CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo

CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo

mwaka huu zanzibar kuna sinema si ya kawaida.

kwa kweli mwaka huu ni mwaka wa historia vitabu vingi vitaandikwa

kwanza mtoto wa muasisi wa mapinduzi na rais wa awamu iliopita hawawivi chungu kimoja na ccm hasa wa zanzibar msimao wake upo wazi anataka mamlaka kamiili

mtoto wa muasisi mwengine mansour yussuf himid na yy ndio hivyo yupo against nao na msimamo ule ule kua mamlaka kamil

mwanasheria aliekua wa serikali ya zanzibar kaonyesha hadharani kua zama zimebadilika hakuna mbili bila ya zanzibar kua na mamlaka kamili

muasisi wa mapinduzi na muasisi wa hio ccm na miongoni wa waandishi wa katiba ya mwanzo nassor moyo na yy ndio kajiunga na teller hasikii wala haoni zaidi ya mamlaka kamili

katibu mkuu wa baraza la mapinduzi la mwanzo na yy yupo kwenye timu ya mamlaka kamili

jumbe msimamo wake unajulikana aliekua rais wa pili na mwenyekiti wa mwisho waASP kwa kweli kazi ipo

hawa wote ni wana ccm damu walikua si waarabu si mahizbu hawa ila kwa kweli wanataka mamlaka kamiiili


mwaka huu kwa waasisi waliobaki ccm labda mmoja mzee hamid ameir na yy hana nguvu yyte wala ushawishi

Mkuu, hii ya leo kumfukuza Mh Mzee Nassor Moyo kwenye CCM, inanikumbusha tukio la Rais mstaafu wa Nigeria Gen Olusegun George Obasanjo alivyochana kadi ya PDP. Mzingira ni yale yale. Leo Gen Buhari anasubiri kuapishwa may 29.
 
Muungano haudumishwi kwa kufukuzana. Nina wasiwasi ikiwa ccm itabaki zanzibar na hasa wakishindwa kushika dola; ASP inarejea...

Naamini kuna waunguja wachache wanaomdanganya rais shein ila wakmfukuza mzee Moyo ndio mwisho wa ccm zanzibar na ninavyomjua mzee moyo huwa si mtu wa kumumunya maneno atakubali haraka
 
Pia halmashauri ya chama mkoa haina uwezo wa kumvua mtu uanachama maamuzi yote yanatolewa na NEC na mkutano mkuu
 
Nyuma ya pazia ya yote haya ni maridhiano ya kisiasa yaliyozaa SUK Zanzibar. Pamoja na mafanikio ya hayo maridhiano lakini kinyume chake ndiyo haya tunayoyaona sasa.
 
Kama umemsikiliza Lembeli leo ITV utagundua kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya CCM. Amewaambia wananchi wa Kahama wafanye kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 
Daah maamuzi ya CCM ni kinyume kabisa,kwenye NDIYO kwao ni HAPANA,Mzee ukweli unakufanya udumu katika historia ya mashujaa wa mapinduzi ya kweli.
 
TAARIFA MUHIMU:

Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kupitia kikao chake kilichomalizika muda huu Kimemvua Uanachama wa C.C.M Mzee HASSAN NASSOR MOYO na hivyo kuanzia sasa Mzee Moyo si mwanachama tena wa Chama Cha Mapinduzi.

moyo+px.jpg

Hassan Nassor Moyo​

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


Self defeat; CCM is but sending message to EL that oncea similar decision is done against him none, including him will do anything.

Lowasa tia maji! Kinyozi amepanda meli kuelekea bara
 
Back
Top Bottom