CCM yapata aibu kubwa huko Temeke

bennymas

Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
68
Reaction score
30
Mbunge wa Temeke mh, Abasi Mtemvu na diwani mh. Zena Mgaya jana walipata aibu kubwa katika kata ya Tandika baada ya kuhutubia watu kumi katika viwanja vya Mbonde yangu macho.



Mtevu amewadanganya wananchi wa Temeke kwamba Temeke kuna barabara nzuri kuliko Masaki na mwisho kaishia kuwatuhumu
CHADEMA kwamba wanawadanganya watu wa Temeke kwamba CCM aifai.
.
 
Rest in hell magambaz!!mmewapa wananchi maisha magumu na laana hii haitawaacha salama...
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kusema kweli mimi binafsi nina m-admire mbunge wa temeke kwa kazi nzuri ya kuhakikisha barabara zinakuwa za lami kwenye vichochoro vyote. Kwa hili nampongeza huyu mbunge. Hakuna wilaya ambayo barabara zake nyingi ni lami kama temeke.

Tiba
 
Sina uhakika sana kama dada Tiba kama unaishi Temeke na hisi na wewe pia unaishi Kawe na Mtemvu, je Temeke inafanana na Kinondoni mnako hishi nyinyi au ndio mmefanya wanatemeke makarai yenu, kwamba sisi ni wajinga sana umefika kilakala, vituka, Buza ,keko kurasini ,mibulani na changombe niwapi kunalami kila kichocholo kama sio kwa mama yake mzazi kata ya Azimio tu.
 
Heri kuuza sera kuliko kuuza Sura!!
 

naunga mkono hoja
 
Tanzania ndio nchi pekee dunia ina misitu mikubwa ila wanafunzi wanakaa chini na temeke ni moja ya wilaya zenye uhaba mkubwa wa madawati sasa Mtemvu amafanya kipi hapo?
 

wewe unaongelea temeke ipi? kati ya wilaya za dar temeke ndo ipo nyuma kimiundombinu kuliko wilaya zote za dar au hayo maendeleo unacompare na wilaya au sehemu zip apa dar?
 
Hata upande wa maji sasa Temeke hawana shida sana kama zamani, hili ndilo jimbo lililokua linaongoza kwa shida ya maji.
 
haaah,haaah,Pamoja daima ya magamba noma sna.usikute kutano lilikuwa na kadi
 
Siamini kama huyo Mbunge alijenga hizo barabara kwa pesa za mfukoni mwake! Pesa zinazojenga barabara hizo ni zile za walipo kodi wote wa Tanzania. Mbuge huyo alibahatika tu kurithi jimbo ililokuwa na barabara nyingi za lami!! Nani mwenye nia Njema CCM? Wote wezi tu wa mali za umma. Na hiki ndicho kilichowafanya wana Temeke wasusie mkutano wake jana.
 
Acha kutuzugz tuna macho ya kuona ,mbona watu nyomi.Mpaka wamesimama nje ya turubai ambalo ndio ilikuwa makadirio yetu ya awali.Hivyo tumevuka lengo
 

naunga mkono hoja,ni kweli kwa miundombinu temeke ipo juu kuliko wilaya zote za dar,mitaa ya tandika,tmk,yombo ni ful rami vichochoroni.big up mtemvu
 
Wameingia gharama za bure ya kufunga mispika mikubwaa. Halafu bado tunaamini na kujikita kwenye propaganda badala ya kutatua kero za wananchi.
 
Hahaha huyo green guard hapo mbona yupo lege lege sana
 
Aibu gani wamepata hivi kuna aibu kama kupora mke wa mtu na kutelekeza familia au kuzaa nje ya ndoa.
 
Ni kweli hapo kuna nyomi ya kuua mtu,alafu pia sisi CCM hatuhitaji kuwaita watu kuwaelezea tulichokifanya kwani ni nani hajui nchi hii tumeijenga sisis?so watu wanaelewa hilo that is why hawaoni kama kuna haja ya kuja kusikiliza vitu wanavyo vijua
 

Hebu tujuze, anatoa wapi hela? Nijuacho mimi miradi yote inatekelezwa kwa fedha za Halmashauri inazopata kupitia kodi na ruzuku (kama ipo) toka Serikali Kuu. Halmashauri ya TMK ina mpango kazi wake na vipaumbele vyake. Hivyo miradi ya barabara inatekelezwa baada ya kupitishwa na baraza la madiwani. Anachofanya Mbunge/Diwani ni kusimamia na kupaza sauti za wananchi waliomchagua basi, si kutoa hela mfukoni mwake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…