CCT, TEC na BAKWATA mtahukumiwa

CCT, TEC na BAKWATA mtahukumiwa

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
12,361
Reaction score
6,441
Nawaomba hao niliowataja hapo kwenye heading, wawajibike kuepusha lolote linaloweza tokea tarehe 1 Sept. Wamekaa kimya kama vile sio sehemu ya waumini wao. Ukimya huu mtahukumiwa.

Mchungaji Kasupa amejitahidi kutoa ushauri. Nguvu zenu zikiungana mnaweza kutenda jambo jema! Lakini mnamuogpa Bwana Mkubwa kumwambia ukweli. Basi mshaurini Mbowe (CHADEMA) tusikie neno lenu kama Mkubwa mnamuogopa.
 
Nawaomba hao niliowataja hapo kwenye heading, wawajibike kuepusha lolote linaloweza tokea tarehe 1 Sept. Wamekaa kimya kama vile sio sehemu ya waumini wao. Ukimya huu mtahukumiwa.
Mchungaji Kasupa amejitahidi kutoa ushauri. Nguvu zenu zikiungana mnaweza kutenda jambo jema! Lakini mnamuogpa Bwana Mkubwa kumwambia ukweli. Basi mshaurini Mbowe (Chadema) tusikie neno lenu kama Mkubwa mnamuogopa.
Chadema mlizoea kudekezwa,yaani mbembelezwe!Kama Mbowe ni muumini wa kweli basi anajua wajibu wake,hakuna haja ya kutisha taasisi za kidini kwa matatizo ya kujitakia
 
Duuh.. mtukufu kawafumba midomo na vipande vya noti
 
Wa kuwajibika hapo ni CHADEMA wanaotaka kumjaribu Rais
Hajaribiwi hana cha kujaribiwa ni uimla wa maziwa makuu unamsumbua. Anahisi yupo Rwanda au Burundi.

Halafu wewe sikiliza Mbowe siye pekee yake anaethiriwa na udikteta wa vikabila vidogo vidogo vya maziwa makuu. Hata wewe unaathirika ila kwa kuwa ni taahira huoni tofauti.
 
Hawa wote kwasasa ni wachumia tumbo tu siwaamini ni mawakala wa chama cha mafisadi
 
Katika dola isiyofungamana na dini yoyote, viongozi wa Kanisa hawana amri juu ya vyama vya siasa au serikali kuhusu jambo lolote. Sababu ni hii: hawana locus standi inayowawezesha kufanya jambo hilo. Kwa nini? Mamlaka ya viongozi wa kisiasa na mamlaka ya viongozi wa kikanisa vina machimbuko mawili tofauti. Wakati mamlaka ya viongozi wa kisiasa yanatoka kwa watu moja kwa moja kupitia sanduku la kura, mamlaka ya viongozi wa dini yanatokana na "kuteuiliwa na Mungu" asiyetambulika serikalini. Kwa kifupi, mambo yako hivi:

"In a secular democratic society power of governance comes from the people. In the church, on the contrary, power of governance or jurisdiction does not originate from the will of the community of the faithful who constitute the ecclesial society. Instead, its origin is sacramental. It comes from its Founder, Jesus Christ himself. It is based on the power given to Peter and other apostles (Mt. 16: 18-19; 28:18; Jn. 20:22-23). Even today it is to the pastors chosen by him that the power of governance is given. For example, a parish priest who preaches the Gospel with all his apostolic authenticity and who presides over the Eucharistic celebration is the one who is not elected by his parishioners by voting but sent by his bishop. The same logic applies to the Bishop who is sent from Vatican to the Diocese by the Pope."

Sasa watu wa aina hii wanawezaje kuwa na mamlaka juu ya serikali iliyochaguliwa kidempokrasia? Kwa unyenyekevu mkubwa napenda kusema kwamba watu wa aina hii hawana locus standi inayowapa mamlaka juu ya serikali isiyofungamana na dini yoyote. Hii ndio maana niliwahi kulikosoa Jukwaa la Wakristo pale walipoanza kubeba ajenda ya Lowassa dhidi ya JPM bila kutambua.
 
Back
Top Bottom