Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 255
Mheshimiwa 'Spika' naomba kutoa taarifa kuwa mashindano ya CECAFA yamefanyika na kukamilika kwa muda uliopangwa. Aidha timu ya Azam ilitolewa na El-Merreikh na kwamba hao El-Merreikh wameifunga timu ya APR 1-0 katika mchezo wa fainali. Kwa matokeo hayo El-Merreikh wamevikwa taji la ubingwa wa Vilabu vya Musonye Afrika Mashariki na Kati mwaka 2014.
Mheshimiwa 'Spika' naomba kutoa hoja.
Timu ya Azam FC leo tarehe 08. 08. 2014 inajitupa kiwanjani hapa mjini Kigali Rwanda katika mchezo wake wa Kwanza dhidi ya Rayon Sport, katika mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENG CUP.
Wanaotuwakilisha leo ni hawa hapa
1. MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. GADIEL MICHAEL
4. DAVID MWANTIKA
5. AGGREY MORIS
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. JOHN BOCCO
10 KIPRE TCHETCHE
11. KHAMISI MCHA
AKIBA
AISHI MANULA
MUDATHIR YAHYA
SAID MORAD
ABDALLAH KHERI
FARID MUSSA
DIDIER KAVUMBAGUMungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Azam FC.
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
Yanga SC ilitakiwa hadi jana jioni kuwa imethibitisha na kutuma kikosi, lakini haikufanya hivyo na CECAFA ikawasiliana na TFF kuwaambia wapeleke timu nyingine iliyo tayari, ndipo zali likawaangukia Azam FC.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Mabingwa; Azam FC wamechukua nafasi ya Yanga SC Kombe la Kagame[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Yanga SC ilitaka kupeleka kikosi cha vijana kwenye nashindano hayo, jambo ambalo CECAFA waliwakatalia wakiwaambia hiyo si michuano ya watoto.
Azam FC, mabingwa wa Tanzania Bara, sasa wanaingia Kundi A katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame ya 40 pamoja na wenyeji, Rayon Sport, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L'Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital'O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Timu 14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo kuanzia Agosti 8 hadi 24 mwaka huu- jumla ya mechi 34 zikichezwa katika viwanja vya Amahoro na Nyamirambo, Kigali.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
Wizara ya Michezo ya Rwanda na mashirika mengine yatadhamini michuano hiyo, itakayokwenda sambamba na maazimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbari.
Televisheni ya kulipia ya Supersport ya Afrika Kusini ambao ni maswahiba wa muda mrefu wa CECAFA, ni miongoni mwa wadhamini pia na wataonyesha mechi zote za michuano hiyo moja kwa moja.
Kwa kuwa Azam imechukua nafasi ya Yanga, sasa itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka huu, mchezo ambao utatanguliwan na mechi kati ya KMKM ya Zanzibar na Atlabara ya Sudan Kusini.
Azam FC itarudi tena dimbani, Agosti 10 kumenyana na jirani zao KMKM, kabla ya kucheza na Atlabara Agosti 12 na kukamilisha mechi za kundi lake, kwa kumenyana na Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
Chanzo: BinZubeiry Blog
we nadhani ni moja ya viongozi wa ile timu inayohonga mil150 ili tu kushinda ligi kuu ya mil70. Mapovu naona yanakutoka na mwaka huu utakonda sana,utahonga na utapigwa
Sour grapes if you ask me!
Simba walishika nafasi ya 4 hawawezi kufikiriwa hata kama Azam wangegomaDakika za mwanzoni tu Azzam FC mabingwa wa Tz Bara wapo uwanjani dhidi ya mabingwa wa Kagame Cup, Rayon Sports. Vijana wamelitembelea lango la wapinzani mapema. Mungu awafanikishe ili muendelee kuwafundisha soka wakongwe wa siasa la soka (Ndala) ambao wametimuliwa katika kombe hili kwa kuleta mizaha ya akina Akili utajiri waliowarithisha hata makocha wenye majina ya ajabu ie; Machisimo. Simba wasingefanya ujinga huu
my friend, umeona walivyoboronga, hakuna mtz hata mmoja aliyefanya vizuri, yule muaivoricost tu ndio kajaribu sana, na kati ya watu ambao huwa sisapoti wawepo hata timu ya taifa stars ni mtu mmoja anaitwa joni boko, ni mrefu na ana umbo la mpira lakini hautumii mwili wake, na hana stamina, si mwanamichezo mzuri kwa kifupi.Simba walishika nafasi ya 4 hawawezi kufikiriwa hata kama Azam wangegoma
Sour grapes if you ask me!
Hawa wawakilishi wa TFF katika BONANZA LA MUSONYE wanafnya kazi ya kubutuabutua tu dk ya 45 bado bilabila. Mashabiki kiduchu,nadhani Musonye mwakani ataileta Tanzania.
Fungu la kukosa.
Hawa wawakilishi wa TFF katika BONANZA LA MUSONYE wanafnya kazi ya kubutuabutua tu dk ya 45 bado bilabila. Mashabiki kiduchu,nadhani Musonye mwakani ataileta Tanzania.
Huku asije kabisa, kuna watu wataunda Kamati iitwayo: 'Saidia Musonye afe mapema'. Inambidi asome majira, akijileta kizembe itakula kwake.
Yes. What did you expect?Rayon 0-0 Azam, right?