CCM yavuruga MIPANGO yake

CCM yavuruga MIPANGO yake

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Baada ya mimi kuripoti humu JF jana kuwa CCM imeanza kujiandaa kwa Kampeni za Sumbawanga Mjini,jana kilifanyika kikao kingine. Nashukuru hawakunifahamu hivyo kutonitenga. Nikawepo tena kwenye Kikao cha pili cha dharura. Kikaoni,tukaanza kutemewa mkwara na 'Mwenyekiti' wa kikao ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

' Tumepokea taarifa kuwa yupo mtu humu anaweka mipango yetu wazi kwenye mitandao. Tumeshamjua. Tunamuonya asirudie. Na leo tumemtenga rasmi kwenye vikao vyetu vya kimkakati. Hatahudhuria hadi atakapotubu' alitamba 'Mwenyekiti' huyo. Nusura nicheke. Kweli CCM ni waongo na waliojaa propaganda. Mbona mimi nipo?! nilijiuliza kimoyomoyo.

Eti, taarifa ikatolewa kuwa mipango ya awali ya kumteua Mwigulu na timu yake ya Kampeni na nini sijui imesitishwa. Imesitishwa kwakuwa imevuja. Ikaundwa Kamati Ndogo itakayoshughulikia kisirisiri mipango hiyo ya Sumbawanga Mjini. Nami pia nimo. Raha ilioje! Mwaka huu,hadi kieleweke. Nilifundishwa jeshini enzi hizo kuwa ukitaka kumjua adui vyema,jiunge naye kwa juhudi zako zote. Ndivyo nilivyofanya. CCM hawatapata pakutokea.
 
Ha ha ha haaaaa,,, Mzee Tupatupa bana una mambo...

Poa sisi yetu maskio we endelea kutujuza. Nepi alikuwepo kikaoni?
 
Dah,mkuu,upo kwenye mapambano,sasa ulivyoandika hivi si watavunja kamati yote na wakateuliwa watu wengine kabisa?????ni hatari,lakini mungu akutangulie.
 
Tumepokea taarifa kuwa yupo mtu humu anaweka mipango yetu wazi kwenye mitandao. Tumeshamjua. Tunamuonya asirudie. Na leo tumemtenga rasmi kwenye vikao vyetu vya kimkakati. Hatahudhuria hadi atakapotubu' alitamba 'Mwenyekiti' huyo. Nusura nicheke. Kweli CCM ni waongo na waliojaa propaganda. Mbona mimi nipo?! nilijiuliza kimoyomoyo

hahahahahaaaaa..... hapo kwenye red! Kizunguzungu!
 
Nimecheka sana na kufurahi hapo uliposema "Ikaundwa kamati ndogo itakayoshughulikia kisirisiri mipango ya Sumbawanga Mjini Nami pia nimo". Hahahaaaaa haki ya mama nchi hii hatuhitaji TISS/ UWT, JF inatosha. Mulika mwizi kamanda!!!!
 
nipo nafuatilia hizi thread zako kwa karibu sana .... tusubiri
 
Au we ndio mwenyekiti mwenyewe? Kazi nzuri sana. Nadhan tumekuelewa.
 
Kweli wewe jembe, komaa nao mkuu! Ndo uzuri wa akili ndogo kuongoza kubwa...kwi kwi kwi kwiii!
 
Siku ya kufa ikifika bwana,huwezi kuchomoa.
 
Waachane wafu watangulie na GUTA! CHADEMA tunakuja na Chopper.tuone nani mjanja.
 
Nakumbuka hata ile sekretarieti ya CCM ya wajumbe tisa tu, siri zilivuja na wakawa wanalalamika nani kavujisha? Mimi nahisi mvuzishaji siri huyu ni Mh. NAPE. Na hawataweza kumbaini mpaka atakapokiangusha chama chetu sikivu.
 
Nakumbuka hata ile sekretarieti ya CCM ya wajumbe tisa tu, siri zilivuja na wakawa wanalalamika nani kavujisha? Mimi nahisi mvuzishaji siri huyu ni Mh. NAPE. Na hawataweza kumbaini mpaka atakapokiangusha chama chetu sikivu.


Mwacheni Nape amalizie kazi aliotumwa. Msitangaze watamwangosi halafu tukaharibu.
 
Isije ikawa mzee Tupa Tupa ndio Wilson Mkama mwenyewe, JF Kiboko
 
Back
Top Bottom