CDM; Kwa nini ishindikane? Nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM; Kwa nini ishindikane? Nini kifanyike?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gagurito, Mar 11, 2011.

 1. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ndugu wanaJF wenzangu, natumai mu wazima wa afya jema na mpo tayari kubadilishana mawazo km kawaida yetu.
  Napenda kuanza kwa kuwatakeni radhi pale mawazo yangu yatakapo contradict na uelewa wenu, Haya ni mawazo binafsi yatokanayo na uelewa wangu.
  Ndugu wanaJF nitambuavyo mimi na ndivo ilivyo ni kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo CDM kimapatwa kuungwa kwa wingi na wasomi, wanazuoni, wananchi na wafanyakazi wenye uelewa mkubwa wa mambo, isitoshe wabunge wake karibia wote ni wasomi walio na shahada katika fani na taaluma mbali mbali.
  Ndugu wamaJF nadhani ninyi ni mashaidi, ktk siku za karibuni CDM kiliandaa Maandamano yaliyopokelewa vilivyo na wananchi hasa wale wa Kanda ya Ziwa, maandamano yaliyofanikiwa kuamsha hofu kwa Chama tawala pamoja na serikali yake, hofu iliyosambaa mpaka kwa Msajili wa vyama vya siasa na mpaka kutishia kukifuta chama cha CDM.
  Swali langu kuu hapa wanaJF ni juu ya mwenendo wa siasa nchini, rafu zichezwazo na ushiriki wa wanachama na wananchi wa kawaida ktk siasa. Hata najaribu kuhuhisha wingi wa wananchi wajitokezao ktk mikutano, uhodari wa wanachama, wafuasi na wabunge wa CDM Kielimu na ktk ujengaji wa hoja u mkubwa, sasa inakuwaje washindwe? Na nini kifanyike wasishindwe? Na nin msaada wa wasomi ambao ni hazina ktk chama kwa CDM?.
  Ndugu wanaJF nawasilisha hoja!
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Karibu sana hoja nzuri sana hii nawewe unashauri nini kwanza kifanyike kabla ya watu wengine kushauri ili kuanzia hapo ndo twende pamoja.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  CHADEMA hawajawahi kushindwa mkuu... what you see is sustainable progressive growth... Haiwezekani kulinganisha mbuyu wa miaka 50 na mbuyu wa miaka 7

  actually ungeniuliza mimi ningesema... CHADEMA wanawezaje kupita malengo yote tuliyoyategemea?

  :washing:
   
 4. m

  motenya Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Viongozi na wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wanatakiwa kuwa makini na ghiliba za utawala uliopo madarakani juu ya kutaka kukihujumu chama kwa malengo ya kukidhoofisha ili waendelee kutawala hata kama wameshindwa kuwatatulia matatizo mbalimbali watanzania tuangalie ukweli wa mambo tunayoambiwa na viongozi hawa na kuyachuja, kutoa elimu kwa watanzania juu ya masula yanayowahusu si dhambi kwa viongozi wa CHADEMA.Hata watanzania wenyewe wanayaona na kuyasikia.
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  hoja nzuri. kimsingi chadema inakwenda na accelation njema tu...

  however, acceleration hiyo inakwamishwa na serekali kuwawekea usiku watumishi wake ambao wanaonekana wanawerza kuwa na mchango au wanajishughulisha na chadema... lakini hii ni ajabu kwamba watumishi wa serekali ambao wanajishughulisha na ccm hawasumbuliwi na wanakesha wakikiuka hata miiko na maadili ya kazi.

  however, serekali hii ambayo inapoteza command yake kwa kasi hata miongoni mwa watumishi wake haina tena bao.

  katiba mpya ni dawa nzuri sana ya shida zote hizi!
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kwa nin Makamanda tunaowategemea kuinua chama wanahama? SHITAMBALA alikua hazina kwa CDM, kuondoka kwake kumeniumiza sana. Swali; KUMEALIBIKA NINI? IMEKUWAJE? NIN KIFANYIKE?
   
 7. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu wa namna hii hutawaliwa na masilahi binafsi na ya haraka. Wako tayari kupokea chochote toka cccm kwa kubomoa upinzania. Isikuumize kichwa ila songa mbele kuelimisha umma kuwa maendeleo ya kweli yataletwa na wale waliotayari ku-sacrifice. Kutojari masilahi yao binafisi bali huweka mbele maslahi ya watanzania walio wengi.
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hofu yangu ni jinsi kinavyosakamwa na vyombo vya dola. Matumizi ya pesa yametawala kuchukua wanachama wake. teh! UMAKINI NA MIKAKATI ENDELEVU NI MHM!
   
Loading...