CCM yatamba haiogopi mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatamba haiogopi mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Apr 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  CCM yatamba haiogopi mafisadi

  Imeandikwa na Juma Mohammed, MAELEZO, Zanzibar; Tarehe: 18th April 2011


  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema uamuzi wa chama hicho kuwapa miezi mitatu wajumbe wa NEC wanaotuhumiwa kwa ufisadi, haina maana ya kuwaogopa.

  Bali amesema ni utaratibu uliowekwa akiufananisha na wavuvi wa pweza wanapomtengeneza kwa ajili ya kuliwa supu kirahisi.


  "Msiwe na wasiwasi ni kama kumvua pweza baharini, akifika nchi kavu unamtandika mikwaju kisha mnampika baada ya kulainika na ndivyo tafsiri ya muda waliopewa," alisema Nape Aprili 17 wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembe Kisonge, mjini hapa.


  Nape alikilinganisha na kitendo cha kujivua gamba kwa CCM na kuwasha Mwenge unaomulika kwenye chuki, pasipo na matumaini, pasipokuwa na nidhamu na kupaweka sawa na kwamba Mwenge huo hautazimika.


  Sekretarieti mpya ya CCM iliyopokewa kwa kishindo visiwani hapa ilitangaza operesheni fagio la chuma ndani ya chama, kwamba inaanzia ngazi ya tawi kuwataka viongozi wenye tuhuma kujivua gamba wenyewe.


  Wakihutubia kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara, viongozi hao walisema CCM imeamua kuwasha Mwenge nchi nzima na kuleta matumaini mapya kwa Watanzania.


  Nape alisema baada ya kuanza kwa operesheni ‘jivua gamba' baadhi ya watu waliotoswa ndani ya chama hicho wameanza kutumia baadhi ya vyama vya upinzani, vyombo vya habari na hata wasanii.


  "Tunazo taarifa kwamba baadhi ya watu waliotoswa katika chama chetu wameanza kutumia magazeti. Tunawaambia hawatashinda vita hivyo, CCM ni chama kikubwa na makini," alisema Nape huku akishangiliwa na wana CCM wa hapa.


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Chiligati, aliwataka wanachama wanaojiona wamechafuka ama kwa tuhuma za ufisadi kuanzia ngazi ya matawi, majimbo, wilaya, mikoa na kwenye NEC wajiondoe kwenye nyadhifa zao.


  "Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa safishasafisha ya CCM itaendelea hadi kwenye matawi...tunataka chama chenye nidhamu," aliahidi Chiligati.


  Chiligati alisema anawashangaa wanaobeza uamuzi wa NEC kujiuzulu kuwa wajaribu katika vyama vyao, kama havikusambaratika, kwani ni uamuzi mgumu ambao CCM iliuchukua na imevuka salama.


  "Kuachia ngazi ni jambo gumu sana na si la kubeza hata kidogo, tumelazimika kujiuzulu kukinusuru chama, ingelikuwa vile vyama vingine mngevisikia vimesambaratika … wajaribu
  waone," alisema Chiligati.

  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, mbali ya kuelezea historia ya kujivua gamba kwa chama hicho, alielezea mpango mkakati wa CCM katika kujenga chama kipya chenye matumaini kwa Watanzania.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana ni bomu kweli kweli kwa sababu asichojua tatizo la CCM ni utamaduni wa kulindana ambao kiini chake ni ukosefu wa demokrasia halisi ndani ya chama hicho unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na katiba yenye misingi ya chama kimoja..................
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  SISIEM IKIWAFUKUZA KWELI KWENYE CHAMA AKINA EL NA RA...! SIKU HIYO MVUA YA CHAPATI ITANYESHA...!

  kwani nyoka akijuvua gamba huwa anakuwa jongoo..????


  ITS THE SAME ODD CCM ..NO MATER WHAT..!!!!
   
 4. Monasha

  Monasha JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Nadhani sasa ifike wakati kwa viongozi wa CCM kutoogopa chochote ndani ya chama kwani hicho ndicho kinachowanyima uhuru na hatimaye kuleta migogoro ndani ya chama. Unakuta kiongozi anajua ukweli upo wapi lakinin kutokana na kuogopa na kutaka kulinda maslahi ya chama chake, basi analazimika kuvunga tu. we jiulize kwanini watu kama akina sita wamenza kuangaliwa kwa macho ya kushoto??? Ni kwa sababu wanajaribu kuwa wakweli kwa kufichua mambo.

  Hasa huyu NNape naye asibweteke, hata kama wakijaribu kumnyamazisha sisi wananchi tuwe mstari wa mbele kumtetea na kumsaport ili wasimgandamize. Maana wamezoea sana mtu akiwa mbele, wanamficha au akumtafutia namna asisikike.
   
 5. k

  kyerwa Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inayaogopa mbona hawatutajii hayo mafisadi ? angalia tusichezewe akili, hivi Januari makamba anaweza kumtosa baba yake? tumia akili
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kwa siasa hizi nafikiri CCM haijivui gamba bali inajivisha gamba!!!! Mimi sio nabii ila 2011 patachimbika!!!!
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Joka haliwezi kuogopa joka lenye gamba.:whoo:
   
 8. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  R.i.p ccm
   
 9. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mtu anapokuwa amenyamaza kimya utaona anabusara sana, sasa ngoja aanze kuzungumza ndipo utakapo jua yupi ni pumba na yupi ni mchele.

  Huyu Nape baada ya kupata haka kawadhifa ndio ameanza kuonyesha udhaifu wake kwa kuongea vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Anaongea vitu ambanyo sio analytical, huyu ni tatizo jingine katika siasa za bongo.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Maneno yako nisawia kwani nyoka akijivua gamba anabaki nyoka tu na wala hawi Kinyonga; sasa hawa jamaa wanamfukuza Chenge kwenye cc yao na kumuingiza Emmanuel Nchimbi ambae ni part ya ile ile EPA syndicate!!
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  CCM isitafute mchawi
  [​IMG]

  Christopher Nyenyembe ​

  [​IMG] KIKULACHO ki nguoni mwako huu unaweza kuwa msemo dhahiri unaothibitisha wazi kuwa sasa CCM wanatafunana wao kwa wao na kusingizia kuwa kazi kubwa ya kuwamaliza inafanywa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA.
  Ni dhambi na pengine haifai kusomeka mbele ya watu makini kuwa mmomonyoko wa chama fulani kilichodhani kuwa kinaweza kuwatawala wanachama wake milele na kushindwa kuwapa sauti na uhuru wa kukosoa kunasababishwa na chama kinachojijengea umaarufu mkubwa kama CHADEMA.
  Ni vigumu kuamini kuwa haya yote yanayotokea ndani ya CCM yanasababishwa na nguvu ya upinzani kutaka kukidhoofisha chama tawala, lawama hizo haziwezi kupata nafasi kwa kuwa CCM wanamalizana wao kwa wao na hakuna mchawi anayewaloga.
  Katika mambo mazito na ya msingi chama hicho kinapaswa kutambua ukomo wa kiutendaji na kuamini fika kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, leo wanachama wanaondolewa enzi zao walionekana kutambuliwa vyema na kuheshimika kwa kiasi kikubwa lakini sasa wanaitwa mafisadi sugu,eti ni gamba la zamani.
  Kudhoofika kwa nguvu na mvuto uliokuwepo ndani ya CCM ikumbukwe kuwa ni matokeo ya hila,chuki na uhasama uliojengwa miongoni mwao wa kupigania madaraka hata kwa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kuongoza wamejiingiza katika siasa kwa ajili ya fedha zao.
  Kwa mazingira hayo kamwe CHADEMA hakiwezi kuwa chama kinachofanya kazi ya kuiloga CCM ili chama hicho kishindwe kuendelea kudumu.isipokuwa wachawi wa CCM wamo ndani ya CCM kwa kuwa wanajuana kwa sura na tabia na jinsi wasivyoweza kuvumiliana nyakati hizi kutokana na uzito wa makundi yasiyoshabihiana.
  Hawa mafisadi waliojibanza ndani ya chama hicho kama mdudu ruba anayeogopwa kwenye mashamba ya mpunga wamekuwa wakinyonya damu ya wanachama waaminifu, wamewachafua na kuwadhoofisha kabisa ili wasiweze tena kusimama na kuimba nyimbo za kukitukuza chama chao kwa kuwa nyimbo hizo sasa haziimbiki na idadi ya wanachama wanaovaa sare za kijani inazidi kupungua.
  Kiini cha mpasuko mkubwa ndani ya CCM sio CHADEMA isipokuwa hoja ya msingi ya ufisadi iliyokuwa ikipigiwa kelele ndiyo hiyo iliyoibuka hivi sasa kuwa CCM wameamua kujivua gamba na haieleweki ni nani mwenye ujasiri wa kuwavua gamba wenzake akawa si fisadi.
  Hoja za ufisadi zilizoibuliwa kwenye mikataba mingi ya ulaghai ya Dowans, IPTL, Meremeta, Kiwira, Buzwagi na mabilioni ya fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA) hakuwezi kuiacha CCM ikaendelea kuwa salama kwa kuwa waliohusika wako humo humo.
  Haiwezekani wezi na mafisadi katika mipango hiyo yote leo hii wavigeukie vyama vya upinzani kuwa vina lengo la kukidhoofisha chama hicho tawala kumbe hoja zilizo mbele ya jamii za ufisadi zimechochewa na viongozi wa kisiasa ndani ya CCM na kutekelezwa na watendaji wa serikali waliopewa mamlaka ya kulinda na kusimamia raslimali za nchi.
  Kama ufisadi umeweza kuwajengea umaarufu viongozi wa CCM na wengi wakawa na kiburi kwa kuwa wamefanikiwa kuunda kampuni hewa za Kagoda na leo hii wanatolewa kwa dizaini ya kuvuliwa gamba, hakika itakuwa vigumu kuweza kujisafisha hata kama kitahitaji kujisafisha kwa kauli za upole na unyenyekevu wakitaka wasamehewe na umma walioutafuna.
  Umaskini huu na kilio cha wananchi wengi kuhusu hali ngumu ya maisha, kupanda kila siku kwa gharama za maisha, kupanda juu kila siku kwa bei ya mafuta ya dizeli na petroli, kushindwa kuboreshwa kwa huduma za kijamii na miundombinu imara huko kote kumesababishwa na ufisadi uliokuwa ukilelewa kama yai sasa limegeuka tufe la chuma cha pua kila mtu anaogopa kuliyeyusha.
  Hayo yote hayajaletwa na CHADEMA, wala CUF,wala NCCR-Mageuzi, wala TLP wala chama chochote cha upinzani, madhambi ya ufisadi ndio tunda la usaliti kwa kuwa viongozi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali hawawezi kukisafisha chama chao hata kama wamevuliwa gamba nikiamini kuwa madhara ya ufisadi yaliyowaumiza wananchi wanyonge hayawezi kufutika.
  Ikumbukwe kuwa CHADEMA wanafanya kazi ya upinzani kamwe hawawezi kufanya kazi ya kukisifia chama tawala kilichojiharibu chenyewe kwa makovu yasiyoweza kufutika ya ufisadi, wanachokifanya CHADEMA ni kuwaambia ukweli wananchi jinsi nchi ilivyotafunwa na mafisadi waliopewa dola kwa miaka yote hii tangu nchi ilipopata uhuru.
  Harakati za kambi ya upinzani ni kuhakikisha kuwa mabaya yanayofanywa na chama tawala na serikali yake yanawekwa hadharani, ukiona chama cha upinzani kinatetea uozo wa chama tawala ujue hapo kuna ajenda ya siri na ajenda hiyo haiwezi kufika popote kwa kuwa wananchi wanajua fika wapi walipotoka na wapi wanakwenda.
  Inaumiza tena inauma sana kuona ongezeko la matabaka kati ya matajiri na maskini linazidi kuongezeka, watu wenye fedha wanazidi kujitenga kwa mbali na kundi la wanyonge,masikini wasiokuwa na chochote ambao waliamini kuwa hawa wanaowaongoza ni waadilifu lakini sasa wanashangaa kuona eti binadamu nao wameanza kujivua gamba mithiri ya nyoka.
  Wiki iliyopita nilisema Gamba la CCM haliwezi kuvulika, nairudia kauli hiyo nikiamini kabisa kuwa ni vigumu sana kuijenga upya Tanzania imara na yenye uchumi madhubuti kama mfumo wa kiutawala uliojiotesha mizizi mirefu ndani ya chama hicho kwa sura ya ufisadi haiwezi kung'olewa.
  Ndani ya CCM kuna miungu watu na ndani ya watendaji wa serikali kuna miungu ya ufisadi ambao madhara ya uswahiba na kulindana kwa sura za kuoneana aibu ndiko kuliko ifikisha CCM hapa ilipo, hakuna mchawi anayekiloga chama hicho na wala CCM wasilalamike kuwa mlozi wao ni CHADEMA katika hali ya sasa lawama hizo haziwezi kuwaingia watu makini, CCM wanajimaliza wenyewe.
  Hakika naamini hivyo na bila shaka wale waliotolewa kafara kuwa ndio gamba la ufisadi waliojiuzulu na wanaotakiwa kujiuzulu kwa imani hiyo,CCM inaweza ikawa imefanya kazi ya kuzalisha maadui zaidi wa ndani kuliko kuponya mtafaruku uliokuwepo kabla kwani kila kiongozi aliyeondoka ana kundi la wafuasi wake watiifu na kama uwezo wa kuupata urais mwaka 2015 wanao kwa kuwa wana pesa.
  Naamini kwa kuwa pesa ndizo zinazomchagua kiongozi wa CCM na mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho,maajabu yanaweza kutokea ndani yake kwa kuwa uasi wa mafisadi wenye fedha unaweza kufanya kazi kubwa ya kuua nguvu za wanachama waadilifu wachache waliobaki nao wakavishwa gamba la ufisadi na kuamua ndivyo sivyo ili kuweza kumpata rais fisadi ajae kutoka CCM 2015.
  Hapo CCM hawapaswi kumtafuta mchawi na wala CHADEMA si mlozi wao, wanayoyatenda leo ndio mwanzo wa maandalizi kabambe ya kumpata mgombea urais kutoka CCM atakayeweza kusimama na kupambana na vyama vya upinzani na ili asiwe fisadi, Mungu ibariki sijui atatoka kambi ipi ndani ya mtandao au nje?
  Ili yale yaliyoandikwa katika historia ya CCM yaweze kutimia basi chama hicho kina kila sababu ya kuwaondoa bila aibu mafisadi wote kwa kuwa wanajuana kwa majina na makazi yao na miradi yao na idadi ya watoto wao wanaosomeshwa nje ya nchi kwa fedha za wanyonge lakini wao kwa wao wanapongezana huku wakiwaacha watoto wa makabwela wakihangaika kutafuta elimu kwenye shule za kata zisizokuwa na walimu.
  Kwa haya yote na mengine mengi yaliyoifikisha CCM hapa ilipo na kile kilichoelezwa kuwa wamejivua gamba,hayo yanaweza kuwa maajabu,lakini ndani yake kuna chuki na visasi ambavyo hakika,CCM haina haja ya kutafuta mchawi na kudhani kuwa adui yao mkubwa ni CHADEMA kumbe CHADEMA sio walozi,itafute mlozi wao, vinginevyo makubwa yatatokea na rais bora atayeyuka miongoni mwenu.


