CCM yamzidi Kete Warioba!

CCM yamzidi Kete Warioba!

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,377
Kama ni uhuni katika Mchakato Mzima wa Katiba, ulianzia katika tume ya Warioba kwa kuchakachua Maoni ya Watanzania waliowengi na hasa Waislamu kupitia Maoni ya Mtu mmoja mmoja na taasisi zao. Mimi ni mmoja wa Watanzania niliotoa maoni, miongoni mwao ni Kuanzishwa Mahakama ya Kadhi kwa Mujibu wa Katiba kama ilivyo kwa nchi za Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini, Uingereza n.k.

Lengo ni kuzipa nguvu Mahakama hizo ili maamuzi yake yaweze kuheshimiwa na mahakama nyingine, kwa Mujibu wa mfumo mzima wa Kimahakama ulivyo.

Taasisi karibia zote za kiislamu zilitoa maoni hayo hayo pamoja na mengineyo. Tume ya warioba pia iliwaalika jumuia na taasisi hizo pale Karimjee hall, na taasisi hizo zikapeleka maoni yale yale kwa Maandishi na kwa mdomo.

Lakini kinacho onekana, Mheshimiwa Jaji warioba na kundi lake, walifanya kazi ya uwakala wa kanisa na bila woga, kutupililia mbali maoni hayo kabla ya hata kufikishwa bungueni kujadiliwa.

Sasa inashangaza sana kuyaita Maoni ya Tume ya Jaji warioba kua ni Maoni ya Watanzania.

Kwahiyo basi, walicho fanya CCM, nikuona kwamba huyu kama ameweza kuchakachua maoni ya wananchi na bado wana mshangilia, kwanini na sisi basi tushindwe.

Hivyo basi CCM chini ya MFUMO kristo ambao unaendelezwa kiujanja ujanja wanafanya hicho kinacho endelea sasa.

Ilikuondao utata katika jambo hili, hebu tuangalie nini Masheikh wamezungumza:-

Waislamu watibuka kuzikwa Mahakama ya Kadhi

attachment.php

Waumini wa Kiislamu wakiswali

NA ELIZABETH MJATTA

WAKATI Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba, akitarajia kutoa msimamo wake leo kuhusu hatua ya Bunge Maalumu la Katiba kuzika suala la Mahakama ya Kadhi, Waislamu kupitia Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat), wameapa kuipigia kura ya hapana Rasimu ya Katiba pindi itakapofika kwa wananchi.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Naibu Katibu Mkuu wa Hayat na Mwenyekiti wa Jukwaa la Waislamu la Kuratibu maoni ya Katiba, Sheikh Mohamed Issa, alisema kama Bunge hilo litarudisha Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba kupigiwa kura na wananchi ikiwa haina kipengele cha Mahakama ya Kadhi, wataipigia rasimu hiyo kura ya hapana.

Alisema kitendo cha wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walio wengi kutogusia suala la Mahakama ya Kadhi ni mwendelezo wa kuwanyima Waislamu haki yao ya muda mrefu.

"Lakini hili tumeliona toka katika Tume ya Jaji Warioba walipotuambia kwamba suala hili lisiingizwe katika maoni ya Rasimu ya Katiba hadi nchi mbili washirika kwa maana ya Zanzibar na Tanganyika zitakapokuwa na Katiba zao na waliingize suala hili katika katiba hizo," alisema Sheikh Issa.

Alisema walihoji jambo hilo, lakini majibu yaliyotoka waliona hayakuwa na nia njema katika kuleta Kadhi katika nchi hii.
"Tulipata majibu ambayo yalionyesha kabisa mwelekeo mzima juu ya Kadhi ni ‘negative', kwahiyo toka ilipoanzia na hapa ilipofikia hatushangai," alisema Sheikh Issa

Sheikh Issa alisema kwa sasa wataendelea kuhamasishana kwa nia ya kupiga kura ya hapana katika rasimu itakayorudishwa kwa wananchi
"Mimi sielewi kwanini katika nchi hii tunaogopa Kadhi, majirani zetu wa Kenya wameingiza Kadhi kwenye Katiba yao, jambo hili tumeliomba siku nyingi na tuliambiwa tusubiri mchakato wa Katiba, lakini mchakato ndiyo huu na mambo ndiyo hayo yanayotokea," alisema Sheikh Issa.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Simba, alipotafutwa na MTANZANIA Jumapili juzi kuhusu suala zima la Mahakama ya Kadhi, alisema angetoa tamko lake jana baada ya kukutana na viongozi wa Baraza la Maimamu (Ulamaa).

