CCM yatamba kushinda majimbo yote

CCM yatamba kushinda majimbo yote

Com hawashindi,zinazoshinda ni bunduki,Mapanga na ubabe.magufuli vs lowasa maongezi ikulu, "Rudi ccm, chama kimekufa" kununua viongozi upinzani ni ushahidi tosha.mtanunua wachache,ila walio wengi hatuipendi wala kuitaka ccm.ndo mnatumia nguvu kubwa sana kutafuta muonekano wa kukubalika.
 
kumbe leo uchaguzi . duh kweli maisha yana kwenda kasi.. jaman mwenye picha tuone kama vituo vilikuwa na watu
 
Shithole
CCM.jpg

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kitaibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo matatu ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu CCM, Humphrey Polepole ambapo amesema kuwa Chama hicho hakina hofu ya ushindi.

Amesema kuwa Chama hicho kimefanya maandalizi makubwa hivyo kwao ushindi ni lazima katika majimbo yote yanayorudiwa uchaguzi.

“Tumekuwa tukifanya tafiti nyingi kuhusu shida za wananchi, na endapo tukifanikiwa kuchaguliwa katika majimbo hayo, kazi kubwa itakuwa ni kwenda kutatua changamoto za wananchi ambazo tayari tumeshazijua,”amesema Polepole

Hata hivyo, amewataka wapiga kura kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza
 
Wanashindana na nani kwanza??

Hivi timu inaweza kuingia uwanjani na timu pinzani isitokee, halafu huo ushindi wa "kupewa" uushangilie kweli??
Hahhaa wanashindana na hewa hawa si wataalam.wa mambo ya hewa, ukaguzi hewa, wafanyakazi hewa, vyeti hewa, they are hewa specialists
 
Kodi gani inachezewa? Hii ndo gharama ya Demokrasia. Longido mbunge wake alitenguliwa na mahakama. Singida kaskazini mbunge wake alijivua uanachama wa CCM akaenda CDM na Songea mjini mbunge wake alifariki dunia. Sasa ulitaka hayo majimbo yawe wazi bila uwakilishi? Jambo la msingi hapa ni kuwalaumu wale waliosusia uchaguzi kwamba wamewaokosesha wananchi haki ya kuchagua mtu wanaemtaka.
kuna haki gani ambayo cdm wamemkosesha mwananchi mbn chaguzi ndogo iliyopit kuna maeneo wananchi walichagua upinzan lkn wasimamizi wa chaguzi wakalazimish kupitish w ccm.uamuzi wa kukacha uchaguzi n sahihi %
 
CCM.jpg

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kitaibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo matatu ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu CCM, Humphrey Polepole ambapo amesema kuwa Chama hicho hakina hofu ya ushindi.

Amesema kuwa Chama hicho kimefanya maandalizi makubwa hivyo kwao ushindi ni lazima katika majimbo yote yanayorudiwa uchaguzi.

“Tumekuwa tukifanya tafiti nyingi kuhusu shida za wananchi, na endapo tukifanikiwa kuchaguliwa katika majimbo hayo, kazi kubwa itakuwa ni kwenda kutatua changamoto za wananchi ambazo tayari tumeshazijua,”amesema Polepole

Hata hivyo, amewataka wapiga kura kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza
Sina wasi wasi na ushindi katika majimbo hayo kabisa.Ninacho omba hata hivyo ni kwamba tubaki on course hasa katika kutatua matatizo ya wananchi na tuepuka manageable and obvious mistakes ambazo zinaweza kutu-cost 2020.Mtaji wetu mkubwa katika hili ni viongozi wenye weledi na uaminifu usiotiliwa shaka.Viongozi wababaishaji na wasio na weledi ni vema wakaenguliwa mapema.Tunajua matatizo ni mengi na tutayatatua hatua kwa hatua, ila ni lazima wananchi waone kwamba there is something being done na wayaone maendeleo kwa macho,sio ya kutafuta kwa tochi.Tukumbuke kwamba 2020 is just around the corner.
 
Nao tume wanatusumbua tu, wamesikia chadema wametema kugombea bado wanatusisitiza tukapoteze muda vituoni eti kupiga kura, si wangetangaza tu mshindi mchezo unaisha. Haiwezekani ukahangaika kupanda daladala toka kinzuti hadi uwanja wa taifa kuiangalia yanga vs simba kucheza wakati umeshatangaziwa kwamba simba hawatakuwepo uwanjani.
 
Ukiweka mpira kwapani unapoteza pointi zote na kupewa mpinzani wako.
 
Ni uchaguzi au ni kiini macho cha uchaguzi? Wanashindana na nani? Leo hakuna polis wala waleta vurugu kwa sbb wanashindana na hewa wanajua watashinda ,hawana aibu wala huruma ,nawaambia what goes around comes around, ipo sku na wengine itakuwa zamu yao kusherehekea ushindi ,only time will tell
 
Kwani ilikuwa inashindana na nani?? Cuf Lipumba ambae anajulimana ni nani kwenye siasa za Tz?
 
Kwan wakishinda kutakua na jipya.kama wameongoza nchi toka uhuru na hakuna jipya sembuse sasa.
 
Back
Top Bottom