CCM yampuuza Dk. Slaa

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumatano, Agosti 22, 2012 06:03 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

nape.jpg
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepuuza tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alimtaka Dk. Slaa kuacha siasa, kwani hivi sasa anazeeka vibaya.

Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Dk Slaa kuibua madai mazito dhidi ya CCM, akikituhumu chama hicho kuwa kimeingiza silaha, zikiwamo bunduki bila vibali wala kuzikatia leseni, kwa lengo la kutaka kukihujumu.

Nape alivitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi juu ya madai hayo, kwa kuanza kumhoji Dk. Slaa kama shahidi namba moja juu ya uingizwaji wa silaha hizo.

"Kwa alivyo Dk. Slaa hivi sasa, huenda mzee huyo nazeeka vibaya na huenda ana tatizo, hivyo tunaviomba vyombo vya usalama vifanye kazi ya kumhoji.

"Dk Slaa amekuwa akitoa tuhuma nzito eti CCM tunanunua silaha kwa ajili ya kuwapa vijana wetu waliopo kwenye makambi yetu, si kweli, hakuna kambi hata moja ya vijana ila tunaona sasa Dk. Slaa, ameamua kutunga uongo.

"Mwaka 2010, wakati wa kampeni Dk. Slaa, alizua uongo na kusema kuwa kuna kontena limebeba masanduku ya kura kinyemela, nasi CCM tulimsamehe kutokana alikuwa na kihoro cha kushindwa.”

Nape alitumia nafasi hiyo kumshauri Dk. Slaa afanye kazi nyingine iwapo ameshindwa kufanya siasa na akishindwa kabisa basi anaweza hata kuchukua jukumu la kulea familia yake.

MTANZANI ilimtafuta msemaji wa Jeshi la Polisi ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo, huku msemaji wake, Advera Senso, akiahidi kulifuatilia jambo hilo kwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro.
 
Nape angalia japo siasa ndio inakufanya uwe tofauti ila Dr. Slaa is like your father or your teacher my brother. Laana nyingine sio lazima utukane au laa. Jaribu kuwa na adabu usifikie ukajiona wewe mungu mtu kwa sababu ya watu wanaokutumia na kukutupa kama zana za vitandan.
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia kauli aliyoitoa mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza silaha nchini.

"Kauli hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya siasa inamshinda hivyo awaachie vijana" alisema Nape na kuongeza kwamba anatambua kuwa uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza siala kinyemela ni dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.
 
"Kwanza huyu Mzee inaonyesha ni jinsi gani ufuatiliaji wake wa mambo ni vinyu, kutoa madai kwamba tumeagiza siala kinyemela kwa ajili ya makambi ya vijana wetu, wakati inafahamika kwamba wakati huu CCM imo katika uchaguzi mkuu hatuwezi kabisa kuandaa wala kufanya makambi ya vijana", alisema Nape.
 
"Kutokana na kauli hizi za uzushi, tunazitaka mamlaka zinazosimamia ulinzi na usalama kumtaka Dk. Slaa awapatie ushahidi wa kina kuhusu mtu au tasisi yoyote ambayo inaingiza silaha nchini kinyemela, na kama ushahidi wake utawezesha kupatikana yeyote basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria", alisema.
 
"Huyu Mzee imekuwa kawaida yake kuandaa uongo kila anapoona kwamba anakabia kushindwa katika operesheni au mipango yake au ya Chama chake kisiasa. Wakati ule wa Uchaguzi mkuu, alipoona kwamba atashindwa, alizusha kwamba CCM imeingiza kura nchini kutoka nje ya Nchi, lakini ikabainika kuwa ni uzushi", alisema.
 
Alisema, hatua ya Dk. Slaa kuzusha uongo ni njama ya kuandaa fujo zitakazofanywa watu walioandaliwa na Chadema, kufanya fujo mitaani wakati wa mikutano wa chama hicho mkoani Morogoro. " sasa anatoa uongo huu, ili watu wao waliokusanya watakapofanya fujo azushe kwamba ni vijana waliotumwa na CCM".
 
Naona huu uzi kabla hamjarusha mlijipanga kwanza. Haiwezekani wote mnarespond baada ya kurushwa hewani. Hata hivyo, kwa sasa tuhuma za kutunga dhidi ya Dr Slaa hazitawasaidia sana. Mimi naona kama mnamwongezea umaarufu. Watu wana hasira na maisha magumu yaliyopo. Kwa hiyo, kadri mnavyomtukana Dr Slaa anayewasema watz ndivyo mnavyodisha chuki dhidi ya ccm. Nape & co you are not helping ccm at all.
 
magamba na nape imbeni wimbo huu peeeeeeeeeeeeeeeoooooooopleeeeezzzzzzzzzz haya malizia kwa pamoja twendee poooooooooweeeeeeeeeeeer. Nyinyi magamba mmkua wazembe sana sasa ni kwata kwa kwenda mbele mpaka twent15 mpaka muwe sawa
 
wala hawajampuuza, bali wameshindwa kujibu, ukweli ni kuwa wabishe kwa hoja, waache kuleta porojo

watu wanataka data
 
Nape anamshauri Dr. Slaa.....!!!!! maajau haya.

Nape alitumia nafasi hiyo kumshauri Dk. Slaa afanye kazi nyingine iwapo ameshindwa kufanya siasa
 
Back
Top Bottom