"Nimekutana na Ulamaa, katika makubaliano yetu tunasubiri kukutana na wawakilishi wetu wa bungeni watupe taarifa rasmi ili tunapotoa tamko tusije tukapishana wakatulaumu kwamba hatujawashirikisha," alisema Mufti Simba jana wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kikao chake na Ulamaa kilichofanyika juzi.
Wakati Mufti akisema hayo, Msemaji wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania (Forum), Sheikh Rajab Katimba, alisema Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi si jambo la huruma bali ni haki yao.

"Mimi nashangaa kwanini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakataa Kadhi wakati ilikuwa moja ya jambo waliloweka katika Ilani ya chama chao, najiuliza kwanini watu hawa hawa wakati ule waone linafaa na sasa hivi waone halifai, wanataka kutuaminisha kwamba wao ni vinyonga wanabadilika badilika au vipi, lakini wafahamu kabisa kwamba jambo hili ni haki ya Waislamu na wanachofanya ni kuukataa ukweli kwa muda tu," alisema Sheikh Katimba.

Suala la Mahakama ya Kadhi liliibua mjadala mkali katika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hadi kuundiwa kamati ndogo iliyokuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu.

Hata hivyo, juzi wakati kamati hiyo ikiwasilisha maoni yake, suala hilo lilionekana kuzimwa kwa sababu ambazo hazikuelezwa bayana.

Ilidaiwa baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo waliweka misimamo ya kutozungumzia suala hilo ingawa baadhi ya wajumbe wachache wa kamati namba nne na tisa waliibua licha ya kutopata mwitikio kama ilivyokuwa katika vikao vya awali.

Chanzo: Mtanzania
07/09/2014
 
Attachments

  • Waislamu.jpg
    Waislamu.jpg
    41.9 KB · Views: 556
Maoni yoyote yalitegemea mambo haya;

Idadi ya waliyoyatoa;
Sababu za kuyatoa maoni hayo;
Faida na hasara za maoni hayo;

Niseme wazi nami, nilipinga kabisa mahakama ya kadhi. Anayesema kuna mfumo kristo hana uthibitisho, kama upo uletwe. Hatutafanya jambo simply kwakuwa wengine wanafanya.
Hatutachangia mahakama ya dini yoyote kupitia kodi.
Kama kweli Waislam wanahitaji, waanzishe wenyewe kwa gharama zao na namna yao.
Tume ilifanya mema na iliundwa na waislam pia. Bunge la katiba linafanya uhuni mwingi na uchakachuaji. Kama kuna jema katika bunge hilo basi ni kwaajili ya manufaa ya ccm
 
Mzimu Tume ya Warioba haikutupilia mbali maoni yenu ya kutaka mahakama ya Kadhi. Warioba na Tume yake walishauri kuwa nchi washirika wa Muungano ziangalie uwezekano wa kuweka mahakama hiyo kwenye katiba zao. Kwa maana kuwa mahakama ya kadhi ikikubaliwa ianzishwe sambamba na mahakama nyinginezo zitakazokuwa chini ya Tanganyika kama vile sasa mahakama hiyo ilivyo chini ya nchi mshirika ya Zanzibar.

Kwa maana nyingine Warioba na Tume yake walitaka mahakama ya Kadhi isiwe jambo la Muungano bali liwe jambo la nchi washirika. Kwa muktadha huo sio sahihi kumbebesha Warioba na Tume yake mzigo wa lawama bila sababu. Walaumu CCM kwa kuitupia mbali rasimu ya katiba.
 
Well said Kinyungu. Kweli kuna watu wanaweka chuki mbele hadi kushindwa kuuona ukweli
 
Maoni yoyote yalitegemea mambo haya;

Idadi ya waliyoyatoa;
Sababu za kuyatoa maoni hayo;
Faida na hasara za maoni hayo;

Niseme wazi nami, nilipinga kabisa mahakama ya kadhi. Anayesema kuna mfumo kristo hana uthibitisho, kama upo uletwe. Hatutafanya jambo simply kwakuwa wengine wanafanya.
Hatutachangia mahakama ya dini yoyote kupitia kodi.
Kama kweli Waislam wanahitaji, waanzishe wenyewe kwa gharama zao na namna yao.
Tume ilifanya mema na iliundwa na waislam pia. Bunge la katiba linafanya uhuni mwingi na uchakachuaji. Kama kuna jema katika bunge hilo basi ni kwaajili ya manufaa ya ccm

Hoja ya kodi ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu yoyote ambae ameenda shule na kuelewa masomo yake vyema. Kwani ni wakristo peke yao ndio wanaolipa kodi?. Basi sisi waislamu tunataka kodi zetu zigharamie Mahakama ya kadhi!. Sasa wewe shauri utaratibu gani utumike kuzitenganisha kodi hizo!.
 
