhusu Tanzania! SHAME ON US!
 
Back
Top Bottom