CCM yapokonya uhuru na haki ya mahakama kwa mabavu-CHADEMA yatetea mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yapokonya uhuru na haki ya mahakama kwa mabavu-CHADEMA yatetea mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DENYO, Apr 17, 2011.

 1. D

  DENYO JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WAZIRI KIVULI WA KATIBA NA SHERIA AKISHIRIKIANA NA WABUNGE WOTE WA CHADEMA KWA SAUTI MOJA NA UHAKIKA WAMEDHIHIRISHA KWAMBA WAPO KWA MANUFAA YA WATANZANIA NA KUHAKIKISHA UTAWALA BORA WA VITENDO UNAPATIKANA -NGUVU YA UMMA INAHITAJIKA KUFANIKISHA HILI MANAKE BUNGE LA SASA LIMEBAKWA.

  1. Chadema kupitia Tundu lissu imeonesha jinsi CCM imedhamiria kuifanya mahakama idara mojawapo ya CCM kama ilivyo takukuru na UVCCM-wamelazimisha kupitia kada makinda kuwaingiza makada wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia nidhamu na utendaji wa mahakama hii ni balaaaa

  2. Chadema kupitia Tundu lissu wameonesha jinsi viongozi wa serikali na ccm kwa ujumla walivyowavivu kutumia takwimu zilizokusanywa kwa kutumia pesa za walipa kodi katka kufanya maamuzi badala yake wapo teyari kulamisha mahakma iendelee kuwa ombaomba kwa serikali ni pale walipokataa hoja ya mheshimiwa lissu kuwekewa kiwango maalum cha % katika bajeti kama ilivyo kwa vyama vya siasa

  3. Chadema kwa kupitia Tundu lissu wameonesha jinsi walivyotayari kuhakikisha Rais anaheshimu mgawanyo wa madaraka ili kuleta ufanisi lakini CCM -Mavuvuzela wanapenda kuifanya idara ya mahakama tawi la ccm kwa kuwa wamelazimisha kumfanya Chief Court Administrator kuteuliwa na Rais na kuwajibishwa na Rais huku ni kuingilia uhuru wa mahakama na haki ya mhimili huu mkuu katika mihimili mitatu, hii ni pamoja na kulikataza bunge lisithibitishe jina la chief court administrator CCM mavuvuzela wanabaka haki ya bunge na mahamakama katika check and balance of prinicple of separation of powers.

  4. CCM wameteka utungwaji wa sheria kwa kuwa kura hupigwa kwa kulazimishwa useme kila kada makinda anataka useme -huku ni kupoteza mwelekeo wa bunge na kulifanya bunge letu lipoteze haki yake,

  HOngera CHADEMA na Hongera waziri kivuli umeonesha kwamba mh. mbowe hakukosea kukuteua katika nafasi hiyo. Keep it up Lissu
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Kuwa na mahakama huru ni sehemu muhimu ya jamii yoyote yenye demokrasia. Ingawa tunajua kuwa mahakimu na majaji ni binadamu na si malaika lakini wakiwekewa viwango na maadili na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi itakuwa ni mfumo bora. Hii ya kuweka watendaji wa rais kama DC na RC kuwa na usemi wowote kuhusu mahakama ni ya kipekee nadhani it's a first in the world!
  Inasikitisha kuona kuwa wabunge wameamua kuleta ligi ya vyama badala ya kuangalia maslahi ya taifa.
   
 3. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kazi bado ni kubwa mbele yetu wajameni! Loh..
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hapo ndipo wanatakiwa wapiga kura kuwa makini na kuangalia viongozi wanao wapeleka bungeni wako pale kwa maslai yao binafsi au kwa ajili ya wananchi
   
Loading...