CCM yatapatapa; Masha asema chama kimemeguka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatapatapa; Masha asema chama kimemeguka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  KATIKA hali ya kuonyesha Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatapatapa baada ya kuanguka katika majimbo kadhaa nchini, viongozi wa chama hicho wameanza kutoa matusi dhidi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Matusi yaliyotolewa juzi na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Maburuki Igogo jijini Mwanza yaliwalenga Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

  Akihutubia mkutano huo wa kuwashukuru wananchi wa wilaya ya Ilemela na Nyamagana, Lusinde alimwaga matusi ambayo hayawezi kuandikika na kuwashushia tuhuma mbalimbali viongozi hao wa CHADEMA.

  Hata hivyo, kauli hizo zilionekana kuwakera baadhi ya wananchi huku baadhi ya wana CCM wakionekana kushangilia.

  Naye waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi na aliyekuwa mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, aliwashukia wana CCM wenzake na kuwataka kuacha majungu na kwamba chama hicho kimemeguka makundi, kuna CCM A na B.

  Aidha, aliwarushia madongo watu waliomsakama na kumpikia majungu wakati wa uchaguzi na kusema "Walidhani watanikomoa…sasa nani wamemkomoa?" alihoji Masha.

  Wakati huohuo, umoja wa vijana wa CCM umesema utahakikisha unafanya kila njia ya kuwadhibiti baadhi ya wanasiasa wa CCM wanaotoa kauli za kupingana na viongozi wa chama hicho.

  Mwenyekiti wa umoja huo taifa, Beno Malisa, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa baraza la vijana lililofanyika mjini Dodoma.

  Alisema kuwa wapo baadhi ya wana CCM wamekuwa wakitoa matamko ya kupingana na viongozi wa chama kwa lengo la kujitafutia umaarufu na kuongeza kuwa kikao hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha viongozi ndani ya CCM ambao wanatoa matamko kwa kutofuata utaratibu hawapati nafasi yoyote ndani ya chama.

  Mbali na hilo katika maazimio yao vijana hao wa CCM wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapambana na CHADEMA kwa kila namna ili kisiendelee na maadamano nchini.

  Katika maazimio ya baraza la vijana pia wameitaka serikali kutatua mara moja matatizo yanayojitokeza katika vyuo vikuu na kusababisha kuwepo kwa migomo ya mara kwa mara bila kuwapo sababu za msingi.

  Walisema serikali inatakiwa kushughulikia mara moja masuala yanayohusiana na mikopo katika vyuo vya elimu ya juu ili kuondokana na tabia ya wanavyuo kukosa pesa za mikopo na kusababisha migomo na kuwafanya wanavyuo kusoma kwa shida. Hata hivyo, katika kikao hicho cha baraza la vijana wa CCM wameunda tume ya watu nane ambayo itashughulikia masuala ya vijana pamoja na kuboresha kufanya uchunguzi wa sehemu ambazo zinasababisha chama kuyumba.

  Tume hiyo ya vijana inaundwa na Riziki Pembe ambaye ni mjumbe toka UVCCM Zanzibar, Fadhili Njagilo mwenyekiti vijana Iringa, Hussein Bashe, mjumbe bara ambaye pia ni mwenyekiti wa tume hiyo, Rogas Shemwelekwa mjumbe UVCCM Tanga, Daud Smail toka UVCCM Zanzibar, Ashura Shengondo toka UVCCM bara na Anthon Mavunde mjumbe toka UVCCM bara.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Waislamu wa5.

  Makafir wa2


  kweli BAKWATA ni TAWI mama la CCM
   
 3. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wamnanchi wa Mtera walidhani wamemkomoa mzee Malecela kwa kumnyima kura na kumpa huyu mhuni Lusinde. Lusinde ndio alikitia aibu chama chake kwa kudai bungeni kuwa watachapana makonde ndani ya bunge...kweli wananchi wa mtera wamedandia treni kwa mbele! teyari ukiongea naop wengi wao wameishaanza kujuta kumchagua bishololo mwenye uharo wa mdomo (mouth diarhorrea)
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Duh Kumbe Masha bado yupo?

  Huyo Lusinde aangalie operesheni Sangara itatua Mtera watu kule wanaishi nyumba za Tembe na maskini wa kutupwa.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Masha anasema CCM kimemeguka!
  Angeshinda ubunge angesema hivyo?
   
 6. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  Wadau, nimesoma mahali fulani kuwa Huyu Lusinde amewatukana viongozi wa CDM matusi makubwa. Je alisemaje? Mtujuze mlio karibu na magazeti ya leo au jana sijui ni lini ilikuwa?
   
 7. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Acha ufala ww Jerusalem..nani kakwambia kuwa jina linamaanisha dini???!!! Mbona askofu mkuu wa Nigeria anaitwa hussein? Acha upuuuzi wako...
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  amemegwa yeye analalamika.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu wamesema hayaandikiki! sijui ni yepi labda $#$##$$$ CDM%%%%$#$$# DR N.k
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  ndoi hao wanabaka vitoto kanisani. walianza project za kuijipenyeza kwenye kanizsa siku nyingiiii. wauwe kanisa, waeneze uislam. tunajua sana. sasa wanafanya mabmbo yao. lakini kanisa halitatetereka kamwe.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hata hapa JF hayaandikiki si unajua yule jamaa shule ndogo sijui kaishia darasa la sita.
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  punguza spidi
   
 13. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Masha inamuuma sana alizani uongozi ni kuuza sura rose garden na kina kibonde eeeeh!:hatari:
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Wanawashukuru wana nyamagana/wanailemela kwa lipi??waende na Mbeya/Iringa mjini ili tuendelee kuambiwa A ni akina nani na hao B ndo wapi
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Jamani tuache udini ndani ya hii report; it does not matter if that kamati has more Muslims than Christians kitu bora ni kama ni Chadema how to monopolize the CCM Agendas and not differentiate them through religion ni mbaya baadaye tutaenda kwa ukabila na tuna makabila mangapi? 700...

  Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni mwaka 1961! Toka pale mwalimu Nyerere alitangaza vita dhidi ya maadui watatu wakubwa: Ujinga, Umaskini na maradhi. Leo sisi baada ya miaka 49 tunapigana na maadui wakubwa watano: Ujinga, Umaskini, ......Maradhi, Rushwa na Udini!... Tutafika kweli???
   
 16. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na wetu katika Dayosisi ya Anglikana ya Kilimanjaro alikuwa Ramadhani !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Eh! hapa sijaelewa hivi hii thread ni ya UCHUMI au Biashara? Maana nasikia harufu ya Libya huku.
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  udini upo ndani ya mtu na hiki ndio kipimo cha upumbavu
   
 19. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,882
  Likes Received: 2,832
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani U-MOD unagombewa? Yaani nimepata hasira na huyu mtu!! Kwa kweli ningekufungia milele wala wasingeona tena utambulisho wako wewe!! Watu wanajadili mengine wewe unakuja na udini wako hapa mwone kwanza!!
   
 20. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nafikiri wayapeleke mambo ya wakubwa kule tukayasome live.
   
Loading...