Tume ya warioba ilikuwa na wasomi waliobobea na wanaojua wanachokifanya ,dharau mnazotoa hazina tofauti na zakina Lukuvi ,ile rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ni ya kupigiwa mfano sio humu Tz tu bali Afrika kwa ujumla na nina imani kabisa copy yake itahitajika kwenye nchi zingine.
 
Tumia akili. Hoja ya kodi ni hoja dhaifu kwa mzembe wa kufikiri. Hujui kwamba kila kitu hugharamiwa kwa kodi?
Hakuna namna ya kuzitenganisha ndio maana nikashauri kwamba mfuate ushauri wa Kikwete (mwislam mwenzenu) kwamba mzianzishe na kuzihudumia wenyewe. Tukishakusanya kodi hakuna namna ya kuijua ipi ni ya mwislam au la! Ila ninyi.mkichangishana huko misikitini hilo la kwenu.

Hivi wewe inakuingia akilini kuchangia kitu usichokijua, kisichokusaidia, kisichohusu maisha yako wala hukiamini???

Ninyi inawahusu, kwanini mnahitaji tuwasaidie kuzianzisha?? Anzisheni kwa mpango wenu maana HAZITUHUSU WAKRISTO
 
Mzimu Tume ya Warioba haikutupilia mbali maoni yenu ya kutaka mahakama ya Kadhi. Warioba na Tume yake walishauri kuwa nchi washirika wa Muungano ziangalie uwezekano wa kuweka mahakama hiyo kwenye katiba zao. Kwa maana kuwa mahakama ya kadhi ikikubaliwa ianzishwe sambamba na mahakama nyinginezo zitakazokuwa chini ya Tanganyika kama vile sasa mahakama hiyo ilivyo chini ya nchi mshirika ya Zanzibar.

Kwa maana nyingine Warioba na Tume yake walitaka mahakama ya Kadhi isiwe jambo la Muungano bali liwe jambo la nchi washirika. Kwa muktadha huo sio sahihi kumbebesha Warioba na Tume yake mzigo wa lawama bila sababu. Walaumu CCM kwa kuitupia mbali rasimu ya katiba.

Nakushukuru sana kinyungu. Kwakeli umenielewesha kwa weledi wa hali ya juu. Naomba nikiri kua hilo ilikua mimi silijui. Hili ni jibu la kwanza lililo nitosheleza kiu yangu tangu mjadala wa Katiba Mpya Uanze.

Kama hivyo ndio sahihi, that means, uhalali wa MAHAKAMA YA KADHI upo ndani ya serekali tatu. Napenda kukiri kama kuna ushahidi wowote wa nukuu ya Maneno yako, basi sina uhalali wa Moja kwa moja kuishutumu tume ya Jaji Warioba. Kwa Maana hiyo, jinamizi letu ni CCM, na nakuahidi, they will not live to be in power ever again, starting 2015.

Naomba niwekee wapi nitaiona hiyo nukuu, nianze kuomba radhi na kuelekeza mashambulizi yangu sehemu husika.
 
.... Basi sisi waislamu tunataka kodi zetu zigharamie Mahakama ya kadhi!. Sasa wewe shauri utaratibu gani utumike kuzitenganisha kodi hizo!.
sasa si upendekeze.....
 
