CCM yamtema waziri Aggrey Mwanri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamtema waziri Aggrey Mwanri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by siha tanganyika, Sep 2, 2012.

 1. s

  siha tanganyika Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HALI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imezidi kuchafuka kufuatia vigogo wa serikali kutuhumiwa kuhusiana na kampeni chafu zikiwamo rushwa na fitina, ambapo katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmoja wa mawaziri machachari wa serikali ya Jakaya Kikwete amekataliwa asigombee nafasi nzito ya uongozi aliyoomba.

  Aliyekwaa kisiki hicho ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, baada ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro kugoma kupitisha jina lake kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Habari za kuaminika zimesema kuwa uamuzi wa kufuta jina la Mwanri ulifikiwa katika kikao cha halmashauri ya wilaya kilichokaa Agosti 29, 2012, kwenye ofisi ya CCM ya wilaya hiyo.

  Mmoja wa viongozi wa CCM wa wilaya aliliambia Tanzania Daima kuwa, katika kikao hicho wajumbe wengi walikataa kabisa kulijadili jina la Mwanri, badala yake wakajadili majina mawili ya waombaji wengine ambao walitajwa kuwa ni Joha Mtawazo na Meejo Laizer.

  Imedaiwa kuwa sababu za kuenguliwa kwa naibu waziri huyo ni kuwa kwake na nafasi nyingi za utendaji ndani ya chama na serikali, ikiwa ni pamoja na nafasi yake ya ubunge, na kwamba hawakuwa tayari kurundika vyeo vingi kwa mtu mmoja, wakati kuna vijana wengi wenye uwezo na moyo wa kukitumikia chama.

  "Maamuzi ya viongozi wetu ambayo yameungwa mkono na baadhi ya wajumbe ni mazuri kwani kwenye wilaya yetu kuna wanachama wengi tu wenye sifa na wanaweza pia kutuwakilisha vizuri kwenye mkutano wa halmashauri kuu sasa, kwa nini mbunge yeye awe ndo kila kitu," alihoji mwanachama mmoja bila ya kutaka kutajwa jina lake gazetini.

  Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Oscra Jeremia bila kukubali wala kukataa kuhusiana na uamuzi wa kufuta jina la Mwanri, alisema kuwa ni jambo la busara sasa kwa viongozi wa chama kufanya maamuzi sahihi katika mgawanyo wa uongozi kisiasa na kuachana na mtindo wa kumuachia mtu mmoja kubeba vyeo vingi wakati kuna wanachama wengine wenye sifa.

  "Ni bora kama wapo waliojitokeza na wana sifa wakaachiwa, kwani ukimuachia mtu mmoja kila kitu inaleta balaa zaidi hivyo mbunge inabidi aache busara itumike kwa sababu si vizuri kuchukua kila kitu," alisema.

  Hata hivyo, alikiri kuwasiliana na waziri huyo ambaye amedai kuwa baada ya kujua kuwa kuna wagombea wengine waliojitokeza kwenye nafasi hiyo, alikubaliana na uamuzi wa kuondoa jina lake.

  "Ni kweli mbunge alikuwa amechukua fomu lakini kanuni zilikataa, hivyo ikabidi aombwe. Sasa kama wapo wenye sifa ni bora wapewe," alisema.

  Rushwa, vitisho, ukabila vyatawala
  Tuhuma za kukithiri kwa kampeni chafu zimeendelea kuripotiwa sehemu mbalimbali nchini, huku Jumuiya ya Wanawake wa CCM, ikionekana kuelemewa na uchafu mwingi.

  Huko Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa kuwa siasa chafu na utoaji rushwa wa waziwazi unadaiwa kufanywa na wagombea, huku watendaji wa serikali wakidaiwa kuwa vinara wa mchezo huo.

  Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa wagombea katika uchaguzi huo, zinasema kuwa katika uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti uliofanyika Agosti 23, uliompa ushindi Hapsa Kilingo, baadhi ya viongozi wa CCM na serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, anayedaiwa kutoa hongo ya fedha na vitenge kwa baadhi ya wajumbe ili ‘mtu' wake ashinde.

  Habari pia zinadai kuwa, kampeni zilitawaliwa na siasa chafu zilizobeba udini, ukabila na kuingilia mambo binafsi ya kifamilia ili kuchafuana.

  Kiongozi mwingine wa CCM (jina limehifadhiwa) inadaiwa aliwasafirisha wajumbe kwa magari huku akitambua kuwa ni kinyume na sheria za uchaguzi wa CCM toleo la Februari 2010 ibara ya 33 (13).

  Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, aliliambia Tanzania Daima kuwa pamoja na kuwepo kwenye uchaguzi huo, hakuhusika kwenye kampeni zilizokiuka kanuni za uchaguzi na kama kuna mwenye ushahidi wowote juu ya hilo auwasilishe katika sehemu inayohusika.

  "Ni kweli nilikuwepo kwenye uchaguzi huo kama mjumbe lakini sikushiriki kwenye kampeni zinazokiuka kanuni za uchaguzi," alisema Mgalu na kuongeza kuwa ikiwa mlalamikaji anao ushahidi, ni vema akaupeleka katika vyombo vinavyohusika ili hatua za kisheria zichukuliwe badala ya kulalamika tu katika vyombo vya habari.

  Chenge awania ujumbe wa NEC
  Baadhi ya wabunge katika mikoa wa Simiyu na Shinyanga, akiwemo Andrew Chenge, wanadaiwa kujitosa kuwania nafazi za ujumbe wa NEC, huku kukiwa na habari za kuibuka kwa siasa za chuki, fitina na uhasama wa hali ya juu.

  Aidha baadhi ya wabunge wanawania nafasi ya uenyekiti ambapo katika Mkoa wa Simiyu nafasi hiyoinawania pia na Mbunge wa Afrika, Luhaga Mpina, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa, wilayani Meatu.

  Nafasi hiyo pia inawania na aliyewahi kuwa mbunge wa Afrika Mashariki, George Nangale na Dk. Titus Kamana, Mbunge wa Jimbo la Busega.

  Mkoani Shinyanga, vita kubwa imeibuka baina ya mahasimu wawili, mwenyekiti wa sasa Hamisi Mgeja na James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama. Wengine ni aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Leonard Derefa na Ahmed Salum, Mbunge wa Jimbo la Solwa.

  Kuna madai kuwa, makundi ya Mgeja na Lembeli yameanza kampeni nzito na kila moja linatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa jina la mmoja wao halirudi.

  Kada apinga matokeo ya uchaguzi Songea
  Huko Songea Kada wa CC katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, Laula Malekela, amepinga matokeo ya uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) yaliyomwezesha Anna Hinju, kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

  Malekela anadai hakutendewa haki mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa UWT Wilaya ya Songea Mjini.

  Malekela alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na mizengwe mingi, ambapo mmoja wa watendaji wakuu wa CCM alionekana akimfanyia kampeni za waziwazi mmoja wa wagombea kinyume cha utaratibu.

  Alisema kuwa amewasilisha barua yenye kumb, Na. MGO/SW/002 ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma na kupeleka nakala kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa na Katibu wa UWT Taifa.

  Iringa hakukaliki
  Huko Iringa taarifa zimesema kuwa baadhi ya wagombea mbalimbali katika chaguzi hizo wanaendesha kampeni chafu za udini na ukabila hali ambayo inaendelea kukigawa chama katika makundi.

  Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Wilaya ya Iringa Mjini, Abeid Kiponza, amesema kuwa hali ya chaguzi katika manispaa si shwari kutokana na kukithiri kwa kampeni chafu za udini na ukabila pamoja na vitendo vya rushwa.

  "Ninachosema ni kwamba kuna fununu za baadhi ya wagombea na wanachama ambao wamekuwa wakihusishwa na siasa chafu ambazo kimsingi hazina tija kwa chama.

  "Ni kweli kumekuwa na baadhi ya wagombea na hasa vijana wamekuwa wakitumika vibaya kufanya kampeni mapema kabla ya muda wa kufanya hivyo. Kuna baadhi ya wagombea walianza kampeni toka mwaka jana. Wapo watu ambao kwa makusudi wamekuwa wakikiuka taratibu za uchaguzi ndiyo maana tumekuwa tukipata viongozi wabovu, wasio na sifa, jambo hili linakera kwa vile linaleta mvurugano na msuguano usio wa lazima miongoni mwetu na jamii kwa ujumla," Alisema.
   
 2. commited

  commited JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ukiondoa rushwa ndani ya ccm, basi unaenda kuizika na kuisahau ccm. Hicho chama kipo kwa sababu ya rushwa viongozi wake woote anzia juu mpaka chini kabisa ni wezi na wala rushwa wakubwa, sitegemei jipya toka kwa hicho chama hata wakae mika 200000000.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hata nasikia pale wilayani Monduli wamemkatalia EL!

  Ningependa wapepetane mpaka kila mahala ibaki kweupeeeee!

