Waziri mkuu Pinda amefanya ziara isiyokuwa na miguu wala kichwa nchini Uingereza. Akiwa huko alipata habari za uwepo wa mkutano wa wanachadema uliongozwa na Wenje amabye ni mkurugenzi wa mambo ya nje wa CDM na Munishi ambaye ni katibu Mkuu wa BAVICHA.
Habari zilizovuja zinasema Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA" siku ya Jumanne ya terehe 16/10/2012 ubalozini baada ya kusikia CHADEMA wamekutana ijumaa iliyopita na kuazimia kuisambaratisha CCM Uingereza.
Katika mkutano huu walijitokeza watu wasiozidi 15 na taarifa za ndani zinadai Pinda ametamka ndani ya kikao hicho kuwa CHADEMA ni "KIBOKO" kwani siku za nyuma walizoea kupata mapokezi makubwa yenye mbwembwe kama viongozi wa serikali lakini baada ya CDM kujikita nje kwa siku za hivi karibuni , hali hiyo imetoweka na kuwaduaza viongozi wa serikali.
Ikumbukwe wiki tatu zilizopita, makamu wa rais Gharibu Bilal alifanya ziara kama hiyo nchini Uingereza na kuambulia patupu.
Viongozi wa CDM walifanya mkutano wao tarehe 12/10/2012 jijini London na kukusanya idadi kubwa ya watu kutoka miji ya Reeding, Birmingham na London na baadhi ya watanzania waishio huko walijiunga na CDM.
Source: Mtanzania aliyekuwapo mkutanoni kwenye ubalozi wa Tanzania London.
Ukweli husemwa:
Wewe ndiyo umekurupuka bila kuisoma post yake vizuri. Amesema, Waziri Mkuu hayuko UK kwa shughuli za kisiasa na wala hajafanya mkutano wa kisiasa.
ok.. ningesema hizi...Mh. Pinda alikutana na Watanzania waishio Uingereza na kuzungumzia mustakabali wa maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, n.k. It does not matter whether or not huo mkutano ulikuwa wa kisiasa. Kinacho-matter ni kwamba whether or not alizungumzia mambo ya kisiasa kwenye huo mkutano hata kama ulikuwa ni wa kidini.
Sikuzumgumza 'subjectively' intentionally lakini kwa kujibu yaliyoulizwa na scolari...
Ukweli husemwa:
Watanzania bana.
Ndiyo maana nchi yetu imefika hapa ilipo. Wananchi Wengi ni waongo, wanasiasa ndiyo usiseme.
Tunakuwa wachakajuaji na waongo wa kupindukia. Kumbuka ukweli mara nyingi husimama pale penye uongo. Unaandika uongo ili kuwafurahisha watu humu JF. Ninaamini umeandika wakati moyo unakusuta na full of guilt conscience.
Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye huo mkutano na watu naweza kusema walikuwa ni zaidi ya 50. Halafu naomba ujue UK siyo Tanzania. Watu wengi huku maisha ni kazi na kazi mara nyingi watu wengi wanamaliza kazi saa kumi na moja za jioni, halafu siku hiyo ilikuwa ni jumanne.
Tujaribu kuwa wakweli angalau hata kidogo.
Habari na makala yako imejaa maneno ya udaku.
Na wewe inabidi ufikirie critically sometimes. The fact kuwa haukuwa mkutano wa kisiasa haina maana kuwa hakuzungumzia mambo ya kisiasa.
Katika kuhitimisha hotuba yake Mh. Pinda aliongelea hali ya kisiasa nchini. Kwa mfano, alizungumzia matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala, na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya kutisha ya RPC Barlow.
Hata hivyo, mleta mada kudai eti walikuwepo watu 15 tuu kwenye mkutano ni uongo mtupu. Propaganda za Chadema huko UK wabaki nazo huko huko.
Ukweli husemwa:
Watanzania bana.
Ndiyo maana nchi yetu imefika hapa ilipo. Wananchi Wengi ni waongo, wanasiasa ndiyo usiseme.
Tunakuwa wachakajuaji na waongo wa kupindukia. Kumbuka ukweli mara nyingi husimama pale penye uongo. Unaandika uongo ili kuwafurahisha watu humu JF. Ninaamini umeandika wakati moyo unakusuta na full of guilt conscience.
Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye huo mkutano na watu naweza kusema walikuwa ni zaidi ya 50. Halafu naomba ujue UK siyo Tanzania. Watu wengi huku maisha ni kazi na kazi mara nyingi watu wengi wanamaliza kazi saa kumi na moja za jioni, halafu siku hiyo ilikuwa ni jumanne.
Tujaribu kuwa wakweli angalau hata kidogo.
Habari na makala yako imejaa maneno ya udaku.
Kimsingi mleta mada ana kiwanda cha uongo. Kwa mfano anasema kuwa Mh. Pinda aliamua kumshinikiza Balozi wa Tanzania Uingereza kuitisha mkutano wa wana CCM kwa mgongo wa jina "WATANZANIA".
Ina maana hao wana CCM wasingekuja kama angeitisha mkutano wa Watanzania?
Ina maana wana CCM walingizwa mkenge kuwa utakuwa mkutano wa CCM kumbe ni Watanzania?
Hivi wana CCM UK siyo Watanzania eh?
Na Wana Chadema je?
Vi vema wewe umesema labda wataacha longolongo na chumvi chumvi....
Sidhani kama unajua unachoongea au upo kwenye majonzi baada ya Ponda kukamatwa! kwanza unafahamu UK yote acha England kuna watanzania wangapi jumla??Kama hujui nitakupatia statistics za Watanzania wote waliopo UK!
haha ha uingereza uijue wewe?? usiniache hoi! mm siwezi kuijua moshi sana maana huwa naenda tu kikazi au kwa matembezi! ila uingereza huwezi kunificha kitu, naifahamu maana nimesoma elimu yangu yote humo!!wewe kama waja na kuondoka sisi twaishi humu!Utanipatia statistics wewe balozi wa Tanzania nchini Uingereza? Halafu kuhusu Uingereza kaa kimya kabisa Uingereza naijua kuliko wewe unavyoijua Moshi.
Vipi una viwanda vingapi vya uongo?
kwanza uingereza magaidi hawaruhusiwi!!Utanipatia statistics wewe balozi wa Tanzania nchini Uingereza? Halafu kuhusu Uingereza kaa kimya kabisa Uingereza naijua kuliko wewe unavyoijua Moshi.
Vipi una viwanda vingapi vya uongo?
Chadema bana badala ya kujenga chama vijijini mnakimbilia London.
Chadema bana badala ya kujenga chama vijijini mnakimbilia London.