  [​IMG]
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  CHADEMA sasa ndicho chama ‘tawala'
  [​IMG]

  Martin Kaswahili ​

  [​IMG] TANGU kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge, na madiwani mwezi Oktoba mwaka jana, nchi yetu imeshuhudia matukio kadhaa ya kipekee ambayo huenda yakawa kiashirio cha matukio mengine makubwa na ya kihistoria katika siasa za Tanzania katika siku za usoni.
  Si nia yangu katika makala hii kudodosa kila jambo lililojitokeza wakati na baada ya uchaguzi huo ambao matokeo yake, hasa yale ya urais, yaliacha minong'ono na miguno miongoni mwa wananchi kiasi cha kuamsha chuki na uasi wa kimoyomoyo (passive resistance), uliopelekea kujengeka kwa ujasiri wa kupinga waziwazi yale yanayofanywa na watawala. Ujasiri huo ndiyo umekuwa chanzo cha maandamano makubwa na ya kihistoria ambayo yameitisha si serikali iliyoko madarakani tu bali hata chama kilichotakiwa kuwa chama tawala. Nitafafanua.
  Kwa kawaida, baada ya uchaguzi kumalizika na serikali kuundwa, kazi kubwa ya serikali mpya ni kuanza kutekeleza kwa vitendo ahadi zilizoahidiwa na viongozi wa chama tawala wakati wa kampeni za uchaguzi kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi. Kwa upande mwingine, vyama vya upinzani navyo huanza mara moja kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia wa kuikosoa, kuisimamia, na kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani, kwa njia ama ya bunge (kama chama kimepata wabunge) au kwa njia nyingine za kisiasa.
  Kwa mantiki hii, mara baada ya uchaguzi wananchi hutarajia kuona serikali yao ikianza kwa nguvu kutimiza wajibu wake wa kutatua kero zao bila kujali mashambulizi ya vyama vya upinzani kupitia bunge au majukwaa ya kisiasa. Hii ndiyo kawaida katika ulingo wa siasa za vyama vingi katika nchi zote zinazofuata mfumo wa kidemokrasia.
  Hutasikia mahali popote serikali iliyowekwa madarakani kwa kura halali za wananchi walio wengi ikitolewa kirahisi kwenye ajenda yake muhimu ya kuwatumikia wananchi walioichagua na kuanza kutumia muda wake mwingi kushughulikia chama au viongozi wa upinzani, kama inavyotoea sasa hapa nchini.
  Kwa upande mwingine, kazi ya chama kinachokuwa kimeshinda uchaguzi ni kuisaidia serikali na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao ya kufanyia kazi yale yaliyoahidiwa katika ilani ya chama hicho. Chama tawala hutakiwa kuwa mlinzi wa serikali iliyopo madarani kwa kuikumbusha wajibu wake na kuitetea kwa wananchi kwa njia za kisiasa.
  Kwa maneno mengine, CCM kwa kutumia jukwaa la kisiasa, kilitakiwa kuwa cha kwanza kuitetea serikali yake dhidi ya mashambulizi toka vyama vya upinzani badala ya kuiachia serikali kujitetea yenyewe kwa kutumia nguvu ya dola ya vitisho, mabavu, na propaganda za enzi za mfumo wa chama kimoja.
  Tangu siku ya kikao cha kwanza cha bunge la sita, ambapo wabunge wa CHADEMA waliamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati ya hotuba ya Rais ya ufunguzi wa bunge kuthibitisha msimamo wao wa kutokubaliana na ujanja uliotumika katika kuhalalisha ushindi wa rais Kikwete, serikali na chama tawala viliingia katika majaribu makubwa ambayo bado hawajaonekana kuyashinda.
  CHADEMA, kama chama cha upinzani chenye nia ya dhati ya kutwaa madaraka ya nchi kwa njia ya kidemokrasia, kilikuwa kimejipanga kuihenyesha serikali iliyoko madarakani tangu siku hiyo ya kwanza kazini.
  Na kwa vile wengi wetu tulikuwa hatujawahi kuona siasa za upinzani wa kweli zinavyofanya kazi, tuliduwazwa na kitendo cha wabunge wa CHADEMA kuondoka bungeni kiasi cha kuingiwa na hofu kuwa serikali na chama tawala wasingekubali kurambwa chenga za maudhi katika dakika hizo za mwanzo kabisa za mchezo bila wao kujibu mapigo kwa pupa. Tulihisi kuundwa haraka kwa mkakati maalumu wa kuichezea CHADEMA rafu za kila aina ili wasizidi kuiadhiri serikali na chama chake kwa kutumia mbinu zao za siasa za kidot.com!
  Na kama ilivyotarajiwa baada ya tukio hilo la kushtukiza bungeni, CCM walijipanga kuhakikisha CHADEMA inanyamazishwa kwa njia yoyote ile. Mbinu ya kwanza ilikuwa ya kutumia ‘vitisho' kupitia katibu wa itikadi na uenezi wa wakati huo, yaani John Chiligati.
  Kwa mtindo wa amri za kijeshi unaotokana na kazi yake ya zamani, Chiligati alitoa aliwaamuru wabunge wa CCM kuangalia uwezekano wa kupeleka azimio la ‘kuwafukuza' bungeni wabunge wote wa CHADEMA kwa kitendo chao cha kumdalilisha Rais wa nchi.
  Baadhi ya watu waliamini jambo hilo lingewezekana na kwa hiyo wabunge wa CHADEMA wangesimamishwa wasihudhurie vikao vya bunge. Lakini kwa wale wanaelewa demokrasia ya vyama vingi, na hasa inapotokea kuna chama makini cha upinzani kama CHADEMA inavyoinukia wakati huu, mbinu za CCM na serikali yake zilionekana za kizamani na hazikufua dafu mbele ya chama kinachoungwa mkono na nguvu kubwa ya umma uliochoshwa na ubabaishaji wa muda mrefu wa serikali ya CCM.
  Mwisho wa siku wabunge wa CHADEMA hawakufukuzwa au kuzuiwa kuhudhuria vikao vya bunge, na kazi ya kuihenyesha serikali ndio kwanza ikashika kasi. Umaarufu wa CHADEMA kama chama chenye msimamo na kisichobabishwa ukazidi kuongezeka. Kwani kila aliyekuwa na hofu kwamba CHADEMA ingetishwa, ingeminywa, na hatimaye kufyata mkia, alishangaa kuona ujasiri mpya wa kidemokrasia ukiota mizizi nchini.
  Vidonda vya maumivu ya ‘kuporwa' matokeo ya urais waliokuwa nayo wananchi nchi nzima yalianza kupata ahueni ya ghafla. Matarajio ya CCM na serikali yake ya kujiendeshea mambo kama vile nchi hii ni mali ya kundi dogo la watu wanaojiona wenye bahati ya kipekee yalianza kutoweka ghafla. Hofu kuu ikaanza kuwaingia viongozi wa serikali na Chama tawala, na mkakati wa kuibinya CHADEMA ‘kwa nguvu zaidi' ukapangwa.
  Yaliyotokea kwenye maandamano ya Arusha ulikuwa ni ushahidi wa wazi wa kuwepo kwa mkakati maalum wa kuhakikisha CHADEMA haiendelei kuipigisha kwata serikali na kukifunika chama tawala, kama ilivyotokea katika awamu ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Mabavu yaliyotumika kushambulia waandamanaji na hata kuzuia mkutano halali wa kisiasa, vikifuatiwa na propaganda za kufunika ukweli wa kilichotokea huko Arusha vilinikumbusha utawala wa kikomunisti wa Urusi ezi zile.
  Ni mtindo huo huo uliotumiwa zamani na wakoloni kwa lengo la kuwadhibiti waafrika wasidai haki yao ya kuwa huru kwa njia ya maandamano na mikutano. Kwa wanaoelewa historia ya serikali zinazotumia udikteta wa kidemokrasia, ukatili wa askari wetu kule Arusha ulikuwa wa kisiasa zaidi badala ya mbinu za kawaida za kuthibiti fujo.
  Linganisha matukio ya Arusha na maandamano yaliyofuatia kanda ya ziwa ambapo katika mikoa minne hakuna mtu hata mtu mmoja aliyeripotiwa kupoteza hata ‘kandambili' kwa kukimbia kipigo cha askari! Kule Arusha askari ndio waliowashambulia wananchi wasiona na silaha wala nia ya kupambana na mtu yeyote. Watanzania hawana utamaduni wa kushambulia askari bila kuchokozwa.
  Lengo la matumizi ya mabavu katika maandamano ya Arusha ilikuwa ni kutengeneza jukwaa la propaganda maalum ya kuuaminisha umma kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, kinachochea vurugu na ni hatari kwa nchi. Hata hivyo pamoja na jitihada za serikali na CCM kuelekeza lawama kwa CHADEMA kama chanzo cha vurugu na mauaji huko Arusha, wananchi waliamua kuzipuuza propaganda hizo na kuzidi kuiunga mkono CHADEMA.
  Kinyume na mipango na matarajioa ya CCM na serikali yake, tukio la Arusha liliamsha hasira ya wananchi nchini nzima dhidi ya uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji wa serikali ya chama tawala ambao huko nyuma ulivumiliwa kwa maumivu ya kimya kimya. Hali ya uasi wa kimomoyo ikazidi kushamiri. Huruma kwa wahanga wa mauji ya Arusha ikaongeza hamu ya wananchi kutaka kuwaonesha hadharani nguvu walio nayo kupitia chama kinachotetea maslahi ya wanyonge walio wengi.
  Kwa wepesi wao wa kuelewa mambo, CHADEMA wakaamua kukidhi kiu ya walio wengi. Wakaanzisha maandamano ya kupinga unyonyaji, unyanyasaji na dhuluma za wazi zinazofanywa na viongozi wa serikali na chama tawala.
  Hata hivyo kabla CHADEMA hawajanza maandamano yao nchi nzima, CCM wakapanga mkakati mwingine wa kucheza rafu bungeni. Kwa kumtumia spika wa bunge, ambaye tangu kuchaguliwa kwake ilijulikana wazi jinsi ambavyo asingeweza kuvaa viatu vya mtangulizi wake, wabunge wa CCM waliamua kupindisha kwa makusudi kanuni za bunge ili kuizuia CHADEMA isiunde kambi rasmi ya upinzani, kama ilivyokuwa kwa CUF katika awamu mbili huko nyuma.
  Mpango huu ulilenga kuzuia uwezo wa CHADEMA kuibua uoza ndani ya serikali kupitia kamati tatu za fedha wabungeni. Mkakati huu pia ulilenga kukigombanisha CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ili kuwaaminisha wananchi kwamba CHADEMA wanapenda kujitega na ni chama chenye ubinafsi.
  Kwa bahati mbaya mkakati huu ulifanikiwa kwa sehemu kubwa, na wananchi wakajionea wenyewe mchezo unaochezwa na CCM dhidi ya upinzani nchini. Vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP, CUF, na UDP vilijikuta vikiungana na Chama tawala katika kuunda ‘kambi isiyo ramsi ya upinzani' dhidi ya CHADEMA.
  Na kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi nchini, chama tawala ‘kilivipiga busu' vyama vidogo vya upinzani kwa lengo la kukishambulia chama kikuu cha upinzani! Siku hiyo CHADEMA kilionekana kama ndio chama tawala kwa jinsi kilivyovizidi umaarufu na mbinu vyama vingine vyote hata wakajikuta wanafunga ‘ndoa ya dharura' (marriage of convenience) ili kukikabili.
  Na tangu siku hiyo CCM na vyama vingine vimekuwa vikifanya kazi kama ndivyo vyama vya upinzani dhidi ya ‘chama tawala CHADEMA'. Lakini hata baada ya kuvipa ‘kumbato' vyama vingine vya upinzani bungeni, serikali na CCM hawakujua kuwa bao jingine la kisigino lilikuwa linakuja muda si mrefu.
  Maandamano ya kihistoria ya Mwanza yalipeleka msiba mwingine kwenye kambi ya CCM na serikali yake. Tofauti na matarajio ya wengi kwamba vurugu na kipigo cha Arusha vilikuwa fundisho tosha kuwatisha waandamanaji wengine kujitokeza kuwaunga mkono CHADEMA, maandamano ya Mwanza yalidhihirisha kile ambacho watawala wetu wamekuwa wakidhani hakipo yaani ujasiri wa watanzania kujitokeza hadharani na kuwaambia watawala ‘hatutaki kusukumwa'!
  Watu wa Mwanza, ambao huko nyuma walionekana kama ‘wateja watiifu' wa CCM, waliushangaza ulimwengu kwa kuonesha ujasiri ambao haujazoeleka hapa nchini. Damu ya mauaji ya Arusha ilikuwa imeanza kujenga taifa la wanaoweza kudai haki zao bila kutishwa na binadamu wenzao.
  Kuanzia Mwanza, Mara, Shinyanga hadi Kagera, CHADEMA walibeba kilio cha wanyonge juu ya ugumu wa maisha, kupanda kwa bei za bidhaa kulikochochewa na kupanda kwa bei za umeme, na wakati huo huo kuwepo kwa mgao wa umeme nchi nzima. CHADEMA iliwakumbusha wananchi juu ya ahadi walizopewa na viongozi wa CCM na jinsi ambavyo ahadi hizo zilikuwa hazitekelezwi kwa visingizio vile vile vya siku zote vya ‘kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia' na ‘kuharibika kwa uchumi wa dunia'.
  Kwa umahiri wao mkubwa katika kuwasilisha ujumbe, viongozi wa CHADEMA waliendelea kuushawishi umma kwamba serikali iliyopo madarakani haina uwezo wala nia ya dhati ya kutatua matatizo yao sugu bali ipo kwa ajili ya kuneemesha vigogo wachache na familia zao kwa njia za kifisadi kama vile ya Dowans, ambayo serikali ilikuwa tayari kuilipa mabilioni ya fadha za walipa kodi bila hata chembe ya woga wala aibu.
  Kama chama cha siasa chenye kuzijua kanuni za mchezo wa siasa za kidemokrasia, CHADEMA waliishambulia serikali kiasi cha kuifanya ilazimike kutekeleza baadhi ya madai halali ya wananchi. Moja ya mambo ambayo serikali ilikubali kuyatekeleza baada ya shinizo la CHADEMA ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa kuandika upya katiba ya nchi, kitu ambacho CCM haikuwa tayari kukifanya na wala haikukiingiza katika ilani yake ya uchaguzi uliopita.
  Jambo jingine lililotimizwa na serikali kwa shinikizo la maandamano ya CHADEMA ni amri ya Waziri Mkuu ya kuwataka wafanya biashara wa sukari nchini kushusha bei ya bidha hiyo toka shilingi 2000 hadi 1700. Suala hili lilitekelezwa muda wa saa chache tu baada ya CHADEMA kuanza kulitumia kama mfano wa bidhaa zinazozidisha ugumu wa maisha ya wananchi wa kawaida.
  Baadaye tukasikia Rais, akiwa katika ziara ya kutembelea wizara ya nishati na madini, akiomba bei ya umeme ipunguzwe ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi. Yote haya yalikuja kutokana na shinikizo la chama kimoja cha upinzani kinachojua wajibu wake. Kweli CHADEMA waliipelekesha serikali utadhani wao ndio chama tawala!
  Hata hivyo, wakati CHADEMA wakifanikiwa kuiadabisha serikali kiasi cha kuanza kutimiza matakwa ya wananchi, CCM waliamua kuja na rafu kali zaidi kuizuia CHADEMA isiendelee kuchukua nafasi yake. Safari hii Rais na mwenyekiti wa CCM aliingia ulingoni kuongeza nguvu za mapambano dhidi ya CHADEMA. Kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa pili, Rais aliudhirishia umma wa Tanzania jinsi CHADEMA ilivyokuwa inaihenyesha serikali yake.
  Mbali na kujikuta akijibu baadhi ya madai ya CHADEMA yaliyotakiwa kujibiwa ndani ya siku tisa, Rais alianzisha propoaganda mpya za kuishambulia CHADEMA kwa kulalamika kuwa ilikuwa ikiwachochea wananchi waanzishe vurugu za kuipindua serikali yake kwa njia ya maandamano. Wengi waliduwazwa na maneno hayo ya woga kutolewa na amiri jeshi mkuu wa nchi.
  Hata hivyo baadhi yetu tuligundua mapema kuwa huu ulikuwa ni mkakati mwingine wa kuhakikisha CHADEMA inadhibitiwa. Mpango huu ulilenga mambo kadhaa. Kwanza kuwatisha tamaa wananchi ili wasizidi kuiunga mkono CHADEMA, kwa kuwaaminisha kuwa CHADEMA kilikuwa kinaandaa maasi nchini, kitu ambacho serikali ingekuja kukizima kwa nguvu ya dola na kusababisha wananchi wengi kuumia vibaya.
  Pili, kuharibu taswila CHADEMA kwa kukionesha kuwa ni chama cha vurugu na viongozi wake washari wanaopenda madaraka kwa gharama yoyote.
  Tatu, kuwapa makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa serikali, hasa mawaziri, kitu cha kufanyia propaganda nchi nzima kwa lengo la kuuaminisha umma kwamba mandamano ya CHADEMA hayana lengo zuri la kisiasa hivyo wananchi wasiyaunge mkono na ikishindikana nguvu zitumike kuyadhibiti, ikiwa pamoja na viongozi wake kupigwa, kuumizwa, au hata kuundiwa mashitaka ya uongo kwa kisingizio kwamba ‘serikali ililazimika kuchukua hatua za ziada kuepusha umwagaji damu nchini'.
  Sote tunakumbuka kilichotokea baada ya hotuba ya Rais. Waliokuwa wametayarishwa katika mkakati huu walianza kujitokeza. Kwanza tulimskia waziri wa nchi mahusiano, Stephen Wassira, kama kawaida yake, akitumia lugha za kibabe kuwatisha CHADEMA eti ‘wasije kuilaumu serikali' kwa kutumia nguvu kuwashughulikia kama hawataacha uchochezi kwenye mikutano yao.
  Kisha tukamsikia msajiri wa vyama vya siasa bwana John Tendwa akiwaandikia CHADEMA barua ya kuwaonya wasitumie ‘lugha za matusi' katika mikutano yao vinginevyo angekifutia chama usajiri wa kudumu. Baadaye wakafuata kina Anna Kilango Malecela na viongozi wengine wa aina hiyo, kabla Sophia Simba na Bernard Membe hawajaja na mpya kwa kudai kuwa maandamano ya CHADEMA yalikuwa yanafadhiliwa na mataifa ya nje kupitia balozi zake hapa nchini. Kana kwamba haitoshi, tukasikia vijana wa Dar es Salaam wameandaa maandamano kupinga maandamano ya CHADEMA.
  Nasikia maandamano haya ya vijana yalizuiwa na polisi kwa kisingizio cha kuleta usumbufu kwa wakazi wa jiji. Taarifa zilizoko ni kwamba mpango huu wa maandamano ya vijana ulipangwa ili polisi wawanyime kibali cha maandamano kwa lengo la kuandaa mazingira ya kuja kuwanyima CHADEMA kibali cha maandamano watakapotaka kuandamana popote Dar es Salaam. Tunasubiri kujionea.
  Baada ya kiini macho cha maandamano ya vijana wa Dar es Salaam, yalifuatia maandamano ya kina mama kupinga maandamano ya CHADEMA, ambayo pia hayakuleta mvuto wowote. Baadaye tukasikia mpango wa maandamano ya vyama vyote vidogo vya siasa nchini kupinga maandamano ya CHADEMA, kabla hajatokea Profesa Lipumba huko Tanga na kuwashangaza wengi kwa kuishambulia CHADEMA kwa namna ambayo iliwadhihirishia wengi kwamba kweli sasa CUF ilikuwa imeungana rasmi na CCM kikishambulia CHADEMA.
  Hapa ndipo nilipoamini bila shaka yoyote kwamba kwa sasa, CHADEMA ndio chama tawala, ambacho hakikupewa tu nafasi ya kuunda serikali kutokana na kuibiwa matokeao ya uchaguzi mkuu. Itakuwaje serikali na vyama karibia vyote vya siasa vijikute vikiungana katika kuishutumu, kuibeza au kuishambulia CHADEMA kana kwamba ndio chama tawala?
  Ndio maana wananchi wameamua kuweka pamba masikioni na kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuihujumu CHADEMA. Tangu Rais alipotumia muda wake mwingi wa hotuba kuishambulia CHADEMA ikifuatiwa na maandamano-maigizo na vitisho vyote vya kuishughulikia CHADEMA, wananchi wamezidi kuelekeza mioyo yao kwa CHADEMA huku wakiiona CCM na serikali yake kama wasaliti.
  Iweje chama ambacho hakina serikali, hakina idadi kubwa ya wabunge, na hakina pesa kama CCM, kitese akili za viongozi wa nchi kwa kiasi hiki? Kwa nini chama kinachounda serikali kiungane na vyama vingine vyote nchini kukishambulia chama kimoja tu cha upinzani utadhani ndio chenye serikali iliyoko madarani?
  Kwa nini serikali ihangaike kuandaa watu, vikundi, na hata dola kushughulikia namana ya kuzima harakati halali za kisiasa za chama kimoja tu cha upinzani nchini? Nadhani haya yote yanatokea kwa sababu moja tu, kwamba katika mioyo ya watu wengi, CHADEMA kwa sasa ndio chama tawala japo hakiongozi toka ikulu. Ukweli ndio huo.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  UVCCM yaipa CCM siku 30


