CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho.

Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.

Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.

Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.

Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.

Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.

"Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani," alisema Nape.

Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.

"Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

"Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam," alisema Nape.

Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.

Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.

CHADEMA yaipa masharti magumu
Akizungumzia mkutano huo wa CCM, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.

Akizungumza kutoka Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema CCM inatakiwa kuwaambia Watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za Watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.

CHADEMA pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa CCM waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie Watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

"CCM isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.

"Tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo," alisema Dk. Slaa.

 
Mamluki wamekodiwa kutoka vijijini, na kadi mpya za CDM zimesha kuwa printed ili mamluki wajidai wanazirejesha.

Malipo kwa mamluki hao ni sh. 10'000/=

Mdogo wangu alipewa kazi hiyo na amekataa kupokea hiyo hela.
 
Hata cdm si pia mnawalipa mamluki nani hajui ,,,,, kwa hiyo ngoma droo
 
Mbona mnaogopa vivuli vyenu wenyewe? Tulieni watoto moto bado haujawashwa.
 
attachment.php
 
Wakuu nimepita magomeni sehemu nafanya service gari yangu nimezipata hapa nyepesi nyepesi kwamba zimechapishwa kadi nyingi sana zinazofanana na za CHADEMA zimegawiwa kwa watu kibao, wakati wa Mkutano wa CCM leo hao watu watajifanya ni wanachama wa CHADEMA waliochoka na udini na ukabila ndani ya CHADEMA hivyo wameamua kujiunga na CCM. Subirini mtaona hiki kituko baadaye.
 
Du kama ni kweli CCM ni sikio la kufa, hizi mbinu mbona za kizamani sana, watu washalichoka hili lichama lao, wangekubali tu kuliko kuendelea kutumia pesa zetu kwa upuuzi kama huu.
 
ccm chama makini weye,,, hakuna feki ,,, je shybuda akirudi ccm naye ni feki .
 
Hawa watu Diamond, Marlaw, Frola Mbasha wako kibiashara na siyo uzalendo.
 
Hata watumie mbinu gani, CCM imekufa
Wakuu nimepita magomeni sehemu nafanya service gari yangu nimezipata hapa nyepesi nyepesi kwamba zimechapishwa kadi nyingi sana zinazofanana na za CHADEMA zimegawiwa kwa watu kibao, wakati wa Mkutano wa CCM leo hao watu watajifanya ni wanachama wa CHADEMA waliochoka na udini na ukabila ndani ya CHADEMA hivyo wameamua kujiunga na CCM. Subirini mtaona hiki kituko baadaye.
 
Inasikitisha sana kuona mamilioni ya pesa yanavyotumika hovyo kwa mambo ya kijinga kabisa na huku wagonjwa wakikosa dawa hospitalini na kwenye vituo nya afya! Hakika CCM ni wauaji! Tutawapuuza!
 
Wakuu nimepita magomeni sehemu nafanya service gari yangu nimezipata hapa nyepesi nyepesi kwamba zimechapishwa kadi nyingi sana zinazofanana na za CHADEMA zimegawiwa kwa watu kibao, wakati wa Mkutano wa CCM leo hao watu watajifanya ni wanachama wa CHADEMA waliochoka na udini na ukabila ndani ya CHADEMA hivyo wameamua kujiunga na CCM. Subirini mtaona hiki kituko baadaye.
Acha unafiki,mbona mm naishi hapa hapa migomigo na sijaona hizo pumba unazoziongea?
Acha hizo bana,ccm ndio mambo yote.
 
Back
Top Bottom