CCM yapata kiwewe Dar?!

CCM yapata kiwewe Dar?!

Dar wala msijidanganye, kila mkutano wenu unabuma, msitake kufanya kigamboni ndio mtaji wa siasa.
Anayetaka kufanya kigamboni mtaji ni nani? kilicholetwa hapa ni maneno ya Mkuu wa Mkoa juu ya tuhuma kwa magamba wenzenu na mkutano upi wa CDM uliobuma ndugu, endelea kujipa moyo maana CCM mna roho ya paka mambo yanavyokwenda mrama kwenye chama chenu mnajifanya kama hamuoni.
 
Mh!Ngoma inogile.,ninaskia raaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaha.
 
haaaaaaaa,,,,,,,,,ngoja ni cheze kwanza,,,,,,,,,,,:msela:,,,,,,,haaaaaaa,,,hiki chama sasa kina jizika chenyewe,,,,,kwa maneno haya ni wazi ccm,haipo kuwatumikia wananchi,,,,bali,,,,kipo kutekelaza maslahi ya chama ambayo ni wizi wizi,wizi wizi,haaaaaaaaaaaa,,,,,,wajinga ndio waliwao,,,,,,,,ni nani mjinga,,,,,,ni,,,,yule,,,,ambaye,,,bado,,,,,,anaishabikia,,,,,,ccm,,,,,,na,,,,kuipigia,,,,,kura,,,,,,,,maneno hayo ni ushaidi,,tosha,,,,,,,ccm,,,,,,,,,nichama kilichopoteza sifa,,,,,kuendelea,,,,,,kuongoza,,,,,,ndungu lile,,,,,,vp,,,,,upo,,,,,,mjomba,,,,,,,sasa,,,jiandae,,,,,kupigwa,,,,,chini,,,,,,,kwenye,,,,kura,,,,,za,,,,maoni,,,,,,,,chadema,,,,,,, wamesha tangaza,,,,awachukui,,,,tena,,,,gamba,,,,,,,,,,,haaaaaaaaaa,,,,
Ukiona kada mkuu wa CCM wa mkoa na kipenzi cha JK analalama ujue maji yamefika shingoni!
 
Nafikiri huyu Mzee amesahau jukumu la serikali na yeye kama mtumisi wa serikali jukumu lake nini. Na ndio sababu kubwa ya CCM kuonekana ni chama kisichosimamia maslahi ya wananchi na kukimbiwa. Kimsingi kuhusu suala ambalo linaonekana ndio kiini cha hii kauli ya Meck Sadick yaani mji mpya kigamboni hali hitaji mjadala kwa mwanasiasa makini kwani ni wajibu wa serikali kuona wananchi wanapewa kipaumbele katika jambo lolote linaloguswa ustawi wa jamii yao. Maoni yangu kama mkazi wa Kigamboni ni haya serikali itafute eneo ijenge nyumba bora zinazoendana mahitaji ya sasa na baadae ya watu wa Kigamboni ijenge miundo mbinu kama barabara na mifumo ya maji safi na maji taka kisha ndio ifanye mazungumzo na watu wa kigamboni juu ya mpango wake kwani nina amini watu wa kigamboni wanapenda sana maendeleo na kuishi kisasa, hii habari ya kuwalipa watu kiujanja ujanja kwa nguvu haita leta muafaka wowote balia serikali itegemee maafa makubwa ambayo yanaweza zuilika kama haitaafikiana na wakaazi wa Blue Diamond (Kigamboni). Mbunge wetu Ndungulile nampa hongera kuwasimamia wanaKigamboni dhidi ya manyang'au wachache wanaotaka kudhulumu na kuzorotesha maisha ya Blue diamond.
CCM yapata kiwewe Dar NA MOSHI LUSONZO 2nd March 2013 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick amekiri ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna baadhi ya viongozi wanafuata sera ya vyama vya upinzani na kusababisha vurugu kwenye chama. Akitoa siri hiyo kwenye kikao cha Madiwani wa Manispaa ya Temeke juzi, Sadick alisema suala hilo limefikishwa mbele ya viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ili watu wa aina hiyo washughulikiwe. Akiongea huku akionekana kukerwa na jambo hlo, asema wapo baadhi ya viongozi wa CCM wanaimba sera za vyama vya upinzani kila siku na inafikia hatua ya kuwazuia viongozi wa Serikali wasikanyage kwenye eneo lao kama sio wana-CCM. "Kuna viongozi wetu wa CCM hivi sasa wamegeuka kama mawakala wa vyama vya upinzani, wanaongea lugha na kufuata sera zao," alisema Sadick. Alisema mradi wa Mji mpya wa Kigamboni umeweza kubainisha viongozi hao baada ya madiwani kuwa kwenye mpasuko mkubwa uliosababisha chama kutetereka. "Nimezungumza hili na Mwenyekiti wa CCM Mkoa ili kutafutia ufumbuzi, leo hii kiongozi wa CCM anadiriki kumzuia Waziri asiende kwenye eneo lake, tusipoangalia hata Rais atazuiwa eti mpaka atimize masharti yao," alisema Mkuu huyo wa Mkoa. Aliongeza, "Kuanzia sasa mikutano na kutumia lugha za upinzani zikome, tuwe wamoja tuondoe tofauti zetu kwa nini tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja?" Hata hivyo, bila kuwataja viongozi hao, alisema kikao maalum cha kutafutia ufumbuzi wa suala hilo kinaandaliwa na kiongozi yeyote aliyeonekana kwenda kinyume na sera za chama hicho atawajibishwa kulingana na kanuni na misingi ya maadili ya chama. Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, imekuja baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kuonyesha mgawanyiko mkubwa baada ya kuwepo na kundi la madiwani wanaopinga mradi wa mji mpya wa Kigamboni kwa madai ya kutoshirikishwa na wengine kukubaliana na mradi huo. CHANZO: NIPASHE
 