  na Grace Masha, Meru


  [​IMG] UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha umetoa siku 30 kwa CCM Taifa kushughulikia kero zinazoukabili umoja huo vinginevyo watajivua uongozi.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano juzi, Katibu wa UVCCM, jimbo la Arumeru Mashariki Christopher Palangyo, alisema tayari wameshapeleka barua makao makuu ya CCM Dodoma kuelezea azma yao hiyo.
  Wana UVCCM hao wanataka kupatiwa ofisi na vyombo vya usafiri vitakavyowawezesha kuwafikia wananchama wao kwenye maeneo yote ya jimbo hilo kwani suala hilo linaelezwa kuwa kero kubwa kwa wanachama hao hivyo kusababisha wengine zaidi ya 2,000 kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Alisema kuwa walifikia uamuzi huo baada ya kuona viongozi pamoja na watendaji wengine wa umoja huo wanakosa ofisi maalumu ya kufanyia kazi zao huku wakitembea kwa miguu umbali wa kilomita zaidi ya 100 ili kuwafikia wanachama hao.
  Alisema katika barua hiyo walitaka CCM Taifa kuhakikisha kuwa jimbo la Arumeru Mashariki linapewa hadhi ya wilaya kichama ili kufanya kazi kwa urahisi zaidi kwani kwa sasa kutokana na hali ya kijiografia kuwa mbaya husababisha baadhi ya viongozi kushindwa kufika kwenye maeneo yote hasa ya jimbo hilo.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Jamii Forum yaijibu CCM


  na Hellen Ngoromera


  [​IMG] MTANDAO wa Jamii Forums umesema madai ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Tanzania Bara), Pius Msekwa, kuuhusisha mtandao huo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ya kubuni na yana lengo la kuwatisha Watanzania kutoa maoni yao kwa uhuru kupitia mitandao mbalimbali.
  Mtandao huo ulianzishwa mwaka 2006 na madai hayo kwamba mtandao huo unafanya kazi hatarishi dhidi ya CCM na serikali yana lengo la kuuchafua na kuuvunjia hadhi ambayo imejijengea kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu.
  "…Ni jaribio dhaifu la Chama cha Mapinduzi kubebesha lawama mitandao ya intaneti kwa mapungufu na migongano iliyojitokeza ndani ya chama chao katika miaka michache iliyopita na siku za karibuni," ilisema taarifa hiyo.
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mtandao huo unaotembelewa na wastani wa watu 20,000 kwa siku umekanusha madai hayo kwa maelezo kuwa hayana msingi wala ukweli.
  "Tunapinga vikali madai yasiyo na msingi ya Chama cha Mapinduzi kuhusu umiliki, malengo na nafasi ya JF (Jamii Forums) katika medani ya vyombo vya habari nchini na mchango wake katika mijadala ya kisiasa nchini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
  Ilisema kwa mara ya kwanza waliyasoma madai hayo yakiwa yameripotiwa kwenye magazeti mawili ya kila siku.
  Kwa mujibu wa mtandao huo hawajawahi kufadhiliwa na CHADEMA lakini wanaamini kuwa wamelengwa na CCM kwa sababu katika miaka mitano iliyopita mtandao wao umekuwa ukishiriki vilivyo kufichua kashfa mbalimbali ambazo zimelindima nchini hatimaye kusababisha chama tawala kuamua kujivua gamba.
  Mtandao huo umesema madai hayo yamesomwa na kusikiwa na watu wengi nchini hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa. Yamesababisha wasiwasi usio wa lazima kwa wanachama 40,000 ambao wametawanyika pote nchini na katika kila kona ya dunia.
  Madai hayo ya CCM yalitolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Msekwa wakati wa kutambulisha uongozi mpya wa chama hicho.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  CCM inajiandalia anguko jingine!
  [​IMG]

