CCM yapata kiwewe Dar?!

CCM yapata kiwewe Dar?!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,837
Reaction score
21,666
CCM yapata kiwewe Dar

NA MOSHI LUSONZO
2nd March 2013


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick amekiri ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna baadhi ya viongozi wanafuata sera ya vyama vya upinzani na kusababisha vurugu kwenye chama.

Akitoa siri hiyo kwenye kikao cha Madiwani wa Manispaa ya Temeke juzi, Sadick alisema suala hilo limefikishwa mbele ya viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ili watu wa aina hiyo washughulikiwe.

Akiongea huku akionekana kukerwa na jambo hlo, asema wapo baadhi ya viongozi wa CCM wanaimba sera za vyama vya upinzani kila siku na inafikia hatua ya kuwazuia viongozi wa Serikali wasikanyage kwenye eneo lao kama sio wana-CCM.

"Kuna viongozi wetu wa CCM hivi sasa wamegeuka kama mawakala wa vyama vya upinzani, wanaongea lugha na kufuata sera zao," alisema Sadick.

Alisema mradi wa Mji mpya wa Kigamboni umeweza kubainisha viongozi hao baada ya madiwani kuwa kwenye mpasuko mkubwa uliosababisha chama kutetereka.

"Nimezungumza hili na Mwenyekiti wa CCM Mkoa ili kutafutia ufumbuzi, leo hii kiongozi wa CCM anadiriki kumzuia Waziri asiende kwenye eneo lake, tusipoangalia hata Rais atazuiwa eti mpaka atimize masharti yao," alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Aliongeza, "Kuanzia sasa mikutano na kutumia lugha za upinzani zikome, tuwe wamoja tuondoe tofauti zetu kwa nini tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja?"

Hata hivyo, bila kuwataja viongozi hao, alisema kikao maalum cha kutafutia ufumbuzi wa suala hilo kinaandaliwa na kiongozi yeyote aliyeonekana kwenda kinyume na sera za chama hicho atawajibishwa kulingana na kanuni na misingi ya maadili ya chama.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, imekuja baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kuonyesha mgawanyiko mkubwa baada ya kuwepo na kundi la madiwani wanaopinga mradi wa mji mpya wa Kigamboni kwa madai ya kutoshirikishwa na wengine kukubaliana na mradi huo.



CHANZO: NIPASHE
 
Kwani huo mradi ni kwa maslahi ya chama au wananchi?
Kama sikosei mbunge wa Kigamboni amekuwa akiwakilisha maoni ya wananchi waoishi maeneo hayo ambao ni waathirika wa mradi. Kama chama na serikali yake wapo kwa maslahi ya wananchi ni kwanini wasiwasilize na kuangalia maslahi yao?
Vinginevyo serikali na chama chake wanaong'ang'ania kupokonya ardhi ya wananchi wazawa ambao hakuna sehemu yoyote duniani wanapoweza kumiliki ardhi zaidi ya hapa motherland yao, wanakosa uhalali wa kutawala. Nadhani wengi wanajua kwamba baadhi ya viongozi katika serikali hii ni makuwadi wa wageni na baadhi ya so callled wawekezaji wenyeji (ma---------) ambao mguu mmoja upo hapa na mwingine nje wakijaribu kila njia ya kuchukua rasilimali za nchi kwa manufaa yao.
 
amesahau kila enzi ina mwisho wake na enzi za CCM sasa bye.. anashangaa TMK? aangalie Bkb,Shy,Mwnz,Mby n.k then atajua.
 
Hapo na Dr wa Medicine Ngugulile anatafutwa. Kama kweli yupo genuine atasimamia msimamo wake, lakini kwa vitisho vya Meck Sadik anaweza kunywea c unajua tena magambaz
 
Kweli jamaa wanakiwewe, hata msemo aliyoutumia wa "kwa nini tunagombea FITO wakati tunajenga nyumba moja" ujenzi siku hizi ni nondo na simenti + mchanga. Fito ni za 47.
 
haaaaaaaa,,,,,,,,,ngoja ni cheze kwanza,,,,,,,,,,,:msela:,,,,,,,haaaaaaa,,,hiki chama sasa kina jizika chenyewe,,,,,kwa maneno haya ni wazi ccm,haipo kuwatumikia wananchi,,,,bali,,,,kipo kutekelaza maslahi ya chama ambayo ni wizi wizi,wizi wizi,haaaaaaaaaaaa,,,,,,wajinga ndio waliwao,,,,,,,,ni nani mjinga,,,,,,ni,,,,yule,,,,ambaye,,,bado,,,,,,anaishabikia,,,,,,ccm,,,,,,na,,,,kuipigia,,,,,kura,,,,,,,,maneno hayo ni ushaidi,,tosha,,,,,,,ccm,,,,,,,,,nichama kilichopoteza sifa,,,,,kuendelea,,,,,,kuongoza,,,,,,ndungu lile,,,,,,vp,,,,,upo,,,,,,mjomba,,,,,,,sasa,,,jiandae,,,,,kupigwa,,,,,chini,,,,,,,kwenye,,,,kura,,,,,za,,,,maoni,,,,,,,,chadema,,,,,,, wamesha tangaza,,,,awachukui,,,,tena,,,,gamba,,,,,,,,,,,haaaaaaaaaa,,,,
 
