CCM Zanzibar yanyweshwa sumu takatifu

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Katika jambo linaloonekana kwa CCM Zanzibar kuridhia kunyweshwa sumu takatifu huku ikijenga uhasama kwa wanachama na raia zake bila wenyewe kujitambua, limezusha hofu kubwa Visiwani .

Katika Mkutano uliohutubiwa na na Rais wa Tanzania mjini Unguja, JPM alionesha wasiwasi wake kwa Dk. Shein kuwachagua wapinzani wake kisiasa, kuwapa Uwaziri na hata kuwaingiza katika Baraza la Mapinduzi

Mmoja wa wapinzani- rafiki amekuja na hoja, nje ya Wizara anayoiongoza, ya kimazingira ambayo haikufanyiwa hata utafiti,na imebeba maslahi binafsi kuwa Zanzibar inakabiliwa na upungufu mkubwa wa upatikanaji wa Mchanga.Kwa tamko hilo tu lilitosha kupandisha bidhaa hiyo adhimu mara dufu na hivyo kurejesha nyuma jitihada za wananchi wa kawaida kujijengea nyumba bora.

Aidha sasa amekuja na hoja ya kujitajirisha kuwataka watu wabadilishe utamaduni wao wa Ujenzi na kuanza kutumia matofali ya udongo (Interlocking Clay bricks). Makampuni yanayoweza kutengeneza matofali hayo ni machache kama yapo,na ni yao wenyewe,ni ghali kwa mtu wa kawaida kuweza kumudu. Sasa anasema watu wanaotaka kuleta mchanga Zanzibar wamfutae na atawaelekeze vya kufanya.Bei ya tufali moja la Mchanga sasa halinunuliki na linakimbilia dola moja ya kimarekani.

  • Kipi kibaya zaidi kwa Zanzibar kutumia mchanga au Udongo kutengeza tofali kwenye kisiwa kidogo kama Zanzibar? Zanzibar ni kisiwa katu hakiwezi kuishiwa mchanga hata siku moja.
CCM sasa inavurugwa kuanzia ndani. Watu wanapoteza hamu.
 
Halo Makame vipi meli ya mchanga ishatia nanga bandarini?
Sheikh Barwani mchanga wa Dar es saalam haufai subiri meli MV Muscat inawalisili Kesho na mchanga wa Dubai huu mzuri zaidi!
 
hawa watu wa kafu wana mtindio wa akili.mara Lipumba anatumika,mara Sefu aseme hivi karibuni nitapewa serikali.
Kila siku tamthilia mpya
 
Bado kidogo Zanzibar itakuwa mkoa

Nakubali kwa mtindo huu tunaopelekeshwa Mkoa huo unanukia! N hiyo ndio Ajenda.
Halo Makame vipi meli ya mchanga ishatia nanga bandarini?
Sheikh Barwani mchanga wa Dar es saalam haufai subiri meli MV Muscat inawalisili Kesho na mchanga wa Dubai huu mzuri zaidi!
Mchanga wa Tanganyika haufai. Zanzibar ina mafungu mengi tu Baharini, kama itabidi tutakimbilia huko Tunaambiwa Matumbawe hayatakiwi kujengea nyumba eti mazalio ya Samaki yataharibika. Mji Mkongwe wote umejengwa kwa matumbawe na Samaki wanapatikano kibao Sokoni na rahisi kuliko bara .
 
Back
Top Bottom