  Absalom Kibanda ​

  [​IMG] CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara nyingine tena kimechafua hali ya hewa kisiasa nchini, safari hii kikija na kaulimbiu tata ya kujivua gamba iliyoasisiwa, ikaratibiwa (Waswahili wanasema – kimkandamkanda) na kuendeshwa kimafia na Mwenyekiti wake wa taifa, Rais Jakaya Kikwete.
  Sina shaka hata kidogo kwamba, wasomaji wazuri wa gazeti hili, watakuwa wamepata picha halisi ya kile kilichotokea mjini Dodoma hivi karibuni, kikianzia katika kikao cha Kamati Kuu (CC) na baadaye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC).
  Mchezo. Nauita mchezo kwa kuwa hauna tija wala matokeo yoyote ya mabadiliko ya kimfumo au kifalsafa, ulianza katika Kamati Kuu iliyoketi kwa siku mbili na kuhitimishwa na hatua ya Kikwete kumtumia mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika, Abdulrahman Kinana kubeba ajenda yake.
  Ajenda katika mchezo huo wa kuigiza na uliokuwa umepangwa mapema kabisa, ilikuwa ni pendekezo la kuwalazimisha wajumbe wote wa sekretarieti na kamati kuu ya chama hicho kujiuzulu nafasi zao.
  Maelezo yasiyo ya kisayansi yaliyotolewa na ambayo tayari yalikuwa mitaani wiki mbili kabla ya kikao chenyewe yalikuwa na maelezo dhaifu: Kwamba wajumbe wa vikao hivyo viwili walikuwa wameshindwa kumsaidia Mwenyekiti wao, Rais Kikwete.
  Watu wenye akili zao ndani ya kikao hicho na nje, walijua fika kwamba, walengwa wakuu katika ajenda hiyo walikuwa ni aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusufu Makamba, Rostam Aziz na Andrew Chenge.
  Kwa muda mrefu hoja dhidi ya Makamba kwamba alikuwa ameshindwa kazi, ilikuwa mtaani na yeye mwenyewe mara kadhaa alishapata kujaribu bila mafanikio kuitolea ufafanuzi.
  Kwa upande wao, Chenge na Rostam walitakiwa kutemwa, lengo la kwanza likiwa ni kuifanya ile kauli aliyoitoa Rais Kikwete, Februari 5, mwaka huu wakati chama hicho kikisherehekea miaka 34 ya kuzaliwa kwake, alipotumia kaulimbiu ya kujivua gamba ionekane ilikuwa halisi na yenye mwelekeo madhubuti.
  Panga lililowalenga wanasiasa hao watatu, kwa bahati mbaya au kwa kupangwa lilijikuta likimkumba pia Bernard Membe, mmoja wa wanasiasa waliokuwa wakiunda sekretarieti, akiwa Mkuu wa Idara ya Siasa na Mambo ya Nje na mjumbe pia wa Kamati Kuu.
  Hatua ya Rais Kikwete kutolirudisha jina lake ili lipigiwe kura tena wakati alipokuwa akipendekeza majina mapya ya wajumbe wa CC baada ya ile ya kwanza kujiuzulu, bado imeacha maswali mengi.
  Wako wanaoamini kwamba, msingi wa hatua hiyo ya Rais Kikwete ilikuwa ni kuwaweka kando wanasiasa wote ambao tayari walikuwa wameshaanza kukigawa chama katika misingi ya makundi ya urais wa mwaka 2015.
  Jina la Membe kama yalivyo majina ya wanasiasa wengine kama Profesa Mark Mwandosya, Emmanuel Nchimbi, Edward Lowassa, Samuel Sitta, Frederick Sumaye na Mathias Chikawe, yanahusishwa na urais na hakuna hata mmoja miongoni mwao ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu.
  Ukiliacha hilo na kurejea katika hoja ya ufisadi, ni wazi kwamba tuhuma dhidi ya Chenge na Rostam zilikuwa ni moja ya majibu rahisi yaliyokuwa yakificha maelezo halisi yanayokihusisha chama hicho na swali gumu linaloitaka CCM ieleze kwa kina ni kwa namna gani dhana hiyo nzima ya kujivua gamba itamaliza wingu hilo linalokitafuna chama hicho na serikali yake kwa miaka mingi sasa.
  Ni jambo la kutia shaka sana kwamba wakati kina Kikwete, Kinana na wenzao wakikuna vichwa kutafuta majibu ya haraka haraka ya kukinusuru chama chao na hatima iliyo wazi ya anguko lake linalokuja kwa kujongea kadiri muda unavyozidi kusonga mbele, walisahau kabisa kuzigeuza fikra ili zimuelekee mwenyekiti binafsi na kumchambua ni kwa kiwango gani, yeye mwenyewe alikuwa ameshindwa kufanya kazi na sekretarieti na kamati kuu yake.
  Kwa namna ninavyomfahamu Kinana, ninao uhakika wa asilimia 100 kwamba wakati wote walipokuwa wakijadiliana na wenzake ndani ya chama chake kuhusu hatua wanazopaswa kuzichukua, ukweli kwamba moja ya matatizo makubwa yanayokikwamisha chama hicho ni Kikwete mwenyewe aliliona.
  Tunapaswa kuomba Mungu katika siku isiyo na jina huko tuendako, tuje kumsikia Kinana kwa maneno yake mwenyewe akikiri kwamba tatizo la kwanza na la msingi ambalo limekikwamisha chama chao na hususan serikali ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni mwenyekiti wake, Rais Kikwete.
  Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, leo hii unapoandika maneno ya namna hii, yenye mwelekeo wa kumsema vibaya Kikwete, marafiki zake na wale wataalamu wa masuala ya intelijensia, wanaofanya mambo yao wakitumia kanuni moja tu ya hesabu za kujumlisha na mbinu ya kuoteshwa majibu ya matatizo ya taifa hili huwa wepesi kuzusha na kutunga uongo kwamba fulani ametumwa na fulani ili amchafue fulani.
  Wazushi hawa ambao baadhi yao ni makachero wanaopaswa kujua mapana na marefu ya kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuwahadaa viongozi wetu wakuu ndio ambao walikuwa nyuma ya ajenda nzima ya CCM kujivua gamba.
  Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wazushi hao ambao leo hii wamefikia hatua ya kuwa ndiyo ‘think tanks' ndani ya CCM na serikali yake wakiongozwa na kachero mmoja mwandamizi aliyeingia katika siasa, ndio waliokuwa pia nyuma ya hoja ya kuwapa siku 90 baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi walio wajumbe wa NEC ambao kwa muda mrefu majina yao yamechafuka.
  Ni wazushi hao ambao kwa kujua au kutokujua baada ya hoja yao hiyo ya kuwaandama watuhumiwa wachache wa ufisadi kuonekana ikipwaya na hata kufikia hatua ya kushambuliwa katika vyombo vya habari na ndani ya vyama vya siasa, wameanza kupindua maneno.
  Sasa wazushi hao wanayatuhumu baadhi ya magazeti, likiwamo hili kwamba eti yanatumiwa na mafisadi ili kumchafua Rais Kikwete.
  Kwa kauli hiyo hiyo, wazushi hao wamemlisha ujinga wao, Katibu wa Idara ya Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, ambaye naye hata kabla ya kufikiri na kuchanganua mambo ameanza kupita akikishambulia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa kwa kutumiwa na mafisadi eti kumchafua Rais Kikwete.
  Nape na wazushi wenzake hao wanasahau kwamba, msimamo wa magazeti wanayoyashambulia kama ‘Tanzania Daima' kuhusu Kikwete na ufisadi wanaojaribu kuufanyia usanii hata kabla hawajabuni nadharia yao ya kujivua gamba haujapata kubadilika na utaendelea kubakia na kuwa ule ule siku zote.
  Hivi Nape na makachero wengine wanaoasisi michezo ya kisiasa ndani ya CCM wanapojaribu kuitumia dhana ya kujivua gamba kama mkakati wa kuzima kishindo cha mabadiliko kinacholikumba taifa leo wanadhani Watanzania hawajui kwa mapana na marefu ukweli wote kuhusu ufisadi hapa nchini?
  Hivi CCM hii inayojaribu leo hii kujiokoa kwa gharama ya kusalitiana, kulana wenyewe kwa wenyewe kisiasa (political cannibalism) na kutoana kafara hata katika kashfa kama za Kagoda na Richmond haijui kuwa tuko wengi tunaojua kuwa ushiriki wake ni mpana zaidi na unawagusa wakubwa wengi zaidi ndani ya chama hicho tawala na serikali yake?
  Itakuwa ni dharau mbaya dhidi ya Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima iwapo wanasiasa wa aina ya Nape na wenzao watafikiri kwamba wanaweza kutujumuisha katika kundi la watu wanaoyashangilia mageuzi hewa yanayoendelea kufanywa ndani ya CCM leo kwa lengo la kuwahadaa wananchi.
  Litakuwa ni jambo la kututia aibu iwapo sisi wa Tanzania Daima pia tutaingizwa kichwa kichwa katika sanaa mpya ya CCM ya ‘kujivua gamba' hata tukaisahau na kuipuuza orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa 11 wa ufisadi iliyosomwa na Dk. Slaa, Septemba 15, mwaka 2007.
  Yatakuwa ni matusi dhidi ya uwezo wetu wa kufikiri iwapo CCM itafikiri kwamba hiki kiinimacho chao kipya wanachokifanya sasa kinaweza kikatufanya tuweke kando madai yenye harufu ya ukweli yatakaoendelea kuitafuna Serikali ya Awamu ya Nne kwamba iliingia madarakani kwa ushawishi wa nguvu ya fedha, ilipatikana kutoka katika Akauti ya EPA na kupitia katika akaunti ya Kagoda.
  Itakuwa ni fedheha kwetu iwapo tutaupuuza ukweli ulio dhahiri kwamba tatizo la ufisadi ndani ya CCM na serikali yake haliwezi kumalizwa kwa kuwaruhusu viongozi na makada wa chama hicho wahujumiane kisiasa kwa malengo ya kusaka madaraka, tena kwa gharama za kufifisha upepo wa mabadiliko ya kisiasa ambao kwa sasa unaongozwa na CHADEMA.
  Rais Kikwete na timu yake mpya ya uongozi ya CCM wanapaswa kutambua kuwa kama walivyokwama wakati walipojaribu kuinunua ajenda ya ufisadi kwa njia mbalimbali kupitia bungeni, mahakamani, TAKUKURU na kwingineko ndivyo watakavyokwama pia safari hii wanapojaribu kupanda farasi mpya waliyempachika jina la kujivua gamba.
  Kwa sababu hiyo, wanapaswa kuanza kutambua mapema kabisa kwamba, maamuzi waliyofanya Dodoma hivi karibuni, japokuwa leo hii yanashangiliwa na wengi ndani na nje ya chama hicho ni kaburi walilojichimbia wenyewe.
  Nyuma ya mabadiliko hayo ya CCM Dodoma, naona kuzaliwa Maalim Seif mpya. Naona kuibuka kwa Jacob Zuma mwingine na kwa hakika tunaweza tukampata Raila Odinga wetu. Tusubiri tuone. Huko ndiko TUENDAKO.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  CCM na ‘gamba' la ufisadi
  [​IMG]