  Kupasuka kwa pakacha, nafuu kwa mchukuzi!
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  Siasa za urais Hizo ......Rais Hatatoka kaskazini..,,.any potential candidate wanamwekea vikwazo.....

  Sokoine ..Walimuuwa..
  Msuya ....kura hazikutosha....
  mrema ..,,wakamuwekea kigingi cha degree...
  mramba ...mahakamani.....
  Sumaye ...anapigwa vita
  Lowassa anawekewaa zengwee
  Chami wamemtosa uwaziri...hata hivyo U- Nec kapita bila kupingwa....
  mwamry ..,,wamemlazimisha aondoe jina....
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mtu mmoja kulindikiwa vyeo vingi wakati kuna wengi wanaofaa na pia kuwezesha kutanua wigo wa ajira, ni busara kabisa kwa CCM Moshi kumwengua Waziri Aggrey Mwanri katika nafasi hiyo na kuwapisha wengine ambayo hawana ajira. Mwanri ni waziri na mbunge, bado anatamani nafsi zaidi, hapo si sawa.
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ujumbe wa NEC siyo ajira, haina mshahara. Ni kazi ya kujitolea.
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Unasema kweli mkuu?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo la ajira linasababishwa na walioajiriwa hasa wenye nafasi kuzidi kuchukua nafasi zaidi katika ajira wakati wanazo nyingi ambazo zinawazidi nguvu.
  Mwanri ni mbunge na waziri na bado anang'ang'ania NEC, kama kiongozi kwa nini asiachie nafasi hii apate ajira mwingine? Mtu mmoja anataka kupata mishahara mitatu ndiyo aliyokataa Nyerere kwamba mwenye cheo zaidi ya kimoja mshahara utakuwa mmoja tu, hilo lingeendelea hatungeona watu kung'ang'ania nafasi hata wakati wana vyeo vingi.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama hakuna malipo kwa nini wanapigana vikumbo hadi kutoa rushwa?
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Power. Ndani ya chama mjumbe wa NEC ana heshima na power kubwa kuliko mbunge.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Actually mojawapo ya kigezo cha kuchaguli ni kuwa mgombea awe na reliable source of income. Mtu asiye na ajira haqualify kuchaguliwa ujumbe wa NEC.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naweza kukubaliana nawe, lakini kadiri ya chama cha kifisadi kilivyo posho walizojiandalia huko pengine ni zaidi ya zile anazopata Mbunge, vinginevyo watu wasingeingia kwa gharama kubwa hizi hadi kutishiana maisha kwa trigger.
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  You will be surprised, lakini u-NEC hauna pesa yoyote.
  Kambi ziko kwenye kusuka timu ndio maana unaona trigger zinataka kuvutwa. Mchezo 2015, sasa hivi makocha wanapanga timu tu.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa, ndio ule mfumo wa capitalism wakati tunasema nchi yetu ina sera za ujamaa na kujitegemea ndivyo ilivyo katiba ya CCM iliyotokea enzi za TANU.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo imeelezwa kwa maandishi kabisa katika nyaraka za kikazi za CCM na ilikuwa hivyo tangu TANU.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mtoto na familia maskini katu hawaingii huko, maana kipato cha jembe la mkono na hata mbuzi na ng'ombe si kigezo cha kipato ambacho wanatakiwa ku-represent kwa vile hazina hizo hazijawa recorded rasmi kwenye mfumo wa mapato. Kwa hiyo uongozi CCM ni mfumo wa kupokezana vijiti, anafaa au hafai ila hali halisi ndiyo hiyo.
   
 17. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Itakuwa poa sana kama wilaya zingine zitafuata uamuzi wa kamati ya ccm wilaya ya Siha ya kuwaengua hasa wabunge kwenye kugombea nafasi za Nec!!
   
 18. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,521
  Likes Received: 10,439
  Trophy Points: 280
  ndio maana wanashikiana bastola. Inaonekana ukiwa ndani ya nec siasa unazimiliki vizuri sana.!
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kilichonivutia katika tukio la CCM Moshi ni kile ambacho tunalalamika mara nyingi mtu mmoja kuwa na vyeo vingi wakati tuna watu wengi wanaofaa ambao hawapewi nafasi, ila hawa wenye vyeo tayari wanavyolindana kujiongezea mapato na maskini kuzidi kukandamizwa.
   
 20. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,545
  Likes Received: 1,591
  Trophy Points: 280
  si kwamba hamna malipo katika hizo nafasi za ujumbe .......
  they are not able to pay for nothin, there are somthing behind u cant know until u will be part of it......

  hizo ndio Si hasa
   
Loading...