Acheni kutudanganya hata sisi tuko dsm, mbona sioni hicho kiwewe!

We [mchongo;5823219] kweli TUPOI huenda ikawa nawe Uli-ZOMBI,usicho-elewa hapo nini au unataka kujaza sever? laanakum bin KILAZA mkubwa.
 
CCM yapata kiwewe Dar

NA MOSHI LUSONZO
2nd March 2013


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick amekiri ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna baadhi ya viongozi wanafuata sera ya vyama vya upinzani na kusababisha vurugu kwenye chama.

Akitoa siri hiyo kwenye kikao cha Madiwani wa Manispaa ya Temeke juzi, Sadick alisema suala hilo limefikishwa mbele ya viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ili watu wa aina hiyo washughulikiwe.

Akiongea huku akionekana kukerwa na jambo hlo, asema wapo baadhi ya viongozi wa CCM wanaimba sera za vyama vya upinzani kila siku na inafikia hatua ya kuwazuia viongozi wa Serikali wasikanyage kwenye eneo lao kama sio wana-CCM.

"Kuna viongozi wetu wa CCM hivi sasa wamegeuka kama mawakala wa vyama vya upinzani, wanaongea lugha na kufuata sera zao," alisema Sadick.

Alisema mradi wa Mji mpya wa Kigamboni umeweza kubainisha viongozi hao baada ya madiwani kuwa kwenye mpasuko mkubwa uliosababisha chama kutetereka.

"Nimezungumza hili na Mwenyekiti wa CCM Mkoa ili kutafutia ufumbuzi, leo hii kiongozi wa CCM anadiriki kumzuia Waziri asiende kwenye eneo lake, tusipoangalia hata Rais atazuiwa eti mpaka atimize masharti yao," alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Aliongeza, "Kuanzia sasa mikutano na kutumia lugha za upinzani zikome, tuwe wamoja tuondoe tofauti zetu kwa nini tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja?"

Hata hivyo, bila kuwataja viongozi hao, alisema kikao maalum cha kutafutia ufumbuzi wa suala hilo kinaandaliwa na kiongozi yeyote aliyeonekana kwenda kinyume na sera za chama hicho atawajibishwa kulingana na kanuni na misingi ya maadili ya chama.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, imekuja baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kuonyesha mgawanyiko mkubwa baada ya kuwepo na kundi la madiwani wanaopinga mradi wa mji mpya wa Kigamboni kwa madai ya kutoshirikishwa na wengine kukubaliana na mradi huo.



CHANZO: NIPASHE
wanachokosea ccm,ni kudhani kwamba miongoni mwao hakuna watu wenye kuwahurumia wananchi
 
Mziki umepigwa vizuri watu wasiamke kwenye viti?Mbado!!!!
 
na hawa wakuu wa mikoa pamoja na wilaya cdm ikichukua nchi 2015 ianze na wao kuwatimua
 
Ni Dr. F. Ndugulile.

Kati ya wabunge wa CCM Dar, ndiye mbunge anayesikiliza wananchi na kujitahidi kwa nguvu zake zote kuwa nao katika kero zao.

Namkubali Dr. F. Ndugulile, japo utendaji na muono wa chama chake unanitia kichefuchefu.

Hivi huyu si alidhulumu kiti, hakujua kama yatamkuta. Ngoja aipate joto ya jiwe
 
Back
Top Bottom