  Bakari M. Mohamed ​

  [​IMG] CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinadai kimejivua gamba! Inawezekana kwa mtazamo wa propaganda ikadhaniwa ni kujivua gamba la nje na kubakisha gamba la ndani lenye ukale na ukuukuu uleule.
  Ni kawaida ya vyama vya siasa vinavyokaa madarakani na kushika dola kwa muda mrefu kama CCM kupoteza mwelekeo wake wa asili kwa kumezwa na viongozi wenye uchu, tamaa na uroho wa kutumia siasa katika kujinufaisha kifisadi.
  Hivi ndivyo CCM ilivyofanya tangu pale ilipopoteza mwelekeo wa kujenga jamii ya watu waliyo sawa na huru. CCM, kama chama kilichofisidika, kilianza kupotea njia yake ya ‘ujamaa na kujitegemea' baada ya kuacha mapendekezo ya chama yaliyotolewa wakati chama hicho kilipokuwa kinatimiza miaka kumi, yaani mwaka 1987.
  Tathmini ya chama ilionyesha wazi juu ya kupoteza mwelekeo katika kusimamia ujenzi wa jamii isiyokuwa na dhuluma, vitisho, uonevu na aina zote za ufisadi.
  Kwa ujumla, viongozi waandamizi wa CCM walimezwa na au kuwekwa ‘mtu-kati' na mafisadi waliojipenyeza ndani ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) na hata kuathiri maamuzi na utendaji wa chama. CCM, badala ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kama ilivyodhaniwa kwenye falsafa ya chama, kiligeuzwa chama cha wafanyabiashara matajiri na mafisadi! Huu umekuwa mwendo wa siasa za ndani ya CCM tangu pale chama hicho kilipoliua Azimio la Arusha na kutupilia mbali maadili ya uongozi wa siasa.
  Siasa imekuwa ikitumiwa na baadhi ya mafisadi kwenye mduara wa ndani wa CCM (CC na NEC) katika kufanikisha mipango ya kimafia na kushadidi kwa vitendo vya ujambazi wa kiserikali. Miongoni mwa mambo anuai yanayoanishwa kwenye gamba la ufisadi lililovishwa kwenye utendaji wa CCM ni: ufisadi wa kimfumo; ufisadi wa ndani ya mfumo; ujambazi wa kiserikali; kunyonga haki ya kukosoa na kukosolewa; na kuwaacha wafanyabiashara waendeshe chama kama kampuni. CCM imefanywa kama "shamba la bibi" kwa wafanyabiashara mafisadi kuwekeza mitaji yao inayotokana na fedha haramu na au fedha chafu!
  Ufisadi wa kimfumo umeifanya CCM inuke ufisadi kuanzia kada za chini (kwenye mashina, matawi na kata), wilaya, mikoa hadi taifa. Uongozi wa CCM, baada ya kuvurugwa kwa maadili ya siasa, umekuwa ukitolewa kwa ununuzi wa kura na wapiga kura na hata wakati mwingine kwa matumizi ya hila, ghiliba, uonevu na vitisho! Mafisadi wenye satwa (uwezo na nguvu) ya fedha wamekuwa wakipanga nani awe kiongozi na awatumikie mafisadi kwenye mfumo na ndani ya mfumo.
  Mfumo wa chama wa ndani (CC), katikati (NEC) na nje (wanachama wa kawaida) umefanywa kuwatumikia watu wachache wenye nguvu ya kuathiri maamuzi vile watakavyo kwa kuwa sehemu kubwa ya viongozi wamerogwa na kurogeka kwa fedha chafu inayotumika katika kuendesha siasa za kifisadi kwa manufaa ya ufisadi na mtandao wa ufisadi wa kimfumo. Hata hivyo, ufisadi wa ndani ya mfumo umeenea kwenye mifumo inayounda mfumo mzima wa CCM – uongozi wa kifisadi unaofanyakazi kwa maslahi ya viongozi mafisadi wa ndani ya mfumo – pamoja na msonge wa utawala wa chama.
  Ndani ya CCM kumevamiwa na watu wenye tamaa ya kushika uongozi na au madaraka ya kuongoza hata kwa kuvuruga mfumo wa kuongoza! Ni rahisi sana ndani ya CCM kuona watu wakifanya urafiki wa moja kwa moja na wafanyabiashara wenye mafungamano ya kifisadi ili chama kishinde! CCM imekuwa ikitumia fedha nyingi na chafu kwenye chaguzi zake katika kuhakikisha kwamba viongozi wenye dhamira ya kuwatumikia mafisadi wanapata nafasi ya kushika nafasi hizo kwa manufaa ya kifisadi na mfumo wa ndani wa kifisadi.
  Chama kimefanywa kama ‘genge' la watu wachache wenye maamuzi ya kuendesha nchi kwa kutumia nguvu ya uwezo inayotokana na mafungamano ya kifisadi baina ya viongozi waandamizi wa CCM na wafanyabiashara matajiri na mafisadi papa wenye nia ya kuwatumia kwa faida ya mtandao.
  Hapa ndipo unapoweza kuona jinsi wafanyabiashara wenye kumiliki siasa za kifisadi walivyoweza kupata nafasi hata za kutumikia CCM kama viongozi waandamizi, kama vile kuwa mweka hazina wa CCM taifa na au meneja wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM (2005).
  CCM isifanye mzaha na hali ya ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo uliopo ndani yake. Kwa kuwa mtandao wake umeenea kwenye ngazi zote na waliyefanyakazi ya kuubuni, kuutengeneza, kuusimamia na kuuendeleza mtandao wa kifisadi ndani ya CCM wana nguvu nyingi na mbinu za mikakati; lazima CCM ijichunguze kutokea nje na ifanyekazi ya ziada kuanzia ndani!
  Mwenyekiti wa CCM taifa lazima ajivue au avuliwe ‘gamba' la uswahiba alionalo baina yake na mafisadi ambao wengi wao ndio waliomuunga mkono na kumpatia usaidizi wa hali na mali kwenye harakati zake za kugombea uongozi wa nchi na chama.
  Uswahiba uliopo kwenye mzingo wa ndani wa CCM (japokuwa CC imepanguliwa) unaweza kuchukua sura mpya ya kuwatumia wajumbe na viongozi wapya kwa utumizi wa mbinu zile zile zilizotumika kuingiza biashara na hatimaye kukifanya chama kuwa kampuni la wenye hisa mafisadi wanaotumia ufisadi kama mtaji wa kuendeleza maslahi ya kifisadi.
  Wengi wa viongozi wa iliyokuwa CC walikuwa na uswahiba wa moja kwa moja na baadhi ya mafisadi ‘papa' na hata wakati mwingine mafisadi hao waliweza kuathiri maamuzi ya kushindwa kutenganisha bishara na siasa!
  Haikuanza jana kusemwa majukwaani na kuandikwa na waandishi, wapembuzi na wachokonozi kwamba CCM ni chama cha mafisadi kwa vile maamuzi yake yanaathiriwa na mafisadi na au mtandao wa kifisadi uliyojikita kindakindaki kwenye CCM na NEC ya CCM.
  Viongozi wa CCM waliziba masikio kwa nta na kuendelea na mwendo mdundo hadi pale walipozidiwa na kuona chama chao kinapoteza ushawishi wake kwa wananchi na hata wananchi kupoteza matumaini na kutafuta vyama mbadala.
  Kutokana na kukomaa kwa ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo, CCM ilikuwa inafanya ujambazi wa kiserikali kwa kuwaruhusu mafisadi kuwaibia wananchi kwa mgongo wa kiserikali kwa serikali kuridhia na au kusimamia kuvunjwa kwa sheria na kanuni mbalimbali kwa maslahi ya mafisadi na mitandano ya kifisadi.
  Mafisadi wamekuwa wakitumia nafasi ya serikali dhaifu kufanikisha mipango yao nyeti katika kujinufaisha na kuunufaisha mtandao wa kifisadi unaounganisha nguvu za mafisadi waliyo ndani ya CCM na wale wa nje (wanaowatumia mafisadi waliyo ndani).
  Kwa jinsi hii, wananchi (wakulima na wafanyakazi) walalahoi wamekuwa wakiminywa na kukamuliwa na mafisadi kwenye nyanja zote za uchumi-jamii na jamii-siasa huku CCM ikibariki dhuluma na hata wakati mwingine kutumia vyombo vya dola kusimamia dhuluma inayofanywa na mafisadi!
  CCM imefikia hatua mbaya sana ya ufisadi hata kusahau dhima yake ya kuwatetea walalahoi wanaodhulumiwa haki na stahili zao za kazi (ujira na mishahara) zenye kuzingatia hali-halisi; na wakulima kupunjwa bei na au kulanguliwa na walanguzi ikiwemo serikali!
  Gamba la ufisadi kwa CCM ni kule kujivisha uwakala wa utawandawazi na ukoloni mamboleo huku chama hicho kikiwachuuza wananchi kwa kunadi kuwaletea maisha bora ilhali maisha yanazidi kuwa magumu na yenye kukatisha tamaa!
  Hivi ndivyo CCM ilivyojivika gamba na hata kwa ngozi hiyo ngumu kukomaa na kuwa kama gamba la kobe au kasa ambalo kuvuka kwake ni kifo cha kobe au kasa! Hakika, CCM ina gamba linalochukiza na kunyong'onyesha.
  Hata kama baadhi ya wana CCM wameanza kusherehekea na au kushangilia kujivua gamba kwa chama hicho, bado kuna safari ndefu ya kukamilisha mchakato wa kujaribu kurudisha imani ya wananchi iliyoyeyuka kama theluji.
  Kama kweli gamba lililovuliwa na CCM ni ufisadi tuna kila sababu ya kudhani kwamba chama hicho kimejengwa kwenye mihimili ya ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo kwa vile wale wanaopewa nafasi ya kujiondoa wenyewe kwenye nafasi za uongozi wa CCM wanapatikana kwenye iliyokuwa CC na wale waliyomo ndani ya NEC.
  Nani asiyefahamu kwamba sehemu kubwa ya viongozi na au wajumbe wa CC na NEC (ya sasa na ya zamani) kwa nanma moja na au nyingine wanahusika kwa njia moja au nyingine na mitandano ya ufisadi? Kama jibu ni ndiyo; je, kuwataka wajiondoe wenyewe ilhali chama kinawafahamu si mzaha?
  Inawezekana kabisa kauli ya viongozi wa CCM, mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu na viongozi wengine juu ya kuwataka mafisadi wajiondoe wenyewe ni mchezo wa kuigiza na au kujaribu kumtaka paka ajifunge kengele!
  Huu ni utani wa kisiasa na inaonyesha kwamba uongozi wa CCM hauna dhamira ya kweli na ya makusudi kushughulikia suala la ufisadi ndani ya chama hicho.
  Ilitegemewa chama kingechukua hatua madhubuti na kuwang'oa mafisadi ili kitoe fundisho la kihistoria!
  Haikuwa na haitokuwa kwa vile CCM ina mtandao wa ndani na ule wa nje unaofungamana moja kwa moja na mafisadi wenye nguvu zinazojionyesha kwenye taathira ya maamuzi yote mazito na au magumu ya chama kuhusiana na suala la ufisadi.
  Kigugumizi cha mwenyekiti wa CCM taifa kinatokana na ukweli kwamba miongoni mwa wanaodhaniwa ni mafisadi wamo watu waliomsaidia katika kupata nafasi ya kuongoza.
  Vilevile wapo wale yeye (kama mwenyekiti wa CCM taifa) aliyewanandi mbele ya wapiga kura kwamba ni watu ‘safi' na hata yaliyowakuta ni ‘ajali ya kisiasa'!
  Ajali ya kisiasa imefanywa mtaji kwa vile kwa sehemu kubwa hakuna mtu anayeweza kusimama na kuwataja mafisadi wakubwa waliyemo ndani ya CCM hata kama dalili na ushahidi wa moja kwa moja unatoa nafasi ya watu hao kutajwa na hatimaye kufukuzwa na CCM.
  Kama CCM ingeliona hili ingelibidi kuchukua hatua za kuwafukuza mmoja baada ya mwingine na au hata kuwachukulia hatua za kisheria kwa vile wamekifanya chama kupoteza haiba ya kisiasa mbele ya wananchi.
  CCM imebakisha gamba lake kwa vile ina nafasi ya ufisadi unaochukua sura ya gamba jipya kwenye mfumo wa zamani!
  Kwa kutumia falsafa, tunaweza kuuliza swali hili; Nani awezaje kumfunga paka kengele? Ikiwa kiongozi wa serikali ya CCM amewahi kutamka hadharani kwamba, "wala rushwa anawafahamu; isipokuwa anawapa muda wajirekebishe." Na vilevile, ushahidi wa wazi unaonesha kwamba wale majambazi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) walipewa nafasi warudishe fedha walizoiba na au kukwapua Benki Kuu! Gamba la ufisadi linaweza kuvuliwa na chama sampuli hii ya CCM?
  Uongozi wa CCM uliojibakisha na kudai wamejivua gamba wana jambo gani la kujivunia juu ya uvuaji wa gamba wa kisanii walioufanya Dodoma? Au tuseme kwamba wamefunika kawa ili mwanaharamu apite?
  Hawajui kwamba hawatahukumiwa kwa maneno yao bali watapimwa kwa matendo yao juu ya dhamira ya kupambana na mafisadi.
  Na kwa kuwa ufisadi umeshachukua msamiati wa siasa katika Tanzania kuna kila sababu ya CCM kuwa chama cha mafisadi hadi pale uongozi wa chama hicho utakapochukua hatua kali dhidi ya mafisadi wanaotamba kukisambaratisha chama hicho.
  Kama wamechukua uamuzi baada ya utafiti wa wataalamu (wasomi) makini na bobezi kwenye kutafiti matatizo ya kudumaa na kukosa mvuto kwa vyama vya siasa; basi kuna kila sababu ya kudhani kwamba ushauri wa kitaalamu uliotolewa hauna mashiko kwa wakati huu.
  Nadhani ushauri muhimu kwa CCM ulikuwa ni kuifumua CCM kuanzia kada za kati ambazo nyingi (wilaya na mikoa) zimeundwa kwa utashi wa mafisadi katika kufanikisha malengo ya ufisadi wa kimfumo katika kujenga mtandao kuanzia wilayani na mikoani. Viongozi wengi wa kada za wilaya na mikoa ni wale waliopewa fedha za kampeni na kufanyiwa kampeni na mafisadi katika kupata uungwaji mkono kwenye kupitisha maamuzi yanayohitaji maamuzi ya wengi.
  Kama kujivua gamba ni kuivuruga CC na NEC ya CCM ilhali mtandao wa wilaya na mikoa na wajumbe wake wanaotokana na mfumo wa kifisadi utabaki kama ulivyotengenezwa na kusimamiwa mwaka 2007 na kama ulivyopangwa mwaka 2002 kuna kila sababu ya kudhani kwamba CCM inachimba kaburi lake na kutamani kujizika yenyewe.
  Hakuna awezaye kuinusuru CCM kama inatamani kujimaliza yenyewe isipokuwa utashi wa kweli wa viongozi wake katika kurudi kwenye asili ya chama (political roots). CCM itambue kwamba ni chama cha wakulima na wafanyakazi walalahoi wenye kutamani ujamaa na kujitegemea kama njia ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
  Wananchi wa Tanzania wanahitaji uhuru! Uhuru wa kweli wa kujitawala kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa haki, usawa na uadilifu. Wananchi wa Tanzania wanatamani kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yao; na kwa jinsi hiyo, CCM ilidhaniwa kuwa ni chama cha kuleta manufaa kwa maisha ya wananchi wengi maskini wa Tanzania. CCM haikudhaniwa kingekuwa chama kinachokumbatia mafisadi wanaonyonya rasilimali za nchi na au kupora na kukwapua bila huruma na insafu.
  Mwisho wa makala ni rai kwa wananchi na wanachama wa CCM; kujivua gamba kwa CCM kusiwafanye msahau na au mjisahau katika harakati zenu za kudai Katiba Mpya itakayoondoa aina zote za dhuluma, vitisho, uonevu na ufisadi unaofanywa na mtu, kundi la watu na au chama cha siasa kinachosimamia maslahi ya mafisadi.
  Ni wakati muafaka wa kutumia nafasi iliyotolewa ya kujenga ujamaa wa nchi yetu. Kila mwananchi wa Tanzania ana wajibu wake; na tutimize wajibu huo bila ya ajizi. Mungu ibariki Tanzania!  [​IMG]

  Mwandishi mwa makala hii anapatikana kwa simu namba: +255 713 593347
  Barua pepe: maligwa1968@yahoo.com , bakari.mohamed@mzumbe.ac.tz
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Mali bila daftari na vitabu vya fedha za umma vinavyoota miguu!
  [​IMG]

