Junior. Cux
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 5,319
- 3,767
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), Kimeanza staili mpya ya kujijenga kwa wanafunzi wa shule za sekondari huku makamu mwenyekiti wake, pius msekwa akidai kwamba chama cha upinzani cha chadema kimeanzisha mtandao wa wanafunzi wa vyuo vikuu.
msekwa alidai kwamba mtandao wa jamii forums unamilikiwa na vijana wa chadema ambao kila mara wanautumia katika kuchochea vurugu na maandamano yasiyo na msingi.
juzi CCM kilikaribisha idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari ya central iliyopo mita chache kutoka ofisi yake ya makao makuu mjini hapa ambako walikula kiapo cha utii kwa chama hicho na kisha kupewa kadi za uanachama.
katika mkutano huo, CCM kilitangaza kuingiza jumla ya wanachama 670 na katika msururu mrefu uliopita mbele ya msekwa kupokea kadi, alikuwepo mtu mzima mmoja huku idadi yote ikiwa ni ya wanafunzi. Hata hivyo baadhi ya wanafunzi waliohojiwa walieleza kukerwa kwao na hatua hiyo, "sisi tuliambiwa asubuhi kuwa tuje huku CCM kuchukua kadi na tulipomaliza mitihani majira ya saa sita mchana tukakalishwa hadi saa tisa alasiri ndipo tunaletwa" alisema mmoja wa wanafunzi ambaye hakutaka kutaja jina lake...
source: mwananchi j1