CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

Binafsi sioni kama ni vibaya maana wanajifurahisha ila ubaya wake utakuja pale na vijana wa cdm na wenyewe wakiamua kuchana bendera ya magamba nafikiri hapo ndipo matatizo hasa yalipo, maadam chama ni sera na itikadi naamini watu wanaelewa sera na itikadi za vyama ndo maana wanazifata binafsi naamini mapenzi ya chama na nchi yako moyoni hivi vingine ni utambulisho tu wa chama
 
Hiki ni kitendo kinachoruhusiwa kwenye siasa?

Naomba msaada

Hapa ni dhahiri walikuwa wakiyafanya hayo kwa hasira ya kuzidiwa nguvu na wahasimu wao ktk kila kona. CDM wazidi kwenda mbele. Ni aibu kwenye chama kingongwe kama hiki kukazana kujibu mapigo ya wapinzani wao...Si kutegemea wangeweweseka namna hiyo.
 
Unalia lia nini hayo ni majibu kwa Chadema, CCM nadhani wanalipiza kisasi tabia ya kuchana kadi za vyama walianza Chadema...umeumia sana mkuu pole sana.
Wewe ukishaambiwa kuwa si ustaarabu na kama kweli sio basi ukubali,sio kupinga tu kila kitu,endelea na uratibu wa usafiri wa watu wa mbagala,kwani ni fuso ngapi vile zinazoelekea mbagala kaka ritz1
 
Watanzania tumenasa kwenye mtego mbaya na siasa za ajabu!! Badala ya kupigania utaifa wetu! kupigania maisha yetu ya watoto wetu na vizazi vijavyo tumetumbukia kwenye ushabiki! oh!! my dear Tanzania! Wanakupeleka wapi? Huduma za afya mbovu! elimu mbovu! maji hakuna! umeme hakuna barabara zimekuwa mahandaki! watu wengi hawana uhakika wa chakula! malazi na mavazi! Mikutano ya vyama ikija tunakusanyika kuvaa sare za kupewa ushabiki wa kurudisha kadi na kuchana kadi na bendera lakini wengi wetu tukitoka hapo hatujui tunaenda kula nini? tunaenda kulipaje kodi za nyumba? bill za umeme na maji? gharama za matibabu ya wagonjwa wetu! ada za shule za watoto wetu!! barabara zetu hazipitiki ?malaria inapukutisha watu!! Jamani tuachane na ushabiki tuwaulize viongozi wanatatua lini na kivipi haya matatizo yetu? wawe ccm wawe chadema waulizeni? waulizeni rasimali zetu madini, maliasili,n.kzinamsaidiaje Mtanzania mmoja mmoja? Tuondokane na ushabiki tuwe wakweli na uchungu na nchi yetu! Tusihalalishe matatizo kuwa sehemu ya maisha yetu!!
 
Acha tu wamwage lakini sisi tunachangiwa wenyewe sijui wanakozitua.2015 huenda wakafungwa wengi sana
 
Jamani kuhusu huyo majembe,nashindwa kuelewa huo uforofesa alipewa na nani,maana namwona kama hajai kwenye huo u-forofesa wake.Au wenzangu mnamwonaje,nisije kuwa simtendei haki forofesa majembe.
 
Binafsi sioni kama ni vibaya maana wanajifurahisha ila ubaya wake utakuja pale na vijana wa cdm na wenyewe wakiamua kuchana bendera ya magamba nafikiri hapo ndipo matatizo hasa yalipo, maadam chama ni sera na itikadi naamini watu wanaelewa sera na itikadi za vyama ndo maana wanazifata binafsi naamini mapenzi ya chama na nchi yako moyoni hivi vingine ni utambulisho tu wa chama

bwn mkubwa na wanajamvi,apa tatizo linalokuja kujitoteza ni dhana mbovu ya kuharibu image ya chama kingne,apa ndo tatzo litakalozaa kuhujumiana na hata kuanza kuwindana kulipa kisasi,iwe imefanywa na ccm au cdm bado ni kitu kibaya,kero yangu ni huu uhuni wa kuandaa kizazi kinatumia jazba kujibu hoja!
 
nakumbuka hata CHADEMA
walishawahi kuchoma moto kadi za Magamba ilikuwa Makumira University,
siasa za bongo zinaonekana ni chuki hakuna fair play

Acha wachome! Si wamezitengeza wenyewe! Magamba bwana, kwisha! alfu sikujua kumbe Magufuri nae mbwiga tu!
 
Wakuu nimepita magomeni sehemu nafanya service gari yangu nimezipata hapa nyepesi nyepesi kwamba zimechapishwa kadi nyingi sana zinazofanana na za CHADEMA zimegawiwa kwa watu kibao, wakati wa Mkutano wa CCM leo hao watu watajifanya ni wanachama wa CHADEMA waliochoka na udini na ukabila ndani ya CHADEMA hivyo wameamua kujiunga na CCM. Subirini mtaona hiki kituko baadaye.
i really like your signature mkuu
 
Yeah lakini havibebi heshima kama Bendera ya Taifa... Bendera za Vyama hazina heshima yoyote hakuna anayeziabudu Duniani kokote kama za Taifa

Kwahiyo Mtu yoyote anaamua lolote; Hauwezi hata kuweka kwenye Katiba ya Nchi; Labda sheria za Polisi kama kuingiliwa

mkuu sheria za polisi?una maana gani apa?hata polisi wana sheria au una maana sheria za nchi zinazolindwa na polisi na kutafsiriwa na mahakama!? Alaf unasema huwezi kufanya lolote-kweli unazijua kanuni na taratibu za uchaguzi?ambazo zote ziko kisheria kufuatwa!?
 
;;;;;;.png
Wakuu hapa vipi????
 
mkuu sheria za polisi?una maana gani apa?hata polisi wana sheria au una maana sheria za nchi zinazolindwa na polisi na kutafsiriwa na mahakama!? Alaf unasema huwezi kufanya lolote-kweli unazijua kanuni na taratibu za uchaguzi?ambazo zote ziko kisheria kufuatwa!?

Ninasema kuchana bendera za vyama vya kisiasa ni issue ya Polisi sio Issue kuu ya kuhusisha kwenye Katiba kama bendera ya Taifa hairuhusiwi kuchanwa au kutumiwa vibaya kama hizo za vyama vya kisiasa
 
Ninasema kuchana bendera za vyama vya kisiasa ni issue ya Polisi sio Issue kuu ya kuhusisha kwenye Katiba kama bendera ya Taifa hairuhusiwi kuchanwa au kutumiwa vibaya kama hizo za vyama vya kisiasa

ok mkuu ila concern yangu haijakaa kikatiba ila ni ktk hali ya ujiran mwema isingependeza kuwa na siasa za chuki!au kuharibiana political images! Tusiendekeze kuharibu political identifications...
 
ok mkuu ila concern yangu haijakaa kikatiba ila ni ktk hali ya ujiran mwema isingependeza kuwa na siasa za chuki!au kuharibiana political images! Tusiendekeze kuharibu political identifications...

As long as they don't kill each other; sio mbaya hiyo ni Misisimko ya kisiasa bila Msisimko nani atatoka nyumbani kwake na
Jua kali kwenda kuhudhuria Mkutano wa chama cha kisiasa kwenye Jua kali? Siasa ni Misisimko, Furaha ndani ya Mikutano na Motisha bila hilo hakuna atakayekupigia kura; labda Uchakachue
 
Back
Top Bottom