  M. M. Mwanakijiji ​

  [​IMG] Kuna msemo wa zamani unaosema kuwa ‘Mali bila daftari hupotea bila habari'.
  Msemo huu ni miongoni mwa kanuni za mwanzo kabisa, mfanyabiashara na mtu yeyote mwenye kutumia fedha zake anatakiwa kujifunza.
  Msemo huu ni somo kubwa la kusimamia fedha kwamba ili ujue fedha zinavyoingia na kutoka ni vizuri uwe na mahali ambapo unarekodi mapato na matumizi yako. Kwa kufanya hivyo utaweza kujua ni wapi unapata faida na ni wapi unapata hasara lakini vile vile unaweza kujua unatumiaje fedha zako.
  Kutokana na nadharia hiyo ya zamani sana jamii zote ambazo zimekuwa na matumizi ya fedha zilijifunza mapema sana jinsi ya kutunza kumbukumbu ya matumizi ya fedha.
  Hii inasaidia mtu kujua amenunua nini, kwa kiasi gani, wapi, na pia inasaidia kujua ni kwa kiasi gani bei ya vitu imebadilika na kumsaidia kulinganisha.
  Kumbe zipo faida nyingi sana ambazo siyo lengo la makala yangu leo zinazohusiana na utunzani mzuri wa kumbukumbu za fedha.
  Mimi mwenyewe nimejifunza umuhimu huu wa kutunza kumbukumbu baada ya kujikuta nalipia kitu kimoja mara mbili na kujitia hasara isiyo ya lazima. Nilifanya malipo ya huduma ya intaneti huku nikiwa nimetumia mfumo wa kibenki kuweka tarehe ambapo kampuni ingechukua fedha moja kwa moja kutoka kwa akaunti yangu lakini siku ya kulipia nilikuwa nimeshasahau kuwa niliweka kiasi na tarehe tayari kwa benki kufanya hivyo.
  Badala yake nikawapigia simu kampuni na kuwaambia wachukua kiasi kingine cha fedha ili wasije kunikatia huduma.
  Baada ya taarifa ya benki ya mwezi kunijia nikajikuta ndani ya siku moja moja nimefanya malipo mawili makubwa na nilikumbuka lile tu nililolipia kwa kupiga simu.
  Nilipoamua kupitia daftari langu la benki ndipo nikakuta kuwa nilikuwa tayari nilikuwa nimewaagiza kampuni kuchukua fedha ya malipo. Bila daftari ningedhani kuna mtu kaniibia! True story.
  Kanuni hii ya kutunza kumbukumbu haihusu taasisi binafsi tu bali pia serikali na taasisi zake vile vile.
  Serikali inakusanya kodi kutoka kwa wananchi na kutoka kwenye huduma na bidhaa mbalimbali na vyanzo vingine vya ‘mapato'. Fedha hizi hutumiwa tena na serikali hiyo hiyo katika kulipa mishahara, kuleta huduma mbalimbali kwa wananchi n.k Hivyo, kanuni ya kutunza kumbukumbu inatakiwa kufuatwa vile vile.
  Serikali haitakiwi hata kidogo kutumia fedha bila maelezo. Serikali ambayo inatumia fedha bila maelezo inawaibia wananchi!
  Ni kutokana na hili basi serikali kama ya kwetu zina mtu anaitwa ‘Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu' ambaye amepewa jukumu la kuangalia ripoti mbalimbali za matumizi ya serikali na taasisi zake na kulinganisha taarifa hizo na vitu vilivyonunuliwa. Njia pekee Mkaguzi (CAG) anaweza kujua fedha zimeingia wapi, vipi na zimeenda wapi, vipi na kwa nini ni kwa kupitia vitabu au madaftari yenye kurekodi matumizi ya serikali.
  Ni muhimu sana kwa vyombo vya umma na vyote vya serikali kuwa na utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu. Bila ya kumbukumbu hatuwezi kujua jinsi gani fedha za umma zimepatikana na kutumika. Inapotokea taasisi au chombo cha umma kinashindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi yake kwa kushindwa kuonesha vitabu vya risiti, au vitabu vya kihasibu kwa kisingizio chochote kila uwezekano ni kuwa kuna kitu kimejaribu kufishwa.
  Baada ya kupitia ripoti ya CAG ya mwaka 2009/2010 na kulinganisha na ripoti nyingine za miaka iliyopita nimegundua kuwa kuna tabia ambayo imekubaliwa na inatarajiwa kuwa kwa namna fulani kuwa vitabu vya hesabu vinaweza kupotea kiana na watu bado wakaendelea kuwa katika kazi zao kama kawaida na kuendelea kupokea mishahara kana kwamba hilo si jambo kubwa.
  Hebu tuangalie ripoti hizo na tuone jinsi gani Watanzania kama taifa wanachukuliwa kama mazoba ambao hawana uwezo wa kuhoji, kufikiri wala kudai watu wawajibishwe.
  Tunapozungumzia ufisadi si lazima watu wawe kwenye Kamati Kuu ya CCM kujulikana kuwa ni mafisadi. Ufisadi mwingine ni huu wa kupoteza vitabu vya hesabu na kwa makusudi kuficha wakaguzi kinachoendelea.
  Kwa sababu vitabu haviwezi kuota mbawa au miguu na kutoweka vyenyewe. Bado haijawahi kutokea kwamba kwenye ofisi fulani ati vitabu ‘havionekani' au vimeshindwa kupatikana.
  Hivi vitabu vinavyoota miguu ni vya aina gani hivi? Vitabu ambavyo vinashindwa kupatikana ati kwa sababu ‘vimeshindwa kupelekwa' vimetengenezwa wapi? Inashangaza serikali ya CCM na viongozi wake wanaisoma ripoti hii na hawasikii hasira.
  Na tatizo siyo tu kutopatikana vitabu wakati mwingine vitabu vinapatikana lakini taarifa za matumizi au mapato yake hazipo wakati watu wote serikalini wanajua kabisa huwezi kutumia mali za umma bila kuweka rekodi lakini viongozi hawa hawa tuliowarudisha madarakani wanavumilia mtindo wa taasisi na idara mbalimbali za serikali kusema kuwa wametumia fedha hivi au vile lakini bila kuonesha risiti au kurekodi mahali popote pale.
  Tuangalie mifano michache ya vitabu vya serikali yetu vinavyoota mbawa na viongozi wake bado wakiwa madarakani wakilindwa na serikali ile ile.
  Kwenye Serikali za Mitaa
  Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 pamoja na mabadiliko yake Halmashauri zote nchini zinatakiwa kuwa na kutunza vitabu vya mahesabu.
  Ripoti inatutaarifu kuwa: 948 vya kukusanyia mapato katika Halmashauri 48 havikuweza kutolewa kwa wakaguzi kwa ajili ya uhakiki, hivyo kupelekea wakaguzi kushindwa kuthibitisha kiasi cha mapato kilichokusanywa kupitia vitabu hivyo. Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro iliongoza kwa kuwa na vitabu 168 ambavyo havikuwasilishwa ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi yenye idadi ya vitabu 101.
  Mtu mwenye akili timamu anatakiwa kujiuliza hivi, vitabu hivyo ‘havikuweza kutolewa kwa wakaguzi' kwa sababu gani? Havikuwepo, havikuweza kupatikana, vilihamishwa, vilifichwa, viliazimwa au viligeuka mvuke vilipoona wakaguzi wanafika basi vikatoweka hewani!?
  Mniruhusu niangalie kwa undani kidogo sakata la vitabu vyenye mbawa kwenye Halmashauri zetu: Nanukuu moja kwa moja kutoka kwenye ripoti ya CAG.
  Wilaya ya Mwanga
  Vitabu 8 vya wazi vya kukusanyia mapato (HW5) na vitabu 28 vyenye thamani ya Sh 8,000,000 havikupatikana wakati wa ukaguzi.
  Mapato yaliyokusanywa kwa kutumia vitabu hayakuweza kuthibitishwa ndani ya vitabu hivyo.
  Wilaya ya Kilwa
  Vitabu 101 vya kukusanyia mapato havikupatikana wakati wa ukaguzi, kwa hali hiyo mapato yaliyokusanywa kwa kutumia vitabu hivyo hayakuweza kuthibitishwa.
  Hati za malipo zenye jumla ya sh 144,994,981 hazikupatikana wakati wa ukaguzi kwa hiyo uhalali wa malipo hayawezi kuthibitishwa.
  Wilaya ya Kilosa
  Vitabu vya kukusanyia mapato vipatavyo 394 havikuwasilishwa kwa wakaguzi vilipohitajika.
  Mifano hiyo ni kidogo tu ya kile ambacho kinaonekana kuwemo kwenye zoezi hili la watendaji kuvipatia miguu vitabu vya mapato na matumizi. Mkaguzi Mkuu anasema hivi kama hitimisho lake kuhusu suala la vitabu kutoonekana:
  "Kwa kuwa vitabu hivi vilikusudiwa kukusanya mapato ya halmashauri, sikuweza kujua mara moja ni kiasi gani kilikusanywa kwa kutumia vitabu hivyo" na anagongelea msumari kwa kututaarifu kuwa "kuna uwezekano mkubwa wa wizi wa mapato ya halmashauri na kupotosha makisio ya mapato ya halmashauri'.
  Unaweza kufikiria tatizo hili la vitabu kuota mbawa ni la halmashauri peke yake.
  Serikali Kuu
  Ofisi ya Rais jumla ya sh 11,870,000 zililipwa kwa watu mbalimbali bila kuwa na nyaraka timilifu.
  Wizara ya Fedha
  Wizara ilihamisha kiasi ya sh 70,000,000,000 (bilioni 70) kwa kipindi kilichoishia Juni 30, 2010 kwenda TIB kwa ajili ya kubadilisha TIB kuwa taasisi ya Maendeleo ya Fedha na pia kufungua benki kwa ajili ya shughuli za kilimo.
  Kwenye hili Mkaguzi aliomba nyaraka zifuatazo na nyaraka hizo hakupewa. Nyaraka zingemsaidia kujua fedha bilioni 70 za Watanzania zimetumiwa vipi:

  1. Taarifa ya akaunti ya benki kwa kipindi kilichoishia Juni 2010.
  2. Dondoo za ripoti ya fedha kuonyesha mapokezi yote, malipo na urari wa mfuko huo.
  3. Hatua zilizochukuliwa ili kuzuia uwezekano wa mfuko huo kuanguka kutokana na ukweli kuwa mkataba hauwabani TIB kuwajibika waliochukua mikopo wanaposhindwa kulipa.
  4. Kibali cha baraza la mawaziri kuanzisha taasisi hizi mbili. Yaani taarifa hizo zilishindwa kupelekwa kwa Mkaguzi Mkuu!
  Wizara ya Mambo ya Ndani
  Malipo ya sh 423,183,545 yalifanywa kwa watu wengine, lakini hayakuonyeshwa katika vitabu vya fedha kinyume na viwango vya kimataifa vya uhasibu (IPSAS).
  Katika hili CAG anasema kuhusu wizara hiyo "Kulikuwa na udhaifu katika usimamizi wa mikataba vilevile nyaraka muhimu za mikataba hazikuletwa kwa uhakiki."
  RAS Tabora
  Mali na vifaa visivyohamishika vyenye thamani ya sh 12,233,800 ikiwa ni pamoja na jenereta, kompyuta, samani na friji, hazikuingizwa katika kumbukumbu za vitabu vya mali za kudumu.
  Taarifa za kifedha zimeandaliwa pungufu kwa kiasi cha sh 12,233,800 (inawezekana kuna mtu katumia fedha za umma kujinunulia vitu vyake mwenyewe)?
  Vifaa vyenye thamani ya sh 19,693,560 vilinunuliwa lakini havikuingizwa vitabuni. Hatukuthibitisha kama vifaa hivyo vilipokewa na kufanya kazi iliyokusudiwa.
  Mkaguzi akatudokeza hali ilivyo katika kusimamia fedha za Watanzania:
  Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2010, serikali ilikuwa na madeni yasiyotarajiwa yaliyofikia kiasi cha sh 26,276,785,317 yaliyohusisha mafungu kumi na mawili ambayo asili yake haikuonyeshwa kwenye vitabu. (Yaani kuna madeni ambayo tunajua ni madeni lakini hakuna ushahidi wa maandishi ya kwanini tunadaiwa!)
  Sheria haitakiwi kudhamini deni la chombo chochote kwa zaidi ya asilimia 70 ya fedha zinazokopwa. Mkaguzi Mkuu anatudokeza kuwa hii serikali ya CCM ikiongozwa na watu wale wale imefanya yafuatayo:
  Serikali ilidhamini kampuni tatu zaidi ya kiwango cha mkopo kwa sh 60,864,285,978 kinyume na sheria.
  Mkaguzi akatuambia kitu kingine hapa:
  Kama nilivyobainisha katika Sura ya IV, kwa ujumla mali za serikali zimeongezeka kwa asilimia 13 kutoka mwaka 2008-09 hadi mwaka 2009-10 (kufikia thamani ya karibu shilingi trilioni 8).
  Hata hivyo, serikali haina rejista ya mali za taifa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za mali.
  Kwa maneno mengine ni kuwa tunaambiwa tuna mali yenye thamani ya trilioni 8 lakini tukiiuliza serikali unaweza kutuambia ni mali gani ya taifa hili haiwezi kwani haina rekodi ya mali zetu zote. Kutokana na hilo Mkaguzi anatoa ushauri huu "Ninaishauri serikali kuweka mali za taifa katika daftari au rejista, kufanya usuluhishi mara kwa mara wa kumbukumbu za mali katika taarifa za fedha jumuifu za taifa. Ikumbukwe kwamba mali bila daftari hupotea bila ya habari."
  Mashirika ya umma
  Kama unafikiria tatizo la utunzaji kumbu ni tatizo la serikali za mitaa au serikali kuu peke yake na haliko kwenye mashirika ya umma utakosea na kupaisha kama yule jamaa wa Ghana alivyopaisha kwenye Kombe la Dunia mwaka jana.
  Kwenye mashirika yetu ya umma ambayo mengine viongozi wake wanachukuliwa kuwa ni makini na wana weledi wa hali ya juu. Je, na wao wanajua umuhimu wa kanuni hii ya ‘mali bila daftari'?
  Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
  shilingi milioni 40 - malipo ya simu za mikononi na posho za simu kwa wajumbe wa bodi, kwa viwango vilivyopitishwa vya dola za marekani 600 na posho ya simu dola 350 kwa Mwenyekiti wa Bodi,dola 300 kwa Makamu Mwenyekiti na dola 250 kwa wajumbe wengine wa bodi, hii ni kinyume na taratibu zilizokubalika za utawala bora.
  (Wenzetu wanajilipa kwa viwango vya dola wakati wengine kwenye serikali ile ile labda hata taasisi hiyo hiyo wanalipwa kwa viwango vya madafu!)
  Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Tanga) shilingi milioni 30 - Vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa lakini haikuthibitika kama vilipokewa eneo la ujenzi.
  Mkaguzi Mkuu anatuambia kuwa "Baadhi ya mashirika yameonekana kuwa na kawaida ya kuwa na udhaifu mkubwa katika kutunza kumbukumbu za manunuzi unaosababishwa na ukosefu wa taaluma katika kutunza kumbukumbu, ukosefu wa nafasi katika ofisi za vitengo vya manunuzi na kupoteza nyaraka bila sababu za msingi.
  Madhara ya hali hiyo ni kuwa na manunuzi yasiyofuata sheria, udokozi wa mali na kupotea kwa mali za umma."
  Na akaongeza kuwa "Tulibaini pia kutoweka bayana mapato na matumizi kama inavyotakiwa na matakwa ya viwango vya kihasibu hali ambayo inaweza kusababisha vitendo vya ubadhirifu.
  Kwa upande wa matumizi, tumegundua udhaifu katika mifumo ya ndani ya udhibiti wa malipo, kutokuwepo kwa nyaraka za kuthibitisha malipo"
  Sasa hii yote ni mifano michache tu ya jinsi gani tuna tatizo kubwa sana katika usimamizi wa fedha zetu lakini zaidi tatizo la viongozi ambao wanavumilia tabia hii miaka nenda rudi. Mapendekezo yaliyotolewa na CAG mwaka huu kuhusu utunzaji wa kumbukumbu hayana tofauti na mapendekezo yake ya miaka 5 iliyopita.
  Lakini tufanye nini? Tuendelee kusubiri mwaka mwingine tuone kama tumejifunza somo la ‘mali bila daftari'. Au tuendelee kusubiri viongozi wa upinzani waje na orodha nyingine ya ‘mafisadi'?
  Ndugu zangu, wanaosema ‘wamejivua gamba' wanatutania. Huwezi kujivua gamba wakati chini ya gamba kuna gamba lenye gamba.
  Huwezi kujivua gamba kwa kuwaondoa watu wanne kwenye chama wakati kuna maelfu ya watendaji serikali ambao wanafanya gamba lisiwe gamba tu iwe ni gamba sugu. Gamba hili halivuki kwa kutambulisha viongozi wapya au kwa kubeza watu.
  Gamba linavuliwa kwa kuvunja vunja mfumo wa utawala wa kifisadi ambao niliandika habari zake zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
  Nilisema hivi katika makala yangu ya Septemba 2009 Kuuelewa mfumo wa Utawala wa Kifisadi "Ndiyo maana nimesema awali kuwa tatizo letu siyo Rostam, Lowassa, Chenge au Yona; hawa ni dalili tu ambazo tunaweza kuziondoa barabarani.
  Tutakuwa hatuna hekima kama tunaamini kuwa tukiwaangusha hawa kutoka madarakani basi ufisadi utakwisha. Tusipobadilisha mfumo wa kiutawala wa ufisadi tutaendelea kuzalisha mafisadi tu. Haijalishi ni chama gani kiko madarakani."
  Leo nilichohofia ndicho kimetokea; na wapo watu wanataka tuamini kuwa ati CCM imebadilika wakati sheria na mfumo wa sheria bado upo ule ule. Nilisema kuwa kama kiwanda kinatengeneza magari yenye hitilafu fulani haitoshi kuyaondoa magari hayo barabarani lakini pia kuangalia kiwanda kinachotengeneza na mitambo yake ikoje.
  Ndugu zangu, matatizo haya niliyoyadokeza kwa haraka haraka ni dalili tu kuwa ufisadi si tendo la mtu mmoja ni utamaduni. Tunapozungumzia Katiba mpya kimsingi tunataka kubadilisha kabisa mfumo uliojenga utamaduni wa kifisadi.
  Katiba mpya ni suluhisho kubwa la lazima la kuubomoa mfumo tuliojenga kwa karibu miaka hamsini. Wale wanaodhania Katiba mpya inahusu kuiondoa CCM madarakani hawajajua tunachogombania.
  Tunagombania nafasi ya kujenga upya nchi yetu katika misingi ambayo itahakikisha kuwa ufisadi kweli unabakia ni vitendo vya watu wachache na siyo zao la mfumo uliopo.
  Tunachotaka na kubadilisha kabisa jinsi gani tunatawaliwa, na jinsi gani tunawawajibisha watawala wetu.
  Chini ya mfumo huo mpya watu wote wanaofanya mambo kama haya wanawajibishwa kuanzia mfagizi wa shule ya vidudu hadi mpigiwa saluti mkuu wa taifa letu.
  Lakini hili halitofanikiwa hadi Watanzania tutakaposema ‘imetosha'. Mpaka tutakapoona madudu haya na kuyaona ni kero ya kweli. Tusipofanya hivyo tutaendelea kucheza kwenye hili tope na tusipoangalia tutawaridhisha na watoto wetu mfumo huu ambao unatia kinyaa.
  Katika jitihada za kujivua gamba serikali iwasimamishe mara moja viongozi na watendaji wote ambao wamehusishwa na kuficha vitabu vya mapato na matumizi na ambao wameshindwa kutoa taarifa za fedha za Watanzania zinatumika vipi.
  Wakishawasimamisha wafanye uchunguzi na wale ambao wataonekana wameshindwa kushika nafasi zao watimuliwe ili waingizwe Watanzania wengine.
  Hakuna semina au warsha inayoweza kuwasaidia watu hawa kubadilika. Serikali ikifanya hivyo mara moja ndio tutaanza kuzungumzia kweli ‘kujivua gamba!'


  [​IMG]

  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Wamejivua gamba wakajivika mabomu?
  [​IMG]

  Juvenalis Ngowi ​

  [​IMG] KAMA walivyo wafuatiliaji wengine wa mambo yanayoendelea hapa nchini, Kiona Mbali naye hajaacha kutazama na kusikiliza yale yanayoendelea kwenye ncho hii.
  Tangu ukosefu wa lugha ya staha bungeni kwa baadhi ya wabunge hadi uvaaji wa nguo zisizo na adabu kwa baadhi ya wabunge wasichana kiasi cha Naibu Spika kutaka watu hao watuepushe na vishawishi.
  Naam Kiona Mbali ameyafuatilia hayo yote lakini akili na roho yake ikabaki kwenye igizo la Chama Cha Mapinduzi. Igizo hili lilimfanya Kiona Mbali atafakari sana yaliyotokea maana si busara kupokea mambo bila uangalifu.
  Ni katika hizo tafakari zake Kiona Mbali alipoona tangazo kwenye gazeti linalostahili kusomwa siriazI, si kama yale Anne Makinda, aliyowataka watu wayasome kama barua. (utadhani barua hazisomwi kwa umakini, tumsamehe bure).
  Hili ni tangazo kubwa limechukua ukurasa mzima wa gazeti. Ni tangazo linalofanya moyo wa Kiona Mbali uongeze mapigo na macho yake yafunguke kwa uwazi zaidi ili kujiridhisha na anachokiona. Midomo imeachama kwa mshangao, kama kungekuwepo inzi, bila shaka angewabugia bila kutaka.
  Kiona Mbali anasoma taratibu tangazo lile. Linaeleza kwamba kufuatia kujivua gamba kwa chama tawala (nasisitiza tamka tawala sio twawala), nyumba zote za serikali nyingi zikiwa zilizojengwa wakati wa ukoloni kwa ajili ya watumishi wa umma ambazo ziliuzwa sasa zinarudishwa mara moja serikalini.
  Wale wote waliouziwa nyumba hizo wanatakiwa kuwasilisha mikataba na stakabadhi zinazothibitisha kwamba walilipa fedha ili warejeshewe kile walichokilipa na nyumba zirudi kwenye madhumuni ya awali ya ujenzi wa nyumba hizo. Kiona Mbali anacheka na kutabasamu. Huku ndiko kujivua gamba kwenyewe.
  Anafikicha macho yake na kuzidi kufuatilia tangazo lile. Anaona maelekezo mengine yakitaka wanunuzi wa ile benki yetu waje mezani ili tufanye mahesabu ya chao ni kipi tuwalipe ili waturudishie chetu.
  Na zile kampuni nyingine nazo hali kadhalika wanatakiwa kuja ili tuhakikishe kama walinunua katika mchakato halali na kuangalia uwezekano wa kurudisha hivyo tulivyowapa kama sadaka.
  Kiona Mbali anatikisa kichwa akisema kujivua gamba ndiko huku. Anatazama kwa makini tangazo lile na anaona maelekezo kwa bunge kwamba lifufue vyote vilivyokufa katika kashfa ya Richmond.
  Tangazo linasema wakati wa kuvua gamba wameng'amua kwamba kuna ambayo bado yanahitaji kufafanuliwa na abayo hayakuwahi kusemwa hadharani.
  Hali tangazo hilo linataka Bunge kuunda kamati kufuatilia wizi uliofanyika katika akaunti ya malipo ya nje pale Benki Kuu maarufu kama EPA. Linataka tume maalumu ifuatilie wizi ule na kwa kuanzia ieleze fedha zile zilitumikaje na kama kuna kaukweli kwenye hii minong'ono kwamba eti fedha hizi zilitumika kwenye kampeni za chama kimoja cha kisiasa.
  Pia katika kujivua gamba kamati itaangalia lile agizo la kuwaambia wezi wale warejeshe fedha zile ni nani alirudisha nini kikaenda wapi! Kiona Mbali anatabasamu maana sasa kweli gamba linatoka. Mzizi wa fitna unakatwa. Uamuzi mgumu kweli kweli.
  Mambo hayaishii hapo, Mkurugenzi wa Mashitaka maarufu kama DPP anasema kwenye tangazo lile kwamba ili kuvua gamba kiukweli, ameshaagiza majalada yafunguliwe ili wale wote walioiba au kutafuna rushwa katika maeneo nyeti ikiwemo manunuzi ya mali za umma na utoaji zabuni wafikishwe pasi na shaka mbele ya hekalu la haki, mahakama! Ujasiri gani huu?
  Tangazo lile linawataka wananchi wapuuze kabisa maneno yaliyosemwa wakati wa kampeni kwamba eti baadhi ya watuhumiwa ni wanasiasa safi na wakapipgiwa kampeni na Bwana Mkubwa kisha miezi michache baadaye Bwana Mkubwa anasema au anaamini kwamba wale wale aliowaombea kura ni mafisadi wasiostahili kuwa katika meza yake!
  Maajabu kama ya Wayahudi na Yesu. Kwa Wakristo wanaamini kabla ya kuteswa kwa Bwana Yesu Wayahudi walimpokea kwa shangwe na vigelegele wakimwita mfalme wao, lakini juma hilo hilo wakamtundika msalabani!
  Bwana mkubwa aliwapigia kampeni kwa nguvu na kuwaombea kura kabla hajawageuzia kibao na kuwaambia ninyi ni wachafu! Kiona Mbali anaushangaa ujasiri huu. Anazidi kuzoma tangazo lile.
  Wakati akisoma tangazo linalohusu namna maisha matamu kwa kila mwanakaya yatakavyoletwa, anashangaa akipigwa kofi dogo usoni. Anagutuka kumwangalia nani huyu anayebugudhi wakati akifuatilia tangazo hili muhimu namna gamba linavyovuliwa.
  Anaangalia na kumwona kijana anayemcheka. Kiona Mbali hajielewi, kijana Yule anasema kwa dharau, wewe babu kwa nini usiende kulala kwako? Unasinzia kwenye benchi la stendi halafu unatusumbua na ndoto zako? Umekuwa ukirusha miguu na ngumi huku na huko kama mtu mwenye midadi anayeangalia soka. Kiona Mbali anagutuka kumbe yote yalikuwa ndoto tu!
  Hata hivyo katika kufikiri na kutazama hao wanaosema wamejivua gamba, anaona kwamba ndoto yake ndiyo iliyokuwa uvuaji gamba wa kweli na si huku kuchomoa na kuchomeka sura kama mcheza drafti. Unamtoa baba, unamwingiza mwana. Unamwondoa yule tuliyemzoea unamweka yule tunayemjua hana tofauti na uliyemchomoa. Naam, igizo zuri la kutazama lakini lisilotoa matumaini kwa watazamaji.
  Katika fikra zake Kiona Mbali anajiuliza hivi hawa watu wamejivua gamba na kujivika bomu? Nini mustakabali wa hiki wanachosema kuhusu watu wao wenyewe? Wanatuthibitishia kwamba kwa miaka nenda-miaka rudi tulikuwa tukiongozwa na watu wasiostahili? Mbona magazeti yalipoandika na wapinzani walipohubiri waliambiwa kwamba hao ni waongo tu tena wapuuzwe?
  Imekuwaje ghafla sasa wanasema haya ni magamba? Walikuwa vipofu miaka hiyo wakati wakikaa pamoja katika meza kutengeneza ushindi? Walikosa ujasiri gani wakati wakichuja majina ya wagombea pale Dodoma wasiwachuje hawa tunaoambiwa ni magamba? Magamba yameanza baada ya ushindi wa kinyonge kwenye uchaguzi mkuu? Mbona kama wanajivika bomu wanapojivua gamba?
  Nini matokeo ya chama kufukuza wale waliokuwa kwenye uongozi wake? Hili si bomu ambalo litalipuka siku yoyote mbele ya safari? Sasa nasikia watuhumiwa wanatakiwa kujiondoa kabisa ndani ya siku tisini. Hili ndilo bomu lenyewe.
  Wasipojitoa watawafukuza? Wana ubavu wa kumfukuza mwanachama aliye mbunge? Wakifanya hivyo ndiyo itakuwa kulipua bomu. Lakini kukiri kwamba chama hakipendwi tena hivyo wanafukuza watu bali hawatuambii yale mabaya yaliyofanywa wakati chama hiki kilipolipiga ngwara Azimio la Arusha ni bomu jingine.
  Vilema wa ajali ya Gongo la Mboto wanalia kwa maumivu wakidhani walau katika kujivua gamba wale waliowasababishia baadhi yao vilema vya maisha wangewajibika. Wafanyakazi wanaolilia maslahi zaidi kwao kujivua gamba kunatakiwa kuendane na unafuu wa hali ya maisha.
  Kwa mkulima kujivua gamba ni pamoja na kuondoa maziongaombwe kwenye ruzuku ya pembejeo za kilimo.
  Kutangaza umejivua gamba bila kuwaletea watu maisha yenye neema ni kuvua gamba na kuvaa bomu maana siku ya kura hatutakuuliza uliwafukuza wangapi uanachama, bali ulipowafukuza sisi tulipata nafuu gani.
  Lakini Kiona Mbali anaona mvurugano mkubwa wa ndani ya chama ukija baada ya siku tisini na hilo ni bomu ambalo Kiona Mbali anaona litalipuka kwanza kabla ya kulipua mengine. Angalieni kama mmejivua gamba mkavaa bomu? Ni tafakari tu!