Kazeeka vibaya sana. 2015 watapata pressure za kushuka wakati madaktari nao wanasherehekea!
 
ngoma inogile....mwendo mdundo kuelekea 2015
 
haaaaaaaa,,,,,,,,,ngoja ni cheze kwanza,,,,,,,,,,,:msela:,,,,,,,haaaaaaa,,,hiki chama sasa kina jizika chenyewe,,,,,kwa maneno haya ni wazi ccm,haipo kuwatumikia wananchi,,,,bali,,,,kipo kutekelaza maslahi ya chama ambayo ni wizi wizi,wizi wizi,haaaaaaaaaaaa,,,,,,wajinga ndio waliwao,,,,,,,,ni nani mjinga,,,,,,ni,,,,yule,,,,ambaye,,,bado,,,,,,anaishabikia,,,,,,ccm,,,,,,na,,,,kuipigia,,,,,kura,,,,,,,,maneno hayo ni ushaidi,,tosha,,,,,,,ccm,,,,,,,,,nichama kilichopoteza sifa,,,,,kuendelea,,,,,,kuongoza,,,,,,ndungu lile,,,,,,vp,,,,,upo,,,,,,mjomba,,,,,,,sasa,,,jiandae,,,,,kupigwa,,,,,chini,,,,,,,kwenye,,,,kura,,,,,za,,,,maoni,,,,,,,,chadema,,,,,,, wamesha tangaza,,,,awachukui,,,,tena,,,,gamba,,,,,,,,,,,haaaaaaaaaa,,,,

Nimeupenda huu wimbo mkuu!!
 
Kweli jamaa wanakiwewe, hata msemo aliyoutumia wa "kwa nini tunagombea FITO wakati tunajenga nyumba moja" ujenzi siku hizi ni nondo na simenti + mchanga. Fito ni za 47.
Umenichekesha sana... halafu haka ka msemo naona kama wana ka misuse vile..
 
Acheni kutudanganya hata sisi tuko dsm, mbona sioni hicho kiwewe!
 
Hivi Mbunge wa Kigamboni ni nani?
Ni Dr. F. Ndugulile.

Kati ya wabunge wa CCM Dar, ndiye mbunge anayesikiliza wananchi na kujitahidi kwa nguvu zake zote kuwa nao katika kero zao.

Namkubali Dr. F. Ndugulile, japo utendaji na muono wa chama chake unanitia kichefuchefu.
 
CCM yapata kiwewe Dar

Aliongeza, "Kuanzia sasa mikutano na kutumia lugha za upinzani zikome, tuwe wamoja tuondoe tofauti zetu kwa nini tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja?"CHANZO: NIPASHE

Huyu mzee anataka umoja mwisho wakati muda woooooote amewaacha wahuni, mafisadi na wabinafsi watoboe boti walilopanda hadi maji yameanza kuingia ndani, sasa hivi kila mtu anajaribu kujinasua na dhahama iliyopo mbele yake yeye ndio anataka umoja kweli?????Alikuwa wapi kutoutaka umoja huko mwanzo???Huyu mzee naona hana nia njema anataka wazame wote. Mziki wa waCDM hata kama huutaki utaucheza tu maana upo real!!!
 
amesahau kila enzi ina mwisho wake na enzi za CCM sasa bye.. anashangaa TMK? aangalie Bkb,Shy,Mwnz,Mby n.k then atajua.

mkuu Rweye, sadiki amesahau kuwa hizi sasa ni enzi za real madrid kutawala na si barcelona(tehe tehe real 2 barca 1). sadiki hawezi kuzuia mabadiliko. akiyazuia yataondoka nae.
 
Hili la kigamboni linawatafuna sana na litaendelea kuwatafuna ccm. Na Dr. Ndugulile ameamua kusimama upande wa wananchi kitu kinachowapa shida sana viongozi wa ccm wilaya ya temeke na mkoa wa dsm.
 
Last edited by a moderator:
Dar wala msijidanganye, kila mkutano wenu unabuma, msitake kufanya kigamboni ndio mtaji wa siasa.
 
Kweli jamaa wanakiwewe, hata msemo aliyoutumia wa "kwa nini tunagombea FITO wakati tunajenga nyumba moja" ujenzi siku hizi ni nondo na simenti + mchanga. Fito ni za 47.

mkuu umenena. kwanza fito hata wazaramo wenyewe wenye asili nazo wameacha kuzilima. sasa wanatumia saruji na nondo. magamba wabadilishe usemi huo na kuwa

"nyumba yetu tuijengayo ni yetu sote kwa nini tugombanie saruji na nondo?" hapo wataeleweka
 
Back
Top Bottom