CCM Yapo Wapi Maisha bora.?

CCM Yapo Wapi Maisha bora.?

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
8,652
Reaction score
2,642
Wanabodi.

Ni mwaka mmoja umebaki kufikia uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani.

Ccm ilituahidi Mengi hususana maisha bora,ambapo mpaka sasa utekelezaji wake hakuna.

Vijijini barabara ni mbovu,maji ya shida huku Singida vijijini mpaka Simanjiro,Kigoma kuwa Dubai imekuwa nongwa,Meli kubwa Ziwa Victoria imeonekana ile iliyotengenezwa mwaka 1952,Airpot ya kimataifa Karagwe hadithi ile ile ya miaka mingi ya uongo wa ccm.

Maisha yamekuwa magumu,elimu ya msingi kuwa bure eti mtoto mmoja elfu 45 kwa mwaka..aibu ya ccm iliyopoteza mwelekeo.

Bado muendelee kuaminika?

Wamebaki kuwahadaa watanzania kwa kuwaleza kuwa wapinzani wanavuruga amani,kisa wanakumbushwa 'Maisha bora' walioahidi.
 
Dallai Lama

Naona mjadala wako huu unalenga kuweka chum I kwenye kidonda.

Kati ya mambo ambayo CCM huwa hawapendi kukumbushwa ni pamoja na ahadi hii ya maisha bora kwa kila Mtanzania iliyoahidiwa tangu 2005.

Ni kama vile ambavyo hawapendi kusikia ukiwauliza kuhusu siku 90 za kuwafukuza akina Chenge na Lowassa na Rostam uliishia wapi. Magamba yaliishia kiunoni kama alivyotamba Chenge bungeni.
 
Maswali kama haya CCM huwa wanatoka nduki.
 
Dallai Lama

Naona mjadala wako huu unalenga kuweka chum I kwenye kidonda.

Kati ya mambo ambayo CCM huwa hawapendi kukumbushwa ni pamoja na ahadi hii ya maisha bora kwa kila Mtanzania iliyoahidiwa tangu 2005.

Ni kama vile ambavyo hawapendi kusikia ukiwauliza kuhusu siku 90 za kuwafukuza akina Chenge na Lowassa na Rostam uliishia wapi. Magamba yaliishia kiunoni kama alivyotamba Chenge bungeni.

HILI HAWATAKI KULISIKIA

Ukidai yalipo maisha bora UTAAMBIWA UNAVURUGA AMANI NA MCHOCHEZI.
 
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
[h=1]Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015[/h]
 
Gonga hiyo Link usafishe safishe macho.

Mliahidi matrekta kupitia kilimo kwanza,yako wapi?

Matokeo yake mnawauzia wakulima wa pamba mbegu feki tena Waziri kazindua matumizi yake..

Bado mtakuja mwakani?
 
Wakiulizwa maswali haya wanakuwa na majibu yanayofanana..
'UPEMBUZI YAKINIFU'
 
Tunasubiri 2015 watuletee packet za chumvi, kofia, tshirt na kanga na buku 3 tuwachague tena. Tehe... tehe.! Ccm hoyee!
 
Dallai Lama

Naona mjadala wako huu unalenga kuweka chum I kwenye kidonda.

Kati ya mambo ambayo CCM huwa hawapendi kukumbushwa ni pamoja na ahadi hii ya maisha bora kwa kila Mtanzania iliyoahidiwa tangu 2005.

Ni kama vile ambavyo hawapendi kusikia ukiwauliza kuhusu siku 90 za kuwafukuza akina Chenge na Lowassa na Rostam uliishia wapi. Magamba yaliishia kiunoni kama alivyotamba Chenge bungeni.

Tumaini,
Mimi nadhani watu waiamini Chadema maana katika majimbo yao yote wanayoongoza wametekeleza ahadi kwa asilimia mia moja na watu wamekuwa na maisha manzuri, huduma za afya, elimu, maji safi, umeme na hata kipato kimeongezeka. Vijana wote wamepata ajira na mishahara yao ni mikubwa. Visima vimechimbwa kwa wingi hakuna shida ya maji kabisa. Uongozi wa kiuokoo umeondolewa na demokrasia imetawala. Mikataba yote ya chama imewekwa wazi na mapato na matumizi yote yanaonyeshwa.
 
Mkuu Msalani, maisha bora au maendeleo hayatafutwi kwenye <EM>link</EM> bali ni hali halisi inayopaswa kuonekana kwa wananchi. Wananchi wenyewe inabidi wathibitishe kwamba sasa hivi maisha yao ni mazuri ukilinganisha na takribani miaka tisa iliyopita wakati mhe. sana anashika usukani.<BR><BR>Vinginevyo slogani ya maisha bora ni mwendelezo wa usanii uliotukuka wa chama chetu kikongwe!
 
Back
Top Bottom