Mkuu MZIMU
Kwanza nakuomba utambue kuwa katika Tume ya Mzee Warioba Waislam walikuwa zaidi ya asilimia 80 hivyo wangetaka kupitisha au kuweka jambo lolote lenye maslahi kwa Waislam wasingeshindwa ila kikubws kilichowaongoza ni utaifa. Walitambua kuwa taifa la Tanzania ambalo walikuwa pale kulitungia Katiba itakayo waongoza ktk kipindi cha miaka Hamsini kama si mia ijayo, halina dini hivyo hawezi kuweka jambo lenye maslah kwa upande mmoja wa dini huku likinyonga upande mwingine wa dini. Hiki ndicho kitu kikubwa kilichowangoza na kwahili hawakujali uwingi wa upande flani wa wajumbe wa tume bali WALIRIDHIANA na KUKUBALIANA

Tena ikumbukwe kuwa Watanzania wakristo hawana tatizo na uwepo wa Mahamama ya kadhi ktk katiba, Bali tatizo lao kubwa ni jinsi itakavyoshughulikiwa kwamba iweje kodi ya mkritu ikatumika kuendeshea jambo lisilokuwa na maslah kwake na ambalo ni ibada kwa mujibu wa dini nyingine? Je huku si kulazimishana kuamini kile usichokiamini? Tena kumbuka mkuu jinsi jambo dogo la uchinjaji lilivyoleta utata baada ya kubainika kuwa kwa kufanya hivyo (kuwapa waislam wachinje wanyama) unakuwa unashiriki ibada yao. Kwanini tufike huko wakati uwezo wa kuzuia tusifike tunao?

Jambo ambalo liko dhahiri ni kwamba hiyo mahakama ya kadhi iwekwe tu ktk katiba tena iainisbwe kwamba itashughulikiwa na kuendeshwa/kugharimiwa na waislamu wenyewe (kitu ambacho waislam wengi hawataki kusikia) hapo hamwezi kumwona yeyote akiwalalmikia..huku kudai ni kanisa na mfumo kristu ndio uliosababisha hili jambo kukataliwa au kutowekwa kwenye katiba ni kutojua au kuamua tu kwa maksudi kupotosha kitu ambacho hakina tija si tu kwa waislam wenyewe bali taifa zima kwa ujumla

Nguruvi3 Mag3 mkandala

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:

Nakukubalia respect wa boda. Ila mtego wa Utaifa kwa waislamu ndi Mtego uliwagharimu Waislamu katika nchi hii kwa kiwango kikubwa sana. Tafadhali fuatilia historia ya WATEMI Wailio pigania uhuru, Vita vya MAJI MAJI, TANU, EAMWS, BAKWATA na Julius Kambarage kuandikwa peke yake Katika historia rasmi ya nchi hiii.

Karibia mara zote, Waislamu wa nchi hii wamekua wakiweka Utaifa kwanza na Uislamu Baadae. Kinyume chake kimekuwa kwa Viongozi wakirsto na wakirsto waliopewa dhamana katika nchi hii. Mara zote wameweka Ukristo kwanza na Utaifa baadae.

Tumekuwa tukitoa maelezo mengi sana juu ya hali hiyo katika Munakasha mbalimbali ikiwemo hapa JF. Kwa bahati mbaya sana, kuna baadhi ya Waislamu bado hawajitambui. Wao wameweka Maslahi ya Matumbo yao Kwanza kuliko hata huo utaifa wenyewe. Hivyo Basi hua wanapopata fursa ya kuwekwa kwenye decisions boards, hua ni watu wakuburuzwa tu.

Kwani katika hilo Bunge la CCM linaendelea ambalo limekosa uhalali wa kisiasa, waislamu hao bado wamo. Alhamdulahi, mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othaman kesha shtukia dili lao, kaamua kujitoa. Pamoja kua temesikia katika vyanzo vya siri kua Wabunge Waislamu wanajipanga kujitoa katika bunge linalo endelea kama Mahakama ya Kadhi haitatambuliwa, kama ambavyo waliamamua katika mikutano ya mabaraza ya kanisa kua kama mahakama ya kadhi ingepitishwa na kamati ya Mheshimiwa Brigedia Hassan Ngwilizi nao wangejitoa.

Mimi nadhani hili jambo lazima lijadiliwe kwa kina, faida na hasara zake kwa jamii ya watanzania kabla hali haijakua mbaya.
 
Tumia akili. Hoja ya kodi ni hoja dhaifu kwa mzembe wa kufikiri. Hujui kwamba kila kitu hugharamiwa kwa kodi?
Hakuna namna ya kuzitenganisha ndio maana nikashauri kwamba mfuate ushauri wa Kikwete (mwislam mwenzenu) kwamba mzianzishe na kuzihudumia wenyewe. Tukishakusanya kodi hakuna namna ya kuijua ipi ni ya mwislam au la! Ila ninyi.mkichangishana huko misikitini hilo la kwenu.