  [​IMG]

  0784 265072
  juvengowi@yahoo.com.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Wao na mashangingi, sisi na Ambulance za Bajaj
  [​IMG]

  Mpayukaji wa Msemahovyo ​

  [​IMG] BAADA ya kuona waziri mkubwa akizindua eti Bajaj ya kuzima moto, mie nimeamua kutumia ndege kuzima moto baada ya kuingia madarakani. Kuna jamaa yangu, baada ya kujua mipango yangu nasikia anataka kuzindua Bajaj inayopaa! Itapaaje? Msiniulize.
  Kwanza nilipooana mtu mzima eti anaingizwa mjini na matapeli wanaojiita wawekezaji wakati ni wachukuaji, nilipigwa na butwaa na kujiuliza. Akili zetu zimefichwa wapi kiasi cha kutenzwa hivi kama hatuna ubongo? Hayo ni yao. Tuyaache.
  Kweli waliosema kuwa hizi ni zama za usanii, kutapatapa na ombwe hawakukosea. Tangu lini pikipiki ikawa zima moto kama siyo kutapeliwa na kushinda kutumia bongo sawa sawa?
  Hawa waliotoa hili wazo na wakatengeneza Bajaj ya kuzimia moto wanatudharau sana. Wanatuona wote tu mataahira. Wanajua tunavyofikiri "kibajajbajaj."
  Ambulance Bajaj, zima moto Bajaj bado treni na meli za Bajaj. Ama kweli mmegeuza kaya kuwa Bajaj. Basi tuiiteka kaya ya Vikombajaj. Hii ikichanganyikana na vikombe ndiyo usiseme. Ama kweli la kuvunda halina ubani. Maana kila tapeli anakuja kuchuma Bongolalaland!
  Jamani, kama Bajaj deal kwanini hamzitumii hasa nyie wazito mnaopitisha upuuzi wa kuruhusu zitumike? Kwanini watu wazima mkwepe Bajaj na kuwabambikia wagonjwa tena waja wazito msiwe waroho? Nyie mashangingi na mashangingi yetu wao vibajaj na babaj zao! Mbona kwenye kikombe cha babu hamuweki matabaka mbele kama kweli nyie si wagonjwa?
  Wakati nchi za wenzetu wanatumia midege kuzima moto, sisi tunajisifu upumbavu wa kutumia baiskeli kuzimia moto. Kesho sitashangaa kuona mtaalamu wa "kuzima moto" akimwalika waziri mzito kuzindua chupa ya chai ya kuzimia moto.
  Hivi kweli hili linahitaji kuwa na shahada nyingi kama zangu kujua kuwa ni utapeli tena wa kipuuzi? Kwanini tusijenge miji yetu kisasa kiasi cha kuwa na njia za kuruhusu magari zima moto kupita?
  Hata hivyo, magari yenyewe yako wapi? Yatapatikana vipi na wapi iwapo tumechakachua kila kitu hata uwezo wa kuona na kufikiri? Kwa wale wanaojua lugha ya anga au baharini, tunapaswa kutoa alama ya au mbiu ya "mayday" yaani maafa.
  Kwa ufupi baada ya kuanza mbio za kwenda Ikulu hata kabla ya uchafuzi na uchakachuaji, nimeanza mikakati kamambe ya kuukwaa ukuu na kula bure kama maiti. My blueprint is very simple. I shall be tough and honest. I won't entertain any wanton stupidity. I won't allow any crooks to do as they are wont.
  Sera ninazotumia kwenye kampeni ndiyo nitakazotekeleza bila kupunguza wala kuongeza.
  Nitahakikisha Bajaj hazitumiki kuzima moto wala kusafirisha wagonjwa. Badala ya kupoteza muda na upuuzi kama Bajaj nitahakikisha mipango miji bora na ya karne ya 21. Hili ndilo jibu, Mengine upuuzi.
  Wagonjwa kwa upande wao nitahakikisha kila hospitali ina Ambulance yake na si Bajaj. Bajaj licha ya kuwa usanii uchwara ni uhuni wa mwaka.
  Nilishasema nitapambana na ufisadi hasa wa kiakili. Hakuna ufisadi wa kiakili kama huu ambapo matapeli wachache wanatumia raslimali za kaya yetu kwa manufaa yao huku walevi wakiendelea kusota na kufa malofa. Lazima nipigane vita ya kuwakomboa walevi kifikra na kimkakati tena haraka.
  Pia nitapiga marufuku umalaya wa kujiuza kwa wawekezaji wanaokuja kuchukua. Hamtasikia akina AIPITIELO kwenye serikali yangu wala Reitis ya u*********ni. Lazima kaya ifaidiwe na wana kaya wenyewe kwanza.
  Wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wa kata kwenye serikali yangu mwiko. Kama ni ulaji wa bure utokanao na ushikaji basi wakale lupango. Hawa kwangu ni wakoloni weusi wanamwakilisha mkoloni mkuu ambaye kila mmoja anamjua. Ni yule yule ambaye yuko juu ya sheria akitumia nafasi hii kuwakingia vifua mafisadi wake ambao CHAKUDEMA waliwahi kuwaundia kitu kilichoitwa List of Shame (LOSS).
  Wabunge wa kuteuliwa au kupendelewa hamnei. Kumekuwapo na huu ufisadi mwingine ambao wakuu hutumia kulipana fadhila-ubunge wa kuteuliwa na ule wa upendeleo. Hivi kwangu ni ufisadi hata ningeambiwa nini. Huu ni ufisadi wa kimfumo ambao mkinichagua nitauzika ndani ya wiki moja.
  Kumekuwa na usanii wa muda mrefu na upotevu wa mabilioni ya njuluku kuhusiana na kuhamishia makao makuu Dom. Hili kwangu nalo ni ufisadi.
  Nasema wazi. Kuhamia makao makuu mwiko. Kule hakuna maji wala starehe kama vile totos, mishiko ya vikao na makandokando mengine ya ulaji wa dezo. Isitoshe nani anapenda kuishi katikati ya matatizo?
  Pia na mchezo mchafu unaanza kukubalika miongoni mwa walevi. Ni pale mawaziri na wabunge wavivu wa kusoma wanapojipachika vyeo vya udaktari, uprofesa na madude mengine.
  Nasema wazi. Mawaziri kutumia vyeo wasivyosomea sahau. Atakayeghushi ajue amejifungulia mlango wa gereza. Mie sitazungusha wala nini. Mhalifu huyu atakamatwa mara moja na kufungwa hata akiwa ni kigogo wa chama changu au ndugu yangu. Mie sina ndugu linapokuja suala la uwajibikaji. Walioghushi jiandae naja mkombozi wa walevi.
  Bi mkubwa kudandia mgongoni mwangu ndiyo sahau kabisa.
  Kuna mchezo mwingine mchafu sana. Si mwingine bali vitegemezi vyangu kutanua kwa ukuu wangu. Hili ni kosa la jinai. Nitafunga mtu hata awe mwanangu mwenyewe. Kila mtu ale jasho na akili yake badala ya kuendekeza ukupe.
  Chama changu cha Ugali Nyama na Maharagwe (UNM) hakitashika patamu wala hatamu. Patamu na hatamu si vya vyama bali wanakaya wenyewe. Huu nao ni ufisadi mchafu tena wa kimfumo, lazima nikomeshe haraka mkinichagua.
  Chama changu hakitakuwa na kitengo cha propaganda cha kufichia makapi na vihiyo kama Tambo Hizo, Chitambala, Sambuee, Salimia Msabasi, Twaib, Akuilombezi na wenzake.
  Watu wenye majina ya Ewassa, Rosttamu, Chenga, Jose, Makambale, Chilimugati, Mpukutika na wengine kama hao wasahau kujiunga na chama changu. Sitaki nuksi kwenye chama. Tangu lini wacheza ngoma na wataalamu wa mipasho wakawa wakuu wa chama? Wakae huko huko kwenye chama cha majoka. Mie si mpuuzi ati.
  Angalizo. Nitaahidi pepo. Sasa kama nitawapeleka motoni au Misri msiniulize. Akili kichwani. Kama akili zitakuwa kinywani au tumboni hata kiunoni tusilaumiane baadaye.
  Je, wajua kuwa mimi ni rais wenu mtarajiwa? Acha nisiongee sana wabaya wangu wakasikia.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Azzan atoa siku kumi Sekretarieti kujiuzulu Send to a friend Wednesday, 20 April 2011 08:27

  Vicky Kombe
  MBUNGE wa Kinondoni, Iddi Azzan, ametoa siku kumi kwa Sekretarieti ya CCM na Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es Salaam, kujivua gamba ili kukinusuru chama na hali mbaya ya kisiasa iliyopo.
  Azzan alisema iwapo viongozi hao hawatajiuzulu kwa muda huo, ataitisha mkutano wa vyombo vya habari na kueleza maovu yote waliyofanya wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu mwaka jana.
  Katika muda huo, Azzan alisema anataka viongozi hao kuitisha mkutano utakaojadili tathmini ya uchaguzi wa mwaka jana, utaratibu ambao unatakiwa kufanywa kwa mujibu wa mwongozo wa CCM.
  Akizungumza ofisini kwake Kinondoni, Dar es Salaam juzi, Azzan alisema viongozi hao wanatakiwa kutambua kuwa, CCM sio chama cha mtu mmoja, bali cha jamii ya Watanzania, hivyo kila kiongozi anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa kanuni na taratibu zilizowekwa.
  Mbunge huyo alisema tangu Novemba mwaka jana, aliwataka viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, kuitisha mkutano wa kujadili tathmini ya uchaguzi huo.
  Alisema viongozi hao wamekuwa wakikwepa kuwajibika kwa kutoa majibu ya kubabaisha, kama yaliyopita si ndwele na asitafutwe mchawi.
  Azzan alisema kutokana na hali mbaya ya kisiasa iliyopo Dar es Salaam, amekuwa akiwasisitiza viongozi hao kuitisha mkutano ama kujivua gamba ili ufanyike uchaguzi mwingine, hali ambayo imeanza kumletea vitisho kutoka kwa baadhi ya watu kutumia namba za simu asizozifahamu.
  "Nimepokea simu tatu zinazoniambia kwamba ninyamaze, vinginevyo nitakiona cha moto, nyingine ikaniambia nitanyang'anywa kadi ya uanachama wa CCM, nasema katika kutetea haki na utaratibu stahili wa CCM nitasema ukweli sitamwogopa fisadi yoyote na nimetoa siku kumi wajivue gamba vinginevyo ama zangu au zao," alisema Azzan.
  Awali, Mbunge huyo akiwa Dodoma bungeni wiki iliyopita alitoa wito kama huo, lakini Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda, alikataa kwamba hatajiuzulu.
  Hata hivyo, taarifa ambazo zimevuja kutoka kwenye ripoti ya tathmini ya uchaguzi uliopita ambayo ilitumika kuong'oa Sekretarieti ya CCM taifa, inadaiwa inapendekeza katibu huyo kufukuzwa.
  Azzan alisema Dar es Salaam ilifanya vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka jana na kwamba, hali iliyosababisha majimbo mawili na madiwani wa kata 17 kuangukia mikononi mwa wapinzani.
  Alisema hali hiyo sio kwamba wananchi hawaitaki CCM, bali wagombea waliowataka hawakurejeshwa na viongozi kutokana na fitina, hadi kufikia sekretarieti kuanza kuwaandama wagombea wa chama kama yeye aliyeonyesha msimamo.
   
Loading...