cdm wametuzarau sana labda na cc tujaribu kuwa kama wao tuone tutaishi vp ktk siasa. Maana wao waliona ndo fasheni kudharau mpaka mkuu wa nchi, police na n.k hawana heshima hawa kisa ufisadi kwani ndani ya cdm hakuna ufisadi?.. Wanaonekana wanafaa kwa kuwa upande mmoja umetulia sasa tujaribu na upande mwingine kuwa kama wao kama patakalika.
Mpambanaji,
Nafikiri hata ndugu zetu wenyewe wa CCM wenye upeo na uhuru wa mawazo wameliona hili. Lakini tatizo kubwa sio mabadiliko. Tatizo ni mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa shughuli na maamuzi ya chama. CCM asilia ya akina Nyerere (RIP), Kawawa (RIP), Butiku, Warioba,Salimu na wengineo (siwezi kutaja wote), kwa kiasi kikubwa ilisimamia misingi ya haki na usawa kwa jamii. Ndio maana hapo awali matabaka katika jamii hayakuwa wazi saana. Just imagine, Nyerere amekufa na physical asset gani alitoipata kwa kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20?
Huo wakati CCM kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, na kwa kweli jamii walikuwa na uzalenfo wa kweli na chama chao. Hakikuleta maendeleo makubwa lakini, kila mwanajamii aliona nini kinafanyika katika mfumo uliowekwa na chama (ingawa udikteta ulikuwepo ili ku-maintain status quo).
Sasa hivi CCM academia, ccm ya utandawazi, sisiem ya kupigia magoti wafanyabiashara, sisiem ya kuwahimiza wageni waje kupora rasilimali, sisiem ya poolisi kupambana na raia na kuwaua, sisiem ya kuchakachua, sisiem ya kutukana hadharani..............
Hii nchi ni yetu sote, na hivyo tunastahili wote, bila misingi ya rangi, kabila au dini, kupata maendeleo na huduma za kijamii kutokana na rasilimali zetu. Sio siri tena kuwa hizi rasilimali hazitumiki kwa ajili yetu. Ni kwa ajili ya wachache ambao ni viongozi wa chama, serikali, wataalam washauri, wataalam serikalini, na wawekezaji. Ukichukua tabaka la uongozi uliopo na familia zao hawawezi kufikia hata 5% ya watanzania wote. Sasa hawa watanzania zaidi ya 90% maisha yao yanaendaje?
maji ya shida (acha tu suala la kuwa safi na salama)
afya shida
elimu shida
ajira shida
chakula shida
usafiri shida
ulinzi shida
usalama shida
umaskini umetamalaki
maradhi yametamalaki
mauaji na ukatili vimetamalaki
mfumuko wa bei umetamalaki
maisha ni magumu
ajali
manyanyaso ya raia
uporaji wa ardhi
demokrasia finyu
vita vya ardhi
udugu ktk uongozi
kutukanwa hadharani
nk
Masuala ya msingi kwa maendeleo ya jamii yote yamewekwa pembeni. Taifa halina mwelekeo. Dereva amelala. Maliasili zinaibwa mchana kweupe kwa msaada wa watanzania wenzetu, dola inatumika kulinda wageni na kuua raia, uongozi umekuwa ni zawadi, hupati huduma bila kutoa mlungula, maisha yamepanda
na zaidi ya yote umaskini umetamalaki kwa wananchi.
Ni nani asiyeona haya?
sisi wananchi twafahamu haki zetu ni zipi, ila namna ya kuzipata ndo inakua shida kwa sababu hatuna pa kushtaki.
Tutawaadhibu
Tutawaadhibu CCm
Tutawaadhibu Jk,lowasa,mangula,mkapa,mukama,makamba,nape,jairo,malima, ngeleja nao wote wanaotudharau,wanaouza rasilimali zetu, wanaokula jasho letu huku tukiangamia.
Kwa mazingira hayo kuna haja gani ya kuwasapoti? twajitenga na waovu ili tupate haki.
tumechoka
twataka mkombozi
tutajikomboa wenyewe kwa kuanza na uhuru wa kufikiri na kutenda.
kujua lipi baya na lipi zuri.
ghilba zao tumezitambua.
twataka haki zetu
twataka uhuru wetu
twataka madini yetu
twataka ardhi yetu
twataka heshima ya Taifa kwa maana tumekua ni ombaomba mchana na usiku
twataka maendeleo
Nani atayaleta haya?
yule anayetuibia?
anayeuza ardhi/maliasili zetu?
anayetukana wafanyakazi wake?
anayejiuzia kiwira?
hapana
hapana
Ni yule atanayetupa ukombozi wa fikra
anayetuonesha madhambi tutetewayo
anayepigania haki zetu
aliyetayari kupigwa mabomu kwa ajili yetu
aliye na mawazo huru
Huyu ni nani basi?
zito?slaa?mbowe?lipumba?hamad rashd?kikwete?nape?mrema?sendeka?pinda?
CCM? CDM? CUF? SAU? TLP?
KALAGABAHO!