Hivi wewe inakuingia akilini kuchangia kitu usichokijua, kisichokusaidia, kisichohusu maisha yako wala hukiamini???

Ninyi inawahusu, kwanini mnahitaji tuwasaidie kuzianzisha?? Anzisheni kwa mpango wenu maana HAZITUHUSU WAKRISTO
Vipi hela ya walipakodi inayoendesha na kulipa mishahara ya mahospital ya kanisa?
 
watu kama mtoa mada huyu ni wagumu mno kuelewa. siyo kwamba Waryoba hakuzingatia maoni yenu ila alisema maoni hayo yatumike kwenye uandaaji wa katiba za nchi washirika. Rasimu ya katiba ya Waryoba ilibeba mambo ya muungano tu.
 
Mzimu soma rasimu hapa, utayaona hayo. Attached: RASIMU YA PILI YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA
MWAKA 2013.pdf (1.05 MB)
 
Uelewa ukiwa mdogo ni madhara makubwa.

Hospitali za makanisa na misikiti zote zinawahudumia wananchi wote, hata shule na vyuo huwahudumia wote bila ubaguzi (isipokuwa seminari na hizi hazipati hela ya serikali). Ila mahakama ya Kadhi ni ya Waislam tu, wengine haituhusu kabisa wala hatutakubali ianzishwe hapa. Anzisheni mkitaka kwa gharama na utaratibu wenu.
Kama mna watu wamekosa ajira serikalini mnawaanzishia kwa style ya wao kupata kazi sahau.

Faida zake ni zipi? Mbona hamzisemi?
 
We mzimu kweli.
Hebu tutajie faida za mahakama ya kadhi kwa nchi ya Tanzania

Nakushukuru ndugu Wiston Mtanzania kwa swali zuri na Muhimu. Hili ni swali linalo stahili kujibiwa.

Kulingana na Muda, nitakueleza kwa kifupi lakini vyakutosha.

Kwanza kabisa, Makama ya Kadhi, ni Mfumo wa Kimahakama katika sheria za dini ya kiisilamu. Ieleweke kua, Uislamu ni Mfumo wa Maisha uliotawaliwa na sheria katika kila hatua ya Mwanadamu.

Kwa ufupi, katika Mahakama za kadhi, Waislamu wangependa kupeleka mashauri yao kama Migogoro ya Kibiashara, Ndoa, Mirathi na kila jambo ambalo wao kama waisilamu wangependa kuhukumiwa kwa mujibu wa Mafundisho ya Dini ya kiislamu.

Kwa mfano, katika masuala ya mirathi, kunatofauti kubwa sana kati ya maamuzi ya Mahakama za kawaida na Mahakama za Kiisilamu.

Mahakama za kawaida mara nyingi sana zina mtambua mrithi hasa anapokufa baba kua ni Mama ni Watoto. Katika mahakama za kadhi sio hivyo.

Katika mahakama za kadhi, warithi ni zaidi ya hao. Kwa mfano katika mahakama za kadhi, Wazazi nao pia wanaingia kama warithi wa mali za mtoto aliefariki ambae alioa na kuzaa. Logically, mtu yoyote mpaka anafikia hatua ya kuoa, basi alikuwa na wazazi ambao wamepoteza nguvu zao katika kumlea hadi hapo alipo. Na inawezekana by the time anaoa, wazazi wake wamesha zeeka na wanamtegemea. Sasa leo iweije kufa kweke iwe sentence ya kifo kwa wazazi wake pia, au wazazi wake wabaki ombaomba wakati nguvu zao zote walizutimia kwa mtoto wao?.

Huo ni mfano mdogo tu. Kuna mendi zaidi ya hayo. Sheria katika dini ya Kiisalamu ni somo mahsusi na watu wana specialize katika hilo.

Hivyo basi sio jambo la kuzuka tu au kutamani tu, bali ni msingi muhimu katika dini ya kiisilamu. Kwa hiyo basi ili haki ya Uhuru wa kuabudu katika nchi itendeke vema, hilo nijambo moja wapo katika hayo.
 
swali je! kila Mtanzania anatakiwa kwenda kutoa maoni DODOMA? Ikiwa maoni yashatolewa na wananchi wenyewe au ndo ccm kupinga RASIMU
 
Back
Top Bottom