CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo

CCM yamvua Uanachama Mzee Hassan Nassor Moyo

HASSAN Nassoro Moyo, ni kati ya waasisi wawili wa Muungano kwa upande wa Zanzibar ambao mpaka sasa bado wako hai. Mwingine ni Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

Moyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 80, ni Waziri wa kwanza wa Sheria aliyekula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano, Hayati Mwalimu Julius Nyerere Aprili 27 mwaka 1964, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Yeye ni miongoni mwa wajumbe 20 kutoka Bara na Zanzibar walioongozwa na Hayati Shekhe Thabit Kombo kuunda Katiba ya Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa Mwaka 1977 ambapo Katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho kidogo na kuzaa Katiba ya Muungano inayotumika sasa na ambayo ipo katika hatua za mchakato wa marekebisho yake.
 
CCM...kambi ya wezi, wanafiki na waongo! Mzee Hassan Nassor Moyo anavuliwa uanachama, Andrew Chenge, nyoka wa makengeza, anapewa heshima ya kuandika katiba mpya.[/QUOTE]

Usihofu mkuu, anaenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji..
Kwa heshima zote nakukaribisha Mzee wangu.
 
Hii CCM ikoje ina maana kuna CCM mbili?CCM Zanzibar na CCM Tanganyika?na kwamba CCM Zanzibar ndio inameno ya kung'ata na CCM Tanganyika ni kama kibogoyo?.

Tanganyika ndiko kumejaa wana CCM wengi sana wanaokwenda tofauti na maadili ya chama lakini wengi wao hawachukuliwi hatua zozote, hata pale ambapo hatua zimekuwa zikichukuliwa zimekuwa zinawahusu wale vidagaa, huku wakiachwa mapapa wakiogelea wapendavyo.

Lakini upande wa Zanzibar ina onekana wana CCM wa huko hawana uhuru wa kutoa mawazo yao hadharani na wanapo jaribu kufanya hivyo chama kinawazima mapema.

Umenikumbusha yule mwanasheria mkuu wa znz
 
attachment.php
 
Jifunzeni siasa...CCM hatumzungumzii tena Mansour wala hatutamzungumzia tena Mzee Moyo, enzi yao ndani ya CCM imekwisha..tulikuwa nao tukijenga Chama pamoja nao, tumethamini na kujali mchango wao hata leo ila kwa makosa ambayo KANUNI ziko wazi leo sio wanachama wenzetu ndani ya CCM lakini hawawi tena hoja kwetu.

Mbona mnatirirka humu kumshabikia shemeji yenu Zana za kilimo...
 
Jifunzeni siasa...CCM hatumzungumzii tena Mansour wala hatutamzungumzia tena Mzee Moyo, enzi yao ndani ya CCM imekwisha..tulikuwa k tukijenga Chama pamoja nao, tumethamini na kujali mchango wao hata leo ila kwa makosa ambayo KANUNI ziko wazi leo sio wanachama wenzetu ndani ya CCM lakini hawawi tena hoja kwetu.
Hamumzungzii lakini mumemfungulia kesi ya uongo. Ni lipi bora Kati ya hayo mawili? Tatizo lenu gambas hamna akili ya kupambanua jambo. Mnaandika tu mkifikiri kila mtu ni wa aina yenu.
 
kati ya zito na Mzee moyo nani muhimu kwa ccm?hapo ccm hawajamtukana mmoja Wa waasisi Wa taifa hili?,namtaka yule shehe adondoshe chozi kama alivyomlilia Mzee Nyerere.
 
Jifunzeni siasa...CCM hatumzungumzii tena Mansour wala hatutamzungumzia tena Mzee Moyo, enzi yao ndani ya CCM imekwisha..tulikuwa nao tukijenga Chama pamoja nao, tumethamini na kujali mchango wao hata leo ila kwa makosa ambayo KANUNI ziko wazi leo sio wanachama wenzetu ndani ya CCM lakini hawawi tena hoja kwetu.



Lini ccm imeacha kuzungumzia mtu?,
Hebu tuambie Mbona Bashe na Dr.Salm Ahmed Salm hamjamvua unachama wa ccm,wakati Mh. Mzee na Lt. Makamba kuwa sio raia watanzania?

Au mmewasamehe kwa kuwa wamekaa kimya?
 
Nauliza chama changu. Chama kipo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani,yaani Zanzibar. Kote kuna makada wenye misimamo tofauti. Wapo waitikia ndiyo na wakosoaji kwa uboreshaji. Hatua za kinidhamu chamani huchukuliwa. Kubwa ni kufukuzwa uanachama.

Hivi karibuni,alifukuzwa uanachama Himid Mansour. Leo,amefukuzwa Mzee wangu Moyo. Kwanini wawe wa Zanzibar tu? Bara hakuna mwenye makosa? Bara hakuna wanaotofautiana na chama?

Vipi wale wa kuvuliwa magamba-Lowassa,Chenge na Rostam Aziz? Wanalindwa na kuachwa kwakuwa ni wa kutoka Bara? Kuna jambo halipo sawa mahali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Taarifa zote zitatolewa katika taarifa rasmi ya Chama kuhusu kuvuliwa uanachama Ndg Hassan Nassor Moyo.
laana ya kuwapuuza wazee haitowaacha , hivi kuna wa kumvua uanachama mwadilifu kama mzee moyo ndani ya ccm hii ? yaani chenge na lowasa ni bora kuliko mzee moyo ? unajua bhana kuna mambo ccm inatenda hata shetani ameshika kiuno kwa bumbuwazi !
 
Kwa hali kama hii itafika wakati tutaanza kuambiwa kuwa wazanzibar hawatakiwi kwenye chama cha CCM chama chao ni CUF,kama CCM isivyo wataka wachagga kwenye chama chao kwa kuwaambia kuwa chama chao ni CHADEMA.
 
Back
Top Bottom