Ukiamini utakubalina nami, usipoamini utanipinga,
Katika siasa za kweli kama mdau maarufu wa CCM wote HATUNA AMANI na furaha kutokana na namna CHADEMA kinavyozidi kujijengea umaarufu, kupitia hoja na kuelimisha wanajamii.lAZIMA tujiulize, KWANI CHADEMA kilianza lini?nasie ccm tumeanza lini kusimama kwenye ulingo wa siasa?,CHADEMA wanapoteza nini,sie CCM ndo tunapoteza muelekeo na ukweli utandawazi utatulazimu kujitahidi kuwa wakweli ili wimbi la kukimbiwa lipungue.Tunachoahidi Arumeru kwa sasa ni kiini macho,hakuna litakalotekelezeka kupitia siasa za kukumbatiana.Kama tunajiamini kwanini tutumie nguvu kiasi hili kwenye uchaguzi mdogo?
kwanini tuhahe kwa sababu ya CHADEMA?kwani tusiwajibike?
Ukweli ni kwamba CCM kilichobaki ni kujaribu kuiga mfumo wa CHADEMA ila kweli tumechokwa, hata na wazee wanaipenda CHADEMA?SIASA zetu ni pesa? au kulinda maslahi?
Ni vyema tukubali kuwa CHADEMA ni mwiba na kupitia wao asilimia kubwa ya raia hawadanganyiki tena, wanaotusapot mwisho wa siku wanataka tuwasainishe lunch au dina?Tunaelekea wapi?Imefika wakati nasie tuwajibike ipasavyo kwa wananchi na tuache siasa za jazba na kujibizana na kuchafuana na CHADEMA.Kama ni wazazi CCM ndio wazazi na CHADEMA NI WATOTO.je tunakosa uadilifu kwa watoto kiasi cha siasa za msingi tunayoinesha sasa?
Lazima tukubali kuwa huu ni mpito wa siasa za kweli na hatuna budi kuwajibika kadri ya sera tunazozitoa kwa wapiga kura wote Tanzania.
Kwanini tusioneshe vipaumbele na matokeo yake yaonekanae?Mf.Kufufua viwanda,usafiri wa reli,nenda Tanga kwa Mfano uangalie Railyway station,Kiwanda cha matairi-tufikirie kujenga ajira kwa vijana kupitia mipango mikakati inayoonekana.....
Ukinipenda nikubali ukinikata niache, ila huu ndio ukweli
Badae.
ukiamini utakubalina nami, usipoamini utanipinga,
katika siasa za kweli kama mdau maarufu wa ccm wote hatuna amani na furaha kutokana na namna chadema kinavyozidi kujijengea umaarufu, kupitia hoja na kuelimisha wanajamii.lazima tujiulize, kwani chadema kilianza lini?nasie ccm tumeanza lini kusimama kwenye ulingo wa siasa?,chadema wanapoteza nini,sie ccm ndo tunapoteza muelekeo na ukweli utandawazi utatulazimu kujitahidi kuwa wakweli ili wimbi la kukimbiwa lipungue.tunachoahidi arumeru kwa sasa ni kiini macho,hakuna litakalotekelezeka kupitia siasa za kukumbatiana.kama tunajiamini kwanini tutumie nguvu kiasi hili kwenye uchaguzi mdogo?
Kwanini tuhahe kwa sababu ya chadema?kwani tusiwajibike?
Ukweli ni kwamba ccm kilichobaki ni kujaribu kuiga mfumo wa chadema ila kweli tumechokwa, hata na wazee wanaipenda chadema?siasa zetu ni pesa? Au kulinda maslahi?
Ni vyema tukubali kuwa chadema ni mwiba na kupitia wao asilimia kubwa ya raia hawadanganyiki tena, wanaotusapot mwisho wa siku wanataka tuwasainishe lunch au dina?tunaelekea wapi?imefika wakati nasie tuwajibike ipasavyo kwa wananchi na tuache siasa za jazba na kujibizana na kuchafuana na chadema.kama ni wazazi ccm ndio wazazi na chadema ni watoto.je tunakosa uadilifu kwa watoto kiasi cha siasa za msingi tunayoinesha sasa?
Lazima tukubali kuwa huu ni mpito wa siasa za kweli na hatuna budi kuwajibika kadri ya sera tunazozitoa kwa wapiga kura wote tanzania.
Kwanini tusioneshe vipaumbele na matokeo yake yaonekanae?mf.kufufua viwanda,usafiri wa reli,nenda tanga kwa mfano uangalie railyway station,kiwanda cha matairi-tufikirie kujenga ajira kwa vijana kupitia mipango mikakati inayoonekana.....
Hisia za wengi kwa chama sasa, hiki ni chama cha matajiri na wafanyabiashara...kwanini tuweke taswira ya namna hii kwa uma wa watanzania?
Je ni kweli vijana waiopo ccm wapo kwa mapenzi ya watanzania au kwa maslahi ya mstari wa maslahi..yaani kupeana...hiki hakikisha kinakuwa chetu na sio chao/ kwa umma wa watanzania kwa kihitajikavyo?
Tujitafakari upya....lusinde...kutumia tafsida kwenye fani ya siasa zenye ushabiki hadi wa watoto sio swala la kupuuzwa...chama makini lazima kimwajibishe na umma wa watanzania ufahamu hilo...
Ukinipenda nikubali ukinikata niache, ila huu ndio ukweli
badae.